Inawezekana kuongeza makato ya mkopo benki?

Muuliza swali hataki kukopa tena top up maana yake unaongea mkopo juu ya mkopo muuliza swali anataka amalize kulipa ili awe huru au akakope kwingine. Mjibu kwa muktadha huu na sio wa top up.
Ni kweli kabisa
 
Mkataba wa kukopa ni wa kwako, kwa hiyo unaweza kubadilisha marejesho utakavyo. Cha msingi makato yasizidi kiwango cha ukomo cha kukatwa kilichowekwa na benki na/ama mwajiri.
Anhaa, ahsante
 
Habarini!
Najua kuna kila aina ya wataalamu humu. Nauliza kuna uwezekano wa kuongeza makato yako benki ikiwa mdaiwa umeamua hivyo? Yaani labda ulikuwa unakatwa 200,000 kwa mwezi, sasa umepanda daraja labda na unataka kilichoongezeka kiende ktk makato yako ili umalize haraka deni (ukatwe 300,000/= sasa). Je, inawezekana? Km inawezekana utaratibu upoje?
Inawezekana. Nunua mkopo wako hapo hapo ulipokopa, linalipwa deni na unaanza kutumikia deni jipya kwa makato makubwa. Lakini benki zinatofautiana katika muda ambao unaweza kununua, CRDB hadi uwe umetumikia mkopo wa mwanzo kwa walau miezi sita
 
Yaani amekosa ubunifu wa kuitumia hio income ambayo addition na kuipangia income generating item, aukuoffset potential laps in inflation kwa early purchase ya baadhi ya bidhaa. Generally speaking in financial words
Eh, kiongozi hii naona kama lugha ya kiuhasibu mnooo. Tumia ya kawaida basi kidogo tuelewe sote!
 
Inawezekana. Nunua mkopo wako hapo hapo ulipokopa, linalipwa deni na unaanza kutumikia deni jipya kwa makato makubwa. Lakini benki zinatofautiana katika muda ambao unaweza kununua, CRDB hadi uwe umetumikia mkopo wa mwanzo kwa walau miezi sita
Du, kwa maana kuna kiasi kitaongezeka tena katika deni kuu?!!!!!
 
Lakini pia kitapungua kutokana na kulipa jumla ya riba ndogo maana muda umekuwa mfupi. Kumbuka ukikopa kwa muda mrefu na jumla ya riba inakuwa kubwa kulinganisha na aliyechukua mkopo wa muda mfupi
 
Yaani amekosa ubunifu wa kuitumia hio income ambayo addition na kuipangia income generating item, aukuoffset potential laps in inflation kwa early purchase ya baadhi ya bidhaa. Generally speaking in financial words

Jamaa yeye deni linamkera...hataki kudaiwa.
 
Inawezekana, hata akitaka kulipa deni lote, ili wasiendelee kukata tena.

Namshauri aende tawi lolote la benk husika atapewa mwongozo.
Kama ni CRDB na yuko DSM afike tawi LA Kijitonyama wale loan officers wako vizuri sana.
 
Inawezekana kuongeza marejesho, andika barua peleka kwenye tawi la bank yako.
 
Habarini!
Najua kuna kila aina ya wataalamu humu. Nauliza kuna uwezekano wa kuongeza makato yako benki ikiwa mdaiwa umeamua hivyo? Yaani labda ulikuwa unakatwa 200,000 kwa mwezi, sasa umepanda daraja labda na unataka kilichoongezeka kiende ktk makato yako ili umalize haraka deni (ukatwe 300,000/= sasa). Je, inawezekana? Km inawezekana utaratibu upoje?
Inawezekana kiongozi, nenda benki unayotaka kuongeza makato
 
Back
Top Bottom