Innocent Killer (The Revenge)

Hii ni simulizi ya kijasusi.....ambayo inamhusu kijana mmoja aliyepatwa kuitwa Jason.

Kijana huyu alikuwa ni mdogo wa jaji mkuu wa nchi ya Tanzania. Ambaye alikuwa akisoma ndani ya nchi ya Marekani.

Alikuwa kijana wa kawaida sana kwenye macho ya watu, ambapo alikuwa na mpenzi wake waliyekuwa wakisoma wote.

Mpenzi wake huyo alikuwa ni Agenti wa CIA bila kijana huyo kujua.

Kisa kinaanzia wapi?

Raisi wa nchi ya Tanzania anapigwa risasi tano za kichwa akiwa Tiptop darajani kwenye msafara wake usiku. Kesi hiyo inaangukia kwenye mkono wa jaji mkuu, ambaye alikuwa ni rafiki wa karibu wa raisi, anaapa kumuua aliye husika mbele ya mahakama.

Jaji huyo usiku mmoja kabla ya hukumu anapewa onyo kwenye simu kwamba aupindishe ukweli siku ya hukumu....

Siku ya HUKUMU.
Anamsomea hukumu ya kunyongwa mhusika ambaye ananyongwa mbele ya mahakama. Baada ya kutekeleza hilo anapokea simu ya kumpa dakika 15 tu za kuiokoa familia yake.

Anakimbia na kufika nyumbani anakuta mkewe amechomwa kisu cha tumbo akiwa mjamzito huku mwanae wa kike akiwa ameuliwa.

Anpiga simu kwa mdogo wake kumpa taarifa lakini naye anatokewa na mtu na kuuliwa huku akiwa amefanikiwa kumtamkia mdogo wake kwamba....."THEY HAVE KILLED YOUR BROTHER" (Wamemuua kaka yako).

Mauaji anayofanyiwa yanafanana na namna raisi alivyo uliwa, sasa kama mtuhumiwa alinyongwa vipi mauaji yawe yale yale kama ya raisi? maana yake muuaji hakufa? INAZALIWA SINTOFAHAMU.

Kijana huyo kwa uchungu anarudi kumzika kaka yake na mheshimiwa raisi wa nchi yake ambaye walijuana vyema kwa mengi yaliyokuwa yamejificha nyuma.

Siku kadhaa baada ya msiba, watu wanakutana na tangazo ambalo linawataka wahusika wa mauaji ya jaji mkuu na raisi wajitokeze ndani ya miezi sita, kisha waombe msamaha kwa jamii atawaacha hai..kama muda huo utaisha bila wao kufanya hivyo basi huyo mtu atafanya anavyotaka yeye..

Hapo ndipo tunaenda kumfunua huyo Jason na kumjua yeye ni nani baada ya kuanza kufanya mauaji ya kutisha.

Inaitwa: MUUAJI ASIYE NA HATIA (KISASI)

Softcopy yake inapatikana kwa shilingi 5000 tu.

0621567672 (WhatsApp)
 
Wakuu kwema? Aisee nilipotea sana huku tusameheane tu.

Nilikuwa namalizana na GEREZA LA HAZWA. Ishaisha hivyo tunaendelea huku kama kawaida.

Wasalaam.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 31

SONGA NAYO............
“Sikuelewa tena kitu ambacho kilikuwa kimeendelea pale kwa sababu muda ule ule nilizimia baada ya kuhisi kizungu zungu kikali sana kwa maumivu ambayo nilikuwa nimeyapata kwenye kichwa changu. Nilishtuka nikiwa juu ya kitanda mkononi kwangu kukiwa na mipira ya kuongezea damu nikiwa natoa mwanga hafifu kwenye macho yangu nilikurupuka na kuita “Jason” jina lako ndilo kilikuwa kitu cha kwanza kabisa kunijia baada ya kurejesha fahamu zangu zote kwani nilizoea kila nikiamka basi lazime ningekuona pembeni yangu hivyo siku ile kuamka na kujikuta nipo mwenyewe nilijawa na wasiwasi sana”

“Pole sana unajisikiaje” ile sauti ndiyo iliyo nikumbusha kwamba mle ndani sikuwa pekeyangu, moyo wangu ulitulia kiasi nikiwa nahisi huenda ulikuwa ni wewe lakini nilipata mashaka baada ya kugundua kwamba ile ilikuwa ni sauti ya kike tena ndani ya hospitali, ilinilazimu kutuliza kichwa ili niweze kukumbuka kila kilichokuwa kimetokea mpaka mimi kuwa kwenye hiyo hali, sekunde kadhaa tu ziliweza kurejesha kumbukumbu zangu zote kwenye kichwa changu, nilichanua tabasamu mithili ya mtoto ambaye ananyonya anapomuona mama yake karudi kutoka safari ya mbali ambayo imemfanya kuto mtia machoni kwa muda mrefu baada ya kukumbuka kwamba huyo aliyekuwa pembeni yangu alikuwa ni Prisca lakini tabasamu hilo liliyeyuka mara moja kwa sababu sikuwa na uhakika kama mdogo wangu ambaye ni wewe alikuwa yupo salama”

“Namshukuru MUNGU nahisi nipo salama ila ni muda gani tangu nipo hapa?” nilimuuliza kistaarabu sana mwanamke ambaye uso wake haukuwa na hatia yoyote ile

“Ni jana usiku nilikuja nawewe hapa ukiwa kwenye hali mbaya sana, saivi ni asubuhi na mapema sana nashukuru MUNGU umeamka salama maana niliogopa kukuacha mwenyewe kwa sababu ya hali ambayo uliyokuwa nayo ule usiku wa jana naweza nikasema pole sana ila ni kipi kilikufanya mpaka ukajipenyeza sehemu kama ile wakati unajua pale panalindwa? Maana sikutakiwa hata kukusaidia ni kwa vile sikutaka kukuacha pale maana ningejisikia vibaya sana kusababisha mtu kupata matatizo kwa sababu yangu halafu nikaendelea kumuacha kwenye matatizo ndiyo sababu niliamua kuacha hata kazi iliyo nipeleka pale na kuamua kukusaidia japo sijui hata kama bosi atanielewa kwa hili” aliongea kistaarabu akiwa kama ana majuto ndani yake ambayo hayakuwa na wasiwasi sana hiyo ilinifanya nijisikie vibaya mno kwa kusababisha matatizo kwa mtu ambaye inaweza ikampelekea hata kuikosa kazi yake.

“Naomba unisamehe sana kuweza kukuletea haya matatizo ambayo hata mimi mwenyewe siwezi kuyabeba, mimi ni kijana mdogo tu tena wa kimaskini ambaye siwezi kukulipa kwa wema wako kwangu ila kwa jana nimekuja pale ikiwa ni mara ya pili na sababu kubwa iliyonifanya nije pale ni ile sauti ambayo nilikuwa naisikia, kwenye maisha yangu sijawahi kuisikia sauti nzuri sana ukiacha ya mama yangu ikiniimbia kama yako, siku ya juzi wakati napita ndipo niliisikia vyema nilitamani sana nipate wasaa wa kuisikiliza lakini kwa bahati iliyokuwa mbaya sana wakati nakuja ndipo ulikuwa unaondoka hivyo jana nikajiwekea ahadi kwamba ni lazima niwahi kuja kuisikia siku ya jana ndicho kilicho tokea pale wakati natamani nikuguse tu hata sura yako naomba unisamehe sana kwa matatizo mazito ambayo nimeweza kuyasababisha kwako” niliongea kwa uchungu sana kwa sababu ni kitu ambacho nilikuwa nakiongea kutoka sehemu ya ndani kabisa ya moyo wangu.

“Wala usijali kuhusu hilo limeshapita lakini hapo umesema kwamba ulikuwa ukimsikia mama yako akikuimbia zaidi ya mimi ulivyo nisikia jana kwani huyo mama yako kwa sasa yuko wapi?” swali lake halikuwa baya lakini liliniletea majonzi sana kwenye moyo wangu, nilijikuta nawakumbuka sana wazazi wangu, niliumia sana kwa sababu jukumu la kukutunza lilibaki kwangu kwa sababu yao, alipata kazi nyingine kubwa sana ya kuweza kunibembeleza tena mimi alitumia kama nusu saa ndipo nilitulia kidogo na kumpa taarifa fupi tu kwa sababu sikuhitaji sana yeye aweze kunikumbushia ile sehemu ambayo nilikuwa nimetoka sikutaka aendelee kunikumbushia hayo maumivu

“Mama yangu na wazazi wangu walikufa tena kwa usiku mmoja mbele ya macho yangu, ni usiku mbaya zaidi mimi kuwahi kuuishi kwenye maisha yangu na sikuwa na chochote kile cha kuwasaidia na ukizingatia nilikuwa bado ni mdogo hata hivyo nilikuwa pia nina mdogo wangu ambaye alikuwa kwenye mikono yangu, alihitaji kunyonya kwa ule muda kwani alikuwa mchanga mno na kwa kipindi hicho nilikuwa nina miaka kumi na minne tu pekee hivyo jukumu la kumlea mdogo wangu lilikuwa lipo chini yangu na ndiye huyo ambaye mimi namlea mpaka hii leo, naomba niwahi nikamuone mdogo wangu atakuwa amelia sana kwani hajazoea kulala bila mimi kuwepo huwa lazima anione ndipo alale” niliongea nikiwa najifuta machozi kwenye uso wangu, niliuvuta ule mpira wa damu na kuukata kisha nikanyanyuka kutoka kwenye kitanda, alinionea sana huruma yule mwanamke, alinibembeleza sana na kunitaka mimi nimpeleke mpaka nyumbani nadhani una kumbukumbu nzuri ile ndiyo siku ambayo nilikuja na mwanamke kwenye kile chumba chetu tulichokuwa tumekipanga nilikukuta umelia mpaka unaumwa, nadhani unamkumbuka yule mwanamke ambaye alikubeba kwenye mikono yake wakati tunahangaika kupata usafiri wa kukupeleka hospitali yule ndiye mwanamke wangu, yule ndiye mke wangu ambaye mimi nampenda sana tena sana.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa kukutana na yule mwanamke, baadae alikuja kunipa ukweli wa maisha yake, baba yake na mama yake waliuawa na baba yake mkubwa ambaye alirithi mali zote za yule mwanamke kwao kwa nguvu kwa kigezo cha kuihadaa serikali kwamba atamtunza yule mwanamke lakini baada ya kukabidhiwa mali hizo na kumchukua yule mwanamke ambaye mimi nilimjua kama mrembo Prisca alianza kumtumia kwenye biashara zake za club, alikuwa akimtumia kama kiburudisho kwa wateja na ndiyo sababu alikuwa akitembea kila usiku kwa kutumia sauti yake ili kuwapa burudani wateja kwa kuimba nyimbo ambazo wao walizipenda ila alikuwa ni mwanamke ambaye alifanikiwa kujitunza sana na niseme najivunia sana kuwahi kumpata mwanamke kama yeye”

“Alijaribu Kwenda kwenye sheria kudai haki yake lakini alitishiwa kuuawa na huyo baba yake mkubwa hivyo hakuwa na namna zaidi ya kukubaliana na yale maisha ambayo alikuwa amechaguliwa kuyaishi mpaka siku ile ambayo alikutana na mimi hata yeye mwanzo wake mwema ulianzia pale maana alitoroka kwao akaja kuanza maisha namimi tena tukiwa na wewe kwa wakati ule nikiwa sina chochote na nategemea kuendelea na masomo, alinivumilia sana, alinisaidia sana kukulea wewe hapo mpaka mimi nakuja kuwa mtu mkubwa nchini msaada mkubwa sana ulikuwa ni yeye nadhani unalijua hilo. Baadae baba yake mkubwa alikuja kufilisika vibaya sana baada ya kutapeliwa mali zote na wafanya biashara wenzake mwisho wa siku akawa amejinyonga habari yake ikaishia pale sisi tuliendelea na maisha yetu” hapa najua mengi unayajua kuhusu hili ndiyo maana sikuhitaji sana kupoteza muda kuhusu hili mdogo wangu ila lengo la kuandika MAISHA BAADA YA nilitaka ujue kwa undani na kwa usahihi kwamba kwanini nasema mimi nakujua sana wewe hapo, ujue kwamba ni kwanini nasema nakufahamu kuliko hata wewe unavyo jijua”

“Kitu ambacho unatakiwa kukifahamu ni kwamba mimi ndiye niliye taka wewe uwe mtu wa hatari sana namna hiyo kama ulivyo kwa sasa” Jason alikuwa anasoma kwa kasi ili aweze kumaliza mapema kwani hakuwa amepata kabisa muda wa kupumzika na wakati huo kulikuwa kunakaribia kukucha na siku hiyo alitakiwa kukutana na Alphonce kutoka ndani ya nchi ya Canada kama alivyo muagiza ili amthibitishie aina ya mauaji ambayo yalitokea kisha atoe tamko lake kama alivyokuwa ameahidi ila baada ya kuusoma mstari huo ambao ulikolezwa wino ilimlazimu kwanza kutulia ili aurudie tena.

Alisoma kwa mara ya pili, akaurudia tena, akaurudia tena na tena na tena, alimimina wine kwenye bilauri lake kisha akanywa yote akatikisa kichwa chake na kuirudia sentensi hiyo akiwa anasoma neno moja moja, hakuwa amekosea hata nukta kila kilichokuwa kimeandikwa kilikuwa kipo sahihi kwa asilimia miamoja, nafsi yake ilikataa kabisa kuamini ila macho yalichagua kuyaamini maandishi hayo, kwake ilikuwa ni ndoto ambayo huwa inaotwa na watu wengi ya kuwa matajiri lakini ni wachache huwa inakuwa ya kweli kwao ila kwake ilikuwa ni ya kweli. Hakuamini kabisa ndiyo maana aliirudia sana sentensi hiyo tena mara nyingi sana, kivipi kaka yake ambaye hakuwahi hata kidogo kutaka mdogo wake apate matatizo ndiye aseme kwamba ni yeye ambaye alihitaji kumfanya binadamu huyo kuwa mtu wa kutisha sana namna hiyo? Aliogopa sana kuhusu ndugu yake huyo yeye ndiye aliyekuwa anadhani anafanya siri nzito sana kwa kaka yake lakini kumbe kaka yake ndiye ambaye alikuwa anafanya siri nzito sana kwa mdogo wake na kila hatua ambayo alikuwa anaifanya Jason alikuwa akiijua vyema, alishindwa kuelewa huyo kaka yake alimaanisha nini, alifanya kwa ajili ya nini na kwanini miaka yote hiyo aishi kwa kujifanya hamjui kabisa mdogo wake? Jibu alikuwa nalo mkononi alitakiwa kuimaliza Diary hiyo ili aelewe nini maana ya MAISHA BAADA YA na MAISHA KABLA YA ili aunganishe maana moja kwanini Diary hiyo iliandikwa THE PREDILECTION OF THE HORROR MYTH.



“Upendo ni kitu mithili ya fasihi ambayo haiwezi kukamilika bila kuwa na tanzu zake, ili mtu wa fasihi afanye kilicho bora kwa hadhira wake lazima azijue tanzu za hiyo fasihi ambayo anaiandika ili hadhira wake wapate kumwelewa kwa asilimia zote miamoja hivyo ndivyo inavyokuwa hata kwenye maisha ya kawaida, upendo ulio kamili lazima utoke kwenye moyo wa mwanadamu ndani kabisa, ukapita kwenye hisia zake kisha moyo ukafunguka na kukiri kwamba upo huru kuonyesha mapenzi ya kweli kwa mtu fulani hivyo hupelekea mtu kujihisi mwepesi sana pale anapokuwa anawaonyesha wenzake mapenzi yale ya dhati kabisa tena kwa huo upendo mkubwa sana”

“Upendo unapokosa nyezo zake maalumu za kuukamilisha kama vile moyo, hisia, akili ya ubongo na baadhi ya vitu vingine vya mhimu basi huufanya uyeyuke mithili ya majivu yaliyo pitiwa na upepo hayana ujanja wa kujizuia kabisa Kwenda kwa sababu hakuna kitu cha kuyashikilia pale yalipo na ndiyo sababu upendo ukikosa hizo nyezo ni kama fasihi bila tanzu zake hauwezi kuwepo kamwe kwani mtu atakuonyeshea kwa mdomo kwamba anakupenda lakini moyo na hisia zake vitagoma hivyo kuzalisha unafiki na chuki huanzia hapo”

“Ukiwa kama mwanadamu ambaye umeamua kumkiri MUNGU wako na sehemu ya maisha yako umeamua kuyaweka kwake basi usije ukaruhusu kabisa hilo jambo likatokea hata siku moja litakuwa ni jambo la hatari sana kwani unaweza ukakuta hata ndugu zako unawachukia bila kuwa na sababu ya msingi sana. ukisoma maandiko mengi bila kujali kwamba yametoka kwenye lugha gani basi utakuta kitu kikubwa yanahamasisha sana kitu cha kwanza kinatakiwa kuwa ni upendo ndipo mambo mengine yafuate kwa sababu bila upendo dunia haiwezi Kwenda popote, bila upendo hakuna maendeleo hakuna upendo kabisa, rejea kwenye kumbukumbu za wale watoto wa Adam, Kaini na Habili ukosefu wa upendo ulipelekea ndugu wawili hawa kuuana na hiyo inatuonyesha wazi kwamba upendo haukuwepo, Yusufu anatupatia mfano mwingine kutoka kwa nduguze hawakuwa na upendo kwake baada ya yeye kuonekana anapendwa sana na baba yake na hiyo ilimpelekea yeye kuishi miaka mingi sana utumwani”

“Je nawewe unataka kuwa kama hao watu ambao waliukosa upendo na baadaye wakaanza kujuta kwenye maisha yao? Je nawewe unataka kuchukiwa kama Yusufu? Je nawewe unataka kuikosa amani ya maisha kwa sababu tu ya kukosa kitu kinaitwa upendo? Jibu linatakiwa kuwa Hapana, haijalishi wewe una imani gani, haijalishi wewe ni mtu wa wapi, haijalishi wewe ni rangi gani tusibaguane kwa sababu ya dini, tusibaguane kwa sababu ya rangi, wala tusibaguane kwa sababu ya makabila sisi wote ni wa kupita hapa tuniani na ipo siku tutakufa utafaidika nini kufa ukiwa na vinyongo moyoni mwako? Kipi utakipata ukiwachukia wenzako na kuwatendea mabaya? Itafakari sana kesho yako kisha ujiambie mwenyewe kimoyoyo kwamba utakuwa mtu wa upendo kwenye maisha yako yote mpaka siku unakufa” ni sauti tulivu majira hayo ya alfajiri na mapema sana mida ya saa 12 wakati wa ibada ya asubuhi sana ndani ya kanisa la WITH GOD YES WE CAN, ni kanisa ambalo lilikuwa na nguvu kubwa sana ndani ya nchi ya Tanzania, lilipatikana Kimara Mwisho, watu wengi sana walikuwa wakisafiri kutoka sehemu mbali mbali Kwenda kupata mahubiri ambayo waliamini ni ngumu sana kuyapata sehemu yoyote ile ndani ya dunia hii, ni sauti ya mchungaji ambaye alikuwa ni kipenzi cha watu kila sehemu alipendwa kuliko ilivyo kawaida.

John Mwituka ndilo lilikuwa jina lake, umri wake ulikuwa ni wa kiutu uzima sana, kutokana na kanisa hilo kuwa na watu wengi mno ambao wasingetosha kwa kuwa na misa mbili pekee basi kuna misa ya watu ambao walikuwa wakiingia saa kumi ya alfajiri na kutoka saa moja ili kuwapa nafasi nyingine wale ambao walikuwa wanaingia baada ya huo muda, alitulia kidogo baada ya kuyaacha maneno yake yasambae kwenye vichwa vya waumini wake kisha akaendelea.

Unahisi huyu mchungaji kaingiaje ingiaje humu ndani? Ebu ngoja tuone anatupatia kitu gani ndani ya simulizi yetu.

Sehemu ya 31 sina la ziada tukutane sehemu inayo fuatia.

Wasalaam
Bux the storyteller.
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 32

SONGA NAYO............
“Miaka mingi iliyoweza kupita niliwahi kupata mwaliko wa kidini kwenye nchi ya waitaliano na bahati iliyokuwa njema huko nilikuwa nina rafiki yangu mmoja ambaye tulisoma naye tukiwa wadogo yeye alikuwa anasomea upadri huko basi baada ya kusikia kwamba namimi nimeenda kwenye ile nchi alisema nisije nikaenda kule na nikaondoka kabla sijaonana naye. Sikuwa na namna kwa sababu ulikuwa umepita muda mrefu sana bila ya kuonana, baada ya mimi pia kumaliza mikutano yangu nilienda mpaka sehemu ambayo walikuwa wanaishi, nilibahatika sana kuhudhuria vipindi kadhaa vya mafundisho yao nilistaajabu mno huenda kwa sababu kilikuwa ni kitu kigeni sana kwangu”

“Siku ile nilishangaa mapadri wanasoma mpaka Quran kwa mara ya kwanza nilihisi kama kwa maadili ya dini ya kikirsto walikuwa wakitenda ni dhambi ila kwa baadae nilikuja kugundua kwamba kumbe huwa wanajifunza ili kuweza kuzijua dini zote kwa usahihi na kwamba dini siyo kigezo cha kuwatenganisha watu yaani wakristo na Waislamu sisi wote ni wamoja ila utofauti wetu ni kwenye suala la imani tu na ndiyo maana hata MUNGU tunaye muabudu ni mmoja tu pekee. Kupitia siku ile nilipata somo kubwa sana kwamba kumbe ni ukosefu wa uelewa mdogo tu ndio huwa unatutenganisha na kutugombanisha ila sisi wote tunapaswa kuishi kwa kushirikiana sana kupitia neno upendo hivyo usije ukajiona wewe ni sahihi sana kwa sababu upo dini fulani, una rangi fulani au unatokea kabila fulani maana hata ungezaliwa upande mwingine basi ungeamini hayo”

“Naombeni kwa siku ya leo tuishie hapa ila kila mmoj wetu aondoke kwenye moyo ake akijiahidi kwamba atakuwa mtu wa kwanza kuudumisha upendo wa kweli hapa duniani popote pale atakapokuwepo na kama kuna mtu au watu una kinyongo nao basi kuanzia leo fungua moyo wako baraka tele zitakuwa zi juu yako MUNGU awabariki sana, Amen” mchungaji alimaliza ibada yake na kuanza kukusanya baadhi ya makablasha yake kutoka juu ya madhabahu hapo baada ya kusali

“Ameni” waumini wote ambao licha ya kuwa ni asubuhi na mapema sana waliokuwa wamejaa ndani ya kanisa hilo kubwa sana ambalo lilijengwa kisasa waliitikia na kuanza kupeana mikono ya upendo huku akianza kutoka mmoja mmoja na tayari kulikuwa kumekucha kabisa. Mchungaji huyo akiwa anakusanya hizo karatasi zake ambazo zilikuwa na hayo maandiko aliona kwenye simu yake alama ya kengele ambayo katikati ilikuwa na sifuri, aliangalia huku na huku na kuwaona waumini wakiendelea kutoka humo ndani, alichukua simu haraka na kuingia kwenye chumba chake ambacho ndiyo ilikuwa ofisi yake kubwa alihakikisha ameifunga milango yote na kuzima kamera zote humo ndani kisha akaichukua simu yake na kuifungua upande wa video ambapo aliipiga.

“Dady hello” upande wa pili ilisikika sauti laini ya mideko ya mtoto wa kike akiwa anafurahia kumuona baba yake mbaye aliishia kutabasamu, mwanamke huyo ambaye mchungaji JOHN alikuwa akiongea naye alikuwa ni Monalisa kutoka ndani ya nchi ya Marekani na huyu ndiye aliye jinasibu kwenye simu hiyo kwamba ndiye baba yake.

“Hhahahahah my daughter you are so beautiful, enhe nambie kivuruge wangu kuna nini mpya maana umenishtua ni mapema sana saivi” aliongea akiwa anakohoa kidogo kuliweka koo lake vizuri.

“Nataka kuja huko?” mzee huyo alibaki ameganda kwenye hiyo simu baada ya kuisikia kauli hiyo ni kama hakutarajia kukutana na jambo la namna hiyo ilimlazimu Monalisa arudie tena.

“Unataka kuja huku ili ufanye nini?” swali lake ni kama lilimkera Monalisa
“Siko sawa nataka nije nipumzike huko halafu kuna kazi ambayo inabidi niimalizie huko”

“Kuna kazi gani ambayo unaweza kuimaliza huku? Tuna watu ambao wanaweza kuifanya hii kazi vizuri bila shida yoyote hivyo wewe baki tu huko huko kwanza nitakuita mwenyewe”

“Hii ni amri kutoka juu baba ni lazima nije muda huu nataka nijiandae nielekee airport” mchungaji huyo alimuangalia binti yake huyo kwa hasira sana kwa sababu mpaka hapo hakuwa na namna yoyote ile ya kuweza kumzuia, aliikata simu hiyo kwa hasira baada ya dakika moja akaitafuta namba nyingine na kuipiga muda mfupi baada ya kukata simu ya Monalisa.

“Uko wapi Slyvester?”
“Nipo kwenye gari bosi”

“Njoo ofisini haraka sana”
“Sawa bosi” alikata simu hiyo akiwa anazunguka humo ndani kama hakuwa sawa kimawazo, alionekana kijana mmoja ambaye mwilini mwake alikuwa ndani ya suti nyeusi, huyo wengi walikuwa wanamjua kama mlinzi binafsi wa mchungaji huyo hivyo hata waumini wa kanisa hilo walikuwa wakimjua na hakukuwa na tatizo lolote lile.

“Ulikuwa unajua kuhusu ujio wa Monalisa?” alimuuliza kijana huyo akiwa amemkazia macho yake

“Hapana bosi”
“Huyu mtoto anaanza kunipanda sana kichwani, kalazimisha anakuja huku Tanzania sasa nataka uhakikishe anakuwa salama tangu anatua airport mpaka unamfikisha nyumbani na utawasiliana naye ujue anafikia nyumba ipi kisha utanipa mrejesho”

“Sawa bosi”
“Haya unaweza Kwenda ukaniacha pekeyangu niandae kipindi maana saa nne nina kazi ya kuongoza misa nyingine” aliongea huku akiisogeza tarakishi yake na kuishika vizuri kwenye mikono yake alikuwa na mawazo sana.



Jason akiwa kwenye mshangao mzito sana wa kuhitaji kuujua ukweli ambao ulikuwa umejificha kuhusu kaka yake pamoja na taharuki ambayo alibaki nayo kwenye kichwa chake baada ya kaka yake kumwambia kwamba alikuwa anamjua kuliko hata yeye mwenyewe alivyokuwa anajijua aliufunua ukurasa ambao ulikuwa unafuata ila apate kuelewa ni kwa namna gani kaka yake ndiye mtu ambaye alihitaji awe kama yeye alivyokuwa yupo kwa sasa, lakini kabla hajayatua macho yake hata kwenye neno moja kwenye hiyo diary alishtuka sana baada ya simu yake hiyo kutoa mwanga mwekundu mkali sana ndipo alipokumbuka kwamba alikuwa ameizima, haraka sana aliifunga hiyo diary huku akiwa anaiwasha simu yake hiyo baada ya kuwaka tu simu ilianza kuita.

“Alphonce uko wapi mbona code inasoma kama upo Tanzania na nilitegemea ungechelewa sana kufika kwa sababu ya umbali ambao nilikuwa na uhakika nao kwa mahesabu yangu?”

“Daah bro nimepiga sana nikaona hupatikani nipo airport hapa sielewi hata kwa Kwenda naomba uje unichukue kwanza hayo mengine tutaongea tukikutana” huyo ndiye mwanaume ambaye alikuwa anamsubiri aje ampatie jibu la mwisho kabla ya yeye kutoa maamuzi yake kama alivyo ahidi. Hakuongeza neno lolote lile zaidi ya kuikata simu hiyo na kutoka humo ndani, alisogea mpaka pale nje na kuelekea sehemu ambayo yalikuwa yamehifadhiwa magari ya familia yake hiyo alipanda kwenye gari moja na kutoka humo ndani akiwa na spidi kali sana barabara iligeuka kuwa yakwake kwa muda ambao aliamua kuingia ndani ya barabara hiyo.

Dakika za kuhesabu thelathini tu zilimtosha sana kufika hapo JNIA, aliipiga simu kwa kijana huyo aliyekuwa anaitwa Alphonce, kwa mwonekano wa umri wao hawakupishana sana lakini kijana huyo alionekana kumheshimu mno Jason, mwonekano wake ulikuwa kama wale wamarekani Weusi ambao rangi yao inaeleka kuwa nyeupe ikiwa imechanganyika na wekundu kiasi, asili yake kwa kuzaliwa alizaliwa ndani ya jiji la TORONTO huko ndani ya nchi kubwa zaidi duniani CANADA, walikumbatiana na kulisogelea kisha awakapanda kwenye gari na kuondoka.

Walipeana salamu za kuto onana kwa miaka mingi kidogo kutokana na kila mtu kuwa busy na maisha yake pamoja na pole kwa matatizo yaliyokuwa yametokea ila hatimae kazi zilikuwa zimewakutanisha tena mpaka siku hiyo ambayo alikuwa amepigiwa simu, hawakuwa na muda wa kupoteza sana kilicho fanyika Jason alimsimulia matukio yote namna yalivyokuwa yametokea huku wakiwa mbele ya skrini kubwa sana ndani ya nyumba ya kaka yake Jason baada ya kufika nyumbani ambapo alikuwa ameweka frash ambayo ilikuwa na video ambayo ilikuwa inaonesha kifo cha mheshimiwa raisi huku kwenye meza kukiwa na picha za ndugu zake ambao wao hakukuwa na video yao hata moja ambayo ilikuwa imepatikana zaidi ya kuwapiga picha wakiwa tayari wamepoteza maisha. Alphonce alikuwa makini sana kuiangalia video hiyo ambayo aliihitaji irudiwe mara mbili tu kisha akampa maelekezo Jason aisimamishe kisha akamuuliza Jason kwamba kwenye hiyo video aligundua nini na nini? lakini kabla Jason hajajibu alimwangalia sana kijana huyo mpaka yeye mwenyewe alijishtukia.

“Alphonce wakati nakupigia simu jana ulikuwa wapi mpaka umefika Tanzania haraka sana namna hii?” alimuuliza swali akiwa ana mashaka ndani yake kwani alihisi kwamba huenda kijana huyo kuna mambo alikuwa anamficha umbali wa kutoka Canada mpaka Tanzania na muda ambao alikuwa amefika havikumuingia akilini kabisa Jason.

“Jana wakati unanipigia simu sikuwa Canada, nilikuwa Nigeria” alijibu huku akiinama chini ni kama alikuwa anasikitika sana

“Nini kilitokea?” Jason alimuuliza kistaarabu baada ya kuhisi mtu huyo huenda kuna tatizo kubwa limetokea upande wake.

“Nilifukuzwa jeshini baada ya mheshimiwa Waziri wa ulinzi kugundua kwamba natoka na mtoto wake hivyo kwa sasa huwa nafanya kazi za kukodiwa”

“Mpaka leo haujaacha kuua watu?”

“Hayo ndiyo maisha yanayo nilipa, jana nimetoka kumuua tajiri mmoja Nigeria nimelipwa dola milioni 5 sasa nitafanyaje kaka ndiyo sehemu ambayo inanifanya naendesha familia yangu kule Canada” Jason alimpiga mgongoni Alphonce kama ishara ya kumwambia kwamba wapo pamoja na hapa alikuwa amefika kwa ndugu yake.

“Ulipaswa kunambia mapema kuhusu hili suala tungesha limaliza” aliongea huku wakitabasamu pamoja na kuunganisha mikono yao na hivyo ndivyo huwa wanafanya wanaume kumaliza tofauti zao kama mambo hayajaenda kama vile walivyokuwa wametarajia.

Jason alimweleza kwamba aligundua muuaji na mfanyaji wa hilo tukio alikuwa bado yupo hai licha ya mtu mwingine kuuawa mbele ya mahakama kwa kudaiwa kuweza kumuua mheshimiwa raisi kwa sababu mtu huyo alikuja kuiua na familia yake kwa baadae, Alphonce alisikiliza kwa umakini sana kisha akasimama na kuisogelea ile skrini kubwa ambayo ilikuwa inaonyesha video hiyo.

“Nadhani hili tukio limefanywa na miongoni mwa watu ambao ni wavivu wa kufikiri sana” alitamka akiwa anamgeukia Jason na kumwangalia usoni

“Unamaanisha nini?”
“Duniani hakuna mdunguaji mjinga wa kuacha alama kijinga namna hii na huenda huyu aliyekuwa anafanya hili jambo ni mtu ambaye ana uwezo mdogo sana kwenye hiyo elimu ya udunguaji, mdunguaji anaye ifanya kazi yake vyema hawezi kuua kizembe sana namna hii kasi ya hiyo risasi inavyoonekana kabisa ilikuwa na spidi ndogo sana maana yake hata aliye irusha alikuwa anatumia silaha ya kawaida sana na hata kwenye mikono yake hakuwa na nguvu hata kidogo ila kitu kinacho nishangaza sana ni kwamba mbona wauaji walikuwa wapo wawili tofauti? Hili ndilo swali ambalo kwa mimi naweza kuumiza akili mpaka muda huu ila sio kuhusu huyo muuaji kwani huyu tutampata kwa muda mfupi tu” aliongea kirahisi sana lakini alikuwa akimaanisha sana kile ambacho alikuwa anakiongea

"Una maanisha nini kusema kwamba kulikuwa na wauaji wawili?" Jason aliuliza kwa mshangao kidogo maana hakuona dalili yoyote ile ya uwepo wa watu hao wawili kama ilivyokuwa imesemekana

“Kama una macho mazito kiasi kikubwa basi huwezi ukajua kwamba wapo wawili, angalia wakati hii risasi imetua kwenye kichwa cha raisi kwa mbali hapo unaona kama kuna kitu kinapita kama upepo kuelekea sehemu aliyopo mheshimiwa raisi, huo sio upepo hizo ni risasi za masafa marefu ambazo huwa zinatumiwa na wadunguaji wa aina yangu, hii ikirushwa wanaweza kuiona watu wachache sana kwa sababu huwa zinatoka kwenye mikono imara lakini pia kutoka kwa watu ambao ni wauaji wa kutisha sana” alipumzika kidogo baada ya kuona kama Jason anashangaa sana hicho kitu, Alphonce aliisimamisha na kuanza kuipeleka mbele taratibu video hiyo kisha akaikuza ndipo Jason kwa mbali alipo ona kitu kama risasi kinapita japo kilikuwa kinaonekana kwa mbali sana, alitikisa kichwa chake.

“Ina maana wauaji walikuwa wawili kwa wakati mmoja?” aliuliza akimuangalia Alphonce

“Yes, nadhani walitofautiana tu kwenye suala la muda wa kufanya mauaji ila wote wailikuwa wana lengo moja hilo hilo sasa swali ni je ni watu wawili tofauti ambao walikuwa wanaifanya hii kazi au ni watu ambao walitoka sehemu moja ila walihitaji uhakika wa kazi yao kukamilika? Ila nimeshangaa sana inakuwaje gari ya mheshimiwa raisi inaweza kupitisha risasi kirahisi sana namna hii kwani huwa hamchukui tahadhari kwa viongozi wakubwa?” Alphonce alimuuliza Jason akiwa anarudi kukaa kwenye sofa.

“Gari ya mheshimiwa huwa ina ulinzi binafsi hata kabla ya hatari kutokea lazima itoe viashiria sasa mpaka sasa sijui kilifanyika nini?”

“Kitu cha kwanza kwa sasa inatakiwa hiyo gari ipatikane ili tujiridhishe kuhusu huyu muuaji wa pili kwa sababu huyu ndiye anaonekana kuwa mlengwa na ni hatari zaidi, kwa vile risasi ya kwanza ilikuwa imepenya na mheshimiwa ikamkuta kichwani, maana yake ile risasi ya pili lazima ilimkosa maana mtu akipigwa risasi lazima atapoteza uwezo wa kukisimamisha kichwa chake na atainama hivyo kwa sehemu ambayo yeye alilengwa kichwani kama aliinama basi kuna mawili kama nyuma yake kulikuwa na mtu itakuwa ilimpata na kama hakukuwa na mtu basi ilipasua kitu chochote ndani ya hiyo gari” mtaalamu wa masuala ya udunguaji Alphonce alikuwa anatoa maelezo ambayo yalionekana kumrishisha Jason hivyo walitakiwa kufanyia sana uchunguzi juu ya jambo hilo.

Jason kuna nini hasa mpaka anajiingiza kwenye haya mambo mazito namna hii, watafanikiwa kumpata huyo muuaji? Je atatoa tamko gani kuhusu wahusika wa hayo matukio kama alivyo ahidi?.......32 inafika mwisho tukutane wakati ujao.

Wasalaam

Bux the storyteller.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…