Zakayo Mtoza Ushuru
Senior Member
- Jul 31, 2024
- 149
- 154
Walau kidogo kwa Uzalendo Kafulila wengine hao ni mauza uza tu
Huyu kijana nimemwangalia sana na kumfuatilia sana utendaji wake wa kazi. Nadiriki kusema Tanzania baada ya Samia 2030 huyu kijana ana faa na ana sifa zote muhimu kama kiongozi wa nchi. Kwanini nasema hivyo naweka mambo machache hapa chini. Hata hivyo neno langu siyo sheria.
1. Ni mchapakazi sana na mzalendo mpenda nchi yake kutoka moyoni siyo ile ya kinafiki kama kwa baadhi ya wanasiasa.
2. Anapenda Haki
3. Ana utashi wa kuamua ( hizi character alikua nazo marehemu magu)
4. Ana utulivu
Jamani simjui hanijui ila mtaongezea najua wapo wanaomjua zaidi kuliko Mimi ila nikiulizwa Leo ni nani anafaa kuwa Rais wa Tanzania baada ya Rais Samia nitasema Ndugu Innocent Lugha Bashungwa ni the best candidate. Mungu amuongoze huyu kijana .