Inawezekana lugha inachangia kwa makocha wa kigeni kuwapendelea zaidi wachezaji wa kigeni

Inawezekana lugha inachangia kwa makocha wa kigeni kuwapendelea zaidi wachezaji wa kigeni

Halafu kapteni anapewa mohammed huseni na Dickson job hata kuomba maji kwa kiingereza shida ndio maana team zetu zinaonewa kimataifa.
 
Mara nyingi utasikia watu wanasema "mpira una lugha yake" ila wanachoshindwa kutambua ni kuwa kushindwa kuelewa lugha fulani kunaweza kukupunguzia uwezo wa kuelewa maelekezo kwa haraka na ufasaha na pia kukupunguzia confidence.

Nikiangalia wachezaji wa Simba kama Karabaka, Mashaka, Balua, Chasambi unaona kuwa kutopewa game time ya kutosha na wengine hata kutolewa kwa mkopo kunaweza kuwa kunachangiwa kiasi fulani na kwamba Fadlu Davids na benchi lake wanapata wakati mgumu kuwafundisha na kuzungumza nao ndani na nje ya uwanja.

Watanzania wengi ambao lugha ya kiingereza siyo rafiki sana, wakiwa kwenye mazingira ambayo lugha hiyo ndiyo inatumika zaidi tuna mtindo wa kuwa wanyonge, kujifichaficha na kujitenga tukiogopa "kudhalilika".

Ukifanya hivyo, kocha akasoma "body language" yako kuwa haujiamini, uwezekano wa yeye naye kutokuwa karibu na wewe unaongezeka. Hauwezi hata kupiga naye story mbili tatu mkiwa mnapiga msosi, badala yake muda wote utakaa na washkaji zako mzungumze kimatumbi. Tunashangaa kwa nini Mutale bado anapewa nafasi, hatutambui kwamba lugha inamuwezesha kuchati na mwalimu nje ya uwanja na kujenga ukaribu na ukizingatia ni mtu anayeonekana ni mtu wa matani. Hivi vitu vyote vinachangia katika maisha. Katika maisha, tunashuhudia mara kwa mara watu ambao wanaonekana hawana uwezo wanapewa fursa na wenye uwezo wanaachwa, "social skills" kama hizi zinachangia.

Valentino Mashaka anaweza kuwa msaada sana kwa Simba kipindi hiki ambapo Ateba ameonekana kushuka kiwango kwa kasi. Nawashauri Simba waiombe TFF wamruhusu Mashaka arudi ajiunge na Simba hadi mwishoni mwa msimu kama chaguo la pili baada ya Mukwala.

Edwin Balua angepewa game time ya kutosha angeweza kuwa na ufanisi na mchango sawa au kumzidi hata Ahoua na pia anamzidi mara 100 Ahoua kwenye upigaji wa faulo. Natambua hawa wawili hawachezi nafasi moja ila mapungufu yao ya uchoyo wameonyesha wote wanayo ila Ahoua ameonekana kuvumilika zaidi. Najua Ahoua naye kiingereza hakipandi ila nadhani confidence yake ni kubwa zaidi nje ya uwanja.

Siondoi uwezekano wa upendeleo usiohusiana na suala la lugha ila hilo nalo ni la kuzingatia.

Leo hii watu wanajadili kumuondolea Zimbwe unahodha wake na unakuta sababu kuu ni kushindwa kwake kutimiza majukumu yake ipasavyo kwa sababu ya changamoto ya lugha. Wanasema asilimia kubwa ya mawasiliano ya binadamu ni "body language", hata anapomfuata mwamuzi unaona kabisa hajiamini. Anaenda kinyonge sana.

Wachezaji wa kitanzania, jipigeni msasa, pesa ya kupata walimu wa lugha mnazo, msikae kizembe hadi mnachukuliwa poa. Thamani yenu itaongezeka mara dufu ndani na nje ya nchi mkijiongeza kwenye hili. Ni ushauri tu wa kujenga.

Pia nimewatumia wachezaji hao wa Simba kama mifano, hii inaweza kutumika kwa mchezaji au timu yoyote ile.

Kwann umesema Simba waiombe TFF imruhusu Valentino Mashaka asafiri na Simba,
Amefungiwa au yupo timu za vijana...!??
 
Niliwahi kusema Simba inakalia na haitumii vizuri hazina yake ya wachezaji. Huyu Mashaka alikuwa na mwanzo mzuri sana na inafaa arudishwe kikosini kipindi hiki.

1000075964.jpg
 
Ni ngumu Sana kujifunza lugha mpya ukiwa above 18yrs.. kichwani huwaga Kuna LANGUAGE ACQUIRING DEVICE INAFUNGAGA ukifikisha above 18yrs ndio maana watoto wanajifunza kwa haraka LUGHA MPYA KULIKO MTU MZIMA

Huwezi kua mbobevu kwenye hiyo lugha..
Nilijifunza french nikiwa above 18yrs, but before then nilikuwa na background nzuri ya kingereza. But bado french ilinitesa.

Inahitaji dedication nzito sana, kitu ambacho mtu akifika utu uzima, na majukum muda wa kujifunza anakosa anaona haina haja

It possible but inahitaji dedication nzito sana
 
Nilijifunza french nikiwa above 18yrs, but before then nilikuwa na background nzuri ya kingereza. But bado french ilinitesa.

Inahitaji dedication nzito sana, kitu ambacho mtu akifika utu uzima, na majukum muda wa kujifunza anakosa anaona haina haja

It possible but inahitaji dedication nzito sana
Ni kweli inaitaji dedication kubwa Ila nahisi kiswahili ni rahisi Kuna wa Pakistan Fulani walikuja bongo..English hawajui Ila walipo kaa mwaka wakaanza kuongea KISWAHILI vizuri Sana 😅
 
Back
Top Bottom