Injinia Hersi Said tunataka kuona 'Walk the Talk' yako katika Kuiendeleza Yanga SC yako na siyo 'Talk the Walk' tulioizoea mkiomba Kura

Injinia Hersi Said tunataka kuona 'Walk the Talk' yako katika Kuiendeleza Yanga SC yako na siyo 'Talk the Walk' tulioizoea mkiomba Kura

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Uko vizuri sana kwenye Kuzungumza, Kujisifia Kwingi na kuegemea zaidi katika 'Engineering Theories' zako ila sina uhakika kama utaweza hata kufanya 25% ya Uliyojimwambafai nayo katika Interview yako na Sports Extra ya Clouds FM jana Usiku.

Kitu pekee ambacho Injinia Hersi Said umekisahau ni kwamba hivi Vilabu Vikubwa Viwili vya Yanga SC yako na Simba SC yangu vimejaa Uswahili, Majungu, Wivu na Fitna kiasi kwamba 90% ya Mashabiki wake wanategemea Vilabu hivi Viwalishe na viwaweke hapa Mjini badala ya Wao Kuvisaidia na vipige Maendeleo kama ya Azam FC.

Nakuhakikishia leo hii hii Injinia Hersi Said kuwa pamoja na kwamba utakuwa Rais wa Yanga SC kuanzia leo ila unaenda kupata Upinzani mkubwa wa ndani na tegemea pia Kurogwa sana kwani Waliokuwa wakiitegemea Yanga SC yako Kimaslahi wanajua kuwa ukiingia unaenda Kuwazibia Mirija yao ya Kiuchumi ( Maslahi ) hivyo kamwe hawatokuacha Salama na nakushauri Sali mno.

Nilishangaa zaidi Kukuona Msomi kama Wewe Injinia Hersi Said unahangaika kuutaka Uongozi ndani ya Yanga SC huku ukijua kuwa kwa Asili ya Klabu hiyo na hata yangu ya Simba SC wao Wimbo wa Maendeleo Kwao huwa haupendwi na Wengi waliokuwa na Nia njema kama yako hawakufika Mbali na hata leo hii hawana kabisa hamu na Vilabu hivi kwa mfano Mbunge wa Kinondoni Tarimba Abbas.

Injinia Hersi Said ulishajiuliza ni kwanini Mwenzako wa Simba SC Mwekezaji Mohammed Dewji mpaka sasa hajafikia hata tu 15% ya kile alichokuwa amekipanga ndani ya Klabu yangu pendwa ya Simba SC kiasi kwamba anataka hata Kuachana nayo ila anashindwa tu Kujitoa mazima kwani kuna Vipengele vya Kisheria ameshaviingia na vinambana hivyo analazimika Kuvumilia huku Moyoni akiumia na pengine hata Kuingia Hasara Kubwa tu.

Kwa Msomi wa Kiwango Kikubwa kukubali kuwa Kiongozi wa juu wa Vilabu hivi vya Simba SC na Yanga SC ni Kujidhalilisha na Kuiabisha Taaluma yako na hata kupoteza pia na muda wako kwani Vilabu vinavyotakiwa Kuongozwa na Wendawazimu au Wavuta Bange kwani haingii Akilini vyote vina Umri wa miaka zaidi ya 80 ila vimezidiwa na Azam FC na hata Gwambina FC kwa hatua muhimu na za awali za Kimaendeleo.

Kila la Kheri katika Urais Yanga SC!!!!!
 
MINOCYCLINE mbona tunawasemea Yanga, tuachanane nao tuangaike na Simba yetu.

Billioni 25 + Bililini 20 = 85

Inawezekana Boss ameweka Shilingi 85 kwenye Akaunti ya Club badala ya Bilioni.
 
Ila kati ya vitu vyote; binafsi sifurahishwi kabisa kuona timu kubwa kama Yanga, mpaka leo zaidi ya miaka 80 tangu ilipo anzishwa! Eti haina viwanja vyake vilivyo kamilika vya mazoezi na mechi.

Natamani viongozi wapya watafanya kitu baada ya haya mabadiliko.

Azam wameweza! Gwambina wameweza! Ruvu shooting, Mtibwa sugar, Namungo, Geita Gold! Hizi zote ni timu ndogo tu, lakini zimeweza kumiliki viwanja vyao! Kwa nini Yanga kila siku ni siasa tu?
 
Na Simba nao tumeweza
 
Back
Top Bottom