Mkunazi Njiwa
JF-Expert Member
- Apr 22, 2023
- 8,538
- 7,559
Hapana mkuu ni kukaa kwangu vijiwe vya kahawa hapo vingunguti relini....Saigon k'koo ,pale kwa Mtogole Tandale ,Mbagala R3 karibu na Kisuma ,Majohe Rada kwa Basanza ,Gongo la Mboto Stendi ,Mwananyamala Kisiwani ,kijiwe cha kahawa cha CUF hapo kona kuelekea Masjid Idrissa karibu na Msimbazi Police post ,pale mkabala na makao makuu ya Simba ,Buguruni mkabala na maghorofani kuelekea sokoni ,kijiwe cha kahawa jirani na Buguruni sokoni magari ya kuelekea Muhimbili,Mwenge jirani na kituo cha zamani ,pale Stendi ya Makumbusho karibu na choo Kama unaelekea barabara ya sokoni na kwa dada yetu Shishi baby...Ila ulivyo waelezea ni kama unajielezea ww mwenywe [emoji849][emoji849][emoji849]
Mkuu sisi vijana wanywa kahawa kichangamshi ,Kahawa dawa ,Al Kasus mujarab huwa tunayasikia mengi kuhusu hao jamaa sijajua vijiwe hivyo vina nguvu gani juu ya taifa letu pendwa...wazee huwa wanawaongelea sana kifupi hao jamaa wanaelezewa kuwa ni makatili lakini ni kinyume chake...hao jamaa wana huruma sana ni wazalendo na hawajitangulizi nafsi zao bali watanzania wenzao kwanza ,taifa letu lenye amani kwanza kifupi hawafanani na baadhi ya Polisi wenye kutuonea sisi raia....ukimuona mtu yeyote anasema anawajua ama anajifanya yeye ni mfanyakazi miongoni mwao ujue ni muongo na anakudanganya....ukiwaona wale wanaotutisha raia kwa "vijibastola" ujue ni wakora ama labda ni baadhi ya polisi kanzu tu....
Allah /Yehova /Yahweh aendelee kulilinda taifa letu tuzidi kuwa na amani ,upendo ,utulivu ,mshikamano na atuondolee mifisadi yote inayotukosesha huduma bora za kijamii mathalani vituo vya afya ,maji safi na barabara aaaaaamin aaaaaamin [emoji120]
Tanzania ni "eden" ya dunia...hatutaki kuyaona ya SUDAN ,DARFUR ,CONGO ,MSUMBIJI ,URUSI,UKRAINE wala yale ya Kibiti,kuua watalii kule Zanzibar na ya Mapango ya Amboni Tanga ,aaamin aaaamin[emoji120]
Mola akubariki wewe ,mimi mnywa kahawa na kila mwenye kuipenda kiukweli hii bustani ya Edeni iitwayo Tanzania ,aaamin aaaamin[emoji120]
Peace and love
#Yetzerhatov
#DoNotDoHarm[emoji120]