Innocent Killer (The Revenge)

STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 28

SONGA NAYO............
MBAGALA

Asp Zalimo baada ya kupewa taarifa aliwahi mpaka nyumbani kwa akina Nayrah, baada ya kufika eneo hilo alishtuka sana baada ya kuona kulikuwa kuna gari tatu ambazo zilikuwa ni nyeusi sana, alichukua tahadhari huku mkono wake ukiwa upo kwenye kiuno chake ili kama kuna hatari aweze kuishi nayo kwa namna itakavyo kuja, licha ya kupewa maagizo na IGP kwamba akifika hilo eneo kuna watu ambao atawakuta hapo lakini bado hakuwa na imani sana na usalama wa hilo eneo kwa mazingira ambayo yalikuwa hayaeleweki hata kidogo. Baada ya kusogea zaidi karibu na hilo eneo aliweza kuona mbele yake kukiwa na gari ambazo zilikuwa za bei ghali mno alishtuka sana watu hao walikuwa wamekuja kutafuta nini hapo? Hakupata jibu hivyo alisubiri kama IGP akifika hapo aweze kumuuliza kuhusu ujio wa hao watu na wao ni akina nani hapo.

“Wewe ndiye ASP Bakari Zalimo?” aliuliza mwanaume mmoja ambaye bila shaka alikuwa kiongozi wa hao wenzake ambao walikuwa kama sita hivi, ilikuwa ni tofauti na matarajio yake, kuwa afisa wa polisi alihisi labda watu hao wangemheshimu sana ila kwao alikuwa wa kawaida mno na hata aina ya uulizaji wao ulikuwa ni kana kwamba wanaongea na mtu wa kawaida sana kwao, haikumpa shaka kuhusu kuelewa jeuri ya watu wenye pesa au ambao wanakula pamoja na watu wakubwa kwa mitazamo tu ya suti za bei ambazo walikuwa wamezivaa kwenye miili yao hivyo ilimfanya kuitikia kwa kichwa swali la huyo kijana ambaye kwake alionekana kuwa mdogo sana kwake.

“Yes ndiyo mimi” baada ya kulijibu tu hilo swali haikuchukua muda mrefu sana kijana huyo aliichukua simu yake na kuiweka sikioni baada ya kuwa na uhakika kwamba ilikuwa imepokelewa upande wa pili.

“Bosi huyu ASP amefika hapa tayari”

“Ok subiri dakika moja mlango utafunguliwa hapo ila msiwachukue kabla IGP hajafika hapo” upande wa pili ulijibu

“Sawa bosi” aliitikia na kuikata simu hiyo kitu ambacho kilizidi kumpa maswali mengi sana ASP Bakari kwamba huyo bosi wao ambaye alionekana kumpa maelekezo alikuwa ni nani hasa? Aliamua kuwa mvumilivu ili aje kula mbivu na muda huo huo walisikia mlio wa simu ndani ya nyumba hiyo. Wakati kijana huyo anaipiga hiyo simu yake Kwenda kwa Jason ilimkutia akiwa kwenye pikipiki akiwa anawahi ndani ya Sinza baada ya kupewa taarifa hiyo, aliamua kumpigia simu Nayrah ambaye kweli baada ya simu hiyo kuita tu dakika moja mbele alifungua mlango huo akiwa na mama yake tena wakiwa ni wengi wa wasiwasi sana.

Walishtuka kwani nje walikuta kuna watu kadhaa mbele yao akiwa amesimama ASP ambaye kwao walikuwa wanamjua sana tu, walisikia miingurumo ya mbali ya magari hayo ambayo yalikuwa hayatoi sauti sana ila haikutosha kutowapa wasiwasi maana hawakuwa wakijua ni nani aliyekuwa amekuja na walipewa taarifa na Jason kwamba hawatakiwi kabisa kuufungua mlango kabla ya yeye kuwapigia simu ila walitulia baada ya kumuona ASP ndiye ambaye alikuwa ameongozana na watu hao.

“Shikamoo mama” aliongea kwa sauti ya upole kijana ambaye alikuwa amevaa suti moja ya bei ghali mno.

“Marahaba mwanangu mzima wewe na wenzako” Kabla hawajajibu chochote walisikia muungurumo wa gari ndani ya ghari hiyo alishuka IGP tena akiwa mwenyewe bila kuwa na mlinzi yeyote yule

“Mzee unatembeaje mwenyewe na usiku wote huu?” ASP Bakari alimuuliza mkubwa wake wa kazi huku akiwa anatoa heshima kwa mzee huyo ambaye umri wake kidogo ulikuwa umeenda lakini alikuwa anaonekana bado ni kijana kwa sababu ya kulindwa na maisha mazuri ambayo alikuwa nayo.

“Ni kawaida tu kuna muda huwa natamani nitembee mwenyewe usiku kama saivi kwa sababu natumia gari ambalo hakuna mtu anaweza akajua kwamba mtu kama mimi nipo ndani yake” alijibu huku akisogea eneo ambalo walikuwepo mama na mtoto na kunyoosha ndani moja kwa moja baada ya kusalimiana nao.

“Mimi nadhani mnanijua sana kwa sababu ni mara nyingi sana huwa naonekana kwenye vyombo vya habari” aliuliza kwa sura ya tabasamu ili kuwatoa hofu watu hao

“Ndiyo tunakufahamu sana kwa sababu ni miongoni mwa watu wa mhimu sana kwenye kuchangia usalama wa taifa letu” alijibu mama yake na Nayrah huku Nayrah yeye akili yake haikuwa hapo kabisa alijiona kama vile alikuwa yupo kwenye ulimwengu wa mbali sana

“Sasa yule kijana aliyekuja hapa ni moja ya vijana wangu ambao nawajua kwa muda mrefu sana japo yeye hahusiani kabisa na haya mambo ya kipolisi ameniomba nije hapa ili kuhakikisha usalama wenu lakini pia kufanikisha suala la nyie kuhamishwa hapa na Kwenda kuyaanza maisha mapya huko Kigamboni. Mimi tutaachania hapa hapa kwani mtaondoka na hao vijana ambao wamevaa suti hapo nje ndio waliotumwa na huyo mtu ambaye alikuja hapa hao ni vijana wake hivyo kuweni na amani na muda wowote ule mkihitaji kuwasiliana naye basi mwambieni kiongozi wa hao vijana mtampata kwa wepesi sana japo amesema kwamba kuna muda atapotea kabisa kama miezi sita hakuna ambaye ataweza kumpata popote pale na baada ya huo muda ataweza kurudi yeye mwenyewe”

“Unaweza kuniambia anaelekea wapi muda wote huo na atakuwa salama?” Nayrah alidakia na kumfanya mzee huyo atabasamu sana, kwa wasiwasi wa huyo binti alielewa kilichokuwa kinaendelea hapo

“Kumbe huyu mjinga kujifanya amepata familia mpya ni kwa sababu ya huyu mwanamke” alijiongelesha mwenyewe kimya kimya mheshimiwa IGP huku akikaa sawa ili kumjibu mrembo huyo.

“Kiukweli hata mimi amegoma kuniambia kwamba kwanini anapotea huenda labda ana kazi ya mhimu ambayo anatakiwa kuimalizia ila kuhusu usalama wake usiwe na shaka yule yupo salama kwa masaa 24 ya kila siku ambayo inaenda kwa MUNGU, halafu wewe binti kesho unatakiwa ujiandae keshokutwa unaanza kazi Mhimbili maana ndiyo maagizo ambayo emeniachia hivyo kesho nitapiga simu pale uandaliwe kila siku ikiwemo ofisi yako mengine watakuelekeza wao wenyewe” mzee huyo aliongea huku akinyanyuka ili aondoke, alisikitika sana baada ya kuona namna binti huyo alivyofurahi kusikia kwamba anaenda kuanza kazi ndani ya hospitali ya Mhimbili ambayo ndiyo hospitali kubwa zaidi ya taifa ndani ya nchi ya Tanzania na huenda ni ndoto ya kila mtu anaye somea udaktari kuweza kufanya kazi ndani ya hospitali hiyo.

“Kazi kwenu mimi kazi yangu imeishia hapa” IGP aliwaambia vijana hao ambao walimpa heshima huku yeye akiwa anaelekea kwenye gari yake, alivyo mwangalia ASP Bakari alijua wazi kijana wake huyo alikuwa ana maswali mengi sana kuhusu hayo mambo ambayo yalikuwa yanaendelea hivyo alimpa ishara na kumruhusu aingie kwenye gari hiyo ambapo ASP huyo ndiye aliyetakiwa kuendesha.

“Mzee unajua sielewi elewi mambo yanavyo enda, unajua wakati nakuja huku nimesikia kama mlio wa risasi na kukawa kimya nilitamani sana kuwahi eneo ambalo risasi zilisikika lakini nilisita sana kufanya hivyo kwa sababu ulinisisitiza napaswa sana kuwahi huku halafu tena nafika huku naona mambo yanaenda bila kueleweka yanaendaje kwani ni nini kinaendelea mzee” aliuliza huku akiwa anaingiza gari kwenye barabara isiyo rasmi ambayo ilikuwa inatosha gari moja tu pekee kupita.

“Haya ya huku hayakuhusu kabisa kwa sababu ni mambo ya kifamilia, familia inahama tu basi hakuna kingine ila kuhusu risasi kusikika, kuna mauaji yametokea huko najua na kuna vijana wa kituo cha hapo karibu nimewapigia simu waje hili eneo ili wahakikishe hakuna ambaye anagusa hilo eneo kabla mimi sijaja”

“Whaaaat? Unamaanisha nini kusema unajua maana yake unamjua muuaji?”
“Ndiyo alivyo ua yeye mwenyewe alinitumia meseji kwamba kuna miili inatakiwa kusafishwa hapa kabla ya asubuhi kufika”

“Mzee huyo mtu anatakiwa kukamatwa haraka sana kama unamfahamu nafikiri hatakiwi kufika hata asubuhi akiwa bado yupo mtaani hiyo ni dharau kubwa sana yaani mtu anahusika na mauaji halafu anakutumia taarifa kiongozi mkubwa kabisa wa jeshi la polisi nchini?”

“Achana na haya mambo nitayamaliza mwenyewe” kiongozi wake alimjibu akiwa hana hata wasiwasi utadhani waliokuwa wameuawa hawakuwa watu bali yalikuwa ni machungwa tu na wakati huo walikuwa wamefika eneo hilo ambalo kulifanyika mauaji ya kutisha sana.

“Mzee uko sawa kweli? Yaani leo wewe unaniambia mimi tumuache muuaji? Au umelewa?”
“Ok kama unataka kumtafuta nenda ni huyo ambaye alikuja kwako kuzitafuta taarifa za mauaji ya kaka yake”

“Unamaanisha Jason”

“Ndiye huyo huyo” mzee huyo alimwacha ASP huyo kwenye mshangao mzito sana maana alikuwa haamini kabisa kwa aina ya mtu ambaye alimuona mbeke yake wakati amefika kwake, alikuwa ni mtu wa kawaida mno lakini huenda yeye ndiye ambaye alichelewa sana kumjua mtu huyo. IGP alisogea eneo hilo na kuanza kuikagua miili hiyo, alimwangalia mmoja ambaye shoka ilipita kwenye shingo yake ikawa imebaki kidogo tu itoweke kabisa huku akiwa ameyafumbua macho yake alikufa vibaya sana, aliusogelea mwili mwingine wa mtu ambaye alikufa akiwa hajatoka damu hata tone tu lakini sehemu yake ya kifuani pamoja na prova ambayo alikuwa ameivaa ilibonyea kwa ndani kumaanisha kwamba ni ngumi ya moyo ilipita hapo. Hakuhangaika na waliokuwa wameuliwa kwa risasi hao kilikuwa kifo cha kawaida tu bali alisogea kwenye mwili mwingine ambao ulikuwa upo pembeni pekeyake, kifua kilikuwa kimechanwa vibaya sana mpaka mzee huyo alifumba macho na kuingiza mkono wake mfukoni na kuitoa simu yake.

“Ndo haya mambo ambayo sikutaka kabisa aje kuyafanya, sasa vipi wananchi wakiona wenzao wameanza kuuliwa kwa namna kama hii, shiiiit” alitamka mwenyewe akiwa ameukunja sana uso wake, alipiga simu Kwenda namba ya Jason lakini haikuwa ikipatikana kabisa.

“Pokea simu wewe mtoto, pokea simu” alikuwa akiongea yeye mwenyewe huku akiwa anajaribu kuweza kupiga tena simu hiyo lakini kwa wakati huo haikuwa ikipatikana kabisa. ASP Bakari alikuwa akizunguka kuangalia namna miili hiyo ilivyokuwa imefanyiwa kitu kibaya sana.

“Hapana muuaji hawezi kuwa ni yule kijana, haya mauaji ni ya mtu ambaye hana nafsi ya binadamu, hakuna mtu mwenye roho ya kawaida anaweza kuwaua binadamu wenzake namna hii hapana mzee naomba uniambie tu ukweli kuhusu muuaji halisia ni nani” maneno ya ASP huyo yalimfanya mzee huyo kumgeukia kijana wake huyo na kumwangalia kwa hasira sana.

“Wewe huyo mtu ambaye unadai kwamba hawezi kufanya hivi unamjua? Unajua nini kuhusu yeye wewe hapo mtu ambaye hata kupigana na watu kumi na watano huwezi ila mwenzako hao anaweza kuwaua kwa dakika ambazo hata tano hazifiki na unapata jeuri ya kusema sio yeye"

"Unatakiwa uwe na akili kwamba kwanini alikufuata kwako na kukwambia kwamba ukae mbali na haya mambo siyo wewe wala mimi ambaye ana jeuri ya kulikamata hilo jitu, wewe ongea ongea tu hapo kwa sababu alikuja kwako kilokole mtu ambaye hata raisi wa nchi alikuwa akizungumza naye lugha ya upole itakuwa wewe hapo ambaye unakaa huku Mbagala? Angalia sana kauli zako mdomoni usije ukanifanya nikakupiga vibaya sana usiku huu hapa".

" Sasa nisikilize kwa umakini dakika kadhaa zijazo hawa watu ambao wameenda kuichukua hiyo familia watapita hapa muda sio mrefu wale vijana wake hii miili wameshaiona tangu wanapita mara ya kwanza japo wamepita njia tofauti na hii ila nina uhakika kwamba wameiona miili hii kwa sababu nao ndo wale wale hivyo ile familia ndiyo haitakiwi kujua lolote kuhusu hili wala raia yoyote yule wala chombo chochote cha habari, futeni ushahidi wote na hiyo miili ikazikwe haraka sana kesho watu waendelee na maisha yao kama kawaida wasije wakajua kuhusu haya mambo” aliongea kwa hasira na kupanda kwenye gari yake kisha akaondoka na kumuacha ASP huyo ahisi kama alikuwa anaota, alitamani sana kumtafuta mwanaume huyo ambaye alisifiwa sana mbele yake ili amhoji yeye mwenyewe alikuwa na jeuri gani ya kuua watu hovyo namna hiyo halafu wakuu wa jeshi la polisi wanamfichia hayo maovu yake.

Ngoja tumuone huyu ASP anacho kitafuta atakipta, binafsi sehemu ya 28 naweka nukta hapa tukutane katika sehemu inayofuata.

Wasalaam

Bux the storyteller.
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 29

SONGA NAYO............
Cambridge massachusetts, John F Kennedy Street
Ni maeneo ya Jirani na kilipo chuo ambacho kilianzishwa rasmi mwaka 1636 na kinadaiwa kuwa ndicho chuo bora zaidi kwenye historia ya ulimengu huu au dunia kwa ujumla kama sio kuwa miongoni mwa vyuo bora kabisa duniani, Havard University ndicho chuo ambacho nakizungumzia hapa ambacho kinapatikana katika eneo la Cambridge Massachusetts. Mwanadada Monalisa ambaye sisi tulimjua kama mpenzi wake na Jason alikuwa akikaa mitaa ya mbali na kilipo chuo hicho lakini majira ya usiku wa manane alitoka ndani ya nyumba yake hiyo na kuingia sehemu ambayo ilikuwa na stoo, huko alitoka na piki-piki moja ya bei ghali sana ambayo ilikuwa nyeusi ikiwa inaenda sawa na nguo ambazo alikuwa amezivaa, kichwani kwake alivaa helment ambalo lilimfanya asijulikane kabisa sehemu yoyote ya mwili wake kwani hata sehemu ya mikono yake alikuwa amevaa gloves ambazo zilikuwa rangi sawa na nguo ambazo zilikuwa kwenye mwili wake.

Aliendesha pikipiki yake hiyo mpaka maeneo ya mtaa wa John F Kennedy ambao uliitwa kwa kumuasisi moja ya maraisi ambao waliwahi kuuawa nchini hapo akiwa bado kijana, safari yake ilienda kuishia kwenye moja kati ya club kubwa sana ambazo zilikuwa zinapatikana pembeni kabisa mwa mtaa huo, kwa nje lilikuwa ni jengo la kifahari sana na mlango wake ulikuwa ni moja ya milango ghali mno, kwa mtazamo wake tu ungehisi labda ilikuwa ni ofisi kubwa au jumba la tajiri mmoja akiwa anaishi na familia yake lakini kiuhalisia humo ndani kulikuwa na kila aina ya starehe, sehemu za makasino zilikuwepo humo ndani, eneo la kuchezea kamali za hatari kama kupigana risasi lakini sehemu za wanawake warembo ambao walikuwa wanatembea wakiwa uchi ili kuweza kufanya biashara za miili yao walikuwa wa kutosha hata wale matajiri wakubwa ambao walikuwa wakifika hapo kwa ajili ya kufanya biashara zao za haramu walikuwa wapo wengi sana na wa kutosha bila kuwasahau wale watu ambao huwa wanaenda hapo kuzungumza mambo yao ya siri sana, lakini maeneo kama hayo pia wale makachero na wapelelezi wa vyombo vikubwa vya dola huwa hawakosekani kwa ajili ya ukusanyaji wa taarifa ambazo zinahakikisha usalama wa nchi kwa masaa ishirini na manne.

Usingeweza kuruhusiwa kuingia ndani ya club hiyo bila kuwa na kitambulisho maalumu cha kukutambulisha kwamba wewe ulikuwa ni mwenyeji hapo, huo utaratibu haukuonekana kuwa mgeni kabisa kwa Monalisa kwa sababu baada ya kufika tu hapo alionyesha kitambulisho chake kwenye kioo mtu aliyekuwa ndani alikiscan kabla ya kuingia na kumruhusu mwanamke huyo kuweza kuingia huko ndani. Alitembea kwa madoido akiwa ndani ya suruali ambayo ilimbana sana na kulichora umbo lake ambalo kwa makadirio ya kawaida ni wanaume wachache ana ambao walikuwa wanaweza kupona kuingia kwenye 18 zake, mjongeo wake na sura yake ya chocolate ambayo ilijaa umarekani mwingi ndani yake uliwafanya wanaume ambao walikuwa wapo Jirani na hilo eneo ambalo yeye alikuwa akipita wamgeukie kwa taharuki kubwa, hata hakupagawa nao alikuwa anajijua kabisa kwamba yeye ni mzuri hakuwa na papara kuwatesa wanaume wenye tamaa ulikuwa wajibu wake.

Kuna kijana mmoja alinyanyuka na kumfuata kwa kasi mwanamke huyo ili amsimamishe akijua ni mmoja wa ambao walikuwa wanajiuza mle ndani, mkono wake haukufanikiwa kumgusa mwanamke huyo kwani huyo kijana alipokea ngumi nzito sana, alivyokuja kutahamaki alishangaa anamuona kijana mmoja akiwa kwenye suti nzito na ndiye ambaye alimpatia hicho kipigo, kitu cha ajabu mabaunsa wa humo ndani hawakuwa na msaada naye licha ya kupiga makelele ya kuhitaji msaada walichokuja kukifanya ni kumbeba na Kwenda kumtupia nje.

Kijana huyo aliyekuwa kwenye suti alimuonyesha Monalisa njia ya kushuka ngazi za chini ambako huko walikuwa wanakaa vigogo haswa na wale watu ambao walikuwa na uwezo mkubwa sana wa kifedha, kulikuwa na sehemu mbili tofauti VIP ambayo ilikuwa juu kabisa unapanda ghorofani lakini pia kulikuwa na VVIP hiyo ilikuwa chini ya ardhi na huko ndiko kulikokuwa kunafanyika michezo ya hatari sana na ya kurisk maisha kwa dakika mbili tu, huko ndiko ambako kijana huyo alimuonyesha bibie huyo njia kwamba anatakiwa Kwenda. Hakuonekana kuwa mgeni wa hayo maeneo ndiyo maana hata mwendo wake haukuashiria kabisa wasiwasi wowote ule wakati anatembea.

VVIP
Hii ilikuwa ni sehemu maalumu kwa wale watu wazito ambao hata maisha yao hayakuwa marahisi wala ya kuwaza sana kuhusu kesho kwa sababu mifuko yao ilikuwa inawaruhusu watu hao kuwepo hiyo sehemu, kuanzia upande wa juu unavyo anza kuingia hiyo sehemu kulikuwa na ulinzi mkali sana ni watu ambao walikuwa na vitambulisho tu ndio ambao walitakiwa kuwepo kwenye hiyo sehemu, baada ya kuanza kushuka ngazi hizo walifika floor ya kwanza hapo kulikuwa na vyumba vya kutosha wakati wanatembea Monalisa alisimama kwenye chumba kimoja akiwa anatazama maana mlango ulikuwa wazi kabisa, chumba kilikuwa na watu wa kutosha na watu hao walikuwa wakiila dunia kweli wanaume kwa wanawake walikuwa wapo uchi kabisa wakiyafanya mapenzi kila mwanaume hakuwa na wanawake chini ya wawili, huko hawakukumbuka neno shida wala neno MUNGU duniani, huko walikuwa kwenye dunia yao wenyewe, aliwaangalia kwa muda kisha akajisemea kwenye moyo wake.

“Kwenye maisha yangu yote napenda sana kufanya mapenzi ila mwanaume ambaye ananiweza kwenye mapenzi ni mmoja tu na nimeshachoka sana kutumika, umeenda wapi Jason” alijiongelesha mwenyewe huku akianza kumfuata yule kijana ambaye alikuwa yupo mbele yake akiwa anaongoza sehemu ya mbele zaidi napo hakufika mbali sana baada ya kuona kwenye chumba ambacho kilichorwa alama ya Jokey, aliusukuma na kuingia akiwa anamhitaji kijana huyo amsubiri hapo na hakuna mlinzi hata mmoja ambaye alimzuia ni wazi walikuwa wakimjua kama sio yeye mwenyewe kufahamika sana ndani ya hilo eneo. Hiyo sehemu kama mchoro wake ulivyokuwa unaashiria mlangoni kulikuwa na kamali ya kucheza na maisha ya watu, huko kila sekunde walikuwa wanakufa watu na miili yao inaenda kutupwa kwenye asidi hakuna mtu ambaye alikuwa anayajali sana maisha ya watu huko pesa iliwekwa mbele kwenye kila kitu. kilikuwa ni chumba kikubwa sana ambacho ndani yake pia kulikuwa na vyumba vingine, wanawake waliokuwa uchi kabisa walikuwa wakipita na vibeseni vyao ambavyo vilijaa vinywaji bei ya glass moja tu ilikuwa ni kodi ya mtu kwa zaidi ya miezi sita maeneo yenye maisha mazuri lakini watu hawakuwaza hilo kwao vilikuwa ni vitu vidogo mithili ya supu ya miatano mtaani Tandale pale.

Monalisa aliketi kwenye sofa moja na kumpa ishara mhudumu mmoja kuja mbele yake, alichukua glass moja na kutulia akiwa anaishushia taratibu na ndiye huyu mwanamke ambaye alikuwa mstaarabu sana mbele ya Jason, alikuwa mlokole kwelikweli na ungemuona ungehisi mke huyu hapa leo alionekana kuwa mzoefu sana kwenye eneo kama hili hapa huenda kuna dunia yake ya pili ambayo alikuwa anaiishi yeye na hakutaka mtu yeyote yule aweze kumjua. Kitu cha kushangaza sana yeye hakudaiwa kabisa kama wengine maana baada tu ya yule mhudumu kumpatia kinywaji aliondoka zake sehemu zake za nyuma akiwa anazitingisha na alikuwa uchi kabisa hakujali chochote, kitu kilicho mkalisha Monalisa hapo ulikuwa ni ukumbi mdogo ambao ulijengwa kiufundi sana ulikuwa upo kati kati ya chumba hicho na juu yake paliwekwa viti sita pembeni pamoja na meza ya kioo katikati, karibu na kila kiti palikuwa na bastola juu ya kioo hicho na viti hivyo walikuwa wamekaa wanaume wasaka pesa haswa.

Mchezo ambao ulikuwa unafanyika hapo ulikuwa ni kuweka risasi kwenye bastola unazungusha mara moja kisha unajipiga kichwani, kama ikitokea risasi imetoka basi habari yako inaishia hapo lakini risasi isipo toka basi unakuwa umekula pesa na walikuwa wanaenda wawili wawili mabegi ya pesa ambayo yalijaa yalikuwa juu hapo. Bastola ina matundu sita ya kuhifadhia risasi, kama risasi zikiwekwa zote sita maana yake kila ikiruhusiwa lazima risasi itoke kwa namna yoyote ile kwa sababu hakuna nafasi yoyote ya risasi kutotoka pale inapokuwa inakokiwa lakini kama ikiwekwa risasi moja maana yake kuna matundu Matano yanabaki bila risasi hivyo mtu akiiruhusu basi inaweza kupiga kwenye tundu ambalo halina risasi na kuifanya risasi isitoke na ndiyo michezo ambacho ilikuwa inachezwa ndani ya hicho chumba. Mshindi wa pesa zote hizo akitakiwa kuwa mtu mmoja tu japo ulikuwa ni utapeli ambao ulikuwa unafanywa na wamiliki wa Club hiyo kwa sababu mshindi hakutakiwa kutoka mpaka ahakikishe watu watano hapo wamekufa na amebaki pekeyake ndipo anabeba pesa za wote na alitakiwa kuacha nusu ya kiasi cha pesa hizo ndani ya hiyo club.

Hivyo mshindi wa kwanza kwa watu wawili wa mwanzo alikuwa mmoja akifa basi anaendelea na mwingine mpaka mzunguko wa watu sita uishe na abaki pekeyake huyo ndiye alikuwa anaondoka na pesa za kutosha humo ndani, mchezo ulikuwa unaendelea mwanaume wa kwanza aliiweka bastola yake kwenye kichwa chake na kuikoki, baada ya kuruhusu tu risasi ilitoka na kuzama kwenye kichwa chake habari yake iliishia hapo, Monalisa alitabasamu huku akinyanyuka na kutoka humo ndani kwake hayo maisha yalionekana kuwa ya kawaida sana wala hakushtuka kuona damu ya mtu inamwagika kwa sekunde moja tu mbele ya macho yake. Alitoka mpaka nje ambapo alikuta yule kijana aliyekuwa ameshuka naye huko chini akiwa anamsubiri hapo, basi walinyoosha hatua kumi mpaka mbele zaidi ambako kulikuwa na ngazi za kushuka chini, kijana huyo aliishia hapo na huko chini ilikuwa ni zamu ya Monalisa kuweza kushuka.

Palikuwa na mlango mmoja tu basi ambao ulikuwa umezungukwa na taa zilizokuwa zinawaka mwanga kwa kubadilika badilika na kufanya eneo hilo kupendeza sana pembeni kukiwa na wanaume wawili ambao walikuwa kwenye suti nyeusi, alifika hapo na kufungua mlango huo, ndani ya hicho chumba alikuwa mwanaume mmoja ambaye alikuwa na kitambi cha kutosha, kwenye mwili wake hakuwa na nguo yoyote ile na alikuwa amelala kwenye sofa la gharama sana akiwa amezungukwa na warembo wawili ambao nao walikuwa uchi wakiwa wanamfanyia massage, humo ndani mlikuwa tofauti kidogo kwani hakukuwa na taa zilizokuwa zikibadilika rangi zilikuwa ni taa nyeupe tu ambazo zilikuwa zinawaka na kukifanya chumba hicho ambacho kilikuwa kimepambwa kwa vitu vya gharama sana kuonekana ubora wake halisia. Warembo hao baada ya kuona mlango umefunguliwa na Monalisa ameingia walitoka wakiwa wanakimbia huku wakiwa uchi, mwanaume ambaye alikuwa humo ndani alitabasamu na kuinuka akienda kumkumbatia mrembo huyo.

“Malikia mwenyewe umependeza sana leo ndiyo maana huwa hauniishi hamu kila ninapo kuona kwenye macho yangu” alitamka kwa lugha ya kiingereza huku akiwa anauweka ulimi kwenye sikio la Monalisa ambaye aliyafumba macho kwa hisia ambazo zilimjia, mwanaume huyo aliusukuma mlango huo kwa nguvu na kumvamia Monalisa ambapo alimvua nguo kwa pupa sana hakuchua muda sana wakawa wamezama kwenye mapenzi ambapo alitumia dakika tano tu pekee akawa amefika kwenye safari yake hiyo kitu kilicho mfanya Monalisa asonye kwa hasira na Kwenda kwenye Jakuzi kujisafisha huku akiwa uchi kabisa.

“Niliiona taarifa yako nadhani nitatakiwa mimi mwenyewe pia niende Tanzania” Monalisa aliongea huku akiwa anajisafisha na alikuwa huru kama vile yupo kwake.

“Unataka Kwenda kufanya nini?” mwanaume huyo aliuliza akiwa anaendelea kunywa wine ambayo ilikuwa kwenye bilauri moja kubwa sana.

“Kuna kazi nataka nikaimalizie kule na kuna mtu wangu nahitaji nikamtafute”
“Mhhhh ni yule bwana mdogo”

“Yes, nimetokea kumpenda sana yule kijana”
“Whaaaaat?” mwanaume yule aliongea kwa hasira sana

“Wewe kinacho kuuma nini hapo mimi kuwa na yule mwanaume mbona unataka kuanza kuniingilia mambo ambayo hayakuhusu” baada ya kumaliza tu kuongea alipokea kofi zito sana kutoka kwa mwanaume huyo

“Wewe mpuuzi nakuuliza unanipandishia sauti mimi kumbuka mtu ambaye unaongea naye ni nani na unatakiwa kukumbuka wewe ni nani siyo kuanza kuongea namimi kama nimekuwa mdogo wako, tunatumia pesa nyingi sana kukufanya uishi maisha unayo yataka wewe na kitu ambacho hutakiwi kukisahau you are a CIA agent don’t ever play with me (wewe ni agenti wa CIA usije ukacheza namimi), kuwa na heshima unapo ongea na bosi wako” mwanaume huyo alimeza pombe kwa hasira ili kupuuza machungu mwanamke huyo ilimbidi amsogelee mwanaume huyo licha ya kupigwa alijilainisha na wakajikuta wanarudia tena kufanya mapenzi alikuwa anaelewa kwamba mwanaume huyo udhaifu wake ulikuwa ni huo mwili wake, hakuwa na kauli kila anapo uona mwili wa huyo mwanamke hivyo alikuwa anautumia udhaifu huo kumlegeza.

“Usiwe na wivu kiasi hicho bhana, mimi najua unanipenda sana ndiyo maana ulinunua mpaka hii club ili tuwe tunapata nafasi nzuri ya kufurahia mapenzi yetu mimi na wewe, najua humu ndani wananiheshimu sana kama first lady ndiyo maana naweza kufanya chochote kile hata nikihitaji kuwafukuza watu wote humu ndani lakini kumbuka hii kazi nimepewa nafasi ya kuikamilisha kwa nafasi kubwa sana na kuhakikisha kwamba hakuna makosa yanayo fanyika. Mimi nimekula kiapo cha kulitumikia taifa langu la Marekani na nitakuwa nikiwa kama CIA agent lakini kumbuka sababu iliyo nifanya mpaka nikawa karibu na yule kijana, kumbuka kule kuna mtu wetu ambaye ameishi miaka mingi sana na wananchi wa kule wanamjua kama mtanzania na hata mimi najulikana kama mtanzania hata yule kijana analijua hilo kwahiyo nitaenda kule kumtafuta maana ameondoka ghafla sana na inatakiwa kupitia yeye kazi yangu iwe rahisi sana”, “aaaah baby” aliongea kwa kudeka huku akiwa anamkalia mwanaume huyo juu na kuubugia mhogo wa kiongozi wake huyo kama alivyo jitambulisha, kitendo hicho kilimfanya mwanaume huyo ambaye umri wake ulikuwa umeenda kugugumua kwa raha aliyokuwa anaipata na kumfanya asahau kama ni yeye ambaye alikuwa anamfokea mwanamke huyo.

“Unajua mauaji ya wale viongozi wawili japo tulishirikiana kwa ukaribu sana na baadhi ya watu wa kule ambao wana nguvu sana sina imani kama litaishia hapa lazima kuna watu wanaweza wakaibuka na kuanza kuleta shida baadae na kama unavyojua hatutakiwi kabisa kuacha alama yoyote maana wakija kujua kwamba kuna mkono wetu umehusika tutajichafulia sana jina hivyo nahitaji niende kule ili niweze kufuta ushahidi kama ulibaki mpenzi wangu ili tuwe salama nakupenda sana” aliongea huku akiwa anaongeza kasi ya kukatika hapo juu kitu kilicho mfanya mwanaume huyo kutoa machozi akiwa anakaribia kufika kileleni.

“Niruhusu basi mpenzi niende” alikuwa anaongea huku ulimi wake akiuweka kwenye sikio la mwanaume huyo na kuongeza kasi ya kukatika

“Nenda nenda baby nenda nimekuruhusu ooooooohps” mwanaume huyo alimjibu huku akiwa anafika kweye kilele cha mlima Kilimanjaro, na tayari Monalisa alikuwa amepewa ruhusa ya kuelekea ndani ya nchi ya Tanzania.

Monalisa ni CIA agent kivipi? Na lengo lake hasa ni nini? kwanini ajifanye yeye ni mtanzania? Kuna uhusiano gani wa wao kuwaua hao viongozi wakubwa wawili wa Tanzania? tuna mengi sana ya kuyafunua huko mbele lakini mpaka hapa niseme kwamba tunafika tamati ya sehemu ya 29.

Wasalaam

Bux the storyteller.
 
Wakuu kwema?

Samahanini, kama kuna mtu ana watu wa muaminika ambao huwa wanafanya kazi ya kuingiza sauti kwenye masimulizi anisaidie mawasiliano yao.

Au waweza kunicheki mimi mwenyewe

0621567672 unaweza ukapiga au ukanicheki whatsaAp

Natanguliza shukrani.
 
Mzee baba FEBIANI BABUYA ni kama tumakudsi episodes 3 ama 4....he utatufidia ama [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mkuu kuna story fupi ya maisha inaitwa MIMI NAITWA GAMA....inamhusu jamaa mmoja ambaye aliishi kwenye maisha magumu sana, maisha ya uswahili haswa. Alikuwa na imani kwamba magumu yote anayo yapitia chanzo kilikuwa ni baba yake ambaye alitamani kumuua kwa mkono wake. Hasira za maisha zinamfanya kudondokea kwenye uuaji ambao unampa mwisho mbaya sana........jamaa alikuja kuishi mwaka mmoja tu wa furaha ambao uliacha majonzi makubwa sana kwa familia......ndo nilikuwa namalizia leo, so nikawa naingia jf nachungulia tu GEREZA LA HAZWA Kule naweka, huku nikawasahau kabisa.

Ngoja niweke mkuu.
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 30

SONGA NAYO............
Majira ya usiku sana Jason alirudi mpaka sehemu alipokuwa akIpaita nyumbani kwao na ndipo palikuwa nyumbani kabisa kwa jaji mkuu Markvelous Japhary, hapo alipatambua na kujivunia kuwa ndiko nyumbani kwao ila kwa sasa jengo hilo lilikuwa lipo lenyewe likiwa linamwangalia yeye tu, hakukuwa na askari yeyote hilo eneo kwa sababu alikuwa amempa maagizo hayo IGP aweze kuwatoa watu hao maana hawakuwa kabisa na msaada wowote na chanzo cha kifo cha kaka yake na mheshimiwa raisi alikuwa anakijua. Alifika ndani ya nyumba hiyo na kulifungua geti ambalo lilikuwa limefungwa, nyumba ilikuwa ipo kimya sana alinyoosha moja kwa moja mpaka kwenye maktaba ambayo alikuwa akiitumia kaka yake kwa ajili ya kujisomea, alilisogelea lile kabati la vitabu na kulisogeza pembeni hapo mbele yake kulikuwa na mlango mzito sana wa shaba, aliweka vidole vyake pamoja na jicho lake, iliscan kwa dakika moja kisha lango hilo likafunguka, aliparudishia kama palivyokuwa mwanzo kisha akaingia huko ndani ambako alishuka ngazi kama tano tu akawa amefika kwenye chumba kingine kikubwa ambacho kilikuwa na makablasha machache tu ambayo yalihifadhiwa huko chini kwa siri sana.

Lengo la yeye kushuka huko chini ilikuwa ni kuifuata Diary ya kaka yake, diary hiyo aliwahi kupewa maagizo na kaka yake kwamba aisome siku yeye atakapokuwa amekufa ili aweze kujua baadhi ya maisha ambayo kaka yake alipata kuyaishi kwenye maisha yake, diary hiyo ilikuwa imewekwa ndani ya kioo kimoja ikiwa imejitenga na nyaraka zingine. Aliisogelea taratibu na kuifungua hiyo sehemu akaitoa diary hiyo humo ndani ilikuwa ni kubwa kiasi ambayo ilionyesha kwamba ilikuwa imepangiliwa vyema sana.

Aliufungua ukurasa wake wa kwanza ulikuwa umeandikwa mambo makuu mawili
MAISHA YANGU KABLA YA na
MAISHA YANGU BAADA YA

Hicho ambacho kilikuwa kimeandikwa hapo ilimaanisha ndicho ambacho kilikuwa kimetolewa fafanuzi za kutosha humo ndani ya Diary hiyo alikuwa na tamaa kubwa sana ya kujua mambo hayo mawili yalikuwa yakihusu nini kuhusu kaka yake na kwanini aliwahi kusisitizwa sana kuyasoma hayo mambo mawili, hakuwa na haraka sana alienda kwenye friji moja ambalo lilikuwa humo ndani kulikuwa na vinywaji vya aina nyingi sana ila yeye aliamua kuichagua wine kama kiburudisho chake wakati anaisoma diary hiyo kisha akaenda kuketi kwenye sofa moja safi sana na kutulia hapo ili aanze kuisoma huku akiwa anapata wine hiyo na muda huo ndipo alipokumbuka hakuangalia nje ya kasha la nje kabisa la Diary liliandikwa nini zaidi ya kufunua ndani na kukutana na hayo mambo mawili ambayo yalimpa hamu kubwa sana ya kuweza kuisoma diary hiyo.

Kwa nje diary hiyo kichwa chake kiliandikwa THE PREDILECTION OF THE HORROR MYTH ikiwa na maana ya UPENDELEO WA HADITHI YA KUTISHA, alishtuka sana kaka yake anamaanisha nini kuandika mambo ya kutisha kama hayo wakati yeye alikuwa ni mtu wa kucheza na kalamu ya sheria tu? hakuelewa na hiyo ilimuongezea hamu kubwa sana ya kuhitaji kuisoma diary hiyo, alitoa simu yake mfukoni na kuizima kabisa hakuhitaji kupata usumbufu wakati wa kuisoma diary hiyo, alihitaji kujua kilichopo ndani ila kama nafsi ilikuwa inamsaliti maana alikuwa anaogopa basi alicho kifanya aliamua kuufunua ukurasa ambao unafuata ili aweze kupitia neno ambalo liliandikwa na kaka yake na maneno ya mwanzo yalikuwa hivi;

“Mdogo wangu najua unajua kwamba kaka yako nakupenda sana hilo sidhani hata kama huwa unajiuliza mara mbili kwenye maisha yako, hii ni diary ambayo nimeandika maisha yangu lakini sio maisha yangu tu pia nimeandika na baadhi ya mambo au unaweza ukaita simulizi fupi ya maisha yetu mimi na wewe pamoja na ya shemeji yako ambaye wewe ulikuwa ukimuita mama kwa namna mlivyokuwa mnapendana”

“Mdogo wangu maneno ambayo yameandikwa humu ndani yana sehemu mbili tofauti kama ulivyokutana na vitu viwili nyuma hapo ambavyo bila shaka najua vinakuchanganya sana mpaka sahivi huko uliko, navyosema maisha baada ya maana yake maisha baada ya mimi kuingia kwenye mapenzi na mwanamke ambaye nilimpenda na mpaka naandika haya maneno bado nampenda sana hili sihitaji hata kulielezea sana maana unalijua vizuri lakini nikisema maisha kabla ya namaanisha maisha yangu kabla ya mimi kumpata huyo mwanamke na nahitaji uanze kuyasoma maisha yangu baada ya kwa sababu inawezekana ndio ulikuwa wakati wangu bora zaidi kuwahi kuuishi hapa duniani lakini baada ya hapo utausoma muda wangu wa KABLA YA”

“Mdogo wangu wewe ni mtu ambaye nimekulea mimi mwenyewe kwa mkono wangu, nimekubeba mimi mwenyewe, na nimekulisha mimi mwenyewe bila kusahau nimekubadilisha nguo za kuvaa mwenyewe kwa sababu wewe ni kama roho yangu nyingine, nakupenda kuliko hata ninavyo upenda huu ulimwengu wote huenda ni kwa sababu tulizaliwa wawili tu hivyo wewe ulinifanya nijivunie sana kuwa hapa mimi nilipo na nisijihisi mpweke sana kwenye ulimwengu wa ukiwa. Mimi ndiye mtu ambaye ninakujua wewe kuliko binadamu yeyote yule hapa duniani, ninaweza kukuangalia tu usoni nikajua unacho kiwaza na maamuzi ambayo utayachukua, naweza nikasikia hatua hata kwa umbali wa mita miamoja bila hata kukuona na nikajua ni wewe, naweza kusikia jasho lako tu au namna unavyo ivuta hewa na nikajua kwamba upo ndani ya hilo eneo na ubaya wako huwa hata haujui kuwa muongo hivyo hata ukidanganya kitu ambacho dunia nzima inaweza ikakuamini wewe kwangu mimi haiwezekani hata kama utaigiza vipi bado haitatosha kunidanganya maana nakujua kila kitu kuhusu wewe”

“Mimi najua mpaka uimara na udhaifu wa mifupa yako kwa sababu huo mwili wako nimeubeba tangu ukiwa mdogo unanyonya mpaka unakuja kuwa mtu mzima hivyo najua kila sehemu ya mwili wako na namna ilivyo ugumu wake, udhaifu wake na ulaini wake hivyo hakuna kitu ulikuwa unaweza kunidanganya kwenye maisha yako. Mimi nakujua wewe ni nani kwenye hiyo dunia yako ambayo wewe umeiishi ukiwa unajua unanificha mimi, mimi najua kabisa kwamba wewe ni mtu hatari sana tena sana kama baadhi ya wanadamu wanavyokujua kwenye huo ulimwengu wako, mikono yako imekuwa tofauti sana, umekuwa na mifupa migumu mno ambayo haina hata maji imefikiwa kiwango ukimgusa mtu sehemu mbaya tu basi lazima afe unahisi ningeshindwa kuona hayo mabadiliko kwa mdogo wangu wa pekee hapa duniani? Hapana Hapana Hapana hilo lisingewezekana mimi nakujua wewe kuliko hata unavyo jijua wewe mwenyewe lakini naomba kwanza yasome hayo maisha yangu BAADA YA ili uweze kujua nilichokuwa nimekikusudia na uelewe kwanini nimeamua kuiita hadithi hii ya maisha yetu kama THE PREDILECTION OF THE HORROR MYTH” Jason alikuwa anatoka jasho mwili mzima, alikuwa akitetemeka sio kwa sababu tu ya maneno ambayo yaliandikwa hapo Hapana bali uzito wa mtu ambaye alikuwa ameyaandika maneno hayo. Ameyaishi maisha yake kwa siri kubwa sana tena sana na mtu ambaye alikuwa hahitaji kabisa kuzijua hizo siri zake alikuwa ni kaka yake kipenzi leo kupitia maandishi ambayo aliyaacha kaka yake alimsisitiza kwamba alikuwa akimjua kuliko hata yeye mwenyewe alivyokuwa akijijua ilimtisha sana na aliogopa mno hicho kwake hakikuwa kitu cha kawaida, alitoa kitambaa kwenye mfuko wake na kujifuta usoni pamoja na mikononi ili asiweze kukilowanisha kitabu hicho kabla hata hajakisoma baada ya hapo aliufunua huo ukurasa uliokuwa unafuata wa

MAISHA YANGU BAADA YA.
Anasema “Mimi siyo mwanaume bora sana ila kukutana na huyu mwanamke imenifanya mimi kuwa moja kati ya wanaume bora sana kuwahi kuishi kwenye huu ulimwengu na baadhi ya wananchi wa nchi yangu walikuwa kila wakilala wananiombea kwa sababu ya huyu mwanamke. Hadithi yangu nzito ya maisha ya mapenzi ndiyo iliyo nifanya mimi nikawa na uwezo wa kuyaishi vizuri na kuyaelewa MAISHA YANGU BAADA YA, haya ni maisha ambayo nimeyaishi baada ya kumpata huyu mwanamke mrembo zaidi kuwahi kutokea kwenye macho yangu. Ule usiku wa kwanza kumuona pale DREAM LOVERS LOUNGE ulikuwa usiku bora zaidi kwenye simulizi ya maisha yangu licha ya kubahatika kuisikia tu ile sauti ilinikumbusha moja ya nahau za wanazuoni isemayo DALILI YA MVUA NI MAWINGU, nilikuwa na uhakika kwamba kwa sauti ile basi ni dalili ya uwepo wa mwanamke mmoja mzuri sana ndiyo maana nilikuwa na hamu kubwa sana ya kumuona bahati iliyokuwa kwangu, uso ulitamalaki kwa mikunjo ya ghadhabu baada ya kushindwa kuiona ila sura nzuri sana ule usiku wangu wa kwanza, nilighafilika mithili ya mwanaume aliye mfumania ugoni mwanaume mwenzake kwenye kitanda chake mwenyewe lakini nikaamua kuiamini kesho yangu kwa sababu ilikuwa ni ahadi tu na si uhakika na hata kama mwenye huu ulimwengu angeamua kutonifikisha basi sikuwa na cha kumlaumu zaidi ya kumtukuza yeye na kumshukuru kwa nafasi ya upendeleo ambayo alikuwa amenipa kuiishi mpaka siku hiyo”

DREAM LOVERS LOUNGE
“Ule usiku wa kukosa kumuona yule mwanamke niliumia sana hapa nitaeleweka tu kama umewahi kupenda ule upendo wa kweli mdogo wangu ila kama haujawahi basi kamwe hauwezi kabisa kunielewa mimi ndugu yako wa damu. Kesho yake mapema sana nilikuwepo hapo ili niweze kumuona Princess Prisca kama walivyokuwa wakimnadi tangu siku ya kwanza hahahah nilikuwa kama fala mimi mdogo wangu, ule ndiyo ulikuwa usiku wangu bora zaidi kuwahi kuuishi kwenye maisha yangu kwa sababu ule ndio usiku ambao uliweza kunikutanisha na mwanamke wa ndoto zangu, najua kila kitu kilikuwa kimepangwa na MUNGU kwamba mimi nitakuja kukutana na yule mwanamke ila natanguliza shukrani za dhati sana kwa yule mwanaume ambaye alikuwa mlinzi wa ile sehemu baada ya kunibeba na kunibamiza kwenye ile meza wakati naelekea kwenye ile sehemu ambayo alikuwa amesimama princess Prisca mkononi mwake akiwa na maiki yake tungo nzuri zikiwa zinapita kwenye sauti ambayo MUNGU aliiandaa kwa ajili ya masikio ya mwanaume anaye jielewa”

“simaanishi kwamba nampongeza yule mlinzi wa pale kwa sababu ya kuniumiza lahasha bali ile ndiyo ilikuwa siku yangu ya kwanza kabisa kukutana na yule mwanamke na ndiyo ilikuwa siku ya kwanza kabisa naisikia sauti yake ya moja kwa moja achana na ile ya kwenye maiki mpaka nilitamani kama ningeongezwa tena kuumizwa ili angalau akili yangu itulie na kupoa kwa namna alivyokuwa anafanya. Baada ya kurushwa pale chini niliumia sana tena sana kwa sababu eneo la kichwa changu lilipasuka, kwa kitu ambacho hata sikukitarajia kabisa ni baada ya kumuona yeye akiruka kutoka kwenye sehemu ambayo alikuwa anafanyia tamasha lake na kujongea mpaka pale ambapo mimi nilikuwa nimedondokea”

“Vipi hali yako unajisikiaje” aliongea kwa upole baada ya kufika pale huku akiwa ananishika kichwa changu na kukiweka kwenye mapaja yake, mimi hata sikukumbuka kwamba kichwa changu kina hitilafu nilikuwa nimependezewa sana na kila kilichokuwa kinafanyika pale, sikutamani ule wakati uweze kuisha pale nilitaka iwe milele nilale pale pale, licha ya watu wote mle ndani kushangazwa na hicho kitu na kutuzingira pale wakiwa wanatahamaki ni kivipi mwanamke mzuri kama huyo aende kuchafuka kwenye damu ya mtu maskini kama mimi wakati hiyo ilikuwa ni kazi ya mabaunsa wa mle ndani kwangu ilikuwa burudani tosha sana nikiwa najipatia marashi safi ambayo alikuwa ameyapulizia kwenye mwili wake, ngozi nyororo ambayo ilinishika kwenye uso wangu ilikuw ani EDEN yangu mwenyewe nilichokuwa nakisikia pale ilibaki kuwa burudani isiyo nitoka kichwani mpaka hivi leo ninavyo ongea nampenda sana MKE WANGU” Jason alihema kidogo baada ya kuona hadithi inazidi kumkolea alisogeza wine yake na kuimimina nyingine mpaka juu ya bilauri lake kisha akaufunua ukurasa ambao ulikuwa unafuata alihitaji kujua ni nini kilizidi kujiri kwenye hiyo simulizi ya MAISHA YA KAKA YAKE BAADA YA.

Ebu tuendelee Kwenda sawa na simulizi hii tuweze kujua hiyo DIARY ina nini cha umuhimu, hayo MAISHA BAADA YA na MAISHA KABLA YA yana nini ndani yake, huyo mtu aliweza vipi kumjua mdogo wake wakati ameishi kwa siri kubwa mno kwenye huo upande wake wa pili kama ambavyo inaonekana kabisa kwamba hajulikani na upande huo una nini hasa cha kutisha mpaka anaogopwa sana, lakini tunatakiwa kuipitia Diary hii ili tujue ni kwanini iliitwa THE PREDILECTION OF THE HORROR MYTH.

Sehemu ya 30 inafika mwisho sina la ziada tena panapo majaaliwa tukutane tena wakati ujao.

Wasalaam

Bux the storyteller.
 
Hello wanafamilia wa Story za Bux na mwandishi Febiani Babuya.

Leo nimewaletea andiko lingine fupi.

Kwa wale ambao wanapenda sana simulizi za misuko suko ya maisha pamoja na maisha halisi ya mtaani haswa, basi simulizi ya MIMI NAITWA GAMA ipo kwa ajili yenu.

Simulizi inamhusu jamaa mmoja ambaye alizaliwa kwenye maisha magumu sana tena zaidi ya sana, ukitaka kujua nini maana ya maisha magumu basi wewe lisome jina lake tu hali ambayo inampelekea kuwa muokota makopo mtaani. Ugumu wa maisha yake unamfanya kumtupia lawama zote baba yake mzazi huku akimshuhudia mama yake akifa kikatili mbele ya macho yake mawili.

Anaahaidi kumuua baba yake kwa mkono wake mwenyewe, hasira zake zinampelekea kuishia gerezani kisha kuwa muuaji baada ya kutoka huko.

Maisha ambayo aliyachagua yanamfanya kuishia kuokota makopo na kula jalalani. Mwanaume huyo anafanikiwa kuishi mwaka mmoja tu wa furaha huku mwaka huo ukiacha majonzi makubwa sana kwa familia.

Ni bonge la simulizi hii usiikose kabisa ili uyasome maisha halisi ya mtanzania wa mtaani.

Hadithi inaitwa MIMI NAITWA GAMA na nimeiandika yote mpaka mwisho ila hii haitapatikana huku Jf mpaka ulipie ndo utaweza kusioma.

Unaipata kwa shilingi 1500 tu, yaani elfu moja na miatano tu pekee, yote.

Lipia kupitia namba

0621567672
0745982347

Jina FEBIANI BABUYA

ILI UIFURAHIE WIKIENDI YAKO KWA KUYASOMA MAISHA YA MTANZANIA HALISI WA MTAANI HASWA.

Wasalaam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…