Ingelikuwaje Kama Tanganyika Ingelipata Uhuru Wake Kwa Kuchelewa Kuliko Majirani Zake, Tuseme 2005?

Honk Kong ilikabidhiwa kwa China mwaka 1997 kutoka kwa UK.
Ni sasa tu China imepanda kiuchumi, lakini miaka ya 90 Hong Kong ilikuwa ina uchumi mkubwa kuliko China yote
Unaona sasa! Hivi ni kiherehere gani kiliwasukuma wazee wetu wawafukuze Wazungu mapema? Si wangewaacha alau kidogo?
 
Mwingereza mpaka 2005s aisee timu zetu zingekuwa nazo zinacheza epl na kina manyuu fc
 
Mkuu nashukuru nimepata kitu hapa[emoji1363]
 
Ila kwa kiasi kikubwa tungekuwa tumeendelea x10 ya sasa hv
Kuna baadhi ya miundombinu imejengwa miaka hiyo mpaka sasa hv inatumika
Reli ya kati: Dar - Kigoma, ilijengwa na Mjerumani 1905 - 1914 lakini bado inatumika mpaka sasa.

Ikulu ya Dar Es Salaam ilijengwa na nani? Si Wakoloni?
 
Ndio akili hizi mlizobaki nazo.

Utegemezi ni akili ya wafuasi wa kitumwa na baadhi ya wajinga wasiopenda uzalendo.

Hao wakolon wangekuwepo kwa muda mrefu basi haya yangetokea[emoji116]
[emoji117] ubaguzi wa rangi,
[emoji117] ukabila
[emoji117] ardhi kumilikiwa na wachache haswa walowezi
[emoji117]nchi kumilikiwa kwa % na jamii za walowezi ambao si wazawa bali wahuni/wana wa wakoloni
[emoji117] mauwaji+ ubaguzi wa raia
[emoji117]tamaduni kudhoofika
[emoji117]idadi ya watu isingekuwa kubwa sababu ya kushinikizwa kufuata sheria za kizungu kuhusu mambo ya uzazi na baadhi ya watu haswa wazawa wangekufa sana ktk kesi za kusingiziwa, ubaguzi, kulinda maslahi, na si ajabu wengi humu msingekuwepo.

Hakuna maendeleo yanayoletwa na mgeni cha msingi jengeni vya kwenu acheni kutegemea misaada ya kijinga, kwan wao nchi zao aliwajengea nani?

Kwa mindset za baadhi ya wajinga humu hawakutakiwa kuwepo JF
 
Wengi mnaoamini ktk kutawaliwa kwanini msihamie huko ktk hizo nchi zenye wakoloni?

Mmekazana kuwakumbatia wakoloni mnayajua madhara ya ukolon lkn? Wengi humu ni vitoto hamujui banu zenu waliathiriwa vip mpaka kuwatimu hao wahuni, ni vile historia zinaficha sana lkn kiukwel UTU+Ubinadamu haukuwepo kwa mtu mweusi zaidi ya kufanywa mnyama asiye na thamani, waliogombea uhuru si wajinga, leo hii wapumbavu wachache mliokulia ktk amani mnakuja kuubeza uhuru sababu ya Tamaa zenu za kijinga.

Waulizeni South afrika nchi yao lkn kuna mahala hawana uhuru napo, maamuzi ya nchi yanaamuliwa na hao washenz waliojimilikisha nchi kwa kificho cha mapandikizi ya viongozi.

Hao kenya wenyewe pamoja na kuwakumbatia wazungu ni nini wamepata?

Amkeni nyie wapumbavu, jengeni nchi yenu mpambane mpate vya kwenu.
 
Acha nichukue moja tu, idadi ya watu!

Unasema kwamba watu wangelazimishwa kutumia uzazi wa mpango? Kuna mahali wanakofanya hivyo zaidi ya China?

Kwa Sasa Tanzania ina watu milioni 60's na Denmark milioni 5, kipi ambacho Tanzania yenye idadi kubwa ya watu inanufaika kuizidi Denmark yenye watu wachache?

Unajua, ongezeko la watu linapaswa kwenda sambaba na ukuaji wa uchumi?

Kipi Bora, kuwa na watoto wawili unaomudu kuwapatia huduma zote mtoto anazopaswa kupatiwa au kuwa na timu ya watoto, labda watoto kumi, ambao wengine wanatembea peku kwa kushindwa kuwanunulia viatu?

Kipi bora, nchi kuwa na watu wachache lakini walioelimika au kuwa na idadi kubwa lakini wengi wao ni wajinga mithili ya nyumbu?

Tuliambiwa tufyatue kwa kuwa Elimu ni bure. Ni sawa. Tuliambiwa kama tuna chakula cha kutosha, tufyatue kadri tuwezavyo Ni sawa.

Hata hivyo, chakula si hitaji pekee la mtoto, anahitaji, pamojja na mambo mengine, malezi bora.

Ikiwa utakuwa na timu kubwa ya watoto, unaweza usiweze kuwatimizia wote mahitaji yao, hasa ya Kisaikolojia.

Kuzaa watoto wengi bila maandalizi ya kuwahudumia ni vibaya. Ni kuwasababishia mateso wasiyostahili.

Ingekuwa ni mamlaka yangu, ningepiga marufuku watu kuzaa watoto wasiokuwa na uwezo wa kuwahudumia.
 
Utawala wa mkoloni ulikua bora zaidi, tulipewa uhuru katika kipindi ambacho hatukua tayali kua huru, ndio maana hadi kesho Tutaendelea kutembeza bakuli hadi kwa nchi ambazo tumezishinda rasilimali kupita kiasi
 
Naongezea zaidi:

1. Kilimo cha jembe la mkono kungekuwa Historia nchini Tanzania

2. Vyama vya Siasa vingekuwa vinapikezana kuongoza dola

3. Kusingekuwepo na TASAF

4. Pengine, Tanzania nayo ingekuwa miongoni mwa G40

5. Kusingetokea kile kilichojulikana kama vita na wahujumu uchumi.
 
Hadi muda huu ungekuwa mke wa mkoloni. Acha kutetea upumbavu kijana.
 
Tungekuwa wale wale. Muda usingetubalisha kitu. Sisi ni wale wale na mambo yetu ni yale yale. Afrika Kusini waliopata uhuru juzi wana nini zaidi ya mateso? Sudan ya Kusini walipata uhuru jana. Wana nini zaidi ya matatizo matupu?
 
Baada ya WW2 mjerumani alikuja kutawala Tanzania na akajenga TAZARA? Aisee huu uzi umejaa wapumbavu wengi sana.
 
Ukisoma huu uzi ndo utagundua kwamba vita dhidi ya ushoga ni ngumu sana. Hakuna namna unayoweza kukataa kwamba vijana wanaosema bora tungeendelea kutawaliwa na mkoloni hawana chembechembe za ushoga. Afrika Kusini waliotawaliwa hadi miaka ya 90 wana nini kwa sasa? Namanisha maisha ya weusi wa SA na sio majengo wala barabara zao. Inasikitisha kuona watu wengi hapa ni madebe matupu na hawajui historia ya nchi yao wala madhara ya ukoloni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…