Uchaguzi 2020 Inawezekana vipi gari zote hizi tena aina tofauti ziwe na namba hii ya T 2020 JPM?

Uchaguzi 2020 Inawezekana vipi gari zote hizi tena aina tofauti ziwe na namba hii ya T 2020 JPM?

Uzi kama huu bila picha Ni uchonganishi tu unatafuta
2EAE6E8C-85BC-4609-9D27-209A8A79D8A1.jpeg
0924B9F2-F3C1-42BD-A770-3305898354E0.jpeg
88B7BC97-B29F-4596-9B7D-1C71E8A83AC3.jpeg
2C42A3AA-F4FC-465D-A149-C3C791902C2E.jpeg
62B4FEA8-09A5-40BB-B320-488DDD15F883.jpeg
9A2BD5C2-AB7C-47A7-B3CD-99E05FD68D33.jpeg
 
Hiki kitoyota Wallah hata Magu mwenyewe hafurahii kuona kimewekewa jina lake na nakwambia Traffic watakukamata tu ukizingua road maana inaonekana dhahiri wewe kwny msafara wa Mamba ni kenge tu.

Kuna vyombo kama Discovery 4/5,Ma Range rover,Ma V8(Lc 200),Patrol Y62 nimeziona zina hio No. Plates Ya Magu na ukweli hata road hawatakamatwa maana gari yenyewe tu inajieleza.

Sasa unakuja na ka brevis sijui mark x No. plate Inasoma T2020JPM utapata tabu sana braza.
 
Nimekuwa nikiona magari mengi tofauti yana namba za usajili T2020 JPM, nauliza je hii ni namba halali kwa magari haya?

Nimeona magari zaidi ya 10 yana namba hii. Inawezekana vipi gari zote hizi tena aina tofauti ziwe na namba hii?

Mfano limesababisha ajali nikienda polisi nikiwatajia namba hii watajua ni ipi kati ya hizo nyingi zinazotumia namba hii?

Cc: Mkuu wa usalama barabarani.

Na yale mav8 ya kijani yaliyopo kwenye kampeni za urais ,yote hayapo kwenye registration za CCM.
 
Kuna vigari naviona vimewekwa hio T2020 JPM kama Altezza,Allion,Opa etc halafu nakua siamini amini hivi kweli hawa wamesajili hizi No. Plates huko TRA au wanatania?

Hizo No. plates Kuzisajili TRA unalipa Tsh. 10,000,000(yaani mil. 10) kila baada ya miaka 3,sasa No. plates zinalingana thamani na magari yenyewe husika.

So nafanya conclusion kwamba kuna magari hapa mjini yamechonga tu hizo No. plates na wala huko TRA hawako kwny records zao.
 
Naunga mkono hoja nimeona magari yenye namba hizo pia. Yana rangi za kijani mengine land cruiser hard top, v8, vx nk.

Nilijiuliza sana kama yana usajili halali TRA na kama hizo namba zinalipiwa.

Labda ya ni yale yale ya bwana manoti aliyepania kupata promotion kwa mgongo wa CDM.
 
Kila siku tunapiga kelele kuhusu Serikali hii na CCM yake wanafanya mambo ya kipuuzi yaliyo kinyume cha Sheria lakini hakuna hatua inayochukuliwa. Imagine hayo magari yangekuwa yameandikwa Lissu au Rungwe unadhani yangeruhusiwa kupita Barabarani?
Andikeni tuone kama hayataruhusiwa
 
Hiki kitoyota Wallah hata Magu mwenyewe hafurahii kuona kimewekewa jina lake na nakwambia Traffic watakukamata tu ukizingua road maana inaonekana dhahiri wewe kwny msafara wa Mamba ni kenge tu...
Acha ubaguzi mkuu, kumbe inabidi uwe na gari na si usafiri?
 
Kuna vigari naviona vimewekwa hio T2020 JPM kama Altezza,Allion,Opa etc halafu nakua siamini amini hivi kweli hawa wamesajili hizi No. Plates huko TRA au wanatania?...
Hata mimi nafikiria hivi. Ila hatari yake ikoje iwapo gari lenye namba hii likipiga tukio?
 
Back
Top Bottom