Ingelikuwaje Kama Tanganyika Ingelipata Uhuru Wake Kwa Kuchelewa Kuliko Majirani Zake, Tuseme 2005?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Ukiacha Msumbiji ambayo ilipata uhuru wake mwaka 1975, nchi zingine zote zinazoizunguka "Tanganyika" zilipewa uhuru miaka ya 1960's.

Sasa chukulia Tanganyika ingeendelea kutawaliwa na Wakoloni hadi mwaka 2005, hali ingekuwaje?

Kwamba, labda Ujerumani ingeitawala tokea mwaka 1891 hadi 1975, na kisha Mwingereza kutoka mwaka 1975 hadi 2005 ndiyo Watanganyika wakakabidhiwa nchi yao, hali ingekuwaje?

Majirani zetu wangekuwa wanatuonaje kwa sasa? Wangekuwa wanatuzodoa au wangekuwa wanatuonea wivu?

Tanganyika ingefanana na South Africa au ingechoka kuzidi nchi iliyo choka mbaya Afrika Mashariki kwa sasa?

Watanganyika wangekuwa wanasemaje, "Wazungu wametuchelewesha sana", au, "Bora Mzungu katucheleweshea uhuru?"

Huu ni mfano tu wenye lengo la kufikirisha! Don't take it seriously, please!!!
 
Tufanye 2022 ndio tungepata uhuru ingekua poa sana mana toka 60 hakuna tulichofanya
Usibeze mkuu, kuna mengi yaliyofanyika. Nakutajia machache, alau mawili:

1. Kuukimbiza mwenge nchi nzima kila mwaka, isipokuwa mwaka 2020 pekee, nafikiri kwa sababu ya Corona

2. Kuwapatia viongozi mav8 mazuri kuzidi hadhi ya mauasafiri ya baadhi ya mawaziri wa barani ulaya.
 
Kivipi mkuu? Dadavua kidogo tuipate picha iliyomo kichwani mwako.

wakoloni walileta maendeleo kwenye nchi walizozitawala zaidi hapa Africa kuliko baada ya uhuru. Nchi nyingi waliziacha zikiwa katika mazingira mazuri ya kiuchumi na miaka 10 tu baada ya wao kuondoka zikawa zipo kwenye hali mbaya sana.
Moja ya upuuzi wa nchi nyingi za kiafrika ni kuleta ule ujamaa uchwara baada ya uhuru ambao ulizirejesha nyuma kimaendeleo nchi nyingi sana Africa.
Kwa uhakika kabisa tungeendelea kutawaliwa mpaka 2000's nchi yetu ingelikuwa ina miji ya kibabe, viwanda vya uhakika, elimu yenye ubora, miundo mbinu ya kileo pamoja na mifumo ya maisha inayoeleweka kabisa.
Ubaya wa Wakoloni una overatiwa sana, hao wazee wetu waliokuwa wanalia na wakoloni wangelikutana na huu mziki wa CCM wao wenyewe wangelitia akili. hayo maovu yao tunaojaribu kakaririshwa karibu ya yote tumekuwa tukikutana nayo kwa madikteta wetu wa kiafrika na zaidi ya hayo kabisa.
 
Sijui kwa nini! Nimetokea kuuchukia sana ujamaa. Sijui nani ataweza kunishawishi niamini kuwa ulikuwa mzuri.

Nauona ujamaa kama ulikuwa ni kiwanda cha umaskini, uvivu, kubweteka, unafiki, na kuua ubunifu.
 
wakoloni walileta maendeleo kwenye nchi walizozitawala zaidi hapa Africa kuliko baada ya uhuru. Nchi nyingi waliziacha zikiwa katika mazingira mazuri ya kiuchumi na miaka 10 tu baada ya wao kuondoka zikawa zipo kwenye hali mbaya sana.
Moja ya upuuzi wa nchi nyingi za kiafrika ni kuleta ule ujamaa uchwara baada ya uhuru ambao ulizirejesha nyuma kimaendeleo nchi nyingi sana Africa.
Kwa uhakika kabisa tungeendelea kutawaliwa mpaka 2000's nchi yetu ingelikuwa ina miji ya kibabe, viwanda vya uhakika, elimu yenye ubora, miundo mbinu ya kileo pamoja na mifumo ya maisha inayoeleweka kabisa.
Ubaya wa Wakoloni una overatiwa sana, hao wazee wetu waliokuwa wanalia na wakoloni wangelikutana na huu mziki wa CCM wao wenyewe wangelitia akili. hayo maovu yao tunaojaribu kakaririshwa karibu ya yote tumekuwa tukikutana nayo kwa madikteta wetu wa kiafrika na zaidi ya hayo kabisa.
Pamoja na mapungufu yao, Wakoloni walihimiza shule. Hata mzee Sumaye, kama isingelikuwa jitihada za Wakoloni, inawezekana asingesoma na hivyo asingeingia kwenye Historia ya kuwa Waziri mkuu wa Tanzania kwa miaka kumi mfululizo.

Pamoja na kuonekana wakatili, walikuwa wanawazoesha watu kuwa wachapa kazi. Kwenye Historia tukifundishwa kuwa walikuwa wakiwalazimisha watu kufanya kazi, jambo ambalo sikubaliani nalo kwa sasa. Nisamehewe tu, huenda hisia zangu zisiwe sahihi. Inawezekana mababu zetu walikuwa wakilalamika kufanyishwa kazi kwa sababu, pengine, walikuwa wavivu.

Wewe si unaona hata utendaji kazi wa Waswahili na Wazungu ulivyo? Mswahili asiposimamiwa, inawezekana muda wa kazi akaishia kwenye kijiwe cha kahawa, ingawa si wote wako hivyo.

Hata miundombinu waliyoijenga, japo miaka mingi ilishapita, mingi bado inafanya kazi mpaka sasa. Kuna reli, bandari, shule, mashamba, migodi, n.k.

Mpaka miaka ya tisini, kulikuwa na barabara amabyo inadaiwa ilijengwa na wakoloni lakini haikuwa imerekebishwa mpaka miaka hiyo. Walioishi Arusha miaka hiyo wanaifahamu barabara ya Arusha Moshi kupitia Moshono, Chekereni... ilikuwa imejengwa kwa mawe, na inadaiwa ilijengwa na Wajerumani, na mpaka miaka hiyo ya tisini, ingawa haikuwa imefanyiwa marekebisho makubwa, ilikuwa ingali ikipitika vizuri tu.

Vipi ikulu ya Dar Es Salaam?
 
Pamoja na kuonekana wakatili, walikuwa wanawazoesha watu kuwa wachapa kazi. Kwenye Historia tukifundishwa kuwa walikuwa wakiwalazimisha watu kufanya kazi, jambo ambalo sikubaliani nalo kwa sasa. Nisamehewe tu, huenda hisia zangu zisiwe sahihi. Inawezekana mababu zetu walikuwa wakilalamika kufanyishwa kazi kwa sababu, pengine, walikuwa wavivu.

Wewe si unaona hata utendaji kazi wa Waswahili na Wazungu ulivyo? Mswahili asiposimamiwa, inawezekana muda wa kazi akaishia kwenye kijiwe cha kahawa, ingawa si wote wako hivyo.

Upo sahihi kwa asilimia 100%

Watu weusi uvivu ndio nature yetu. Bila ya usimamizi makini hakuna kitakachokwenda. Wewe tizama huduma katika taasisi za serikali mfano halisi.
 
Bora mkoloni Mweupe kuliko mkoloni Mweusi mpaka sasa bado tunasaidiwa na wakoloni weupe kujenga matundu ya vyoo uku viongozi wetu wakiwaza uchaguzi kuliko kutatua changamoto za wananchi.

"Nadhani kipindi Mungu anamuumba mwafrika Kuna kitu hakumpa ndio maana tunaitwa bara la kiza*
 
wakoloni walileta maendeleo kwenye nchi walizozitawala zaidi hapa Africa kuliko baada ya uhuru. Nchi nyingi waliziacha zikiwa katika mazingira mazuri ya kiuchumi na miaka 10 tu baada ya wao kuondoka zikawa zipo kwenye hali mbaya sana...
Viongozi walileta ujamaa na mfumo wa chama kimoja lengo kuu likiwa kutawala kama Mungu maana walipenda madaraka kuliko kutatua changamoto za nchi.
 
Ukiacha Msumbiji ambayo ilipata uhuru wake mwaka 1975, nchi zingine zote zinazoizunguka "Tanganyika" zilipewa uhuru miaka ya 1960's.

Sasa chukulia Tanganyika ingeendelea kutawaliwa na Wakoloni hadi mwaka 2005, hali ingekuwaje?

Kwamba, labda Ujerumani ingeitawala tokea mwaka 1891 hadi 1975, na kisha Mwingereza kutoka mwaka 1975 hadi 2005 ndiyo Watanganyika wakakabidhiwa nchi yao, hali ingekuwaje?

Majirani zetu wangekuwa wanatuonaje kwa sasa? Wangekuwa wanatuzodoa au wangekuwa wanatuonea wivu?

Tanganyika ingefanana na South Africa au ingechoka kuzidi nchi iliyo choka mbaya Afrika Mashariki kwa sasa?

Watanganyika wangekuwa wanasemaje, "Wazungu wametuchelewesha sana", au, "Bora Mzungu katucheleweshea uhuru?"

Huu ni mfano tu wenye lengo la kufikirisha! Don't take it seriously, please!!!
Tungekuwa zaidi ya Africa Kusini kimaendeleo.
 
Nami nahisi hivyo.

Inawezekana tungekuwa na VIWANDA vya magari, simu, tv, n.k.

Tungekuwa na VIWANDA vya silaha nzito nzito, pengine hata za nuklia.

Inawezekana kusingekiwepo na nyumba za nyasi wala kaya zisizo na umeme na maji safi.

Inawezekana raia kutoka nchi nyingi za Kiafrika na nje ya Afrika wangekuwa wanajitahidi kuzamia ili nao waionje "asali" iliyosheheni Tanzania.

Inawezekana wazee na watu wasio na ajira wangelikuwa wanapewa allowance maalum ya kujikimu kimaisha.

Inawezekana Tanzania ingekuwa kama Dubai.

Inawezekana Tanzania ingekuwa ni miongoni mwa donors countries dunianai

Inawezekana, Tanzania ingekuwa ni Ulaya au Marekeni ya Afrika.

Inawezekana...!!!
 
Back
Top Bottom