Inawezekana kufanikiwa kisiasa bila kuwa "mjanja mjanja"?

Inawezekana kufanikiwa kisiasa bila kuwa "mjanja mjanja"?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Japo siamini kama ni wote, lakini inaonekana kama vile wanaofanikiwa kwenye siasa wana tabia za kipekee kama:

• Bingwa wa kusema uongo
• Mbabe
• Majuzi wa kuiba kura
• Mpenda ushirikina

Ni kama vile wengi wa wasema ukweli na wapenda kufuata njia halali huwa hawakubaliki. Je, ni lazima kuongopea ili kung'ara kisiasa?
Ni lazima kuwa mshirikina ili kukubaliwa na wapiga kura?
Ni lazima kuiba kura ili ushinde uchaguzi?
Ubabe ni wa lazima kwenye siasa?
Nauliza kwamba, unaweza kufanikiwa kisiasa kwa kufuata njia halali pekee bila kuwa mwongo au kucheza rafu? Inawezekana?
 
Hata maisha ya kawaida lazima uwe:-

Muongo
Tapeli
Connections za mjini mjini
Roho mbaya
Sura ya kinyonga
Ushirikina

Mwanasiasa akipata kura ya kuchaguliwa lazima akimbie mtaa anajua mtaani kuna wanga na waongo kuliko yeye😂😂
 
Askofu Gwajima mwenyewe pamoja na kujiita Mtumishi wa Mungu, aliishia kuwapiga uongo watu Kawe.
. Kuwapeleka Birmingham
. Kununua bulldozer
. Kujenga barabara za mitaa

Yote hayo hakuna asilimia Moja aliyotekeleza. Na amini tu, Kama asingesema uongo huo asingepata ushindi kwenye box la kura, labda kwakua Magufol alishaandaa utaratibu wa kuteka ushindi.
 
Hata maisha ya kawaida lazima uwe:-

Muongo
Tapeli
Connections za mjini mjini
Roho mbaya
Sura ya kinyonga
Ushirikina

Mwanasiasa akipata kura ya kuchaguliwa lazima akimbie mtaa anajua mtaani kuna wanga na waongo kuliko yeye😂😂
😀😀😀
 
Inasemekana hata Nyerere alipokuwa akitafuta uungwaji mkono wa Watanganyika, aliwaahidi kuwa wakiichukua nchi hawatakuwa wakitozwa kodi. Uhuru ulipopatikana na "lugha" ikabadilika na kuwa "Kodi kwa maendeleo". Matokeo yake, mpaka sasa Watanganyika wengi hawapendi kulipa kodi, wanachukulia ulipaji kodi kama uonevu wa kikoloni.
 
Tena kudanganya mie siwezi,sa itakuwaje? Ila siasa ni nusu ulozi
 
Tena kudanganya mie siwezi,sa itakuwaje? Ila siasa ni nusu ulozi
Labda uongo siyo lazima! Unajua wanasiasa nao huingia nyumba za ibada? Tena wakati mwingine, ukiwakuta wakiongea kwenye hadhira ya waumini, unaweza ukatamani akabidhiwe msaafu ili ahubiri kabisa.
 
Labda uongo siyo lazima! Unajua wanasiasa nao huingia nyumba za ibada? Tena wakati mwingine, ukiwakuta wakiongea kwenye hadhira ya waumini, unaweza ukatamani akabidhiwe msaafu ili ahubiri kabisa.
🤣🤣🤣🙌🏿
 
Back
Top Bottom