Dr Restart
JF-Expert Member
- Jul 15, 2021
- 4,949
- 24,046
Amani iwe juu yenu wana wa Mungu.
Nina miezi kama mitatu sasa, nyimbo za wahusika zimekuwa zikijirudia katika orodha ya nyimbo ninazosikiliza mara nyingi.
Papi Clever na Dorcas ni wanandoa, Merci Pianist ni mtaalam wa kupiga kinanda kwa kiwango kikubwa sana.
Mimi ni muumini wa nyimbo za taratibu kidogo na zenye mapigo ya vinanda vya kufurahisha. Napenda mno upigaji wa guitar na piano inavyochanganya, aaagh sijajaliwa tu uwezo wa kuipiga. Ninaomba Mungu nistaatu mapema, nikajifunze kuipiga na kumuimbia Mungu. Zinanipeleka mawinguni na kuhisi nipo juu, nikiimba na kusifu pamoja na Makerubi.
Hawa waimbaji kutoka Rwanda wana nyimbo nyingi sana. Mwaka huu 2023, walidondosha Collection ya nyimbo za Wokovu yenye jumla ya nyimbo 16 za Kiswahili.
1. Mwokozi Wetu
2. Roho Yangu
3. Yesu ni Furaha Yangu
4. Fanyia Mungu kazi
5. Ee Mungu mwenye kweli
6. Ee Mungu mwenye haki
7. Msifuni msifuni
8. Nilikwenda mbali sana
9. Pendo la Mungu
10. Yesu Ovukiy'i Bethlehemu
11. Uzima ninao
12. Matendo ya Mungu
13.We Mutima urira
14. Yanyonjiyemo
15. Kisima cha Lehi
16. Siku moja ya mavuno..
Nyimbo zote ni nzuri mno. Ila mimi iliyonibamba zaidi ni Mwokozi wetu
Nyimbo zao nyingine ninazozipenda ni Tu Watu huru
Nyingine inayonibamba na kunivuta katika Wokovu ni ameniweka huru kweli
Hakika ninavutiwa sana na nyimbo zao. Sichoki kuzisikiliza, wala haziumizi masikio. Ile midundo na mapigo ya vifaa ndo vinaniacha katika uwepo mkubwa sana.
Je, wewe unawafahamu? Ingia YouTube, watafute kwa jina lao. Papi Clever & Dorcas.
Karibu utuambie, ni wimbo upi umekubamba?