Inawezekana kubadili chuo kwenda Advance?

Inawezekana kubadili chuo kwenda Advance?

Habari zenu wakuu!

Kuna dogo alipata division 2 form 4 lkn post zilizotoka leo amepangiwa kujiumga na chuo cha CBE kozi ya Marketing. Dogo hataki kwenda huko chuo, anataka kwenda advance akapige PCM. Je inawezekana serikali kumbadilishia post akapige hiyo PCM au ni mpaka aende private school?

Matokeo yake form 4 yapo hivi: CIV - 'C' HIST - 'C' GEO - 'C' E/D/KIISLAMU - 'F' KISW - 'C' ENGL - 'D' PHY - 'D' CHEM - 'C' BIO - 'C' B/MATH - 'C'
Aende chuo au aombe kubadilishwa chuo na tamisemi wenyewe na wanapataga punguzo la ada hata malazi sio kama walio omba wenyewe

Na unakuta analilia kwenda 5 huku kwenye ts9 form aliweka advance last priority

Na advance sio kwamba ni ishu sana mimi nilisoma certificate ya accountant niko kazini saivi naadvance nimemaliza mwaka huu apate ujuz kwanza

Makampuni yenyewe yanaajiri watu wenye elimu ndogo kupunguza cost za mishahara na mavitu vitu kibao
 
mim pia ninashida hiyo hiyo nimepelekwa chuo huasibu arusha ila mim nilitaka kwenda advance
Ufaulu wako ukoje? Hivi mnadhani Tamisemi ni wajinga kukupanga chuo na sio advance?
 
Na comb gan unataka? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwa matokeo hayo, aende tu chuo akasome course za Engineering, ila km n PCM hatoboi hata asome vipi, hivi mziki wa advance ni mchezo? Atajuta baadae, bora aende chuo huko.
 
Siki hizi Tamisemi hawakuchagui kama kwenye kombi yako hauna at least CCC sasa huyo dogo kwenye PCM hiyo D ya Physics imemharibia bora angekuwa aliomba CBG
 
Hivi naomba kuuliza kwa waliopangwa chuo na serikali, ada zao zinakuaje ni nafuu au? Na je chakula wanalipiwa na serekali au
 
Mbadilishie chuo aende dit or vyuo vingine vyenye kozi za engineering asithubutu kwenda advance
 
Back
Top Bottom