Inawezekanaje mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa kujihusisha na ufisadi?

Ila ulivyo waelezea ni kama unajielezea ww mwenywe [emoji849][emoji849][emoji849]
Hapana mkuu ni kukaa kwangu vijiwe vya kahawa hapo vingunguti relini....Saigon k'koo ,pale kwa Mtogole Tandale ,Mbagala R3 karibu na Kisuma ,Majohe Rada kwa Basanza ,Gongo la Mboto Stendi ,Mwananyamala Kisiwani ,kijiwe cha kahawa cha CUF hapo kona kuelekea Masjid Idrissa karibu na Msimbazi Police post ,pale mkabala na makao makuu ya Simba ,Buguruni mkabala na maghorofani kuelekea sokoni ,kijiwe cha kahawa jirani na Buguruni sokoni magari ya kuelekea Muhimbili,Mwenge jirani na kituo cha zamani ,pale Stendi ya Makumbusho karibu na choo Kama unaelekea barabara ya sokoni na kwa dada yetu Shishi baby...

Mkuu sisi vijana wanywa kahawa kichangamshi ,Kahawa dawa ,Al Kasus mujarab huwa tunayasikia mengi kuhusu hao jamaa sijajua vijiwe hivyo vina nguvu gani juu ya taifa letu pendwa...wazee huwa wanawaongelea sana kifupi hao jamaa wanaelezewa kuwa ni makatili lakini ni kinyume chake...hao jamaa wana huruma sana ni wazalendo na hawajitangulizi nafsi zao bali watanzania wenzao kwanza ,taifa letu lenye amani kwanza kifupi hawafanani na baadhi ya Polisi wenye kutuonea sisi raia....ukimuona mtu yeyote anasema anawajua ama anajifanya yeye ni mfanyakazi miongoni mwao ujue ni muongo na anakudanganya....ukiwaona wale wanaotutisha raia kwa "vijibastola" ujue ni wakora ama labda ni baadhi ya polisi kanzu tu....

Allah /Yehova /Yahweh aendelee kulilinda taifa letu tuzidi kuwa na amani ,upendo ,utulivu ,mshikamano na atuondolee mifisadi yote inayotukosesha huduma bora za kijamii mathalani vituo vya afya ,maji safi na barabara aaaaaamin aaaaaamin [emoji120]

Tanzania ni "eden" ya dunia...hatutaki kuyaona ya SUDAN ,DARFUR ,CONGO ,MSUMBIJI ,URUSI,UKRAINE wala yale ya Kibiti,kuua watalii kule Zanzibar na ya Mapango ya Amboni Tanga ,aaamin aaaamin[emoji120]

Mola akubariki wewe ,mimi mnywa kahawa na kila mwenye kuipenda kiukweli hii bustani ya Edeni iitwayo Tanzania ,aaamin aaaamin[emoji120]

Peace and love

#Yetzerhatov
#DoNotDoHarm[emoji120]
 
Wamekula rushwa yako wewe mkuu ?!!!

Mkuu nawe unatupoteza.....mkuu unatudanganya....muogope Mungu.....
 
Duuuh....na kama rais hawezi kuwa fisadi basi ujue hata hao hawawezi kuwa mafisadi.....
 
Wewe tafiti kwanza juu ya aliyewahi kuwa mkuu wa Idara, aliitwa General Kombe, na sababu za kuwa taken out.
Idara ni taasisi ya serikali kama taasidi nyingine, ni kwa vile madudu yake hayadajiliwi hadharani.
Sababu zipi? Unajuaje kama unazijua au huzijui? Huwezi jua wewe ya vichwani mwa watu, mtu yuko barzaq bado mwamuandama
 
Asante kwa kutufurahisha mchana huu.

Hao jamaa wa kitengo, wenyewe wakiisoma komenti yako, nao kwa mshangao mkubwa wanajiuliza: hivi huyu jamaa anawazungumzia jamaa gani hao?
Mkuu umemaliza kumuombea dua mbaya kipenzi hayati BCM ?!![emoji1787][emoji1787]

Toka juzi usiku unahanikiza tu laana juu yake [emoji1787] daaah

Mkuu una "negativity" sana....kwako wewe hakuna kabisa watumishi wa wananchi walio wasafi wa kimaadili....

Pole mkuu
 
Wamekula rushwa yako wewe mkuu ?!!!

Mkuu nawe unatupoteza.....mkuu unatudanganya....muogope Mungu.....
naongea hivi kwasababu naijua hiyo system vizuri kuliko wewe, yule usiyemdhania ndiye huwa ndiye, na yule ambaye ni ndiye huwa anafanya afanyalo ili kupotez amaboya msimshitukie wala kumjua. achana na hao tiss, rudi polisi tu, unafikiri kwanini polisi tukio likifanyika hapa huwa wanajua muda huohuo wakiamua kufuatilia? ni kwamba wanao informers wao kule kule kwenye matukio. na hawa tiss kwa taarifa yako ndio wanakula rushwa kuliko hata polisi huko huko kwenye utendaji wao, though wana namna zao za kuadhibiana.
 
Vipi huyu mheshimiwa aliyetutoka mbona anatajwa tajwa kwenye kashifa za ufisadi na alikuwa kachero mwandamizi?
Mimi nimesikia tu huku vijiweni kuwa hayati Membe ameshawahi kufanya kazi huko kwa weledi mkubwa sana .....

Ila mzee mmoja wa Rondo alipata kunisimulia kijiweni kuwa huyo bwana alikuwa mtiifu na asiyependa ukwasi kabisa....ila alipoanza harakati za kuutafuta urais kama wanasiasa wote duniani alianza kutuhumiwa kuwa ana marafiki matajiri wakubwa nchini.....binafsi sishangai kwani masuala ya KAMPENI za kisiasa from the grass root yanahitaji network na fedha.....eti tukiwaona "aspirants" wote wa nafasi za kisiasa ni MAFISADI basi ni bora tufute kabisa SIASA nchini kwetu [emoji1787][emoji1787][emoji1787]jambo ambalo haliwezekani ni kichekesho na uwendawazimu.....

Mkuu nijuavyo mimi ni kuwa UFISADI hauwezi ukafutwa na kuwa ZERO....duniani kote....bali serikali za kizalendo jukumu lake ni kupambana nao na kuupunguza..... mathalani juzi mh.Rais Chifu Hangaya kupitia kwa mkuu wa TAKUKURU wanajadiliana na wizara ya elimu kuanzisha MTAALA WA "KUKURU" kufundisha watoto wetu......

#SiempreJMT[emoji120]
 
Taifa gani labda? Yani mtu fulani kuwa TISS bas imekuwa matangazo kila sehemu!
 
Nilidhani unajua kusoma, mkuu. Wapi mahali nimemtaja BM? Halafu wapi nimetamka laana kwake (naomba nukuu hiyo, tafadhali).
 
Aaamin aaamin mkuu wangu [emoji120]

Nipe elimu mkuu wangu....kipi kimepelekea baadhi ya hao "intake ya 2010" usemayo kuwa hivyo walivyo?
 
Kuna $20,000,000 zilipelekwa huko lindi kwaajili ya kujenga kiwanda cha Cement, alafu zikapotea sijui ndio wanaita ziliyeyuka kama barafu....🤣
R.i.P Classmate....😥
Tupe ushahidi wa hizo hela
 
System ikiwa corrupt hamna wa kumyooshea kidole mwenzie.
Mafisadi wako ndani ya system wakishirikiana na watu walioko nje ya system.
Mara ngapi CAG anaweka wazi watu waliofisadi fedha ya umma? Ni hatua zipi zimewahi kuchukuliwa?
Hapo ndo utaelewa wahusika ni ndugu moja na system.
 
Tanzania iliishia kwa mkapa baada yapo ikawa kila mtu anaiba, magufuli alipotaka kuirudisha nchi kwenye mstari mafisadi yakaanza kupiga kelele
Mkapa ndiye mwasisi wa wizi na ufisadi nchi hii umezaliwa lini dogo?
 
Wizi ni Tabia ambayo MTU wa kazi yoyote anaweza kuwa nayo.
Kama wachungaji na masheikhe tuu kuna majizi sembuse Usalama wa taifa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…