Injinia Soma hiyoo: Simba yasajili striker kutoka Brazil

Injinia Soma hiyoo: Simba yasajili striker kutoka Brazil

KLABU ALIYOTOKA MCHEZAJI MPYA WA SIMBA
Mabingwa wa Tanzania na wanarobofainali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC, kama kawaida wameshusha silaha nyingine muda ule ule wa siku zote.
Huyu ni Wilker Henrique da Silva kutoka Brazil. Lakini watu wengi wamechanganya kuhusu klabu anayotoka. Hapa chini ni ufafanuzi wake.
Da Silva ni mzaliwa wa mji wa Franca kwenye jimbo la Sao Paulo nchini Brazil. Alizaliwa Oktoba 26, 1995.
Amekuja Simba akitokea klabu Bragantino do Para, iliyopo kwenye mji wa Braganca ndani ya jimbo la Para, lililopo Kaskazini mwa Brazil, likipitiwa na mto maarufu wa Amazon.
Kwenye mji huu kuna timu mbili zinazotumia jina la mji wenyewe. Kuna Bragantino Clube do Pará ambayo ndiyo aliyotoka Da Silva. Kwa kifupi huitwa Bragantino PA.
Halafu kuna Clube Atletico Bragantino ambayo kwa kifupi huitwa C.A Bragantino.
BRAGANTINO YA DA SILVA
Klabu ya Da Silva, Bragantino Clube do Pará, inashiriki ligi daraja la nne ya Brazil ambayo hufahamika kama Campeonato Brasileiro Série D.
Pia inashiriki ligi kuu ya jimbo la Para inayoitwa Campeonato Paraense na katika msimu wa 2018 ilimaliza katika nafasi ya 3.
BRAGANTINO NYINGINE
Ile timu nyingine inayoitwa Clube Atletico Bragantino au kwa kifupi C.A Bragantino, inashiriki ligi daraja la pili inayoitwa Campeonato Brasileiro Série B.
Ilipanda mwaka 2018 kutoka ligi daraja la tatu inayoitwa Campeonato Brasileiro Série C ambako ilimaliza katika nafasi ya 4.
Hii ndiyo tofauti ya vilabu hivi viwili ambavyo vinatoka mji mmoja wa Braganca kwenye jimbo la Para nchini Brazil.
Minnlijua utatoa statistics za magoli na assist za jamaa ktk misimu yote alocheza kabla ya kuja simba
 
Naskia brazil nzima imesimama kwa usajili wa huyu jamaa

Hongeren watan

Pogba atawafaa sana , naskia man u hawamtaki
Pogba hakuna haja ya kumsajili mana kuna wachezaji kibao tu wanaocheza kama yeye. Ni kama Bwalya tu hakusajiliwa kwa sababu pale simba washambuliaji wengi wanacheza kama yeye tu
 
Haswa
Simba namba 4 na 5 Ni tatizo kubwa na wanatakiwa wapate wachezaji wazoefu wa michuano ya klabu bingwa africa lakini wasioienda umri Kama Pascal Wawa, hizo nafasi sio zakuleta wabrazil
As Vita 5 Simba 0
Al Alhy 5 Simba 0
Simba inatakiwa beki zitakazosaidia kufungwa goli chache ugenini
 
Ndio hivyo Mkuu hiyo ndio gharama yake sasa sijajua kama Simba watakua wametoa hiyo hiyoo!
Kama watakua wametoa hy basi wehu ,hy pesa si unapata mchezaji mzuri tu ,tena aliyepo AFCON anayecheza ligi ya Africa yenye ushindani
 
Umenikumbusha M-Brazil wa Yanga, aliyeitwa Jaja. Aliondoka bila kuaga.

Hakuna mchezaji wa Kibrazil anayeweza kupambania namba hapa Bongo. Kuwaacha Kotei na Niyonzima kwa Mbrazil ni sawa na kubeti kuwa Stars itabeba kombe la Afrika kule Misri.

Vv
Huyo niyonzima ni furahisha jukwaa tu.
Miaka miwili ana goli moja.
Niyonzima hana madhara kwa timu pinzani.
 
Back
Top Bottom