Ingekuwaje tungekuwa tunakufa, ila Macho yanaona yanayoendelea, bado tuna uwezo wa Kuongea na Mikono kufanya Kazi?

Ingekuwaje tungekuwa tunakufa, ila Macho yanaona yanayoendelea, bado tuna uwezo wa Kuongea na Mikono kufanya Kazi?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kwa ninavyowajua Marehemu wengine ( hasa Kisaikolojia ) walipokuwa Kamili ( Hai na Kinguvu pia ) kuna uwezekano Waombolezaji tungeumbuliwa nao, tungewambwa ( tungezabwa Vibao nao ) na kuna taratibu zingine tunazowafanyia wangezikataa Mubashara tu kwani wangeona ni Unafiki mtupu na Sanifu tu Kwao.

Ni bahati nzuri tu na yawezekana Baba Muumba ( Mwenyezi Mungu ) alikuwa na Makusudi yake kabisa kwamba Ukifa ( Ukifariki ) tu badi huwezi Kujitambua tena na wala huna hata uwezo wa Kufanya lolote sana sana ni kusubiria tu Ukazikwe zako ili uanze Kuoza na kuwa Mbolea kwa Mazao yetu / Ardhi zetu.
 
Gentamcyne unatuumiza kichwa kwenye masuala yasiyo na Majibu hayo Ni matumizi mabaya ya akili
 
Mambo magumu

...hayo ndio tunaita kuparalize!

Macho yanaona lakini mwili aufanyi kazi
 
Kuna mzee amekufa mwezi huu mwanzoni na aliwaambia wanae akifa azikwe shambani kwake. Aisee ile shida tuliyoipata nilijiuliza kwani anaona? Msipotekeleza atawafuata?
Sometimes tunawasumbua marehem, hata mzee angekuwa na uwezo angeomba apumzike tu.
 
Back
Top Bottom