Mkuu kama CDM na ACT wakikubaliana kumsimamisha mgombea mmoja itabidi mmoja wao, ama Membe ama Lissu asirudishe fomu. Ila hili la kuchukua wote fomu ni la muhimu.Membe keshachukua fomu, NEC watamuweka kwenye karatasi ya kura
Isome vizuri katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977Hawa jamaa walipaswa kumuweka Membe kama mgombea Mwenza na Lissu Rais....Kampeni zisingeshikika
Mimi hiyo Ni proposal yangu binafsi tu, nikimaanisha vyama viachiane sehemu ambazo vina nguvu kuliko kugawana kura na kuipa advantage CCMMkuu tuongee uhalisia hivi unaachiwa vipi kitu ambacho tayari una udhibiti nacho?
CDM wanawezaje kusema wana waachia ACT majimbo ya Zanzibar wakati ukweli ni kwamba wanajua hata kama CDM wakiweka mgombea wao hatamshinda wa ACT?
Bara nako CDM wanasema watawaachia ACT mikoa ya pwani ambako tayari kila mtu anajua ACT au CCM watashinda.
Huu muungano ni wa kuifaidisha CDM tu kiuhalisia hasa hapo kwenye kuachiwa majimbo mengi bara na kuachiwa uraisi wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.
Muungano lazima uoneshe kila mtu anatoa kitu flani siyo yeye anapokea tu na kuongezewa alichonacho na mwenzie haongezewi kitu.
Niwashauri kama wana nia ya dhati ya kuungana basi waachiane hivyo walivyopanga lakini atakaepewa uraisi wa Jamhuri na kushinda basi ateue wabunge wote wa viti maalum vya raisi toka chama kingine kilichokubali kuachia uraisi, pia waziri mkuu atoke chama kilicho achia (kama katiba ina ruhusu) au wagawane nafasi baraza la mawaziri 50/50.
Hii kamari niliyo pendekeza ni kama tu kweli wanajiamini yupo wa kumshinda Magufuli miongoni mwao.
Badala ya kumwambia aisome katiba kwanini usitueleze direct kuna kitu gani.Isome vizuri katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
Uroho wa madaraka na uroho wa RuzukuBaada ya kumuona Membe amechukua fomu ya Urais meo, nimehitimisha hakuna kuungana Kati ya Chadema na ACT licha ya vyama hivyo kupigia debe suala hili kabla hata ya mchakato wa uchaguzi
Nilitarajia Chadema kuwaachia ACT majimbo yote Zanzibar na Urais na majimbo ya ukanda wa Pwani ambako CUF ilikuwa na nguvu kabla ya kumeguka, na ACT walipe fadhila kwa kuinga mkono Chadema kwenye Urais wa Muungano
Nilimsikia Mbowe na Tundu Lissu wakitamka kuwa japo wamesimamisha wagombea nchi nzima na Zanzibar walikuwa tayari kuwaondoa baadhi ya majimbo kwa Sababu walikuwa kwenye mazungumzo na ACT,
Je, ni nini kimekwamisha Muungano huu?
Kama huyo jamaa hawlewi hilo takwa la Kikatiba basi hasaidiki hata akiwekewa Ibara husika hapa. Kwamba hajui huwezi kuwa na mgombea Urais na Mgombea mwenza toka sehemu moja ya Muungano?Badala ya kumwambia aisome katiba kwanini usitueleze direct kuna kitu gani.
Unataka aanze kusoma vifungu na vipi kama hajui kuvitafsiri. Ikishindikana kabisa taja kifungu na ibara.
Huu ni mtego mkali wa panya...CCM kwa sasa hawajui wapange mikakati ipi kupambana na yupi kati ya Membe na Lissu. ...usisahau zenji kuna mzee wa sawa sawa!!Baada ya kumuona Membe amechukua fomu ya Urais meo, nimehitimisha hakuna kuungana Kati ya Chadema na ACT licha ya vyama hivyo kupigia debe suala hili kabla hata ya mchakato wa uchaguzi
Nilitarajia Chadema kuwaachia ACT majimbo yote Zanzibar na Urais na majimbo ya ukanda wa Pwani ambako CUF ilikuwa na nguvu kabla ya kumeguka, na ACT walipe fadhila kwa kuinga mkono Chadema kwenye Urais wa Muungano
Nilimsikia Mbowe na Tundu Lissu wakitamka kuwa japo wamesimamisha wagombea nchi nzima na Zanzibar walikuwa tayari kuwaondoa baadhi ya majimbo kwa Sababu walikuwa kwenye mazungumzo na ACT,
Je, ni nini kimekwamisha Muungano huu?
Asipozirudisha hizo fomu watamuwekaje?Membe keshachukua fomu, NEC watamuweka kwenye karatasi ya kura
Katiba hairuhusu hilo,mgombea mwenza lazima atoke Zanzibar ndio maana salum mwalimu kuchaguliwa kuwa mgombea mwenza wa LissuHawa jamaa walipaswa kumuweka Membe kama mgombea Mwenza na Lissu Rais....Kampeni zisingeshikika
Watamuweka Ikiwa atarudisha formMembe keshachukua fomu, NEC watamuweka kwenye karatasi ya kura
Ni hadi arejeshe ndiyo anaingia kwenye list ya wagombea. Kumbuka unaweza kuchukua form ukajaza vibaya ukatupwa nje, hivyo baada ya kurejesha form iliyokamilika ndipo unaingia kwenye orodha. Kuchukua tu siyo hoja.Membe keshachukua fomu, NEC watamuweka kwenye karatasi ya kura
Ili Membe awe mgombea mwenza lazima aache uanachama ACT na kujiunga CDM. Kumbuka Juma Haji Duni wa CUF 2015, aliondoka CUF na kujiunga CDM ndipo akawa mgombea mwenza wa Mzee White hair.Hawa jamaa walipaswa kumuweka Membe kama mgombea Mwenza na Lissu Rais....Kampeni zisingeshikika
Hivi itakuwa vyema kama nguvu ya ACT na Chadema ikawa moja.Nafikiri bado mazungumzo yanaendelea na ni vizuri kila mgombea akachukua fomu yake lakini bado yawezekana akajiondoa na kumunga mkono mgombea wa chama mshirika. Na ndivyo itakavyokuwa, msihofu.