Injinia Soma hiyoo: Simba yasajili striker kutoka Brazil

Kama watakua wametoa hy basi wehu ,hy pesa si unapata mchezaji mzuri tu ,tena aliyepo AFCON anayecheza ligi ya Africa yenye ushindani
Mkuu usikute hata jamaa yupo vizuri ngoja tusubiri ligi ianze maana wanasema wamescout kwa muda mrefu!
 
Tukubali tu kuwa mchango wa Niyonzima kwenye raundi ya pili ya ligi kuu ulikuwa mkubwa. Hata goli la pili dhidi AS Vita lililoipeleka Simba kwenye robo fainali ya CAF champions league, lilitokana na juhudi zake.

Kuwaacha Niyonzima na Kotei, Simba wanechemka, kuliko kumchukua huyo M-brazil, ni heri wangebaki hata na mmoja kati yao. Hivi huyo Miraji aliyetokea Coastal, anakwenda kuchukua nafasi ya nani?

Vv
 
Nasikia jamaa anashusha wabrazil tu kina wengine wawili wanategemea kutambulishwa next week

Ila kiukweli hawa wabrazil wananipa mashaka
Hahahaha, hayo mashaka yako hata mm ninayo Mkuu , najiuliza wote hao waliwafanyia scouting ,kwenda Brazil kuona uchezaji wao ,au scouting ya kupitia YouTube ambayo unaweza kuweka clip nzuri tu

Anyway ngoja tuone
 
Kwakuwa ametokea amerika ya kusini hatusemi ki2 😁😁 m2 mwenyewe hajulikani. Wabongo bana
 
Huyo niyonzima ni furahisha jukwaa tu.
Miaka miwili ana goli moja.
Niyonzima hana madhara kwa timu pinzani.
Amesahau goli zuri la kuwavusha Simba robo fainali ya champions league lilitengenezwa na nani eeh? Simba huenda wakajutia uamuzi wa kuwaacha Niyonzima na Kotei.
 
Mchezajii wa kimataifa anakosaje kuwa kwnye first eleven ya timu ?
Naheshimu maamuzi ya kocha na benchi la ufundi,
Kotea anataka pesa ambayo Simba haiko tayari kumlipa
 
Mbrazil akija Bongo Kuna walakini. .Ulaya wanababaikiwa sana
 
Straika Simba ashangaa usajili wa Msudan

mwanaspoti.co.tz
Jun 22, 2019 3:00 PM

SIMBA imesajili wachezaji wawili wa kigeni, Mbrazil Wilker Henrique da Silva ambaye ni mshambuliaji na beki Msudan Sharaf Eldin Shiboub.
Usajili huo ni mpya lakini umemshangaza mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel 'Batgol' ambaye amesema uongozi wa Simba unafanya usajili wake bila kufuata matakwa ya kocha Patrick Aussems.
Batgol ameonyesha kusikitishwa na madai ya kuachwa kwa kiungo Mghana, James Kotei na kusajili nyota hao ambao alidai amewafuatilia viwango vyao ni vya kawaida sana na hawastahili kucheza klabu kama Simba ambayo ina malengo makubwa.
"Unamuacha mchezaji mzuri kama Kotei, Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi, Deogratius Munishi 'Dida' unakwenda kusajili Wasudan na Wabrazil, wanatupeleka wapi, inashangaza na kufikirisha kidogo.
"Hata kama hawana nidhamu pengine kama ninavyosikia lakini je kazi yao si wanafanya ama hawafanyi, sidhani kama kuna haja ya kuangalia hilo wakati kazi zao wanafanya vizuri, huu usajili hasa wa wachezaji wa kigeni sikubaliani nao kabisa, ni wa mihemko na matakwa yao," anasema Bagtol
Mchezaji huyo alikwenda mbali kwa kusema; "Ukiangalia usajili wa Simba na Yanga, Yanga wanasajili vizuri kwa kufuata maelekezo ya kocha wao Mwinyi Zahera hata wakija kuchemka mzigo utamwangukia kocha wao na sio Simba.
"Wamesajili Beno Kakolanya ambaye ameachwa Yanga kwa utovu wa nidhamu, huyo ana tofauti gani na hao akina Niyonzima, Okwi na wengineo kwenye suala la nidhamu, nadhani ifike mahala Mohamed Dewji atumie vizuri pesa zake, zisiwasumbue kwa kukusanya tu wachezaji na kuanza upya kuitengeneza, hii itawasumbua na hawatafika mbali michuano ya ndani na nje," anaeleza.

Baadhi ya vitu[emoji115] anavyohoji jamaa hata Mimi nilihoji jana. Wana Simba wengine mnasemaje kuhusu maoni ya Emma!?
 
Kuna taarifa rasmi yoyote kutoka Simba kuhusu kuachwa kwa Niyonzima, na Kotei?kama hakuna kwanini tusisubiri taarifa rasmi then ndio tuhoji?

Kuhusu Okwi nilisikia alisema apewe muda mpaka baada ya Afcon,sasa timu itabaki kumsubiri Okwi tu bila kutafuta mbadala wake? What if kama hana nia ya kurudi tena Simba?

Wakati mwingine tunaweza kuwalaumu viongozi kumbe tatizo lipo kwa wachezaji wenyewe
 
We waacheni waokoteze wauza matikiti maji na Ma Alshabab toka Juba. Watapigwa hadi wachakae, ngoja ligi ianze ndiyo akili itawakaa sawa.
Amesahau goli zuri la kuwavusha Simba robo fainali ya champions league lilitengenezwa na nani eeh? Simba huenda wakajutia uamuzi wa kuwaacha Niyonzima na Kotei.
 
Oooh nimekuelewa ila Mazembe wako wenye miili midogo lkn wanafanya makubwa,miiili midogo iliyojengeka, mfn kalaba,mputu,Elisha,miche ,isama
Ila km MNA timu ya kufanya scouting ni jambo jema , mie nasubiri matokeo chanya juu ya huu usajiri wa mwaka huu
MTC | 101| [emoji769]

Kuna mtu pale TPMazembe anaitwa Meshack Elia Ukimuona Wawa ukilitaja Hilo jina kwa nguvu, Wawa atakimbia Nduki kama kuku aliyemuona mwewe
 
Hahahaha, Meshack Elia a.k.a Vitesse MTU mfupi hatari yule ,ila Jana waganda wamewadhibiti
 
Straika Simba ashangaa usajili wa Msudan

mwanaspoti.co.tz
Jun 22, 2019 3:00 PM

SIMBA imesajili wachezaji wawili wa kigeni, Mbrazil Wilker Henrique da Silva ambaye ni mshambuliaji na beki Msudan Sharaf Eldin Shiboub.
Usajili huo ni mpya lakini umemshangaza mshambuliaji wa zamani wa Simba, Emmanuel Gabriel 'Batgol' ambaye amesema uongozi wa Simba unafanya usajili wake bila kufuata matakwa ya kocha Patrick Aussems.
Batgol ameonyesha kusikitishwa na madai ya kuachwa kwa kiungo Mghana, James Kotei na kusajili nyota hao ambao alidai amewafuatilia viwango vyao ni vya kawaida sana na hawastahili kucheza klabu kama Simba ambayo ina malengo makubwa.
"Unamuacha mchezaji mzuri kama Kotei, Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi, Deogratius Munishi 'Dida' unakwenda kusajili Wasudan na Wabrazil, wanatupeleka wapi, inashangaza na kufikirisha kidogo.
"Hata kama hawana nidhamu pengine kama ninavyosikia lakini je kazi yao si wanafanya ama hawafanyi, sidhani kama kuna haja ya kuangalia hilo wakati kazi zao wanafanya vizuri, huu usajili hasa wa wachezaji wa kigeni sikubaliani nao kabisa, ni wa mihemko na matakwa yao," anasema Bagtol
Mchezaji huyo alikwenda mbali kwa kusema; "Ukiangalia usajili wa Simba na Yanga, Yanga wanasajili vizuri kwa kufuata maelekezo ya kocha wao Mwinyi Zahera hata wakija kuchemka mzigo utamwangukia kocha wao na sio Simba.
"Wamesajili Beno Kakolanya ambaye ameachwa Yanga kwa utovu wa nidhamu, huyo ana tofauti gani na hao akina Niyonzima, Okwi na wengineo kwenye suala la nidhamu, nadhani ifike mahala Mohamed Dewji atumie vizuri pesa zake, zisiwasumbue kwa kukusanya tu wachezaji na kuanza upya kuitengeneza, hii itawasumbua na hawatafika mbali michuano ya ndani na nje," anaeleza.

Baadhi ya vitu[emoji115] anavyohoji jamaa hata Mimi nilihoji jana. Wana Simba wengine mnasemaje kuhusu maoni ya Emma!?
Aliyemwambia Kotei,Okwi kaachwa ni nani? Aliyemwambia hawa wachezaji sio chaguo la kocha ni nani?
 
Back
Top Bottom