Inawezekana kuna Grand Corruption nyuma ya maamuzi haya ya wanasiasa wetu

Inawezekana kuna Grand Corruption nyuma ya maamuzi haya ya wanasiasa wetu

Siku ya jana niliweka bandiko hapa nikionyesha wasiwasi wangu kuwa huenda kuna grand corruption ilionyuma ya usaliti huu wa wanasiasa unaoendelea. Nakumbuka kuna watu humu walinipinga sana kwani wengi wana mtazamo kuwa rushwa ya vyeo na madaraka pekee ndio inawashawishi huku MATAGA wao wakioni mimi kama mzushi au naongea jambo ambalo halipo.

Leo hii nashukuru yule whistleblower maarufu kule twitter kaibua tuhuma hizo na kwenda mbali kwa kuonyesha nia ya kuwaanika wahusika huku akisema liwalo na liwe.

Nashukuru pia kaweka wazi kuwa aliwasaidia CHADEMA kwa kuwapa taarifa, taarifa iliyopelekea baadhii ya watu kuondolewa kwenye kampeni za Lissu na sasa anakusudia kuwaanika wanasiasa wote wa upinzani waliohusika katika tuhuma hiyo ya kupokea mlungula na kusaliti wananchi.

Tusubiri.
 
Kwani Yeye na wewe mnautofauti upi kuhusu ukweli wa Hilo???

Kwa hiyo unadhani watu wa jamii ya Twitter wao wakiongea ndio inakuwa kweli kuliko tulioko mitandao mingine

Akili za machadema ni Sawa na za Baba Yao wa kuleee.....!!!!
 
Siku ya jana niliweka bandiko hapa nikionyesha wasiwasi wangu kuwa huenda kuna grand corruption ilionyuma ya usaliti huu wa wanasiasa unaoendelea...

Kwahiyo sasa tufanyaje? Tuanze kulia? ili nitaarishe machozi?

Nani kawaambia kuna kitu rahisi duniani? Kama upinzani ni team iliyokamilika, mna wasiwasi gani na wasaliti? Wapi ambako hakuna wasaliti?

Mzee baba, mnaanza kutafuta excuse. ili mjifurahishe moyo, kwa kufikiri kusingizia mtu kutabadili hali ya hewa.

Yale makaratasi ya ICC bado Amsterdam anayo, au ameyafanya toilet papers?
 
Kwani Yeye na wewe mnautofauti upi kuhusu ukweli wa Hilo???

Kwa hiyo unadhani watu wa jamii ya Twitter wao wakiongea ndio inakuwa kweli kuliko tulioko mitandao mingine

Akili za machadema ni Sawa na za Baba Yao wa kileee.....!!!!
Kama na wewe ni mmoja wao kutoka watu wa KITENGO, jiandae tu.
 
Siku ya jana niliweka bandiko hapa nikionyesha wasiwasi wangu kuwa huenda kuna grand corruption ilionyuma ya usaliti huu wa wanasiasa unaoendelea...
Akiziweka Chadema inakufa hapo hapo.

Unadhani kwanini Halima Mdee na wenzake wamewahi bungeni?!

Hapo Chadema kamati kuu yote ni mkate tu mbele ya chai CCM!
 
Kunini sasa mkuu,Mambo yenu ya uzushi 98% ukweli wenu misema ni kidogo sana ukilinganisha na uwongo mwingi mnaotapika mitandaoni

Yale ya ICC yako wapi tena, mmedakia mengine tena!!

Ninyi...😂😂😂😂
Kwakuwa kuna suala fulani, basi mengine yasijadiliwe? Mbona tuliambiwa kupitia umeme wa gas tutapata 5,000mg, inakuwaje tumeachana na umeme wa gas hata hatujafikia 2,000, lakini tumerukia umeme wa maji wa 2,115mg?
 
Back
Top Bottom