Seran
JF-Expert Member
- Feb 7, 2025
- 36,315
- 104,500
Habari wana JF,
Naomba msaada wa mawazo kutoka kwa wenye uzoefu. Nina biashara ndogo ambayo kwa wiki inaweza kuniingizia kati ya 50,000 hadi 100,000, ingawa sio kila siku kuna biashara.
Kinachonitatiza ni kwamba, licha ya kuwepo kwa kipato, matumizi yanabaki kuwa makubwa kuliko pesa inayoingia.
Mfano halisi: wiki ikaingia 59,000, lakini matumizi yakafika 38,000. Matumizi hayo yanahusisha chakula, bili za umeme na maji, pamoja na baadhi ya vifaa. Ikabaki 21000, nadhani hapo naelekeka sasa namaanisha nini..
Baada ya kuondoa matumizi, faida inayobaki ni ndogo sana, kiasi cha kunifanya nishindwe kuelewa kama biashara hii inanipa faida ya maana au inanizungusha tu.. income>Expenses, lakini faida ya biashara inaonekana ndogo
Kwa uzoefu wenu:
Cha ajabu kwenye records monthly expenses zinashuka na faida kuonekana ipo, lakini sio kipato nilicholenga kulingana na biashara inavyoenda! Wajuzi mnisaidie naona navurugika kila nikifanya recordings, huwa nina kawaida ya kurecord kila ninachofanya, sasa naona siridhizishwi na haya matokeo ya mwisho!
NB, wale wanaotaka kujua aina ya biashara ni urembo in general..

- Je, hali kama hii ni ya kawaida kwenye biashara ndogo?
- Ni vipi naweza kupumguza expenses bila kuua biashara?
- Au kuna mbinu za kuongeza faisa hata kama mauzo si ya kila siku?