Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Umemaliza kila kitu, nidhamu yao ya matumizi ipo juu sn Waziri wa Denmark anatumia public transport huku WEO anataka afuatwe na V8 kila siku, tuna viongozi wabovu na wezi wakubwa
 
Sahihi kabisa tena sn
 
Hizo ni fikra tu. Hatuna uhakika kama mambo yatabakia vile vile au yatabadilika, kwa sababu hatujawahi kubadili uongozi na mifumo yake hata mara moja. Ila tu tumejazwa na imani kuwa hali itakuwa vile vile.
Point hapo ni kwamba kwa kuwa bado hatujabadili kisawasawa hatuwezi kuwa na uhalali wa kusema wote ni wale wale tu !!
 
Kilo moja ya dhahabu na kilo mia za ugoro kipi kina thamani kubwa?
 
Inaweza kulisha Africa nzima
Hako kanchi kadoogo, ambao unaweza kuingia mkoa wa Tabora mara mbili kanaweza kufanya jambo kubwa kiasi hicho?

Tabora ina kilomita za mraba 76,151, lakini sina uhakika kama imejitosheleza kwa chakula, sembuse kuilisha Tanzania.

Na Denmark ina kilomita za mraba 42,943, lakini mambo yake si ya kitoto.

Ama kweli, ukubwa wa pua si wingi wa kamasi.
 
Kosa mali lakini usikose akili, viongozi aina ya Makamba, Bashe, Ummy, Masauni, Mbarawa, Mwigulu, Nape sijui Aweso ndiyo utegemee watupeleke kwenye matokeo chanya? lazima tuamke
 
Kilo moja ya dhahabu na kilo mia za ugoro kipi kina thamani kubwa?
Sijui mkuu, lakini nakuahidi, ukikubali kuniachia hiyo kilo Moja ya dhahabu halafu wewe ubaki na kilo mia za ugoro, nikitoka tu kuiuza dhahabu, nakupa Asante ya IST mpyaa, zero kilometre.
 
Umemaliza kila kitu, nidhamu yao ya matumizi ipo juu sn Waziri wa Denmark anatumia public transport huku WEO anataka afuatwe na V8 kila siku, tuna viongozi wabovu na wezi wakubwa
Mkuu, waheshimu viongozi. Unataka viongozi wa nchi kuubwa, kama Tanganyika wawaige Mawaziri wa nchi ndoogo, Denmark, watumie usafiri wa umma?

Denmark ni kanchi kadoogo sana, hawana uwezo wa kuwanunulia viongozi wao mav8, ila wanaweza kutupa misaada

Tanzania ni nchi kuubwa, hivyo ni halali kila kiongozi kutumia V8.
 
Ni jambo linaloniuma sana mkuu.
Mungu katuweka kwenye bara zuri lenye kila aina ya utajiri ila akatunyima akili na maarifa ya kuufaidi huo utajiri.

Mim nataman wakoloni wangeendelea kuwepo.
Heee!
 
Singapore ni mdogo wetu🤣.
Ana miaka 58 toka apate uhuru wake ila unamuonaje?
Sisi hata tupewe miaka 1000 kwa akili zetu tutakua hivi hivi
Singapore!!! Mhhh! Singapore!

Unaonaje, ukiondoa nafasi ya Rais pekee, tukilikodi baraza la Mawaziri alau kwa kipindi cha miaka mitano tu?
 
Kwa ujinga huu tuache kulalamika sasa acha wafanye matanuzi
 
Nilitegemea jibu kama Hilo Kutoka kwako (lawama Kwa Nyerere).

Tambua: Uimara wa nchi unategemea sana uimara wa wananchi, hapo nazungumzia uimara wa akili.
Kama taifa linakuwa na wananchi wasiojielewa/Vilaza, pia taifa Hilo litazalisha viongozi wasiojielewa/Vilaza, na kinyume chake ni sahihi. Wananchi ndiyo msingi wa Kila kitu.
Nachoona kwako ni wewe kuwa obsessed na personality ya kiongozi mkubwa wa kitaifa kama ndiyo Chachu pekee ya maendeleo Kwa taifa, na ndiyo mtazamo wako ambao agharabu umejikita zaidi kidini. Kwamba kiongozi flani akiwa wa mlengo flani wa kidini huyo ndiye anayefaa, na pia akiwa wa mlengo flani wa kidini huyo hafai, nakataa asilani.
Wananchi ndiyo wazalishaji wa Kila kitu katika nchi, ikiwemo pia na viongozi hodari wanaokuwa na tija Kwa nchi.
 
Ilikuaje wakawa developed na sisi undeveloped?
Sasa apo kuna mabo mengi sana ambayo yametutofautisha mpaka wao wameweza kuwa developed country, hizi zote zinaweza kuwa na sababu nyingi kama internal forec and external force yaan factors ambazo zimechangia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…