Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Sidhani ni tangu tulipopata uhuru, sema tangu tulipozaliwa.

Maana kama ni misingi mibaya baada ya uhuru, mpaka leo ni miaka mingapi? Hiyo misingi mibaya kwa nini haibadilishwi? Mbona mataifa mengine yaliyopata uhuru baadaye, kama Botswana na Namibia, wao angalao wanapiga hatua kwa kasi?
Gari halijiamulii mwelekeo na Kasi ya kukimbia. Ukiona gari linaenda kwa mwendokasi wowote Ule, ujue halijajiamulia. Sifa na lawama hazipaswi kuelekezwa kwa gari wala abiria.

Tanzania ni kama gari, wananchi ni abiria.

Nani alaumiwe au kupongezwa kwa sababu ya mwendokasi wa Tanzania?
 
Umemaliza kila kitu hapa
Utajiri na rasilimali muhimu ni watu watu wenye akili ya kuchanganua mambo na kutatua changamoto zinazowazunguka
Mafanikio ya mtu yanaamuliwa na kiwango cha uwezo wake wa kuyatawala mazingira yake.
 
Hakukuwa na makosa yoyote maana nchi haikuwa tayari kuingia kwenye Ubepari
Kusema haikuwa tayari kuingia kwenye ubeparie, ni sawa na kusema haikuwa tayari kujitawala.

Kwani kabla ya hapo ilikuwa inatawaliwa na nani kama siyo Mbepari?

Ubepari usingekuwa mpya kwa Tanganyika, Ujamaa ndiyo uliyokuwa ngeni. Pengine, ndiyo maana sera ya ujamaa ilifeli pakubwa, ilikuwa ngeni Tanganyika.
 
Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?

Ukubwa wa bure tu
 
1. Denmark ina uchumi mkubwa na ulojitosheleza na ni ule uitwao Mixed Economy.

2. Denmark wana kiwango kikubwa cha wasomi yaani wananchi wengi wana shahada MUHIMU za chuo kikuu.

3. Denmark ni moja ya nchi zinoongoza kwa sayansi na teknolojia duniani.

4. mfumo wa kodi wa Denmark ni mgumu sana, uko juu na wabana kila senti uipatayo VAT pekee ni asilimia 25. Kodi kwa mashirika yaani corporate ni asilimia 22 na wageni wote wa kitaalam hutakiwa kujiandikisha ili waweze kulipa kodi.

5. Denmark wana kiwango cha juu cha maisha kwa wananchi wake.

Hayo ni baadhi tu ila kikubwa ni kwamba Denmark kama zilivyo nchi zingine za Ulaya watumia akili zao kwa manufaa ya nchi zao.

Na mfano wake ni pale ambapo wazitenga kabisa fedha zao za misaada kwa mataifa yenye kuongozwa na viongozi ambao akili wameweka mifukoni.

Afrika mtu akiwa na nafasi au madaraka akili zetu huamua kuziweka mfukoni na kuiba fedha za kodi na kuwanyonya wananchi wenzake.

Akitokea mwafrika mwenye kutaka kutumia akili kuleta manufaa kwa nchi yake wale waafrika wenzie waloweka akili zao mifukoni, kuamua kuzihamisha kwa muda akili zao na kufanya mambo ya kihuni na kikatili.
Tufanyeje ili na sisi tuwe kama wao?
 
Ukiwaweka hawa viongozi wa Tanzania Denmark au Korea na Viongozi wa Korea / Denmark kila kitu kitakuwa vice versa.

Uzuri wa wananchi wa nchi hizo hawatachukua muda mrefu viongozi wabovu wataondolewa madarakani na kuishia jela.

Kwa wenzetu kuna uwajibikaji, seriousness, wako serious na maisha.
Huku ukimfungulia tu mashtaka kiongozi mkubwa ambaye amekula rushwa kubwa kubwa kama makamba ,ridhiwani mwigulu ,nape utaambiwa unafanya siasa za visasi
 
Ni kweli. Nini kifanyike kubadili huo mwelekeo?
Sidhani kama hiyo Hali itawahi kubadilika kwa sababu hii tabia watoto Wana rithi kutoka kwa wazazi na wanakua wanajifunza kutoka kwa jamii inayo wazunguka, akiwa mtu mzima na yeye anarithisha wanae, ni circle ambayo Iko hivyo tuu, kwa kifupi tutabaki kua hivi hadi mwisho, haijalishi katiba itashuka kutoka mawinguni
 
Wao mipango Yao ya maendeleo inagusa wananchi sisi ni kwa ajili ya kuwafungashia viongozi.
Sijui ikulu mpya,sijui Dodoma,sijui Chato,Mara ma v8 Mara posho nk hivi havina manufaa na mwananchi.
 
Waafrika tulifanya kosa kubwa sana kudai Uhuru hauna msaada kwetu
 
Waafrika tulifanya kosa kubwa sana kudai Uhuru hauna msaada kwetu
Tulipewa uhuru tukiwa bado hatuko tayali kua huru, yani watu walitaka kua huru tuu basi sio zaidi ya hapo, ilibidi mkoloni angeendelea kutawala hadi mwaka 2000 angalau ange tuachia nchi iliyopiga hatua kubwa sana kimaendeleo
 
Wao mipango Yao ya maendeleo inagusa wananchi sisi ni kwa ajili ya kuwafungashia viongozi.
Sijui ikulu mpya,sijui Dodoma,sijui Chato,Mara ma v8 Mara posho nk hivi havina manufaa na mwananchi.
Hayo yote, na hata zaidi ya hayo, ni mazuri, lakini Tanzania haijafikia kipindi cha kufanya hayo. Tungeyafanya hayo "baadaye", tutakapokuwa tumeshatajirika!
 
Tafadhali mkuu, usimfananishe mtu mweusi na nyani, tafadhali!

Ni kweli ujinga bado upo, lakini unaweza kutokomezwa ikiadhimiwa.
Sawa mkuu sitamfananisha tena mtu mweusi na nyani.

Kama una maoni ya jinsi ujinga kwenye ubongo wa mtu mweusi unaweza kutokomezwa tukiadhimia naomba uyaandike hapa.
 
Sidhani kama hiyo Hali itawahi kubadilika kwa sababu hii tabia watoto Wana rithi kutoka kwa wazazi na wanakua wanajifunza kutoka kwa jamii inayo wazunguka, akiwa mtu mzima na yeye anarithisha wanae, ni circle ambayo Iko hivyo tuu, kwa kifupi tutabaki kua hivi hadi mwisho, haijalishi katiba itashuka kutoka mawinguni
Hapana, mimi siamini itakuwa hivyo milele!

Mbona mambo yashaanza kubadilika, japo ni taratibu sana?
 
Back
Top Bottom