Injinia Hersi ulishaharibu tangu mwanzo na sasa hatuna namna zaidi ya kuipongeza Simba kwa ubingwa

Injinia Hersi ulishaharibu tangu mwanzo na sasa hatuna namna zaidi ya kuipongeza Simba kwa ubingwa

Nimetukanwa matusi mengi sana humu kwa kupingana na uamuzi wa kumfukuza kazi Gamondi, na nilisema kabisa kwa uamuzi ule hatutovuka hatua ya makundi ligi ya mabingwa kila mmoja ameona.

Siku hizi hata sifuatilii timu inacheza lini na wapi, na kiukweli itatuchukua muda sana kurudi katika mstari tuliokuwa hapo kabla.
Gamondi ilikuwa laZima aondoke alianza kuharibu dressing room
Wachezaji anawapekeka bar
Anabagua wachezaji wasio rafiki zake hawapi nafasi, anawap nafasi walevi wenzio
Kumwachia bench Kibwana akiwa fit na kuchezesha Nkane kama mlinzi kulia
 
Nimekwambia sajili zote ni kama kamali ni timu Gani Huwa inapatia sajili zote
Ukiona mchezaji kasajili ujue ni pata potea.

Kuhusu Ramovic kuondoka
Huyo ilikuwa laZima aondoke wale wana mkataba pesa ikija wanakaa na waajiri wake wanarejea mkataba
Kwaiyo wewe unataka Ramovic akatae million 100 abaki Yanga analipwa million 36?
Hiyo haiwezakani hata Mimi mwanachama wa Yanga nikipata hiyo fursa natembea
Unadhani Nabi hakuwa na ofa msimu ule wa mwisho kwake?
Alikuwa nazo tena tatu lakini akachagua amalizie project yake mpaka mwishoni mwa msimu ili aondoke au yeye hapendi pesa kama wewe? Hapendi utajiri? Think mzee

Alichagua kusubiri mpaka game ya mwisho pale Tanga mkwakwani final FA ndiyo tukashangaa ghafla anatuaga kumbe sasa baada ya kumaliza project yake ndiyo akaenda sasa

Hao belouzidad wanatafuta immediate coach na amini sio muda atafukuzwa huko na hapo ndiyo maisha ya katanga tanga yataaanza malipo makubwa yanaendana na CV yako Ramovic ana CV gani?

Tuwe tunafikiria sio kila kitu ni pesa unaangalia na future ya career yako ili kuendelea kujitengenezea circle ya pesa zaidi .

Tuwe tunapenda soka sio ushabiki tu
 
Gamondi ilikuwa laZima aondoke alianza kuharibu dressing room
Wachezaji anawapekeka bar
Anabagua wachezaji wasio rafiki zake hawapi nafasi, anawap nafasi walevi wenzio
Kumwachia bench Kibwana akiwa fit na kuchezesha Nkane kama mlinzi kulia
Madhaifu yake yalikuwepo hatukatai ila wewe naona bado hujatuelewa vizuri.

Sasa wamemtimua sawa lakini kwa muda huu alikuwa a right man for champions league sasa tumepata aibu ya kutolewa na wachovu wale kina MC algers!

Kibaya zaidi huyo aliyemshikia kijiti naye ndiyo hivyo hata valentine hajafika kasepa!

Inakuwa safari ya chizi kwenda umbali mrefu kurudi na makopo
 
Unadhani Nabi hakuwa na ofa msimu ule wa mwisho kwake?
Alikuwa nazo tena tatu lakini akachagua amalizie project yake mpaka mwishoni mwa msimu ili aondoke au yeye hapendi pesa kama wewe? Hapendi utajiri? Think mzee

Alichagua kusubiri mpaka game ya mwisho pale Tanga mkwakwani final FA ndiyo tukashangaa ghafla anatuaga kumbe sasa baada ya kumaliza project yake ndiyo akaenda sasa

Hao belouzidad wanatafuta immediate coach na amini sio muda atafukuzwa huko na hapo ndiyo maisha ya katanga tanga yataaanza malipo makubwa yanaendana na CV yako Ramovic ana CV gani?

Tuwe tunafikiria sio kila kitu ni pesa unaangalia na future ya career yako ili kuendelea kujitengenezea circle ya pesa zaidi .

Tuwe tunapenda soka sio ushabiki tu
Sasa hapo Eng Hersi kakosea nini? Coach kawaita mezani viongozi akafuata vigezo vya kuvunja mkataba na kavunja mkataba
Nani na Ramovic hawafanani kila mtu ana vipaumbele vyake kwenye maisha
 
Madhaifu yake yalikuwepo hatukatai ila wewe naona bado hujatuelewa vizuri.

Sasa wamemtimua sawa lakini kwa muda huu alikuwa a right man for champions league sasa tumepata aibu ya kutolewa na wachovu wale kina MC algers!

Kibaya zaidi huyo aliyemshikia kijiti naye ndiyo hivyo hata valentine hajafika kasepa!

Inakuwa safari ya chizi kwenda umbali mrefu kurudi na makopo
Kwa timu ilivokuwa chini ya Gamondi hata robo final isingeenda na usiseme kuwa MC Alger ni timu dhaifu
 
Kuhusu Ubingwa ni mpaka 2030 wengine waendelee kujenga timu.
Ata asiwepo kocha yoyote, Yanga Bingwa, anaye hitajika ni msimamizi wa mazoezi tu, Timu tayari ipo.
Anayehitajika ni msimamizi wa mechi tu yani Kayoko na wenzake wa aina hiyo.
 
Naona unaongea kishabiki wakati leo tumeangalia upande wa pili wa shillingi nisije hapa kushangalia wewe kama nani?

Naongelea usajili mzuri sio majina makubwa wewe unaongelea majina makubwa hao walikuwa tayari mastaa kabla ya kuja man utd sasa casemiro kutumika kote kule Madrid si alienda kula pension tu?

Kwani max alipatikanaje? Sio jina kubwa sana congo ila ni prominent player sio big name hata chama ni big name ila anaishia benchi

Soma hapo juu utanielewa vizuri inashindikana nini kusubiri amalize project yake aliyoianza msimu ukiisha aende?

Hii inafaida kwake kupata pesa lakini hasara kwa yanga na kwake pia Ramovic atakuwa short term plan coach kama.kishingo anavyohangaika sasa hivi

Hata alipokuwepo hakukuwa na coach effect yoyote hakuwa kocha mzuri na kazubaa machi nyingi tu team inashinda kwa uwezo binafsi

MC algers walituthibitishia hilo
Hapa umeongea kiufundi ww utopolo kiben ten...nakuunga mkono
 
Nimetukanwa matusi mengi sana humu kwa kupingana na uamuzi wa kumfukuza kazi Gamondi, na nilisema kabisa kwa uamuzi ule hatutovuka hatua ya makundi ligi ya mabingwa kila mmoja ameona.

Siku hizi hata sifuatilii timu inacheza lini na wapi, na kiukweli itatuchukua muda sana kurudi katika mstari tuliokuwa hapo kabla.
Wewe mshabiki plastic tu.Kabla ya Gamondi timu yenu ilikuwa haishindi?Angekuwa bonge la kocha asingeenda Libya bali timu kubwa za Afrika.
Timu yenu ikishinda unakaa kimya ikipata changamoto unakuja na ngonjera za Gamondi.
 
I salute you kinsmen.

Kwa kweli kwa sisi tulioona mbali tangu muda tulipinga sana kufukuzwa kwa Gamondi. Mkatuona mazuzu kwamba tunamkubali sana noo. Sisi ni yanga sio Gamondi wala Hersi.

Tatizo lilianzia pale alipofukuzwa yule mzee na team ikiwa imeshaclick kabisa kisa kupoteza game chache zile tatu.

Matokeo yake akaletwa Ramovic ambaye hana uzoefu wowote kimataifa yaani alikuja yanga kutafuta experience.

Nyie wenyewe mnaona kabisa kama tungeendelea na Gamondi mwenye experience kubwa kimataifa hakika lile kundi tungeongoza mapema sana kwa kishindo.

Gamondi licha ya madhaifu yake yule mzee alikuwa anajua sana kuzicheza mechi strategically very accurately!

Reference
Game zote mbili na mamelodi sundown fc kama ingekuwa ndiyo said Ramovic basi mpaka leo tungekuwa tunaaibika kimataifa kwa kupewa kichapo kizito sana cha Mabao zaidi ya 5.

Ila mzee akasema no hold my beer, bila pacome, Aucho, Yao na bado yanga wakakiwasha mpaka huko huko bondeni bila mbeleko wa refa ambapo Yanga angepita nusu mapema tu.

Pia game na azam ambayo yanga walipoteza huku tukiwa nusu kumi tu ila azam waliomba mpira uishe mapema tu kwa moto waliokuwa wanapelekewa.

Turudi mwanzo:
Hersi sikuhizi amekuwa mtu wa kukurupuka sana sana. Alianza kuleta saini za kitapeli tapeli na bei rahisi sijui ili iweje. Konkoni, okrah,skudu, na pimbi wengine halafu hapo hapo kocha akifeli anatupiwa mzigo tena ..!

Naambiwa Hersi na makamu wake Araphat kwa muda kidogo haziivi sikuhizi. Araphat hakumtaka Gamondi na Hersi alitaka abaki kwahiyo mwisho makamu akamshinda nguvu BOSS wake!

Mbona mwanzo hersi alikuwa analeta vyuma sana m? Why sikuhizi analeta wachezaji urojo sana?

Wanaume wa ukweli
Fiston mayele
Djuma shaman
Yanick bangala
Aziz ki
Joyce lomalisa mutambala (marcelo)

Sasa hawa aliwapataje?
Abadilike maana sikuhizi amekuwa busy sana kuwatumikia waarabu huko ofisini kwake ACA. Anasahau huku klabu yake , anasahau sisi yanga ndiyo tulimpa platform hiyo aliyonayo

Bila yanga angebaki kuwa mfanyakazi na lapdog wa GSM tu ila yanga imemfanya awe alivyo leo asituchezee..! Gamondi alikubali kubaki hata kwa mshahara ule ambao Ramovic amekataa na kufata pesa za waarabu!

KINGINE.
Matumaini ya kuchukua kombe NBC yamezidi kuwa finyu sana hasa ukizingatia tayari kocha mpya kaja ina maana tunaanza upya tena kule kule kwa Ramovich kupewa muda akae sawa!

Kwanini simba tusiwapongeze mapema simba kwa kuchukua NBC mapema tu?
Wapo na consistency kubwa sana na wapo Well focused why wasichukue kombe?

Tulimfukuza kocha mwenye CV kubwa kimataifa na akatuonyesha kwa vitendo(Gamondi) ila tukaleta mwanafunzi aje kujifunza naye akatuonesha uanafunzi wake kimataifa(Ramovic) na hatimaye kasepa kafata pesa means hakuwa na mapenzi na yanga kabisa

Sasa tusitegemee makubwa msimu huu labda msimu ujao tena..

NYONGEZA.
Hawa wachezaji wafuatao waachwe kwani hawana mchango tena na uwezo umeshuka sana bila kuwachekea

Kennedy musonda(Guede arudishwe)
Guede alikuwa clinical finisher mzuri sana sana ni vile tu mpira wetu upo kihuni alikuja kati kati ya ligi dirisha dogo na akaanza direct kufunga! Wakati tangu ligi ianze hii musonda yupo yupo tu! Aaachwe passport kumchekea.

Aziz andambwile
Huyu amekuwa na msaada kidogo sana anaishia hospital tu kila siku
Anazidiwa hata kina sheikhan Ibrahim wanaonesha kitu wakipewa muda sheikhan ni kiungo profitable sana anacheza namba 8 na 10 kwa ufasaha sana

Mashuti ya yapo, nguvu miguuni zipo, kimo kizuri anacho, jicho la pasi analo apewe muda.

Its Pancho
Pumba tupu.
 
Hii Ngoma ili lia sana mka jisahau dadeki Yanga ndo basi tena
 
Back
Top Bottom