Inawezekanaje nchi ndogo ya Denmark kuipa misaada nchi kuubwa Tanzania?

Sifa ulizonimwagia ni mtego mkuu🤣.
Anyways nina akili za kutosha kuvukia barabara ila hazifikii za wazungu🤣.
Ningekua nina akili kama.za wazungu ningefanya jambo nchi yangu iwe kama Denmark.
Asante kwa pongezi lakini
Naamini hata sasa kuna unachokifanya kimya kimya kwa manufaa ya nchi. Kama ilivyo ada ya wenye akili, huwa hawapigi kelele wanapofanya mambo ya muhimu. Wao hukaa kimya huku kazi zao nzuri zikipaza sauti.

Hayo unayoyafanya yataisaidia nchi. Hata isipokuwa kama Denmark, itaifanya Tanzania kuwa bora zaidi ya ilivyo sasa.
 
Magufuli alipotaka kuigeuza Tanzania iwe sawa na nchi za Ulaya mlimfanyaje? Mnataka maendeleo lakini hamtaki namna ya kuyafikia hayo maendeleo. Maendeleo ni malengo, nidhamu, kujitoa mhanga (self sacrifice), bidii ya kazi, uadilifu na kutambua vipaji na ubunifu na kuvitumia ipasavyo. Ulaya wameweza kuviunganisha hivyo vyote kufikia hapo walipo. Sisi hapa bado tunajitafta na akija mwenye mawazo kama hayo bado hatumwelewi. Tutachelewa sana.
👏👏👏👏👏
 
Naked truth
Yaani itokee tuhamishwe waafrika tupelekwe ulaya na marekani halafu wazungu wake Africa, wakati wa kuhama hamna unachochukua zaidi ya nguo ulizovaa
Baada ya miaka mitano,ni sisi ambalo tutaomba viza na kulia ubarozini ili tukubaliwe kuingia tena Afrika
Hii ni mbaya zaidi!
 
Ukiwaweka hawa viongozi wa Tanzania Denmark au Korea na Viongozi wa Korea / Denmark kila kitu kitakuwa vice versa.

Uzuri wa wananchi wa nchi hizo hawatachukua muda mrefu viongozi wabovu wataondolewa madarakani na kuishia jela.

Kwa wenzetu kuna uwajibikaji, seriousness, wako serious na maisha.
Upo sahihi naunga mkono hoja
 
Magufuli alipotaka kuigeuza Tanzania iwe sawa na nchi za Ulaya mlimfanyaje? Mnataka maendeleo lakini hamtaki namna ya kuyafikia hayo maendeleo. Maendeleo ni malengo, nidhamu, kujitoa mhanga (self sacrifice), bidii ya kazi, uadilifu na kutambua vipaji na ubunifu na kuvitumia ipasavyo. Ulaya wameweza kuviunganisha hivyo vyote kufikia hapo walipo. Sisi hapa bado tunajitafta na akija mwenye mawazo kama hayo bado hatumwelewi. Tutachelewa sana.
NASISITIZA
 
Utajiri mkubwa hapa Ulimwenguni ni akili, wala siyo idadi kubwa ya fisi na pundamilia, siyo dhahabu na gas, ardhi nzuri ya kilimo, maziwa, bahari au hali nzuri ya hewa.
Kwa hiyo wa kwetu hawana akili au!
Semq wa kwetu changamoto nyingi ila pia kushindwa kusimamia uchumi vyema na rushwa juu!
Halafu hatuna vipaumbele vya kudumu kama Taifa, kila anaekuja anakuja na malengo yake.
 
Akili ndo inamfanya MTU afanikiwe

Na mabadiliko huwa yanaletwa na watu wachache only few people brings changes to the masses.

Great thinkers Tz hawapewi nafasi ya Ku-shine na kutumika na mwisho wanakuwa watazamaji tu
 
Wadenish wachache waakili nyingi kuliko watanzania weeengi.

Inawezekana ugali una changamoto nyingi sana, maana huku kusini mwa jangwa la sahara tunakula sana ugali..
 
Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
--short and clear hapo ulipo unawaza upate majumba makubwa na maghorofa ikibidi, ununue nyumba dubai, and alike, na hufikirii upate pesa uboreshe hata kipande kidogo cha barabara mtaani kwako!, ndivyo viongozi wa kiafrika walivyo!
 
Technology mkuu,kutumia akili vizuri,na ufisadi,angalia Benz ya kwanza karibu miaka 200 iliyopita, , angalia Benz Mpya toleo la kisasa,Angalia Mkwea Minazi Africa Miaka 200 iliyopita,na Mkwea Minazi mwaka 2024
1718560721548.jpg
 
Ukiwaweka hawa viongozi wa Tanzania Denmark au Korea na Viongozi wa Korea / Denmark kila kitu kitakuwa vice versa.

Uzuri wa wananchi wa nchi hizo hawatachukua muda mrefu viongozi wabovu wataondolewa madarakani na kuishia jela.

Kwa wenzetu kuna uwajibikaji, seriousness, wako serious na maisha.
Mkuu acha basi!
Mi roho inaniuma sana kutokana na maelezo yako yanayoanika ukweli.
Yananifanya nijute kuzaliwa katika jamii ya hovyo sana.
 
Kwa hiyo wa kwetu hawana akili au!
Semq wa kwetu changamoto nyingi ila pia kushindwa kusimamia uchumi vyema na rushwa juu!
Halafu hatuna vipaumbele vya kudumu kama Taifa, kila anaekuja anakuja na malengo yake.
Vyote hivyo vinahitaji akili.
 
Kosa kubwa alilofanya Muumba ni kuwaumba watu weusi ie waafrika
Duuh, .
Nadhani Wazungu ndio wanaompasua kichwa lakini sio waafrika.
Mana haya yanayoitwa maendeleo ya dunia ndiyo yanayoharakisha kuiangamiza dunia na watu waka.

Waafrika tumeingia tamaa kuiga mambo ya kizungu na sasa tunaelekeza uharibifu mkubwa kwetu.
 
Shida sio kuwa na watu wengi au Wachache
Je mna watu wenye akili na wenye uwezo wa kuzitumia?
Una rasilimali but huna watu wenye akili?
Wao Wana watu wenye akili so they use all of their natural resources to make their life better
Sio sis mpaka Leo tunakomaa na kampeni ya "nyumba ni choo" are you serious?
Au ndio maskini Hana ustarabu
 
Denmark inatarajia kuufunga ubalozi wake nchini Tanzania ifikapo 2024. Ni kati ya nchi ambazo zimekuwa zikiipa Tanzania misaada, tokea ikiitwa Tanganyika hadi sasa ikiwa inajulikana kwa jina adhimu, Tanzania.

Lakini Denmark ni nchi ya namna gani?

Ukifanya ulinganisho, Tanzania imeizidi kwa mambo mengi isipokuwa ujinga na umaskini. Ina rasilimali nyingi sana kuizidi, na hata idadi ya watu tumeipita mbali sana.

Denmark, ni kanchi kadoogo, kenye ukubwa wa kilomita za mraba 42,920 lakini inaizidi kiuchumi Tanzania, nchi Kuubwa kieneo, yenye kilomita za mraba 945,087.

Denmark, ni kanchi kadoogo kenye watu milioni tano lakini inaipa misaada nchi kuubwa, Tanzania, yenye watu milioni sitini na moja.

Ni nini siri ya kanchi kadogo kuizidi nchi kubwa kama Tanzania? Imekuwa ikiisadia Tanzania tokea 1963, enzi hizo ikiitwa Tanganyika, lakini hakuna taarifa ya Tanzania ambayo ni nchi kubwa kuisaidia Denmark kanchi kadogo.

Imewezekanaje kwao lakini kwetu ikashindikana?

Mwingine anaweza kusema ni kwa sababu ya ukoloni, lakini hilo halina mashiko. Hata Korea Kusini ilishawahi kuwa koloni la Japan, lakini kwa sasa wanatukimbiza kiuchumi.

Ni nini walichogundua hao watu weupe ambao weusi wa Tanganyika na Zanzibar hawajagundua?

Angalia, hata eneo la Korea Kusini ni dogo sana ukililinganisha na ukubwa wa Tanzania. Ina kilomita za mraba 100,210 na watu milioni hamsini na moja.

Inawezekanaje kanchi kadoogo, Denmark, kuipa misaada nchi kuubwa, Tanzania?
Tukiendelea na hiki kizazi Cha chawa wanaokula kwq kusigia badala ya kufanya kazi wallah vile tutapewa msaada mpaka na Burundi.
 
Back
Top Bottom