India: Wanafunzi washambuliwa wakiwa katika sala

India: Wanafunzi washambuliwa wakiwa katika sala

Malaria 2

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2023
Posts
6,846
Reaction score
10,288
Wanafunzi wasiopungua wanne wa kigeni wamejeruhiwa baada ya kundi la Wahindu wenye chuki za kidini kuvamia dakhalia ya chuo kikuu katika jimbo la Gujarat magharibi mwa India na kushambulia kundi la wanafunzi waliokuwa wanasali Sala ya Tarawehe katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Wanafunzi walioshambuliwa wamevieleza vyombo vya habari vya ndani kuwa kikundi kidogo kilikusanyika Jumamosi usiku ndani ya majengo ya dakhalia ya wavulana kwa ajili ya Sala ya Tarawehe kwa kuwa hakuna msikiti kwenye chuo kikuu kilichoko Ahmedabad. Muda mfupi baadaye, kundi la watu waliokuwa na fimbo na visu walivamia hosteli hiyo na kuwashambulia wanafunzi hao na kufanya uharibifu ndani ya vyumba vyao.

Mwanafunzi mmoja amesema: "kikundi cha wanafunzi 15 walikuwa wanasali wakati watu watatu walipowajia na kuanza kupiga makelele ya 'Jai Shri Ram' yaani [Salamu bwana Ram]. Walituzuia tusisali hapa”.
Mwanafunzi mmoja kutoka Afrika amesema: "hatuwezi kuishi hivi, tulikuja India kusoma na sasa tunashambuliwa kwa sababu ni wakati wa Ramadhani na kwa sababu Waislamu wanasali".

Tovuti ya habari ya Indian Express imeripoti kuwa wanafunzi wawili walijeruhiwa vibaya na wanaendelea kupata matibabu hospitalini baada ya wanafunzi kutoka Afghanistan, Uzbekistan, Sri Lanka, Bangladesh na nchi kadhaa za Afrika kushambuliwa.

Makundi ya Wahindu ya mrengo wa kulia yenye misimamo mikali na chuki za kidini yamekuwa yakiendesha kampeni za hujuma na mashambulio katika maeneo ya umma dhidi ya Waislamu wanaosali.

Mapema mwezi huu, askari polisi mmoja katika mji mkuu New Delhi alisimamishwa kazi baada ya kuwapiga mateke wanaume Waislamu waliokuwa wakisali kando ya barabara.
 
Uhuru wa kuabudu ni jambo muhimu sana, kila mmoja aachiwe aabudu mambo yake, nafikiri hadi hapo mumeona jinsi wengine hupata kero mnapowazuia kuabudu mambo yao, Wakristo huteswa sana kwenye nchi za Kiislamu, mkuki kwa nguruwe.

Tuheshimiane kwenye imani zetu maana wewe hapo huna uwezo wa kunidhihirishia uwepo wa unayemuabudu hivyo usilazimishe wengine.

Watu wazima wanaandamana kupinga ujenzi wa kanisa.


View: https://www.youtube.com/watch?v=pcwvILodCKM
 
Uhuru wa kuabudu ni jambo muhimu sana, kila mmoja aachiwe aabudu mambo yake, nafikiri hadi hapo mumeona jinsi wengine hupata kero mnapowazuia kuabudu mambo yao, Wakristo huteswa sana kwenye nchi za Kiislamu, mkuki kwa nguruwe.....
Waislam huwa sio waelewq, huwatesa sana Wakristo kwenye nchi zao, lkn wao wakiguswa ni vilio vitupu.

Watu waachwe waabudu wanachokiamini.

Hao wanafunzi wameonewa bure
 
Unapoenda India a ha dining yako nyumbani kwenu
 
Kuna tamaduni hawataki utani na tamaduni zao hata kama ww ni familia yao eti sijui ulienda nchi za kiislam wakakudanganya ukawa muislam unavyo rudi nyumbani inabidi uislam uucha huko huko.
Wahindi ni jamii ya watu wasiyostaarabika. Na si kwenye masuala ya ibada tu bali hata makazini ni jamii ya watu wasiyostaarabika.
 
Wahindi ni jamii ya watu wasiyostaarabika. Na si kwenye masuala ya ibada tu bali hata makazini ni jamii ya watu wasiyostaarabika.
Na wao waislamu hao sio waelewa chuoni hakuna msikiti kwa nini walazimishe kuwemo msikiti? Hao waligeuza hicho chumba walichokuwa wakisalia kuwa msikiti kwa nguvu kuwa eneo la kuswalia waislamu iwe kwa muda mfupi au mrefu

Hao wanafunzi wa kiislamu hawakuwa sahihi.Wahindu walikuwa sahihi kuwavamia

Hawana akili hao wanafunzi
 
Na wao waislamu hao sio waelewa chuoni hakuna msikiti kwa nini walazimishe kuwemo msikiti?
Ndugu, umeisoma taarifa?
Uzi umeelezea kuwa Chuoni hapo hakuna msikiti. Sasa inakuwaje unauliza swali ambalo jawabu lake lilishawekwa?
Hao waligeuza hicho chumba walichokuwa wakisalia kuwa msikiti kwa nguvu kuwa eneo la kuswalia waislamu iwe kwa muda mfupi au mrefu
Ndugu, umeisoma tena taarifa? Wapi maudhui yamesema wamelazimisha hicho chumba kuwa msikiti kwa nguvu?
Hao wanafunzi wa kiislamu hawakuwa sahihi.Wahindu walikuwa sahihi kuwavamia

Hawana akili hao wanafunzi
Narendra Modi hufahamu kuwa chama Chao cha Bharatiya Janata ni chama cha wahafidhina chenye msimamo mkali wa kihindu?

Angalia uongozi wa Modi na PM aliyepita kabla yake mbona hizo jamii ziliishi vizuri misuguano haikuwepo kama Modi na chama Chao kiliposhika madaraka?

Inakubidi ufahamu siasa ya India inavyokwenda ndugu mtanzania.
 
Ndugu, umeisoma taarifa?
Uzi umeelezea kuwa Chuoni hapo hakuna msikiti. Sasa inakuwaje unauliza swali ambalo jawabu lake lilishawekwa...
Mleta uzi kaandika kisaniisanii sana.Wahindu hawataki maeneo yao yatumike kinyume na dini yao.Uelewe hilo.

Hawakuwavamia bila sababu.
 
Waislam wakiwa wachache sehemu huwa wanapenda sana kuplay victim. Wakiwa wengi sehemu wanataka hadi watu wa dini zingine wasio waislam wafate taratibu za uislamu.

Hiyo ni mbinu yao. Amb

Yaani hawa watu ni kero, inabidi kuwavumilia sana, jamaa wanaamua kubinuka binuka na kunyanyua makalio katikati ya barabara kwenye nchi ya watu....
 

Attachments

  • Screenshot_20240319-134516.jpg
    Screenshot_20240319-134516.jpg
    476.2 KB · Views: 5
Yaani hawa watu ni kero, inabidi kuwavumilia sana, jamaa wanaamua kubinuka binuka na kunyanyua makalio katikati ya barabara kwenye nchi ya watu....
Yaani Roho Mtakatifu wako amekutekenya umtukane Yesu na Mitume mingine kuwa walibinuka , au huna dini kafiri wewe ??

Naye Ezra Kuhani akasimama juu ya mimbari ya mti waliyokuwa wameifanya kwa kusudi hilo na karibu naye
akasimama Matithia ....... Ezra akakifungua kitabu machoni pa watu wote (maana alikuwa juu ya wote) na hapo alipokijua, watu wote walisimama Ezra akamhimidia Bwana, Mungu Mkuu. Nao wote wakaitika , Amina, Amina, pamoja na kuinua mikono yao kisha wakainama vichwa vyao wakamsujudia Bwana vifudifudi. (Nehemia 8:4-12; Mwanzo 17:3).

Yesu , Akaendelea mbele kidogo akaanguka kifulifuli akaomba ... (Mathayo 26;39).

Msujudie Mungu. (Ufunuo 22:9).

Musa akafanya haraka akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu. (Kutoka 34:8; 1 Wakorintho 14:25).
 
Back
Top Bottom