Inawezekana kumkaririsha kidato cha pili mtoto aliyefaulu? Utaratibu ukoje?

Inawezekana kumkaririsha kidato cha pili mtoto aliyefaulu? Utaratibu ukoje?

Habarini wanajamvi; wema na wabaya wa mada hii!

Nauliza kama mzazi nina uhuru wa kumkaririsha kidato cha pili mtoto wangu aliyefaulu mtihani wake wa kidato cha pili (FTNA) kwa vile hakufaulu kwa viwango nivitakavyo mimi na vya kumsaidia maisha yake?

Yaani, kwa mfano, mtoto kapiga A na B masomo yote ya arts na kufaulu vzr tu, tatizo ni kuwa sayansi ana C moja na zilizobaki ni D.

Ukimuangalia kwa umakini uwezo anao isipokuwa tu mkazo ulikuwa huko arts. Muelekeo wa dunia unataka sana sayansi kwa sasa nawe unatamani upate muda tena wa kumuandalia mazingira ili apige vzr hayo masomo kwa kuupata mwaka mmoja zaidi. Je, inawezekana?!!!!

Karibuni wajuzi!
Una mawazo ya kishamba sana .

Muache mtoto asome kile anachokipenda na kukiweza.
 
We ndo unataka kumuharibia mwanao mana inabid mtt amalize on time na hakuna science ya darasan haswa ya tz itayomfanya awe vzur dunian ndo mana wana science wa bongo hata kutengeneza panadol hawawez znatoka kenya so muache mtt afanye anachoweza na anachokipenda sio ww unachopenda ww mbona hujawa mwana science mbobevu wa nchi yetu
🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Habarini wanajamvi; wema na wabaya wa mada hii!

Nauliza kama mzazi nina uhuru wa kumkaririsha kidato cha pili mtoto wangu aliyefaulu mtihani wake wa kidato cha pili (FTNA) kwa vile hakufaulu kwa viwango nivitakavyo mimi na vya kumsaidia maisha yake?

Yaani, kwa mfano, mtoto kapiga A na B masomo yote ya arts na kufaulu vzr tu, tatizo ni kuwa sayansi ana C moja na zilizobaki ni D.

Ukimuangalia kwa umakini uwezo anao isipokuwa tu mkazo ulikuwa huko arts. Muelekeo wa dunia unataka sana sayansi kwa sasa nawe unatamani upate muda tena wa kumuandalia mazingira ili apige vzr hayo masomo kwa kuupata mwaka mmoja zaidi. Je, inawezekana?!!!!

Karibuni wajuzi!
HAIWEZEKANI hasa akishafanya paper la kidato cha pili ili mtoto arudie darasa sababu inatakiwa iwe ni UTORO tu na anaemia Kibari ni afisa Elimu mkoa

Utaratibu ni kuandika barua kwenda shule then shule wanapiga muhuri wanaambatanisha na mahudhurio yake kwa kupiga copy ya Attendece

Ukifika kwa afisa elimu mkoa (lazima upite kwa afisa elimu wilaya pia) ndio analia Kibari kwa mazingira haya

•Ujieleze kwann mtoto alikuwa haendi shule (hapa unatakiwa uwe na sababu madhubuti na vielelezo) kama hauna afisa elimu anakuweka ndani kwa kosa la UTORO wa mwanao

So sababu pekee ni UTORO

(Mzazi mwenzangu ni afisa elimu ndio aliyenifafanulia Huyu ndio nilimtoa IT nikampenyeza hapo kwa msaada wa jamaa wa ikuru)
 
Kumkaririsha sio suluhu,mapokeo ya kukaririshwa yakiwa hasi kwake ndio itamfanya arud nyuma zaidi kitaaluma,hapa nna maana kwamba kama atachukulia kitendo hicho kama adhabu ndio atakuja kuferi zaidi na zaidi.
Nini kifanyike? Aendelee na kidato cha tatu na achukue masomo ya sayansi,Mtafutie walimu wazuri watakaoweza kumjenga kwenye masomo hayo aliyoferi,asiishie tu kufundishwa ili mradi mada ziishe,mwalimu amfundishe kwa kudadisi ni wapi mwanafunzi huyo alianza kudondoka kwenye somo husika,pale alipoanzia kudondoka amnyanyue,yaani amfundishe na kumpa mazoezi ya kutosha kwa mada ambazo hakuzielewa vizuri na ambazo alizielewa vizuri pia.
Mbali na sababu zingine,kuferi somo fulani kunachangiwa na msingi mbovu anaokuwa nao mwanafunzi,mfano,ni ngumu mwanafunzi mwenye msingi mbovu std vii hadi form one akafaulu vizuri form 2 kwa div 1,2_3,huyu atafaulu kisiasa (div iv_pass[emoji23])
Mwisho,wazazi na walezi tutenge muda hata mara moja kwa wiki kufuatilia maendeleo ya kitaaluma,tabia na mienendo ya watoto wetu,tuzidi kujenga mahusiano na walimu ambao tumewakabidhi watoto wetu watulelee kwa masaa 9 (day school) na hata boarding pia.
 
Ulipiga HKL nini we dada na kufeli?!!!!
Kuniita dada, haifichi upumbavu wako wa kukariri maisha kama unavyotaka kumkaririsha mwanao ili hali yeye kiupeo kakuacha mbali sana. Una maisha magumu mno na ninaihurumia sana familia yako
 
Ahsante sana kiongozi!
Hiyo aya ya mwisho umeongea jambo zito sana ambalo baadhi yetu humu tunajifanya kulipotezea...
Nashukuru Mkuu

Mara zote watoto hututegemea zaidi Wazazi wao kwenye kuwaongoza vyema.

Ndiyo maana Biblia kupitia Kitabu cha Mithali, kinasema Mlee mtoto katika njia impasayo naye hatoiacha hata atakapokuwa Mzee.

Kwahiyo ukimwandaa mtoto kuwa Daktari atakuwa

Ikiwa rubani atakuwa, muhimu kama Mzazi kumuandalia msingi mzuri wa kumsimamia ili kufikia ndoto zake.
 
Kuniita dada, haifichi upumbavu wako wa kukariri maisha kama unavyotaka kumkaririsha mwanao ili hali yeye kiupeo kakuacha mbali sana. Una maisha magumu mno na ninaihurumia sana familia yako
Yaani we ndo hamna kitu kabisa, changia hoja na Acha kutembea kwenye hisia na ukariri. Humjui mtoto wala matarajio yake; mi ndo namjua......kukusaidia tu we kilaza, hakuna masomo anayoyapenda kama ya sayansi na hata ukimuuliza ndoto zake anakujibu anatamani utabibu; hujui mazingira; mi ndo nayajua, huko shuleni kwake walimu wa sayansi ni sawa na kusema hakuna ilhali wa sanaa ni wengi sana. Hujui mazingira yangu ya kipindi hiko zaidi ya mimi, hujui sasa hv nimeimarika kiasi gani kuweza kumsapoti. Nilichoulizia ni uwezekano au kutowezekana tu basi, na wewe kama ungekuwa na utu uzima wa kutosha basi ungelielewa hilo.
 
Back
Top Bottom