Nafaka
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 12,154
- 31,246
Maswali mengi yameibuka juu ya madai ya serikali ya Haiti kuhusu waliotekelezwa mauaji ya raisi Moise, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi katika hekalu lake liliko Port-au-Prince, Halhamis iliyopita.
Jeshi la polisi na wanasiasa wa Haiti ambao wameingilia ombweila uongozi wa kiasiasa kutokana na kuawa kwa Moise, wote wanadai kuwa alipigwa risasi mnamo saa 7 usiku. Wanadai kwamba mauaji yalitekelezwa na wanajeshi wastaafu wa jeshi la Colombia ambao walikuwa wamelipwa kufanya hivyo. “Raia wa kigeni waliingia nchini na kumuua raisi,“ Mkuu wa Polisi Bwna Charles alinukuliwa akisema.
Hata hivyo, wanasiasa toka vyama vya upinzani na taarifa za vyombo vya habari nchini Haiti na Colombia zinaonyesha uwepo wa mashaka juu ya maelezo haya, huku hali ya kiusalama nchini Haiti ikiwa yenye kutia mashaka hasa katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Siku ya Ijumaa, Steven Benoit, ambaye ni kiongozi wa juu wa chama cha upinzani na senata mstafu, akiongea na kituo kimojawapo cha redio nchini Haiti alisema hivi: “Raisi ameuawa na walinzi wake, wala hakuawa na WaColombia.“
Taarifa kutoka kwenye gazeti moja la Colombia lijulikanalo kama Semana, likinukuu chanzo cha siri, zinadai kwamba wanajeshi wastaafu wa Colombia walisafiri kuelekea Haiti baada ya kuwa wameajiriwa kama walinzi wa Moise, ambaye alikuwa akipokea vitisho vya mauaji mara kwa mara, hivyo wao walikwua wameenda kumlinda wala siyo kumuua.
Pia gazeti la Colombia lijulikanalo kama El Tempo linadai kwamba chanzo kimoja kimeliambia kwamba, video moja iliyonaswa na kamera za ulinzi katika nyumba aliyouawa raisi zinaonyesha wanajeshi wa Colombia waliwasili eneo hilo majira ya saa nane na nusu mpaka saa nane na dakika arobaini usiku wa Jumatano. “Hii ina maana kwamba, waliwasili eneo hilo nusu saa baada ya mauaji hayo kutokea,“ chanzo hicho kimenukuliwa kikisema.
Mapema siku ya Ijumaa, vyombo vya ulinzi vya Colombia vilitaja majina ya washukiwa 13 ambao Haiti inawashikilia kwa kudai kuwa walihusika kwenye mauaji hayo. Majina haya yanajumuisha Manuel Antonio Grosso Gaurin, ambaye ni mmojawapo kati ya wanajeshi wa staafu wa kikosi maalum katika jeshi la Colombia cha kupambana na ugaidi na wauza dawa za kulevya, ambacho pia kinahusika na kuokoa mateka na kulinda VIPs.
Grosso mwenye umri wa miaka 41, inadaiwa aliwasili nchini Haiti akiwa ameambatana na wanajeshi wastaafu 10 , tarehe Jumi baada ya kuwa wamesafiri kupitia mji wa Punta Cana, nchini Dominican, ambayo inamiliki kisiwa cha Hispaniola kwa kushirikiana na Haiti. Kundi la pili la wanajeshi wastaafu waliwasili Haiti mwezi mmoja kabla kwa kupitia Panama.
Mkuu wa polisi wa Haiti aliwaambia waandishi wa habari kuwa, raia wa Colombia 15 wamekamatwa baada ya kuawa kwa raisi, pia watu wawili wenye uraia wa Haiti na Marekani nao wanashikiliwa, ambao majina yao ni James Solages mwenye umri wa miaka 35, na Old Joseph Vicent mwenye umri wa miaka 55. Raia wa Colombia wapatao watatu waliuawa, wakati washukiwa wapatao nane bado wanatafutwa. “Tunaomba wananchi wasichukue sheria mkononi .“
Mke wa mmoja wa watuhumiwa anadai kwamba mume wake aliajiriwa kwenda nchini Dominica ili kutoa ulinzi kwa familia moha ya kitajiri, lakini hakupewa taarifa zaidi ya misheni.
Seneta mmoja nchini haiti kutoka chama pinzani, anauliza kama kweli ni WaColombia waliotekeleza mauaji hayo, kwanini hawakukimbia bado walirudi na kuendelea kukaa kwenye nyumba waliokuwa wanaishi? Na swali lingine ni kwanini hakuna mlinzi yoyote wa raisi aliyejeruhiwa wala hata mbwa wa eneo lile hawakuuawa.
Paul Raymond ambaye ni mwalimu katika mji mkuu wa Haiti anadai kwamba bila shaka wauaji walikuwa wanajua vizuri nyumba ya raisi na si wengine watakwua ni walinzi wake bila shaka waliotekeleza mauaji hayo.
Alfred Antoine mmoja wa wanachama wa barazala Congress anadai kwamba mauaji hayo yatakwua yalitekelezea na watu wenye ushawishi mkubwa katika serikali. Anadai walimuua ili kulinda maslahi yao. People have many good things to say about you, but you will have to die first.