Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
 
Ukiwaweka hawa viongozi wa Tanzania Denmark au Korea na Viongozi wa Korea / Denmark kila kitu kitakuwa vice versa.

Uzuri wa wananchi wa nchi hizo hawatachukua muda mrefu viongozi wabovu wataondolewa madarakani na kuishia jela.

Kwa wenzetu kuna uwajibikaji, seriousness, wako serious na maisha.
 
Ukiwaweka hawa viongozi wa Tanzania Denmark au Korea na Viongozi wa Korea / Denmark kila kitu kutakuwa vice versa.

Uzuri wa wananchi wa nchi hizo hawatachukua muda mrefu viongozi wabovu wataondolewa madarakani na kuishia jela.

Kwa wenzetu kuna uwajibikaji, seriousness, wako serious na maisha.
Ndiyo, wana uwajibikaji hasa. Wanaelewa maana ya uongozi ni dhamana.
 
Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
Linganisha lifestyle ya wanene wa huko na huku kuanzia majumba mpaka magari yao utapata majibu yote unayoyataka !!
 
Tatizo letu ni misingi mibovu iliwekwa toka tulipopata uhuru.
 
Siyo Denmark pekee. Vinchi vyote vidogo huko Ulaya, na baadhi huko Asia, ukilinganisha na Tanzania ni aibu tupu:

Denmark
Norway
Finland
Sweden
Singapore
Switzerland

Utajiri mkubwa hapa Ulimwenguni ni akili, wala siyo idadi kubwa ya fisi na pundamilia, siyo dhahabu na gas, ardhi nzuri ya kilimo, maziwa, bahari au hali nzuri ya hewa.

Hata upewe vyote, ukinyimwa akili, vyote vinakuwa havina maana. Lakini ukibahatika ukapata akili,ni mwanzo wa mafanikio yote. Kwanza utajua ni nini kilicho muhimu, utakuwa na mifumo mizuri ya kuvuna rasilimali, utakuwa na tekinolojia, utakuwa na mifumo mizuri ya utawala, na mifumo mizuri ya kusimamia uchumi kwa ujumla.

Sisi tuna vitu vingi, lakini asilimia kubwa sana ya watu wetu wamenyimwa akili, utashi na maarifa. Ndiyo maana wachache wenye akili, maarifa na utashi, ama wanakuwa frustrated na kukata tamaa au kuishia kwenda kufanya kazi mataifa ya nje kwa sababu nchini mwao ni giza nene.
 
Back
Top Bottom