Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Ukubwa wa pua si wingi wa kamasi.Jiulize ki nchi kama Belgium kutawala linchi likubwa kama Congo -Belge.
Ubelgiji na mfalme Leopard II waliona zao la mpira wakawa wavuna na kupeleka Ulaya kama malighafi ya kutengeneza matairi.

Danlop ni moja ya viwanda maarufu duniani ambavyo malighafi yake ya mpira ilitokea Congo.

Pia Ubelgiji waongoza duniani kwa bidhaa zitokanazo na kakao ni wapenzi wa chocolate mtaelewa.

Mwisho, Antwerp ndipo yalipo makao makuu ya Amasi yote chafu (isiochakachuliwa) kutoka sehemu mbalimbali duniani hususan barani Afrika.

Ni kutumia akili zetu tu si uchawi, maana watanzania tulikuwa na kiwanda cha baiskeli cha Swala ambacho leo hii kipo tu kimetulia.

Hakuna matoleo mapya ya baiskeli wala matairi yake wala angalau baiskeli hata za watoto.
 
Kuna mwingine pia alisema hata kupigana vita ya Kagera kuliigharimu uchumi wa nchi , sijui kama Kuna ukweli wa hili.
Hilo haliwezi kukataliwa, lakini adhari zake zisingepaswa kuwa za kudumu kwa miaka nenda rudi.

Tanzania haikuwa ya kwanza kukabiliana na vita. Kama vita ni sababu ya nchi kuwa dumavu kiuchumi, basi hata Japan na Ujerumani nazo zilipaswa kuwa chini.

Na Rwanda je? Pamoja na vita vya wenyewe kwa wenyewe ilivyokabiliana navyo mwaka 1994, lakini bado kuna vitu inatupita. Kumbuka Rwanda ni kadoogo kieneo, na rasilimali zake ni chache sana ukiilinganisha na Tanzania.

Fikiri tu, kwa mfano, TANZANITE, BANDARI YA DAR ES SALAAM na SERENGETI NATIONAL PARK zingekuwa kwa Kagame, Rwanda ingekuwa wapi kwa sasa?
 
Yeah mtu wa kawaida anaweza kufanya kazi zaidi ya tatu tofauti ili mkono uende kinywani. Waajiri hawana simile au uvumulivu wa uzembe au ubadhirifu wa aina yoyoye ile. Matokeo ya kazi yanapaswa kuonekana sasa hivi ili kujihakikishia kibarua chako ukifanya kazi taasisi ya aina yoyote ile. Huo ni baadhi ya uzoefu wangu tu. Magufuli alileta ile model ya tumbua tumbua na kuonyesha hulka ya kutovumilia uzembe wa aina yoyote ile matokeo yake kale kafala kakaanza kumuita dikteta uchwara. Leo hii eti mnajiuliza Denmark inawezaje?
Nilishawahi kusoma gazetini kuwa Japan ukichelewa kuingia kazini hata kwa dakika Moja tu, unakabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi kwa uzembe.

Hawana utani katika kazi.
 
Afrika kupiga hatua ni kazi sana,watu wenye akili huchukiwa ila vilaza ndiyo hupewa kura Ili wawe viongozi,98%ya Waafrika ni mambumbu na ndiyo wenye nguvu katika jamii zetu.

Naungana na anayesema Mungu aangamize hii race ya mtu mweusi,kwani ni kama inaonewa na imeshindwa kucompete na hizo races zingine
 
Afrika kupiga hatua ni kazi sana,watu wenye akili huchukiwa ila vilaza ndiyo hupewa kura Ili wawe viongozi,98%ya Waafrika ni mambumbu na ndiyo wenye nguvu katika jamii zetu.

Naungana na anayesema Mungu aangamize hii race ya mtu mweusi,kwani ni kama inaonewa na imeshindwa kucompete na hizo races zingine
Basi tuanze vugu vugu la kuikomboa race ya watu nyeusi, uko tayari kuwa miongoni mwa viongozi wa hilo vugu vugu?
 
Magufuli alipotaka kuigeuza Tanzania iwe sawa na nchi za Ulaya mlimfanyaje? Mnataka maendeleo lakini hamtaki namna ya kuyafikia hayo maendeleo. Maendeleo ni malengo, nidhamu, kujitoa mhanga (self sacrifice), bidii ya kazi, uadilifu na kutambua vipaji na ubunifu na kuvitumia ipasavyo. Ulaya wameweza kuviunganisha hivyo vyote kufikia hapo walipo. Sisi hapa bado tunajitafta na akija mwenye mawazo kama hayo bado hatumwelewi. Tutachelewa sana.
Hapa Tanzania ukiwa na akili wanakuua.
 
Kwa Tanzania Mzee Ruksa akaanza kuibomia misingi mibovu,mkapa akaendelea kuisambaratisha, Kikwete akaanza kuijenga upya, Magufuli akajitahidi kuirudisha baadhi ya misingi mibovu ya Nyerere na kuibomia misingi mizuri iliyosnza kujengwa na Kikwete, Mwenyezi Mungu akamstopisha.

Kwabuwezo wa Mwenyezi Mungu katuwekea Mama Samia kurekebisha palipoanza kubomolewa na bwana yule na kuendeleza kuijenga misingi thabiti iiyoanza kujengwa na Kikwete.

Heko mama Samia.
Wewe nawe kumbe hakuna kitu kabisa. Labda unaishi kwa ushabiki kuliko werevu, akili na ukweli.

Mwalimu aluweka misingi mizuri sana ya uchumi mara baada ya kupata uhuru. Alipokuja kuharibu ni pale alipobadili na kujiingiza kqenye siasa za ujamaa mwaka 1967. Lakini kuna baadhi ya vitu alivyovianzisha kama viwanda, taasisi za utafiti, ulikuwa ni msingi muhimu sana kwa maendeleo.

Tuwe wakweli, mzee wetu Rais Mwinyi, uwezo wa kiuchumi ulimpiga chenga kabisa.

Ni wakati wa mwinyi, kwa wakati huo, Tanzania ikawa ndiyo nchi inayoongoza Duniani kwa inflation, mpaka kufikia 30%. Ni wakati wa Mwinyi ndipo nchi ilifikia kiwango cha kitokopesheka. Mikopo na misaada yote ikasimamishwa kwa Tanzania kutokana na corruption. Pesa za wafadhili, 60% ziliibiwa na waliokuwepo Serikali, na hazikuwahi kuingia nchini. Wakati wa Mwinyi, nchi ilupokea misaada mingi kuliko kioindi chochote kile cha uhai wa Taifa letu. Kwa wastani, kila mtanzania, hata mtoto anayezaliwa, alipata msaada wa dola 857. Lakini 60% ya hiyo pesa yote iliibiwa na kuficha mabenki ya nje. Ndipo mataifa wahisani na wakopeshaji wakasimamisha misaada na mikopo yote kwa Tanzania.

Mkapa ndiye Rais pekee aliyepata mafanijio makubwa kwenye uchumi. Aliingia ikulu, hazina ikiwa na zero balance. Aliondoka ikulu akiiacha hazina na balance ya dola bilioni 5. Aliishusha inflation toka 30% mpaka 4%, jambo liliompa kubwa Duniani kwa sababu hakuna Taifa Duniani liliwahi kufanya hivyo ndani ya kipindi cha miaka mitano tu.

Kikwete alipoingia aliharibu uchumi. Pesa iliyoachwa na Mkapa hazina akaitapanya hovyo kwa ule mradi wa mabilioni ya Kikwete. Kilichomsaidia zaidi ni staili.yake ya uongozi ya kuuma na kupuliza. Style hiyo ya uongozi iliisaidia sana Serikali yake kupata misaada mingi toka mataifa hisani. Hata hivyo uchumi haukupata mizizi, ulikuwa uchumi bandia.

Uongozi wa Magufuli ulitegemea sana nguvu kuliko akili. Nguvu bila akili, haiwezi kukupa mafanikio. Hali hiyo iliirudisha nchi nyuma zaidi. Alielewa vitu vinavyohitajika ili kuwa na uchumi imara, lakini alikosa mbinu za kufika alikotaka nchi ifike.

Serikali ya sasa, kwa namna tunavyoenda, tunatafuta unafuu wa maisha, lakini siyo kuwa na misingi imara ya uchumi.
 
Sikia umestaafu nawe pia ulikuwa unatumikia Taifa kama wengine..wengine..ila unaambiwa kuna watu wanapigwa V8..halafu mpya.

Kuna mtu mmoja tu hapa nchini anasepa na 1B kama mafao wakati kuna wapigania nchi hawafiki hata m30 pension na kakaa Miaka 35/40.Sasa sio laana ni nini?

Kuna watu tunawaachia watoto wetu siku 5 kwa week na wengine six months shule..hao wanalipwa hela ukijummuisha wote Tanzania nzima mishahara yao ndio mafao ya watu wawili waliostaafu wakuu waku kule😀😀😀

Lord Lord,sasa fikiria kuna madaktari,wauguzi hawa watu wa afya zetu sisi tia maji tia maji..sikiliza mishahara.yao..

Kuna wahuni wakusanya Kodi kasoma 3 years tu anakunja pesa ya kulipa Madktari zaidi ya ishirini na wauguzi kumi kupitia janja janja tu kubuni kodi??Tena sikia mtu miaka mitatu kazini Mshahara haufiki 5m, ana ghorofa za Billion zaidi ya 15.

Njoo sasa wajuba wa Bungeni,hawa wanakunja 300,000 kusinzia tu pale na kutupelekea matatizo yetu ambayo ni Yao.


Laana na fikra zetu na mambo yetu,waacha tuendelee kula misaada.

Mwisho wa siku pambania Maisha yako,kula kula kwa urefu wa Kamba yako.

Wacha tuendelee kula bangi kwenye Biskuti na Chai Tatepa.
 
Basi tuseme nchi za Afrika matatizo yetu ni yale yale.


South Afrika iliendelea sana kabla ya Weusi kupewa uongozi
Ukitaka kujua kuwa tatizo ni mtu mweusi, angalia nchi kama South Afrika na Zimbabwe. Kabla ya uongozi kuchukuliwa na watu weusi, nchi hizo zilikuwa zinakaribiana sana na baadhi ya mataifa ya Ulaya. Baada ya uongozi kuchukuliwa na watu weusi, mataifa hayo yanakwenda kwa kasi kuyafuata mataifa ya wenzao weusi.

Sasa hivi makaburu wa South Afrika, kila mwaka kwa mamia, wanaihama South Afrika, wengi wakihamia Australia.

Karne ijayo, South Afrika haitakuwa tofauti na mataifa mengine ya Afrika.
 
Kwasababu Africa ina eneo kubwa sana, ni maeneo machache ambayo yalianza kuendelea zamani hizo, maenek kama western Africa, Egypt, Ethiopia na mengine baadhi ndio yalikua na maendeleo na pia serikali zao zilimiliki eneo kubwa sana.

Si ajabu watu wa huko wangeshuka mpaka kusini na kujaribu kutawala/kupigana vita huko basi Africa ingetanuka kifikra kwa huo muingiliano.

Chukulia mfano tu hata hapa Tz, mpaka leo msukuma/mnyakyusa wa huko ndanindani wala hajui kua hii nchi kuna kabila jingine zaidi yao. Hii inafanya kua na fikra mfu kabisa, huna changamoto yoyote utagunduaje vitu??

Tofauti na historia ya bara la ulaya, vita vimepiganwa kwelikweli. Siraha, mbinu na medani za kivita zimefundishwa na kubuniwa mno. Lakini huku ni makabila machache yaliyokua na mbinu za kivita na kujilinda.
Makabila mengine hakukua na hizo changamoto ndio maana hata wakoloni walipokuja hakukua na resistance sana kwa baadhi ya makabila.

Na nchi kutoboa ilikua ni miaka hiyo, sasa hivi nchi kama Tz kuja kua kama hiyo Denmark sio rahisi.
 
Nilishawahi kusoma gazetini kuwa Japan ukichelewa kuingia kazini hata kwa dakika Moja tu, unakabidhiwa barua ya kufukuzwa kazi kwa uzembe.

Hawana utani katika kazi.
Mi nilikuwa Switzerland. Ofisini unaingia saa moja na nusu na milango ya ofisi ufunguo wake ni electronic card kuthibitisha umeingia mda huo. Unachokifanya kwenye computer kinakuwa monitored na team leader wako. Mda wa break unajulikana na ukianza kutokatoka nje wanacalculate tu mda uliopoteza (card ina track mara ngapi umetoka nje ya ofisi). Still kuna waajiriwa kila tathmini inapofanyika wanaonekana hawatoshi na wanakuwa fired. Hapo Magufuli alionyesha ukali tu pale uzembe unapoonekana wazi kwenye ziara zake. Je kila mtu akianza kuwajibika na kuwajibishwa kwa kila sekta na kada impact yake itakuaje kwa nchi? Mi naonaga hapa bongo kila mfanyakazi anafanya kazi chini ya kiwango kwa namna zetu.za kufanya kazi.
 
Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
Jibu ni hao watu milioni tano wenye uchumi mkubwa, na watu milioni sitini wenye uchumi hafifu.
 
Back
Top Bottom