Inawezekana makamanda wa Chadema waliohamia CCM ni magarasa na turufu bado zimebaki Ufipa maana bado wanaonyesha Ufundi!

CCM ni chama kikubwa bwashee...... Ni nyumbani kwa wasema ukweli!

Kina ukubwa wa aina gani au kina uzoto wa kilo ngapi !??.Wacha kisumbua Watu hapa ,CCM mmesha poteza Sifa kitambo sana ya kuwa Chama cha Siasa.Mnaua Raia wenu(R.I.P. Akwilina) mna kanyaga Haki za wengine kupitia Taasisi zetu na juzi kati hapa baada ya kulewa Madaraka Katibu wenu akaweka wazi wazi namna mnavyo faidika na Dola yenu.
 
Hivi kila mpinzani anayehamia ccm kanunuliwa?
Sasa kwa akili yako tu ya kawaida, mtu anaanzaje kuacha udiwani/ ubunge wake ambao aliupata kwa jasho na damu, aache mshahara na stahili zake zote za kustaafu?

Vyote hivyo apoteze halafu eti akaunge juhudi? Juhudi zipi?
Ni mjinga tu anaeweza kuaminishwa ujinga unao uamini wewe.

Hata mitume walimuuliza Yesu "Bwana, sisi tumeacha vyote na kukufuata ww, tutapata nini basi?
Jiongeze

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hichi kikundi chao huwa wanakodi watu ili kuleta fujo
 
Hiyo sentensi ya mwisho ndio imenifurahisha!
 
Hapo ndio mjue kuwa kikitokea kikundi cha uasi cha kupambana na CCM huko porini hakiwezi kukosa pesa kutoka kwa raia
 
johnthebaptist ,

..kuwa mpinzani hapa Tz inahitaji kuwa na WITO.

..bila kuwa na wito ni vigumu kuhimili misukosuko ya CCM ikishirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na mahakama.

..aliyejiungia CDM kwa kufuata ubunge akiona nafasi yake iko hatarini lazima atahamia CCM.
 
Hebu fikiria Hamis Mgeja alijiunga Chadema kumfuata Lowassa.

Siasa za bongo ni pasua kichwa!
 
 
Yaani kwa yule mlevi mbwa walibugi sana. Mtu alikuwa anakunywa hadi anajikojolea pale Banana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…