Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Siyo Denmark pekee. Vinchi vyote vidogo huko Ulaya, na baadhi huko Asia, ukilinganisha na Tanzania ni aibu tupu:

Denmark
Norway
Finland
Sweden
Singapore
Switzerland

Utajiri mkubwa hapa Ulimwenguni ni akili, wala siyo idadi kubwa ya fisi na pundamilia, siyo dhahabu na gas, ardhi nzuri ya kilimo, maziwa, bahari au hali nzuri ya hewa.

Hata upewe vyote, ukinyimwa akili, vyote vinakuwa havina maana. Lakini ukibahatika ukapata akili,ni mwanzo wa mafanikio yote. Kwanza utajua ni nini kilicho muhimu, utakuwa na mifumo mizuri ya kuvuna rasilimali, utakuwa na tekinolojia, utakuwa na mifumo mizuri ya utawala, na mifumo mizuri ya kusimamia uchumi kwa ujumla.

Sisi tuna vitu vingi, lakini asilimia kubwa sana ya watu wetu wamenyimwa akili, utashi na maarifa. Ndiyo maana wachache wenye akili, maarifa na utashi, ama wanakuwa frustrated na kukata tamaa au kuishia kwenda kufanya kazi mataifa ya nje kwa sababu nchini mwao ni giza nene.
Kama sikosei finland bado inaongoza KWA kuwa na watu wenye furaha..africa ni stress tupu hata uwe kiongozi.
 
Mkuu, waheshimu viongozi. Unataka viongozi wa nchi kuubwa, kama Tanganyika wawaige Mawaziri wa nchi ndoogo, Denmark, watumie usafiri wa umma?

Denmark ni kanchi kadoogo sana, hawana uwezo wa kuwanunulia viongozi wao mav8, ila wanaweza kutupa misaada

Tanzania ni nchi kuubwa, hivyo ni halali kila kiongozi kutumia V8.
Duh 🙄 !!
 
Nasikia kipindi fulani Rais wa Marekani alishawahi kuutangazia ulimwengu kuwa hata kama nchi zote duniani zingegoma kuiuzia mafuta, wasingepungukiwa. Wana akiba ya miaka 100.

Sisi tuna akiba ya hela za Kigeni alau ya miaka 2? Sidhani!

Ila tumeweza kumpatia kila "kigogo" V8 la nguvu.
Hapo sasa !!
 
Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
Umejiuliza kwanini na we na ukoo wako wote mpaka leo ni maskini na mafukara? Si mna rasilimali ya ardhi nyie? Jiulize kwanza wewe.
 
Ubarikiwe sana. Ni kweli utupu. Muafirka sio mtu heri ya katuni kuliko mtu mweusi
we ni wapumbavu kuliko hata nyani wa porini. sijawahi ona mtu anajitukana na kujidharau mwenyewe, hiki kizazi cha sasa ndiyo sifuri kabisa. Hivi wazee wetu km baba wa Taifa angekuwa na akili za kipumbavu km hizo zenu nchi hii ingepata hata uhuru? Baba wa Taifa alisimamia utu wa mtu mweusi na kusema binadamu wote ni sawa na wazungu wakamheshimu sana. sasa mapoyoyo km nyie mtaisaidia nini nchi hii km mnajitukana wenyewe? Hovyo kabisa nyie.
 
punguza makelele yanaumiza masikio
 
Umejiuliza kwanini na we na ukoo wako wote mpaka leo ni maskini na mafukara? Si mna rasilimali ya ardhi nyie? Jiulize kwanza wewe.
Hizo ndio fikra za Ubinafsi tunazozizungumzia humu ! Mtu akishakwapua aanze kuwatambia wengine !! Halafu anajiona mjanja !!

Watu wa namna hiyo hawazifikirii Nchi zao kabisa ! Na ndio tofauti kati yetu na hao wazungu !!
 
Umemaliza kila kitu, nidhamu yao ya matumizi ipo juu sn Waziri wa Denmark anatumia public transport huku WEO anataka afuatwe na V8 kila siku, tuna viongozi wabovu na wezi wakubwa
Umenikumbusha kitu! Wakati nikiwa mwanafunzi wa Primary, jirani yetu mwajiriwa wa Tanroad, ilikuwa ni kawaida watoto wake kupelekwa shule kwa gari la Serikali, na kurudishwa Jioni. Huyo hakuwa mkubwa saana, lakini hata watoto wake walikuwa wakihidumiwa na gari la Serikali, vipi kwa wale vigogo hasaa?
 
Kama sikosei finland bado inaongoza KWA kuwa na watu wenye furaha..africa ni stress tupu hata uwe kiongozi.
Nayo pia ni kanchi kadoogo, inaingia Tanzania zaidi ya mara mbili, na kana population ya watu milioni tano tu, lakini inaipa Tanzania misaada.

Ila Wazungu nao!!! Kama vile hawawaamini watu weusi.

Mwaka 2009, niliingia ibadani kwenye Kanisa moja mkoani Kilimanjaro. Mchungaji wa hilo Kanisa alikuwa amerejea kutoka Finland alikoenda kuomba msaada. Katika taarifa aliyoitoa Kanisani ya safari yake, alisema Wafinish wamekubali kuufadhili mradi husika ila hawatatuma pesa, watakuja kuusimamia wenyewe. Walikuwa na mashaka kuwa kama wangewapatia pesa taslimu, huenda zingetumika isivyostahiki.

Yaani hawawaamini hata Wachungajui?
 
Hizo ndio fikra za Ubinafsi tunazozizungumzia humu ! Mtu akishakwapua aanze kuwatambia wengine !! Halafu anajiona mjanja !!

Watu wa namna hiyo hawazifikirii Nchi zao kabisa ! Na ndio tofauti kati yetu na hao wazungu !!
Kama isingelikuwa ninawheshimu Watanzania wenzangu, ningethubutu kusema Watanzania ni "wezi" ila kwa sababu nawaheshimu, nimejizuia kusema.

Tulipokuwa Sekondari, tulikuwa tukiulizana kazi tunazozitarajia kufanya baada ya kuhitimu Vyuo, ungesikia TRA, POLISI, n.k.
Kwa nini huko? Mwingine atakuambia, kwa mfano, ukiwa Trafiki, hata kama hakuna unga ndani, unaweza kuagiza maji yainjjikwe jikoni kwa sababu una uhakika ukishafika barabarani lazima utarudi na unga.

TRA ndiyo usiseme kabisaa. Mtu anayefanya kazi huko asipoonekana akiinuka kiuchumi kwa Kasi, huitwa mjinga.

Yaani asiyeiba ni mjinga????
 
Nayo pia ni kanchi kadoogo, inaingia Tanzania zaidi ya mara mbili, na kana population ya watu milioni tano tu, lakini inaipa Tanzania misaada.

Ila Wazungu nao!!! Kama vile hawawaamini watu weusi.

Mwaka 2009, niliingia ibadani kwenye Kanisa moja mkoani Kilimanjaro. Mchungaji wa hilo Kanisa alikuwa amerejea kutoka Finland alikoenda kuomba msaada. Katika taarifa aliyoitoa Kanisani ya safari yake, alisema Wafinish wamekubali kuufadhili mradi husika ila hawatatuma pesa, watakuja kuusimamia wenyewe. Walikuwa na mashaka kuwa kama wangewapatia pesa taslimu, huenda zingetumika isivyostahiki.

Yaani hawawaamini hata Wachungajui?
Wachungaji pia ni watu. Hata wewe ukikaa na mchungaji, jua kuwa uko na mchungaji lakini pia ni mtu. Zipimeni Kila roho sio ziaminini Kila roho.
 
Kama isingelikuwa ninawheshimu Watanzania wenzangu, ningethubutu kusema Watanzania ni "wezi" ila kwa sababu nawaheshimu, nimejizuia kusema.

Tulipokuwa Sekondari, tulikuwa tukiulizana kazi tunazozitarajia kufanya baada ya kuhitimu Vyuo, ungesikia TRA, POLISI, n.k.
Kwa nini huko? Mwingine atakuambia, kwa mfano, ukiwa Trafiki, hata kama hakuna unga ndani, unaweza kuagiza maji yainjjikwe jikoni kwa sababu una uhakika ukishafika barabarani lazima utarudi na unga.

TRA ndiyo usiseme kabisaa. Mtu anayefanya kazi huko asipoonekana akiinuka kiuchumi kwa Kasi, huitwa mjinga.

Yaani asiyeiba ni mjinga????
Tena ni mjinga wa kutolewa mfano kabisa !!
 
Nayo pia ni kanchi kadoogo, inaingia Tanzania zaidi ya mara mbili, na kana population ya watu milioni tano tu, lakini inaipa Tanzania misaada.

Ila Wazungu nao!!! Kama vile hawawaamini watu weusi.

Mwaka 2009, niliingia ibadani kwenye Kanisa moja mkoani Kilimanjaro. Mchungaji wa hilo Kanisa alikuwa amerejea kutoka Finland alikoenda kuomba msaada. Katika taarifa aliyoitoa Kanisani ya safari yake, alisema Wafinish wamekubali kuufadhili mradi husika ila hawatatuma pesa, watakuja kuusimamia wenyewe. Walikuwa na mashaka kuwa kama wangewapatia pesa taslimu, huenda zingetumika isivyostahiki.

Yaani hawawaamini hata Wachungajui?
Duh !
 
we ni wapumbavu kuliko hata nyani wa porini. sijawahi ona mtu anajitukana na kujidharau mwenyewe, hiki kizazi cha sasa ndiyo sifuri kabisa. Hivi wazee wetu km baba wa Taifa angekuwa na akili za kipumbavu km hizo zenu nchi hii ingepata hata uhuru? Baba wa Taifa alisimamia utu wa mtu mweusi na kusema binadamu wote ni sawa na wazungu wakamheshimu sana. sasa mapoyoyo km nyie mtaisaidia nini nchi hii km mnajitukana wenyewe? Hovyo kabisa nyie.
Mwalimu alikuwa na msimamo huo kwa vitendo sio kwa Maneno ya mdomoni !! Ndio maana Mwalimu hawezi kusahaulika vizazi na vizazi vitakavyokuja !! Mwalimu aliyaishi yale aliyokuwa akiyasema. !!
 
Back
Top Bottom