Indonesia yadhamiria kununua hisa zote kitalu cha gesi Mnazi Bay Mtwara

Indonesia yadhamiria kununua hisa zote kitalu cha gesi Mnazi Bay Mtwara

Waziri January Makamba anabainisha kuwa huko nyuma serikali ilikuwa inapata kupitia faida inayopatikana (profit) lakini mradi huu wa Ruvuma - Mtwara sasa Tanzania itapata kupitia mapato ghafi

JIBU LA KUWEZESHA NCHI KUWA NA MKATABA BORA WA GESI, MADINI, MAFUTA NI KUIGA MKATABA HUU WA BOTSWANA WA MALI KWA MALI

Kujidai kufanya mgawanyo wa mahesabu kwa kuangalia mapato ghafi, bado watacheza na mahesabu. Jibu la uhakika ni kugawana mali kwa mali iliyochimbwa iwe ujazo wa mitungi gesi, vitofali vya dhahabu, mapipa ya mafuta, karai za almasi isiyochongwa .. kila mmoja akauze mwenyewe ..

1 July 2023
Gaborone, Botswana

1692796721104.png



Nchi ya Botswana imepata jibu kuwa mfano Tanzania mkataba wa mgodi na mwekezaji wagawane vitofali vya dhahabu na serikali badala ya kusubiri faida ya kwenye balance sheet.

Mgawanyo wa vitofali au almasi au tanzanite inaipa uhuru Tanzania kuhifadhi kitu halisi na kukiuza kwa thamani ya uhakika bila makando kando ya kusubiri mwekezaji asafirishe madini yote nje na mwisho wa siku akuambie faida ni ndogo kama ripoti yake ya katika mahesabu ya mwaka yanavyoonesha .

1 July 2023
Gaborone, Botswana,

Botswana na De Beers Zasaini Mkataba wa Kuendeleza Ushirikiano Tajiri wa Almasi

Chini ya makubaliano mapya ya uchimbaji madini, Botswana itapata mara moja asilimia 30 ya madini ghafi ya almasi yaliyochimbwa, kutoka asilimia 25, na itapanda hadi asilimia 50 ndani ya muongo mmoja, De Beers na maafisa wa serikali walisema.

Afisa wa serikali ya Botswana na mtendaji mkuu wa De Beers, muungano wa kimataifa wa almasi, walitia saini mikataba ya muda siku ya Jumamosi ili kuendeleza ubia wenye faida, wa miongo kadhaa wa uchimbaji madini ya almasi ambao ulionekana kuvunjika katika miezi ya hivi karibuni.

Dakika chache kabla ya tarehe ya mwisho ya usiku wa manane siku ya Ijumaa, pande zote zilitangaza kwamba baada ya mazungumzo ya miaka mingi, walikuwa wamekubaliana kimsingi juu ya mpango wa kuunda upya ushirikiano ambao unaipatia De Beers sehemu kubwa ya almasi yake na serikali ya Botswana sehemu kubwa zaidi ya mapato yake.

Maelezo ya mpango huo bado yanashughulikiwa, maafisa wa serikali na De Beers walisema. Lakini inashughulikia moja ya matatizo makubwa ya serikali ya Botswana, kuhusu mgao wa almasi ambayo inapokea katika ubia wake wa uchimbaji madini na De Beers.

Chini ya makubaliano ya zamani, Botswana ilipokea asilimia 25 ya mawe machafu yaliyochimbwa, huku De Beers ilichukua mengine. Sasa, Botswana itapata mgao wa asilimia 30 mara moja, na hiyo itapanda hadi asilimia 50 ndani ya muongo mmoja, De Beers na maafisa wa serikali walisema.

Kampuni ya,De Beers ilisema katika taarifa yake kwamba imekubali kuwekeza kiasi cha dola milioni 825 katika kipindi cha miaka 10 ijayo kusaidia kuendeleza uchumi wa Botswana. Makubaliano hayo pia yanajumuisha kuanzisha chuo nchini Botswana ambacho kitafundisha wenyeji ujuzi katika biashara ya almasi, maafisa wa serikali walisema

Source : The New York Times
 
25 August 2023
Lindi, Tanzania

Maonesho ya Madini Lindi yafana


View: https://m.youtube.com/watch?v=8bw2mrNGV9w

Source : Times Majira


Mkoa watajwa wa Tatu kwa wingi wa Madini nchini.
Ruangwa - Lindi


Maonesho ya Kwanza ya Madini na Fursa za Uwekezaji yanayoendelea mkoani Lindi, Tanzania yametajwa kuufungua mkoa huo kiuchumi na kuongeza fursa mbalimbali za uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko Agosti 25, 2023 mkoani Lindi, alipotembelea maonesho hayo na kuzungumza na wadau wa Sekta ya Madini wanaoshiriki maonesho hayo.

Dkt. Biteko amesema, maonesho yamewakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini kutoka nchi zaidi ya 10 waliofika kujifunza na kuangalia fursa za uwekezaji katika mkoa huo.

Mbali na Tanzania wageni wengine walioshiriki wametoka katika Nchi ya China, Marekani, Canada, Australia, Japan, Srilanka na Finland.

"Naomba kutoa wito kwa wananchi wa Lindi kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wanaofika kuwekeza nchini ili kwa pamoja tunufaike na uchimbaji wa rasilimali madini," amesema Dkt. Biteko.

Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amesisitiza kuwa shughuli na biashara katika Sekta ya Madini zifanywe na Watanzania wenye sifa ili wazawa wanufaike na uchumi wa madini na hatimaye kuongeza mchango wa Sekta katika Pato la Taifa.

Naye, Meneja wa Huduma ya Jiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Solomon Maswi akitoa wasilisho katika Maonesho ya Kwanza ya Madini na Fursa za Uwekezaji Wilayani Ruangwa Mkoa wa Lindi. Maswi amesema GST imechora ramani ya Jiolojia ya Mkoa wa Lindi na nchi nzima kuonesha fursa mbalimbali zilizopo kuanzia ngazi ya mkoa na nchi nzima ambayo inapatikana kwa lugha ya Kiswahili.

Aidha, Maswi amesema kuwa GST imefanya Utafiti wa awali na kuja na mapendekezo ya Madini Mkakati 31 na Madini Muhimu 11 kwa nchi nzima ambapo Mkoa wa Lindi una Madini Mkakati sita ambayo ni Chuma, Kinywe, Dhahabu, Shaba, Magnesite, pamoja na madini muhimu manne ambayo ni Jasi, Chokaa, Chumvi na Chuma.

Vile vile, Mtendaji Mkuu wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse amesema, shirika hilo limetelekeza majukumu mbalimbali hususan katika ujenzi wa kiwanda kikubwa cha kusafisha chumvi ili kupata soko la uhakika mkoani Lindi.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi Mkoa wa Lindi Mhandisi Iddi Msikozi amesema lengo la maonesho ya Madini Lindi ni kuonesha dunia kwamba Tanzania kuwa imebarikiwa kuwa rasilimali Madini za kutosha na wadau wamekaribishwa kuwekeza katika mkoa huo ili Watanzania wanufaike na uchumi wa madini.

Wengine waliotoa mada katika maonesho ni pamoja na Kamishna wa Madini Dkt. AbdulRahman Mwanga, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Hassan Ngoma, Mjiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dkt. Japhet Fungo, Mjiolojia kutoka Chuo Kikuu cha Yunnan Prof. Xuance Wang na Katibu Mkuu Umoja wa Wachimbaji wa Madini (UVIWAMA) Castory Mtonga
Source : STAMICO | News
 

Ruangwa, Lindi Tanzania​

[Latest Updates]: Waziri Mkuu Majaliwa Aagiza Kuzalisha Chumvi yenye Ubora​

Tarehe : Aug. 27, 2023, 7:03 a.m.

1693145944835.png

Ahitimisha Maonesho ya Kwanza ya Madini na Fursa za Uwekezaji Mkoani Lindi
#Aelekeza Halmashauri nchini kuandaa Mpango wa Uchimbaji madini endelevu
Ruangwa - Lindi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza wazalishaji wa Madini ya Chumvi nchini kuzalisha kwa wingi na kwa ubora ili kukidhi viwango vinavyohitajika katika soko la ndani na nje.

Amesema hayo, wakati akifunga Maonesho ya Kwanza ya Madini na Fursa za Uwekezaji mkoani Lindi Agosti 26, 2023 Wilayani Ruangwa ambayo yalihusisha zaidi ya washiriki 140 kutoka ndani na nje ya nchi.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema, lengo la maonesho hayo ni kutangaza fursa za Uwekezaji katika Sekta ya Madini zilizopo mkoani humo.

Aidha, ameitaka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kuendelea kufanya tafiti mbalimbali za madini ili kugundua maeneo mapya ya uchimbaji Madini kwa lengo la kuongeza wigo na fursa za ajira kwa Watanzania.

Sambamba na hayo, Majaliwa amesisitiza uongezaji thamani madini kufanyika nchini kwa lengo la kuzalisha bidhaa zenye ubora zinatokana na Madini na kuongeza ajira kwa Watanzania hivyo kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.

Pia, Waziri Mkuu Majaliwa ameziagiza Halmashauri zote nchini kuandaa mpango wa uchimbaji endelevu, salama na utunzaji wa mazingira.

Kwa upande wake, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya Uwekezaji na kuwataka wananchi wa Mkoa wa Lindi hususan Wilaya ya Ruangwa kutunza rasilimali zilizopo Mkoani humo ikiwemo ardhi.

Pia, Dkt Kikwete ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi kuchangamkia fursa za Uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini Mkoani Lindi ili kushiriki kikamilifu katika Uchumi wa Madini.

Naye, Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amemshukuru Waziri Mkuu Majaliwa kwa kukubali kuwa mgeni rasmi katika kilele cha Maonesho hayo Mkoani Lindi ambapo amesema Wizara ya Madini itaendelea kusikiliza maelekezo yanayotolewa na viongozi ili kuipeleka sekta madini mbele.

Dkt. Biteko amesema Sekta ya Madini inaongoza kwa kuliingizia Taifa fedha za kigeni kutokana na kuuza bidhaa za Madini.
Katika Maonesho hayo zaidi ya wadau 140 kutoka Serikalini na sekta binafsi walishiriki katika viwanja vya Kilimahewa Wilaya ya Ruangwa, Mkoani Lindi kuanzia Agosti 21 hadi 26, 2023.

Source : tovuti ya madini.go.tz
 

[Latest News]: Uingereza Kuibeba Bendera ya Tanzania Kutangaza Fursa za Uwekezaji, Biashara zilizopo Sekta ya Madini​

Tarehe : Aug. , 2023,

1693146490655.png

#Madini mkakati yapewa kipaumbele na Uingereza
#Wafanyabiashara wa madini Uingereza kushiriki Jukwaa la Kimataifa Sekta ya Madini mwezi Oktoba 2023.

Wizara ya Madini na Serikali ya Uingereza kupitia Ubalozi wake nchini zimekutana leo Agosti 1, 2023 katika ofisi za Wizara Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma ili kujadiliana kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini na kuzitangaza kwa wawekezaji kutoka nchini humo.

Aidha, mkutano huo umejadili uwezekano wa nchi zote mbili kuwa na ushirikiano katika maeneo mbalimbali katika Sekta ya Madini.

Akizungumza katika kikao hicho, kiongozi wa Ujumbe wa Serikali ya Uingereza ambaye pia ni Mkurugenzi wa Nchi Kitengo cha Biashara nchini Bi. Anna-Maria Mbwette na ujumbe wake alipokutana na kuzungumza wa wataalam wa Wizara ya Madini kuhusu fursa mbalimbali za uwekezaji katika sekta ya madini nchini ikiwemo uendelezaji wachimbaji wadogo.

Kupitia majadiliano hayo, Serikali ya Tanzania na Uingereza zimejadili uwezekano wa kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali katika Sekta ya Madini, hususani shughuli za uongezaji thamani madini; uendelezaji wachimbaji wadogo; uchimbaji; uchenjuaji na uongezaji thamani na biashara ya madini hususani madini mkakati na kujenga uwezo wa Taasisi chini ya Wizara katika usimamizi wa Sekta.

‘’Mambo haya tuliyozungumza ni muhimu sana katika kuendelea kuimarisha mahusiano na katika biashara na uwekezaji wa shughuli za madini kati ya Tanzania na Uingereza.

Tunaahidi kushirikiana na Wizara ya Madini na Serikali kwa ujumla katika kutangaza fursa mbalimbali zilizopo hapa nchini,’’ amesema Mbwette.

Ameongeza kuwa, nchi ya Uingereza imevutiwa na vipaumbele vya Wizara ya Madini hususan katika uendelezaji wa madini muhimu na madini mkakati nchini.

Amesema Serikali ya nchi hiyo itaweka nguvu katika kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza katika madini hayo ya mkakati kama vile madini ya nickel, Cobalt, graphite, lithium, niobium, Rare Earth Elements (REE)

Vile vile, amesisitiza kuwa, Uingereza inatarajia kuweka nguvu katika kuwajengea uwezo wadau wa Sekta ya Madini kuweza kushiriki ipasavyo katika uchumi wa madini.

Pia ubalozi utashirikiana na Tanzania kwa kutumia uzoefu wao katika maandalizi ya kuandaa Mpango Mkakati wa miaka 10 katika Wizara ya Madini.

Katika hatua nyingine, Mbwette amesisitiza kuwa, Uingereza itaweka nguvu kubwa katika kutangaza Jukwaa la Kimataifa katika Sekta ya Madini linalotarajiwa kufanyika Oktoba 25 na 26, 2023 jijini Dar es Salaam ili wafanyabishara na wadau wa Sekta ya Madini waweze kufahamu na kushiriki kwa wingi katika kongamano hilo ili kuendeleza mahusiano ya biashara na uwekezaji.

Naye, Kaimu Kamishna wa Madini Maruvuko Msechu amesema ushirikiano huo kati ya Tanzania na Uingereza utainufaisha nchi yetu kwa kuongeza uzalishaji na hatimaye mchango wa sekta ya madini kwenye pato la Taifa. Amesema vipaumbele hivyo ni muhimu sana kwa sasa hususan duniani kwenye uhitaji mkubwa wa madini hayo muhimu.

Kwa upande wake, Kamishna Msaidizi Uendelezaji Migodi Terence Ngole amesema kuwa lengo la mazungumzo hayo ni kuanzisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili, kuangalia namna kampuni za nchini Uingereza zinavyoweza kunufaika na fursa mbalimbali za uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini.

Aidha, Kamishna Ngole ameeleza kwamba pamoja na fursa nyingi zilizopo katika Sekta ya Madini nchini, hata hivyo majadiliano hayo yalijikita zaidi katika maeneo ya uongezaji thamani madini, uendelelezaji wachimbaji wadogo, kujenga uwezo kwa wataalamu kwenye weledi mbalimbali zinazohitajika katika Sekta (capacity building in relevant Mining Sector skills and technologies) na Utafutaji, uchimbaji na uchenjuaji na uongezaji thamani na biashara ya madini kwa ujumla yakiwemo madini ya mkakati (critical minerals development strategy).

Katika kikao hicho, Uingereza imeikaribisha Wizara ya Madini katika maandalizi ya Mkutano wa uwekezaji (Investment Forum) utakaofanyika Oktoba 16, 2023 nchini Uingereza. Mkutano huo utawakutanisha wawekezaji na wadau mbalimbali katika Sekta ya mbalimbali ikiwemo Madini duniani
 
Back
Top Bottom