Inawezekanaje mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa kujihusisha na ufisadi?

Inawezekanaje mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa kujihusisha na ufisadi?

Ndugu wana JF sina mengi na sitaki niwachoshe ila kuna Jambo moja naomba nipate ufafanuzi kutoka kwenu wajuvi wa idara hii ya usalama wa Taifa.

Tangu nikiwa mdogo nimekuwa nikisikia sikia uwepo wa idara hii na Kwa ufahamu mdogo niliona ni kwamba ili mtu awe recruited na kuwa mtumishi wa idara hii anatakiwa kuwa na uzalendo wa hali ya juu wa kuipenda nchi katika hali zote.

Kadhalika mtumishi katika idara hii anapaswa kuwa si muumini wa vitendo vya rushwa, muhujumu uchumi, ufisadi n.k

Lakini ajabu ni kwamba kumekuwepo na hali ya baadhi ya waliowahi kuwa viongozi waandamizi wa idara hii kuhusishwa na vitendo vya ufisadi na kujilimbikizia Mali.

Nachotaka kufahamu Je, ni kweli kwamba hata watumishi wa idara hii hawana uzalendo kiasi cha kujihusisha na vitendo vya ufisadi na kujilimbikizia mali? na ni kipi hupelekea mtu wa aina hii kuwa recruited katika idara hii nyeti ya nchi?
Ni binadamu ana matamanio kama binadamu mwingine!
 
Kama rais tu anaweza kuwa fisadi inashindikana nini kwa mtumishi wa idara ya usalama alieko chini ya mteule wa rais?

Ufisadi ni tabia ya CCM hivyo ukisikia yoyote anaejihusisha na CCM ni fisadi ujue ni sawa na simba kumtafuna swala porini. Ni sehemu ya maisha yao.
ACHA KELELE WEW CCM KUKUJENGEA BARA BARA , HOSPITAL ,SGR, BOMBA LA MAFUTA, MADARASA , ELIMU KIMARIKA MAJI UMEME, NK NDIO UFISADI
 
ACHA KELELE WEW CCM KUKUJENGEA BARA BARA , HOSPITAL ,SGR, BOMBA LA MAFUTA, MADARASA , ELIMU KIMARIKA MAJI UMEME, NK NDIO UFISADI
CCM haijawahi kufanya hayo mambo mbuzi wewe. Kodi za wananchi ndio zinafanya hizo kazi nyambaff
 
Huo usalama wengi ni watu wao.

Yule mwendazake alikuwa na mwanaye anazunguka na mfuko wa hela utakuta naye ni wa kitengo.

Mtaani pia wapo wahuni wanaojiita usalama na ndo hao mafisadi
 
Mtoa mada una viashiria vyote vya kuwa kada wa Chama Cha Masela au chawa mwandamizi wa Bi'mkubwa.
#Enewei wasalimie mitaa ya Lumumba.
 
ACHA KELELE WEW CCM KUKUJENGEA BARA BARA , HOSPITAL ,SGR, BOMBA LA MAFUTA, MADARASA , ELIMU KIMARIKA MAJI UMEME, NK NDIO UFISADI
Unachukua posho shingapi mkuu?😂
#Just joking
 
Nimepata habari huku vijiwe vya kahawa na wazee waliowahi kuwafahamu hao jamaa....huwa ni wazalendo haswa....hao jamaa hawashiriki rushwa kabisa kabisaaa..hao jamaa wana moyo wa kulipenda sana taifa lao yaani kwa kifupi hao jamaa ninasikia huwa wana sifa za ziada za utii....wanalipenda sana taifa lao...wale wanaojulikana mitaani wakatajwa kuwa ni wakosefu wa adabu ,heshima na utii kwa nchi hao sio hao jamaa....hao ni ama WANAJIFANYA tu ama wanatumwatumwa sasa kwa sababu watu wamezoea kila mwenye kuvaa kaunda na kinembo kifuani ni hao jamaa hapana hao sio.... Mwenyezi Mungu awabariki popote huko waliko hao jamaa...Mwenyezi Mungu azidi kuwapa afya njema ,uhai mrefu ,awaondolee husda ,mitihani ,ajali na madhila ya binadamu aaamin aaamin[emoji120]

Mwenyezi Mungu azidi kulilinda taifa letu dhidi ya MACHAFUKO ,UFISADI ,ULAFI ,VITA NA UGAIDI aaamin aaamin[emoji120]

Aisee hao ni wazamani hawa wasasa ni wapigaj sana ebu angalia uko SGR wapo kibao lkn madudu na upigaj kama kawa
 
Aisee hao ni wazamani hawa wasasa ni wapigaj sana ebu angalia uko SGR wapo kibao lkn madudu na upigaj kama kawa
Achilia mbali mradi wa SGR nenda hata pale bandarini wamejazana kibao lakini ndiko kunaongoza Kwa upigaji wa kutisha na hapa ndipo napata walakini kuhusu hii idara yetu
 
Na weee ukipata upenyo pigaa

Usione huruma

Ova
 
Nafasi watu wanapeana peana unategemea nini..
Nchi imeoza kila mahali hii, kila mtu mwizi, kila mtu anakula kwa urefu wa kamba yake.
 
Nimepata habari huku vijiwe vya kahawa na wazee waliowahi kuwafahamu hao jamaa....huwa ni wazalendo haswa....hao jamaa hawashiriki rushwa kabisa kabisaaa..hao jamaa wana moyo wa kulipenda sana taifa lao yaani kwa kifupi hao jamaa ninasikia huwa wana sifa za ziada za utii....wanalipenda sana taifa lao...wale wanaojulikana mitaani wakatajwa kuwa ni wakosefu wa adabu ,heshima na utii kwa nchi hao sio hao jamaa....hao ni ama WANAJIFANYA tu ama wanatumwatumwa sasa kwa sababu watu wamezoea kila mwenye kuvaa kaunda na kinembo kifuani ni hao jamaa hapana hao sio.... Mwenyezi Mungu awabariki popote huko waliko hao jamaa...Mwenyezi Mungu azidi kuwapa afya njema ,uhai mrefu ,awaondolee husda ,mitihani ,ajali na madhila ya binadamu aaamin aaamin[emoji120]

Mwenyezi Mungu azidi kulilinda taifa letu dhidi ya MACHAFUKO ,UFISADI ,ULAFI ,VITA NA UGAIDI aaamin aaamin[emoji120]
 
Attachments

  • 5117362-148efa178040dfcd6b51b581965e1bf3.mp4
    25.4 MB
Mkuu pole sana kama unaamini katika usalama wa taifa,wale watu wanapokea rushwa tena live,nina mifano mingi sana,japo na mimi ni mnufaika wa utoaji rushwa hiyo
 
Back
Top Bottom