Ingawa sijawaona Pele na Maradona, ila nina uhakika hawamfikii Gaucho

Ingawa sijawaona Pele na Maradona, ila nina uhakika hawamfikii Gaucho

kwa show game gaucho yuko poa lakini hajadumu kwenye game bana..
Jay Jay Okocha alikuwa na show-game na kuleta impact kwenye timu na amedumu kwa kipindi kirefu, sema tu ni mwafrika ndio maana historia yake imefutika kwa kipindi kifupi

To me okocha alikuwa na kiwango kikubwa sana cha kucheza na mpira, kiukweli alikuwa na madhara kidogo sana ukifananisha uwezo wake wa kuchezea mpira, hilo ndio lilimwangusha okocha, nina bahati nimemwona vizuri sana na baadaye gaucho pia. hili la kwamba kabaniwa kwa sababu ni mwafrika nafikiri mkuu umekariri mesemo ambayo hujaifanyia kazi kiufasaa. kama wazungu kuchukia wanachukia rangi nyeusi kusifiwa na si uafrika au unini sijui wao ishu ni rangi nyeusi, ndo shida. hebu tujikumbushe wachezaji wengine kipindi cha okocha au hata kabla yake.

  • george opong weah alichukua uchezaji bora wa ulaya na baadaye wa dunia, vipi hapo?



  • afu unacheza timu gani, ligi yenye ufundi kiasi gani, timu inashiriki mashindano gani, usisahau hizo fact, ni muhim sana, okocha kacheza, ufaransa, ujerumani na si munich, bayer leverkusen wala welder bremen wala borussia, toka hapo karudi wingereza sio man u, wala chelsea, wala aresernal, wala liverpool.
  • kashiriki uefa akiwa na psg, na alifanya nini, na kipindi hicho psg ya kiwango gani, lazima ujiulize
  • kutokana na madhara ya kawaida kabisa ya okocha timu kubwa hazikupigana vikumbo kumchukua, na kuna transfer 3 okocha katolewa free.



  • okocha alikuwa mzuri sana kuchezea mpira ila alikuwa na uwezo wa kawida katika kuorganize timu kama kiungo mshambuliaji, kuwatafuta maforwad, hilo ni tatizo kubwa sana kwa mafanikio ya timu, tatizo hilo hilo liliwahi kumkuta hata rivaldo, wabrazil kwa ujanja wakamshauri abadilishe namba, ahamie namba kumi uwanjani, hivyo akawa anasaidia tu midfielders but not complete, ndipo akwa na madhara mno na success ikaja.
  • kingine mkuu, kuna wachezaji walicheza muda mbaya yaani okocha na henry wenye rangi nyeusi kwa weupe tucheki kama nao walibaguliwa, mf, hawa hapa dell piero, nyota yake ilizibwa na wear na de lima, the victims wengine walikuwa, baggio alizimwa na romario, shearer, mc manaman, david ginora, george hagi (mromania), zamorano, salasi, simeone inzaghi, mdogo wa philipo, diego simeone, raul, redondo, pavel nedved, mandieta n.k. Usisahau hawa ni wachezaji waliokuwa hatari sana ila muda wao ulimezwa na magwiji ambao kulikuwa hakuna ubishi walikuwa comp[lete players kwa ufundi na madhara. hivyo hao na uzungu wao wote walipanga foleni kwa waamerika na kina zizzou na figo.

leo seacrh mtandao wowote tafuta mchawi wa mipira ya ajabu web iwe ya wazungu, waafrika au waarabu, okocha utamkuta pale.

Mkuu pia uwe na data kamili gaucho kwenye ground ana miaka 16, wakati okocha toka scratch kadumu miaka 9, hapo gaucho namhesabia alipoanza kuvuma team ya taifa 1999 after world cup, akacheza vizuri sana akafanikisha kuchukua copper amerika, ukijumlisha gaucho toka anachukuwa uchezaji bora wa dunia under 21, utapata miaka kama 19.
Gaucho, alikuwa na madhara na unono, vyote pamoja. hiyo ilimpandisha mno, kama vp mkuu mimi ndo burudani yangu ni pm, nikumpe video za zaidi ya wachezaji 25 waliotamba na wanaotamba, utang'amua nisemayo mkuu.

kuhusu mleta maada, kuwa makini wazungu hawfurahii mtu mweusi kama mkaa yaani pele aendelee kuwa mfalme wa soka, wangependa awe mweupe hata kama anatoka afrika, lakini waliomwona ni wengi tu bado wapo, na bado wanaona na leo, wanasema bado, labda tufunge ukrasa wa karne hii tusubiri, maradona na pele walikuwa very very granted.

BINAFSI NLICHOONA KUPITIA VIDEO ZA PELE NA MARADONA WALIKUWA COMPLETE PLAYERS. YAANI;
  • Wafungaji
  • Wapiga chenga
  • Wapiga faulo, yaani kaka wanafunga mno
  • wanaamua matokeo
  • hawakabiki

Kumbuka mimi ni wa kizazi cha leo sina sababu ya kuwatetea tetea pasipo sababu, walikuwa granted, ni kama jamaa alivyosema kuhusu okocha, tunapoambiwa vitu vyake ilikuwa magic, kuna mtu atakuja miaka 245, atona watu wakibetua mipira kwa nyuma kiajabu afu atwambie huyo okocha hamna kitu, afu sisi tunasema tumewaona wote, okocha ni kiboko yeye akabisha.

NI PM NKUPE KITU CHA OKOCHA HAMNA ANAYEPIGA, NI CHA AJABU, YEYE ANAFANYIWA INTERVIEW ANAELEZA ANAVYOFANYA, NA ANARUDIA KAMA MARA NNE UWANJANI WANAPOMUHOJI AFU WANAONYESHA ANAVYOFANYA KWENYE MECHI.
 
Wakati Dihno the Saint anashangaza ulimwengu na Mbingu huyo overrated Messi wenu alikuwa benchi anajifunza Wema,Utukufu na Utakatifu wa Dihno kwenye Soka. Dihno kachukua makombe na tuzo zote kwenye soka,huyo Messi wako WC Cup na Copa America anaiona kwenye tv tuu.

Umetema madini
Messi World Cup ataiona kwenye tv tu
 
Lete wewe stats za Gaucho kwa klabu na taifa, mimi naleta za Messi.

Statistics za St. Gaucho kwa makombe aliyochukua akiwa na Timu ya Taifa ya Brazil ni kama ifuatavyo...

* Fifa World Cup 2002,South Korea and Japan

* Fifa Confiderations Cup 2005,Germany

* Copa America 1999,Paraguay

* Fifa U17,Egypt

* South America U17 1997,Paraguay.

Haya naomba uniletee statistics za Messi za Timu ya Taifa kwanza then tuje kwa Clubs.
 
Statistics za St. Gaucho kwa makombe aliyochukua akiwa na Timu ya Taifa ya Brazil ni kama ifuatavyo...

* Fifa World Cup 2002,South Korea and Japan

* Fifa Confiderations Cup 2005,Germany

* Copa America 1999,Paraguay

* Fifa U17,Egypt

* South America U17 1997,Paraguay.

Haya naomba uniletee statistics za Messi za Timu ya Taifa kwanza then tuje kwa Clubs.


heh heh heh akirudi bila bla bla huyo mi najing'ata mgongoni
 
Yaani nyie hovyo kabisa, kwahiyo mchezaji akianza kushuka kiwango chake basi Milan ndo sehemu ya kwenda kutulia si ndivyo? Poleni sana.
Mpo nafasi ya 11, piganeni mpeleke timu top 2, acheni hayo mambo ya miaka ya nyuma. Leo uko wapi?


hah hah hah hapa ndo utagundua utamu wa Soka...
kwenye Soka huwezi kuwa mbabe siku zote.
kuna muda utaanguka kisha utaamka na kujikung'uta na kusimama sawa...

labda umgeni wa Soka na ndo maana unashangaa hali hii kwa Buluda
 
Ni kweli hajafika, Messi kaweka Record za kutikisa ulimwengu, Gaucho kaweka zipi?


pia utagundua kuwa Dinho Magic mambo mengi saana kayapata kwa kuyatolea jasho...tofauti na huyo eskimo anaringia tuzo ambazo wapiga kura wenyewe hata Aleyn ndugu yangu huwajui...kwi kwi kwi Dinho hebu anzisha Dini uje umuokoe Aleyn maana anaelekea pabaya
 
Dinho alishushwa Na Mungu kuja kuuchezea mpira

hao wengine wamejifunza tu huku huku duniani


na ndio maana hata goli lake la kwanza kufunga akiwa Barca pasi aliipokea toka kwa Nabii wa mwisho wa Soka...

forza Dinho
 
na ndio maana hata goli lake la kwanza kufunga akiwa Barca pasi aliipokea toka kwa Nabii wa mwisho wa Soka...

forza Dinho

Ronaldinho ni kama yule nabii aliyetumwa kuandaa mapito ya Nabii Mkuu, hiyo pasi ilikuwa ni kuandaa tu mapito ya mchezaji ambaye Dinho mwenyewe amekiri kwamba anacheza katika kiwango cha juu sana ambacho akina Dinho hawajawahi kukiona kabla katika maisha yao yote ya soka!
 
Hujakosea, wachezaji wengi wamekuja na kupotea lakini ukiwalinganisha walipokuwa kwenye peak zao toka nami nimeanza kuangalia mpira hakuna kama Ronaldinho, alikuwa na vitu adimu sana ambavyo havionekani popote.

Ronaldinho alipokuwa kwenye kiwango chake cha juu huwezi kumlinganisha kabisa na Ronaldo wala Messi.

Nakubaliana na wewe.
 
Kwani huyo Pep ndio nani mpaka maneno yake yawe ndio sheria au amri?si huyu huyu Pep kwa ubaguzi wake akamfanyia St Dihno fitna mpaka akaondoka Barca sasa leo unategemea aseme ukweli kwa kumpa sifa stahiki kuhusu St Gaucho

Dinho alikuwa ameisha, asingeweza kupata namba
 
Ronaldinho ni kama yule nabii aliyetumwa kuandaa mapito ya Nabii Mkuu, hiyo pasi ilikuwa ni kuandaa tu mapito ya mchezaji ambaye Dinho mwenyewe amekiri kwamba anacheza katika kiwango cha juu sana ambacho akina Dinho hawajawahi kukiona kabla katika maisha yao yote ya soka!

Acha maneno yako ya Mkoleni wewe,huyo Nesi wako hajamfikia St. Gaucho hata nusu ya uwezo wake na isitoshe huyo Nesi wako anacheza mpira kipindi ambacho hakuna mabeki wa ukweli na wenye roho ngumu bali kuna mapazia tuu. Kingine na kama Barca haimbebi kwa kuwa na wachezaji talented wengi kwanini timu ya Taifa hafanyi vizuri?
 
Dinho alikuwa ameisha, asingeweza kupata namba

Ameisha kwa vigezo gani,unakumbuka kuwa huyu huyu Pep alimfanyia fitna pia Eto'o kwa vigezo hivyo hivyo unavyosema wewe cha ''kuisha'' akaondoka akaenda Inter Milan chini ya Morihno na akachukua UEFA kubwa?
 
Back
Top Bottom