20 February 2021
Denver, Colorado USA
Ndege moja ya abiria ya shirika la ndege la United Airlines aina ya Boeing 777 mruko namba 328 toka kiwanja cha ndege cha mji wa Dever kwenda Honolulu injini yake moja ililipuka ikiwa angani kiasi cha futi 13,000 (ft) na kusambaza mabaki yake ktk kitongoji cha Broomfield.
Ilikuwa na abiria 231 na wafanyakazi 10, abiria waliokuwamo angani ndani ya ndege hiyo waliweza kuchukua picha za video. Unaweza kutazama video iliyochukuliwa na abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo angani huku wakiwa wamekumbwa na taharuki pia tahayari (awe) kubwa, wakati ndege hiyo ikirudi kwa dharura kwenda kutua ktk kiwanja cha ndege cha karibu.
Video kwa hisani source: schengen story news
Mamlaka ya Usalama wa Anga nchini Marekani (FAA) zimewataka wananchi kutokuchukua au kuhamisha mabaki ya injini ya ndege yaliyotapakaa ardhini ili waweze kuendesha uchunguzi vizuri wa tukio hilo.
Updated February 20, 2021 at 3:31 pm
Picha ya idara ya Polisi ya Broomfield ktk Twitter, ikionesha sehemu ya mabaki ya injini ya ndege ktk kitongoji cha Broomfield. Polisi pia imewasihi wenyeji kutohamisha mabaki ili yasaidie Mamlaka za Usalama wa Anga yaani FAA na NTSB kufanya uchunguzi.
Ndege hiyo ilifanikiwa kutumia injini yake moja iliyokuwa nzima kumalizia safari ya kurejea kwa dharura kutua ktk kiwanja cha Denver.
Habari kwa hisani kubwa ya gazeti la The Seattle Times Boeing 777 lands safely in Colorado after engine failure rains debris on suburb
........................................................................
Muonekano wa ndege aina ya Boeing 777