Inaweza kukugharimu kiasi gani kujenga Ghorofa kama hili?

Wazungu siku hizi siyo watoaji wa hovyo kama zamani..inflation imewanyoosha
 
Mkuu si unaangalia tu na kukadiria. Mwamba hapo juu anadai 900 million. Kama ni kweli nina uwezo wa kujenga kama hizo 20.
Maghayo mwenye uwezo wa kujenga hizo 20 kwa 900 m hawezi kutaka ushauri kutoka kwa Isanga Family sema unataka kujenga ila unauliza uliza usije ukapewa makadilio makubwa na mafundi wetu.

Ujenzi unategemea unataka kujenga Mkoa gani na eneo gani maana kinachoongeza gharama au kupunguza ni upatikanaji wa Material mpaka site basi daslm wapo wachina wanauza Zege kwa kiwango bora kabisa mnakadiriana harafu wanakuja kumwaga mzigo mafundi wako watahangaika na ujenzi wa Tofali na mambo mengine sio Zege...
 
Sikiliza mdogo wangu.
Umeuliza swali linaelea hewani hayupo atakayekupa jibu sahihi.

Yeyote atakayekupa makadirio ni muongo kwa sababu hii hapa;

1. Katika kukadiria majenzi ma QS ( QUANTITY SURVEYORS)

huwa wana muongozo maalum wa kukokotoa gharama za ujenzi yaani kutengeneza BOQ.

2. Miongozo hiyo hutegenea kuwa jengo ni;
-residential house
-hospitals
-schools
-Godowns buildings

Katika kina hizi za majengo kila aina ya jengo lina bei ya muongo au elekezi (wastani wa gharama)

Mfano tu:

1. Hospital =1,000,000/m²
2. Godown=800,000/m²
3. Residential hse=1,300,000/m²


Kwa hiyo unachotakiwa kufanya ni kuwa na michoro kuanzia G floor, 1 floor hadi ya mwisho.
IKiwa G floor ina upana 10m na urefu ni 15m....
Utafanya; 10x15x1,300,000=195,000,000.

Hii ni thamani ya floor, then unazidisha mara idadi ya floor zako kwa idadi yake.

Note: kwa wale wa kukurupuka huu ni wastani tu ambapo gharama yaweza kushuka kidogo au kupanda lakini ni makadirio ya wastani.

Mwisho; huu ni mfano tu namna ya kupata gharama, hivyo namba zaweza zisiwe sahihi
 
Mk
MKuu mjengo huo umevuka level ya mafundi..
Huo ujenzi utahitaji ma consultants watatu na mjenzi wa 4.
1. Architect
2. Qs
3. Structural engineer.
4. Ndipo mjenzi.

Hapo hakuna ubabaishaji.
Sema mwamba anaweza kujiendea tu
 
GT am overwhelmed with gratitude for your comment. Thanks so much.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…