Sahihi kabisa matumizi yake ni kwa ajili ya kunawia uso kama huna mpango wa kuoga.. Uso hauhitaji hata robo lita
Sasa wengi wafanyacho kwenye sink anafungulia maji yanamwagika bila kutumia huku anapiga mswaki kisha ananawa uso huku maji bado yanatiririka.. Yaani kunawa uso pekee kunaweza kutumia lita nzima wakati glass moja tu ingetosha
Nilichogundua hawa watu weupe ni wachungu sana kwenye matumizi ya pesa zao, na hicho kinawatofautisha na sisi ambao hatujali namna tunavyotumia kipato chetu hata kama tumekipata kwa shida.
Wao akiba ni kipaumbele kuwawezesha kesho yao na mwezi ujao kiwa na uhakika wa hela, chakula, maji, n.k.
Ushuhuda, kuna dada mmoja aliolewa na hawa watu weupe akaenda kuishi huko kwao weeh kilimramba...!!
Anakwambia kuoga anaambiwa bili ya maji itakuja kubwa kama sio mchafu huna lazima ya kuoga, wakampa wet tissue ajifute maeneo muhimu 😅.
Na akioga pamoja na baridi maji asiweke yamoto sana aweke medium karibu na baridi heater inakula umeme...!
Vyombo wanatumia disposable kusave maji ya kuoshea vyombo, umeme wa dishwasher na muda wa kusimama kupanga vyombo...!!!!
Saa ingine wanaagiza kusave umeme wa kupikapika au wanapika mara moja halafu wanakuwa wanapasha moto viporo alooo!!!
Unaweza kuona ni uwendawazimu, ila wamelelewa hivyo ili wafikie malengo na hatimaye wakijakupanda mlima kilimanjaro na kuogelea bichi za zanzibar tunaamini wanamahela mengi tuwaibie au tuwalipishe bei kubwa.
Kumbe wanajibana matumizi ili wafikie malengo.
Sijui niko nje ya mada....🤪