Kwa Tanzania Mzee Ruksa akaanza kuibomia misingi mibovu,mkapa akaendelea kuisambaratisha, Kikwete akaanza kuijenga upya, Magufuli akajitahidi kuirudisha baadhi ya misingi mibovu ya Nyerere na kuibomia misingi mizuri iliyosnza kujengwa na Kikwete, Mwenyezi Mungu akamstopisha.
Kwabuwezo wa Mwenyezi Mungu katuwekea Mama Samia kurekebisha palipoanza kubomolewa na bwana yule na kuendeleza kuijenga misingi thabiti iiyoanza kujengwa na Kikwete.
Heko mama Samia.
Wewe nawe kumbe hakuna kitu kabisa. Labda unaishi kwa ushabiki kuliko werevu, akili na ukweli.
Mwalimu aluweka misingi mizuri sana ya uchumi mara baada ya kupata uhuru. Alipokuja kuharibu ni pale alipobadili na kujiingiza kqenye siasa za ujamaa mwaka 1967. Lakini kuna baadhi ya vitu alivyovianzisha kama viwanda, taasisi za utafiti, ulikuwa ni msingi muhimu sana kwa maendeleo.
Tuwe wakweli, mzee wetu Rais Mwinyi, uwezo wa kiuchumi ulimpiga chenga kabisa.
Ni wakati wa mwinyi, kwa wakati huo, Tanzania ikawa ndiyo nchi inayoongoza Duniani kwa inflation, mpaka kufikia 30%. Ni wakati wa Mwinyi ndipo nchi ilifikia kiwango cha kitokopesheka. Mikopo na misaada yote ikasimamishwa kwa Tanzania kutokana na corruption. Pesa za wafadhili, 60% ziliibiwa na waliokuwepo Serikali, na hazikuwahi kuingia nchini. Wakati wa Mwinyi, nchi ilupokea misaada mingi kuliko kioindi chochote kile cha uhai wa Taifa letu. Kwa wastani, kila mtanzania, hata mtoto anayezaliwa, alipata msaada wa dola 857. Lakini 60% ya hiyo pesa yote iliibiwa na kuficha mabenki ya nje. Ndipo mataifa wahisani na wakopeshaji wakasimamisha misaada na mikopo yote kwa Tanzania.
Mkapa ndiye Rais pekee aliyepata mafanijio makubwa kwenye uchumi. Aliingia ikulu, hazina ikiwa na zero balance. Aliondoka ikulu akiiacha hazina na balance ya dola bilioni 5. Aliishusha inflation toka 30% mpaka 4%, jambo liliompa kubwa Duniani kwa sababu hakuna Taifa Duniani liliwahi kufanya hivyo ndani ya kipindi cha miaka mitano tu.
Kikwete alipoingia aliharibu uchumi. Pesa iliyoachwa na Mkapa hazina akaitapanya hovyo kwa ule mradi wa mabilioni ya Kikwete. Kilichomsaidia zaidi ni staili.yake ya uongozi ya kuuma na kupuliza. Style hiyo ya uongozi iliisaidia sana Serikali yake kupata misaada mingi toka mataifa hisani. Hata hivyo uchumi haukupata mizizi, ulikuwa uchumi bandia.
Uongozi wa Magufuli ulitegemea sana nguvu kuliko akili. Nguvu bila akili, haiwezi kukupa mafanikio. Hali hiyo iliirudisha nchi nyuma zaidi. Alielewa vitu vinavyohitajika ili kuwa na uchumi imara, lakini alikosa mbinu za kufika alikotaka nchi ifike.
Serikali ya sasa, kwa namna tunavyoenda, tunatafuta unafuu wa maisha, lakini siyo kuwa na misingi imara ya uchumi.