Uchaguzi 2020 Inavyoonesha CHADEMA na ACT-Wazalendo hawataungana. Nini kimekwamisha?

Uchaguzi 2020 Inavyoonesha CHADEMA na ACT-Wazalendo hawataungana. Nini kimekwamisha?

Baada ya kumuona Membe amechukua fomu ya Urais meo, nimehitimisha hakuna kuungana Kati ya Chadema na ACT licha ya vyama hivyo kupigia debe suala hili kabla hata ya mchakato wa uchaguzi

Nilitarajia Chadema kuwaachia ACT majimbo yote Zanzibar na Urais na majimbo ya ukanda wa Pwani ambako CUF ilikuwa na nguvu kabla ya kumeguka, na ACT walipe fadhila kwa kuinga mkono Chadema kwenye Urais wa Muungano

Nilimsikia Mbowe na Tundu Lissu wakitamka kuwa japo wamesimamisha wagombea nchi nzima na Zanzibar walikuwa tayari kuwaondoa baadhi ya majimbo kwa Sababu walikuwa kwenye mazungumzo na ACT,

Je, ni nini kimekwamisha Muungano huu?
Tamaa na ubinafsi. STOP
 
Wamekubaliana kwamba wote waingie kwenye kampeni alafu watapima upepo wiki mbili kabla mmoja atajitoa.
 
Wanasiasa wanafikia makubaliano pale wanapoona watanufaika vinginevyo...
 
We tulia Membe na Zitto hawawezi toboa bila kuungana wanalijua ilo Rais ni Lissu
Mkuu hivi ni Vituko vya mwaka,eti hawawezi toboa ,watoboe waende wapi wakati mlidai tume ya uchaguzi ni ya CCM, unaamini kabisa kwa akili za chekechea lissu mzee wa lopolopo atashinda uchaguzi huu
 
Mkuu tuongee uhalisia hivi unaachiwa vipi kitu ambacho tayari una udhibiti nacho?
CDM wanawezaje kusema wana waachia ACT majimbo ya Zanzibar wakati ukweli ni kwamba wanajua hata kama CDM wakiweka mgombea wao hatamshinda wa ACT?

Bara nako CDM wanasema watawaachia ACT mikoa ya pwani ambako tayari kila mtu anajua ACT au CCM watashinda.

Huu muungano ni wa kuifaidisha CDM tu kiuhalisia hasa hapo kwenye kuachiwa majimbo mengi bara na kuachiwa uraisi wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Muungano lazima uoneshe kila mtu anatoa kitu flani siyo yeye anapokea tu na kuongezewa alichonacho na mwenzie haongezewi kitu.

Niwashauri kama wana nia ya dhati ya kuungana basi waachiane hivyo walivyopanga lakini atakaepewa uraisi wa Jamhuri na kushinda basi ateue wabunge wote wa viti maalum vya raisi toka chama kingine kilichokubali kuachia uraisi, pia waziri mkuu atoke chama kilicho achia (kama katiba ina ruhusu) au wagawane nafasi baraza la mawaziri 50/50.

Hii kamari niliyo pendekeza ni kama tu kweli wanajiamini yupo wa kumshinda Magufuli miongoni mwao.
CHADEMA Ni matapeli Fulani halafu huwa wanaona Kila mtu mjinga.

Mbowe Ni mbinafsi mno.

Wanachotaka kufanya Ni saws na CHAUMA waseme wanajitoa kugombea ili Magufuli ashinde.

Ujinga mtupu.
 
Baada ya kumuona Membe amechukua fomu ya Urais meo, nimehitimisha hakuna kuungana Kati ya Chadema na ACT licha ya vyama hivyo kupigia debe suala hili kabla hata ya mchakato wa uchaguzi

Nilitarajia Chadema kuwaachia ACT majimbo yote Zanzibar na Urais na majimbo ya ukanda wa Pwani ambako CUF ilikuwa na nguvu kabla ya kumeguka, na ACT walipe fadhila kwa kuinga mkono Chadema kwenye Urais wa Muungano

Nilimsikia Mbowe na Tundu Lissu wakitamka kuwa japo wamesimamisha wagombea nchi nzima na Zanzibar walikuwa tayari kuwaondoa baadhi ya majimbo kwa Sababu walikuwa kwenye mazungumzo na ACT,

Je, ni nini kimekwamisha Muungano huu?

Bado, usihitimishe....

Uchaguzi wa mwaka huu ni so trickery...

Unapaswa kufikiri 1000 miles mbele ya NEC - CCM na wote wanaotaka Jiwe awe peke yake....

Tutasema imeshindikana iwapo Tundu Lissu atachukua fomu na kuirudisha NEC na Membe akafanya hivyo hivyo....

Kwa hatua hii, unaweza kuchukua fomu NEC na usiirudishe na mambo yakawa hivyo...
 
CHADEMA Ni matapeli Fulani halafu huwa wanaona Kila mtu mjinga.

Mbowe Ni mbinafsi mno.

Wanachotaka kufanya Ni saws na CHAUMA waseme wanajitoa kugombea ili Magufuli ashinde.

Ujinga mtupu.
Daah nimecheka sana hapo kwenye mfano wa CHAUMA, lakini ni kweli tupu usemayo.
 
Ili Membe awe mgombea mwenza lazima aache uanachama ACT na kujiunga CDM. Kumbuka Juma Haji Duni wa CUF 2015, aliondoka CUF na kujiunga CDM ndipo akawa mgombea mwenza wa Mzee White hair.
Ninafahamu, ila kumbuka kuwa penye nia ........
 
Katiba hairuhusu hilo,mgombea mwenza lazima atoke Zanzibar ndio maana salum mwalimu kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Lissu
Katiba haijasema mgombea mwenza kutoka Zanzibar, wametukaririsha tu! Kama vile akitoka Mkatoliki Rais anayefuata Muislamu, je hii nayo ni katiba? Hebu nitajie Makamu wote wa Rais wa Tanzania tangu Uhuru
 
Nachohisi mimi ni
1. Membe kachukua fomu kama back up ya figisu za Lissu kama atafanyiwa.
2. Ni poteza maboa tu wasimsumbue Lissu ila fomu yake hatairejesha hivyo jina lake halitatoka kwenye makaratasi ya wagombea na kumpa fursa ya mkumsaidia Lissu kubaki kupambana na John
 
ACT kama NCCR wanataka waachiwe majimbo wayauze kwa ccm, lakini wanataka CHADEMA ikishinda wagawane ruzuku kwasababu eti iliwaachia majimbo.

Kwa msingi huo, Kila chama kipambane kivyake, ili kila mmoja avune alichopanda.
Waungane ili iweje?!

Malalamiko yao ilikuwa kwamba, wakati wa UKAWA Chadema iliwatumia, sasa unadhani hiyo dhana itawaisha?!

Waliionea wivu CHADEMA na kuanza kuihujumu kwa kupeleka uongo huko ccm ,kwasasa kila mtu aende kivyake.

Ukipigwa, ujue ulipigwa kihalali, na ukishinda tembea kifua mbele.

ACT ikishinda Zanzibar haita share madaraka na yeyote, kila mmoja aweke nguvu anapoona anakubalika. Hakuna haja ya kuungana kisha muanze kuoneana wivu na kuanza kusalitiana.

Akishinda sawa, na ukishindwa usilaumu muungano wala nini ukae mbali.

CCM hawataki kuungana na chama chochote, kwanini nyie muungane?!

Walipaswa waungane 5 yeas kabla ya uchaguzi, lakini sio wiki moja kabla ya uchaguzi, hii itawaletea shida.

Kila chama kipige push up zake. Kikapambane kivyake, wengi wanafiki.
Hasa Mbatia na Zitto ni wanafiki sana.

Mbatia anajiona bonge la mwanasiasa, na alijiona kaibeba CHADEMA alipokuwa UKAWA.

Zitto hakutaka UKAWA akiamini angeweza bila UKAWA, leo muungano wa nini?

Lipumba wote mnafahamu alivyo msaliti na kaishiwa hana cha kuchangia kwenye muungano, hivyo aachwe, hata asijadiliwe.
Kwa hiyo kwa jinsi ulivyoandika ni kama vile vyama vingine ndo vevyee nakosa ila CDM wao ni mungu watu wao hawakukosea .madhifu ni ya vyama vingine tu ya ACT ,NCCR na CUF

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Kama unafahamu walichokosea Chadema wakiwa UKAWA andika hapa, hili jukwaa huru.

Hakuna nilipomtaja Mungu wala kusema Chadema ni miungu, wewe toa maoni yako kwa hoja iliyopo jukwaani.
 
Tulieni kwanza dawa iwaingie yaani mnataka mmoja asichukuwe fomu ili atakaye chukuwa mumuwekee pingamizi!? Hapo najuwa mmepingwa chenga ya mwili dadadeki watu wamejipanga mzee picha ndokwanza linaanza kesho
 
Baada ya kumuona Membe amechukua fomu ya Urais leo, nimehitimisha hakuna kuungana Kati ya Chadema na ACT licha ya vyama hivyo kupigia debe suala hili kabla hata ya mchakato wa uchaguzi

Nilitarajia Chadema kuwaachia ACT majimbo yote Zanzibar na Urais na majimbo ya ukanda wa Pwani ambako CUF ilikuwa na nguvu kabla ya kumeguka, na ACT walipe fadhila kwa kuinga mkono CHADEMA kwenye Urais wa Muungano

Nilimsikia Mbowe na Tundu Lissu wakitamka kuwa japo wamesimamisha wagombea nchi nzima na Zanzibar walikuwa tayari kuwaondoa baadhi ya majimbo kwa Sababu walikuwa kwenye mazungumzo na ACT,

Je, ni nini kimekwamisha Muungano huu?
Wote wanachukua form
Baada ya kupitishwa na NEC ndio Ushirikiano unaanza
Unataka wasichukue form achukue mmoja halafu NECCM ifanye uhuni wa Kumuengua
 
Mkuu tuongee uhalisia hivi unaachiwa vipi kitu ambacho tayari una udhibiti nacho?
CDM wanawezaje kusema wana waachia ACT majimbo ya Zanzibar wakati ukweli ni kwamba wanajua hata kama CDM wakiweka mgombea wao hatamshinda wa ACT?

Bara nako CHADEMA wanasema watawaachia ACT mikoa ya pwani ambako tayari kila mtu anajua ACT au CCM watashinda.

Huu muungano ni wa kuifaidisha CDM tu kiuhalisia hasa hapo kwenye kuachiwa majimbo mengi bara na kuachiwa uraisi wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.

Muungano lazima uoneshe kila mtu anatoa kitu flani siyo yeye anapokea tu na kuongezewa alichonacho na mwenzie haongezewi kitu.

Niwashauri kama wana nia ya dhati ya kuungana basi waachiane hivyo walivyopanga lakini atakaepewa uraisi wa Jamhuri na kushinda basi ateue wabunge wote wa viti maalum vya raisi toka chama kingine kilichokubali kuachia uraisi, pia waziri mkuu atoke chama kilicho achia (kama katiba ina ruhusu) au wagawane nafasi baraza la mawaziri 50/50.

Hii kamari niliyo pendekeza ni kama tu kweli wanajiamini yupo wa kumshinda Magufuli miongoni mwao.
Wewe li CCM yetu upinzani hayakusu
 
Back
Top Bottom