STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
STORY WRITER: BUX THE STORYTELLER
WHATSAPP : 0621567672
EMAIL:
thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA 32
SONGA NAYO............
“Miaka mingi iliyoweza kupita niliwahi kupata mwaliko wa kidini kwenye nchi ya waitaliano na bahati iliyokuwa njema huko nilikuwa nina rafiki yangu mmoja ambaye tulisoma naye tukiwa wadogo yeye alikuwa anasomea upadri huko basi baada ya kusikia kwamba namimi nimeenda kwenye ile nchi alisema nisije nikaenda kule na nikaondoka kabla sijaonana naye. Sikuwa na namna kwa sababu ulikuwa umepita muda mrefu sana bila ya kuonana, baada ya mimi pia kumaliza mikutano yangu nilienda mpaka sehemu ambayo walikuwa wanaishi, nilibahatika sana kuhudhuria vipindi kadhaa vya mafundisho yao nilistaajabu mno huenda kwa sababu kilikuwa ni kitu kigeni sana kwangu”
“Siku ile nilishangaa mapadri wanasoma mpaka Quran kwa mara ya kwanza nilihisi kama kwa maadili ya dini ya kikirsto walikuwa wakitenda ni dhambi ila kwa baadae nilikuja kugundua kwamba kumbe huwa wanajifunza ili kuweza kuzijua dini zote kwa usahihi na kwamba dini siyo kigezo cha kuwatenganisha watu yaani wakristo na Waislamu sisi wote ni wamoja ila utofauti wetu ni kwenye suala la imani tu na ndiyo maana hata MUNGU tunaye muabudu ni mmoja tu pekee. Kupitia siku ile nilipata somo kubwa sana kwamba kumbe ni ukosefu wa uelewa mdogo tu ndio huwa unatutenganisha na kutugombanisha ila sisi wote tunapaswa kuishi kwa kushirikiana sana kupitia neno upendo hivyo usije ukajiona wewe ni sahihi sana kwa sababu upo dini fulani, una rangi fulani au unatokea kabila fulani maana hata ungezaliwa upande mwingine basi ungeamini hayo”
“Naombeni kwa siku ya leo tuishie hapa ila kila mmoj wetu aondoke kwenye moyo ake akijiahidi kwamba atakuwa mtu wa kwanza kuudumisha upendo wa kweli hapa duniani popote pale atakapokuwepo na kama kuna mtu au watu una kinyongo nao basi kuanzia leo fungua moyo wako baraka tele zitakuwa zi juu yako MUNGU awabariki sana, Amen” mchungaji alimaliza ibada yake na kuanza kukusanya baadhi ya makablasha yake kutoka juu ya madhabahu hapo baada ya kusali
“Ameni” waumini wote ambao licha ya kuwa ni asubuhi na mapema sana waliokuwa wamejaa ndani ya kanisa hilo kubwa sana ambalo lilijengwa kisasa waliitikia na kuanza kupeana mikono ya upendo huku akianza kutoka mmoja mmoja na tayari kulikuwa kumekucha kabisa. Mchungaji huyo akiwa anakusanya hizo karatasi zake ambazo zilikuwa na hayo maandiko aliona kwenye simu yake alama ya kengele ambayo katikati ilikuwa na sifuri, aliangalia huku na huku na kuwaona waumini wakiendelea kutoka humo ndani, alichukua simu haraka na kuingia kwenye chumba chake ambacho ndiyo ilikuwa ofisi yake kubwa alihakikisha ameifunga milango yote na kuzima kamera zote humo ndani kisha akaichukua simu yake na kuifungua upande wa video ambapo aliipiga.
“Dady hello” upande wa pili ilisikika sauti laini ya mideko ya mtoto wa kike akiwa anafurahia kumuona baba yake mbaye aliishia kutabasamu, mwanamke huyo ambaye mchungaji JOHN alikuwa akiongea naye alikuwa ni Monalisa kutoka ndani ya nchi ya Marekani na huyu ndiye aliye jinasibu kwenye simu hiyo kwamba ndiye baba yake.
“Hhahahahah my daughter you are so beautiful, enhe nambie kivuruge wangu kuna nini mpya maana umenishtua ni mapema sana saivi” aliongea akiwa anakohoa kidogo kuliweka koo lake vizuri.
“Nataka kuja huko?” mzee huyo alibaki ameganda kwenye hiyo simu baada ya kuisikia kauli hiyo ni kama hakutarajia kukutana na jambo la namna hiyo ilimlazimu Monalisa arudie tena.
“Unataka kuja huku ili ufanye nini?” swali lake ni kama lilimkera Monalisa
“Siko sawa nataka nije nipumzike huko halafu kuna kazi ambayo inabidi niimalizie huko”
“Kuna kazi gani ambayo unaweza kuimaliza huku? Tuna watu ambao wanaweza kuifanya hii kazi vizuri bila shida yoyote hivyo wewe baki tu huko huko kwanza nitakuita mwenyewe”
“Hii ni amri kutoka juu baba ni lazima nije muda huu nataka nijiandae nielekee airport” mchungaji huyo alimuangalia binti yake huyo kwa hasira sana kwa sababu mpaka hapo hakuwa na namna yoyote ile ya kuweza kumzuia, aliikata simu hiyo kwa hasira baada ya dakika moja akaitafuta namba nyingine na kuipiga muda mfupi baada ya kukata simu ya Monalisa.
“Uko wapi Slyvester?”
“Nipo kwenye gari bosi”
“Njoo ofisini haraka sana”
“Sawa bosi” alikata simu hiyo akiwa anazunguka humo ndani kama hakuwa sawa kimawazo, alionekana kijana mmoja ambaye mwilini mwake alikuwa ndani ya suti nyeusi, huyo wengi walikuwa wanamjua kama mlinzi binafsi wa mchungaji huyo hivyo hata waumini wa kanisa hilo walikuwa wakimjua na hakukuwa na tatizo lolote lile.
“Ulikuwa unajua kuhusu ujio wa Monalisa?” alimuuliza kijana huyo akiwa amemkazia macho yake
“Hapana bosi”
“Huyu mtoto anaanza kunipanda sana kichwani, kalazimisha anakuja huku Tanzania sasa nataka uhakikishe anakuwa salama tangu anatua airport mpaka unamfikisha nyumbani na utawasiliana naye ujue anafikia nyumba ipi kisha utanipa mrejesho”
“Sawa bosi”
“Haya unaweza Kwenda ukaniacha pekeyangu niandae kipindi maana saa nne nina kazi ya kuongoza misa nyingine” aliongea huku akiisogeza tarakishi yake na kuishika vizuri kwenye mikono yake alikuwa na mawazo sana.
Jason akiwa kwenye mshangao mzito sana wa kuhitaji kuujua ukweli ambao ulikuwa umejificha kuhusu kaka yake pamoja na taharuki ambayo alibaki nayo kwenye kichwa chake baada ya kaka yake kumwambia kwamba alikuwa anamjua kuliko hata yeye mwenyewe alivyokuwa anajijua aliufunua ukurasa ambao ulikuwa unafuata ila apate kuelewa ni kwa namna gani kaka yake ndiye mtu ambaye alihitaji awe kama yeye alivyokuwa yupo kwa sasa, lakini kabla hajayatua macho yake hata kwenye neno moja kwenye hiyo diary alishtuka sana baada ya simu yake hiyo kutoa mwanga mwekundu mkali sana ndipo alipokumbuka kwamba alikuwa ameizima, haraka sana aliifunga hiyo diary huku akiwa anaiwasha simu yake hiyo baada ya kuwaka tu simu ilianza kuita.
“Alphonce uko wapi mbona code inasoma kama upo Tanzania na nilitegemea ungechelewa sana kufika kwa sababu ya umbali ambao nilikuwa na uhakika nao kwa mahesabu yangu?”
“Daah bro nimepiga sana nikaona hupatikani nipo airport hapa sielewi hata kwa Kwenda naomba uje unichukue kwanza hayo mengine tutaongea tukikutana” huyo ndiye mwanaume ambaye alikuwa anamsubiri aje ampatie jibu la mwisho kabla ya yeye kutoa maamuzi yake kama alivyo ahidi. Hakuongeza neno lolote lile zaidi ya kuikata simu hiyo na kutoka humo ndani, alisogea mpaka pale nje na kuelekea sehemu ambayo yalikuwa yamehifadhiwa magari ya familia yake hiyo alipanda kwenye gari moja na kutoka humo ndani akiwa na spidi kali sana barabara iligeuka kuwa yakwake kwa muda ambao aliamua kuingia ndani ya barabara hiyo.
Dakika za kuhesabu thelathini tu zilimtosha sana kufika hapo JNIA, aliipiga simu kwa kijana huyo aliyekuwa anaitwa Alphonce, kwa mwonekano wa umri wao hawakupishana sana lakini kijana huyo alionekana kumheshimu mno Jason, mwonekano wake ulikuwa kama wale wamarekani Weusi ambao rangi yao inaeleka kuwa nyeupe ikiwa imechanganyika na wekundu kiasi, asili yake kwa kuzaliwa alizaliwa ndani ya jiji la TORONTO huko ndani ya nchi kubwa zaidi duniani CANADA, walikumbatiana na kulisogelea kisha awakapanda kwenye gari na kuondoka.
Walipeana salamu za kuto onana kwa miaka mingi kidogo kutokana na kila mtu kuwa busy na maisha yake pamoja na pole kwa matatizo yaliyokuwa yametokea ila hatimae kazi zilikuwa zimewakutanisha tena mpaka siku hiyo ambayo alikuwa amepigiwa simu, hawakuwa na muda wa kupoteza sana kilicho fanyika Jason alimsimulia matukio yote namna yalivyokuwa yametokea huku wakiwa mbele ya skrini kubwa sana ndani ya nyumba ya kaka yake Jason baada ya kufika nyumbani ambapo alikuwa ameweka frash ambayo ilikuwa na video ambayo ilikuwa inaonesha kifo cha mheshimiwa raisi huku kwenye meza kukiwa na picha za ndugu zake ambao wao hakukuwa na video yao hata moja ambayo ilikuwa imepatikana zaidi ya kuwapiga picha wakiwa tayari wamepoteza maisha. Alphonce alikuwa makini sana kuiangalia video hiyo ambayo aliihitaji irudiwe mara mbili tu kisha akampa maelekezo Jason aisimamishe kisha akamuuliza Jason kwamba kwenye hiyo video aligundua nini na nini? lakini kabla Jason hajajibu alimwangalia sana kijana huyo mpaka yeye mwenyewe alijishtukia.
“Alphonce wakati nakupigia simu jana ulikuwa wapi mpaka umefika Tanzania haraka sana namna hii?” alimuuliza swali akiwa ana mashaka ndani yake kwani alihisi kwamba huenda kijana huyo kuna mambo alikuwa anamficha umbali wa kutoka Canada mpaka Tanzania na muda ambao alikuwa amefika havikumuingia akilini kabisa Jason.
“Jana wakati unanipigia simu sikuwa Canada, nilikuwa Nigeria” alijibu huku akiinama chini ni kama alikuwa anasikitika sana
“Nini kilitokea?” Jason alimuuliza kistaarabu baada ya kuhisi mtu huyo huenda kuna tatizo kubwa limetokea upande wake.
“Nilifukuzwa jeshini baada ya mheshimiwa Waziri wa ulinzi kugundua kwamba natoka na mtoto wake hivyo kwa sasa huwa nafanya kazi za kukodiwa”
“Mpaka leo haujaacha kuua watu?”
“Hayo ndiyo maisha yanayo nilipa, jana nimetoka kumuua tajiri mmoja Nigeria nimelipwa dola milioni 5 sasa nitafanyaje kaka ndiyo sehemu ambayo inanifanya naendesha familia yangu kule Canada” Jason alimpiga mgongoni Alphonce kama ishara ya kumwambia kwamba wapo pamoja na hapa alikuwa amefika kwa ndugu yake.
“Ulipaswa kunambia mapema kuhusu hili suala tungesha limaliza” aliongea huku wakitabasamu pamoja na kuunganisha mikono yao na hivyo ndivyo huwa wanafanya wanaume kumaliza tofauti zao kama mambo hayajaenda kama vile walivyokuwa wametarajia.
Jason alimweleza kwamba aligundua muuaji na mfanyaji wa hilo tukio alikuwa bado yupo hai licha ya mtu mwingine kuuawa mbele ya mahakama kwa kudaiwa kuweza kumuua mheshimiwa raisi kwa sababu mtu huyo alikuja kuiua na familia yake kwa baadae, Alphonce alisikiliza kwa umakini sana kisha akasimama na kuisogelea ile skrini kubwa ambayo ilikuwa inaonyesha video hiyo.
“Nadhani hili tukio limefanywa na miongoni mwa watu ambao ni wavivu wa kufikiri sana” alitamka akiwa anamgeukia Jason na kumwangalia usoni
“Unamaanisha nini?”
“Duniani hakuna mdunguaji mjinga wa kuacha alama kijinga namna hii na huenda huyu aliyekuwa anafanya hili jambo ni mtu ambaye ana uwezo mdogo sana kwenye hiyo elimu ya udunguaji, mdunguaji anaye ifanya kazi yake vyema hawezi kuua kizembe sana namna hii kasi ya hiyo risasi inavyoonekana kabisa ilikuwa na spidi ndogo sana maana yake hata aliye irusha alikuwa anatumia silaha ya kawaida sana na hata kwenye mikono yake hakuwa na nguvu hata kidogo ila kitu kinacho nishangaza sana ni kwamba mbona wauaji walikuwa wapo wawili tofauti? Hili ndilo swali ambalo kwa mimi naweza kuumiza akili mpaka muda huu ila sio kuhusu huyo muuaji kwani huyu tutampata kwa muda mfupi tu” aliongea kirahisi sana lakini alikuwa akimaanisha sana kile ambacho alikuwa anakiongea
"Una maanisha nini kusema kwamba kulikuwa na wauaji wawili?" Jason aliuliza kwa mshangao kidogo maana hakuona dalili yoyote ile ya uwepo wa watu hao wawili kama ilivyokuwa imesemekana
“Kama una macho mazito kiasi kikubwa basi huwezi ukajua kwamba wapo wawili, angalia wakati hii risasi imetua kwenye kichwa cha raisi kwa mbali hapo unaona kama kuna kitu kinapita kama upepo kuelekea sehemu aliyopo mheshimiwa raisi, huo sio upepo hizo ni risasi za masafa marefu ambazo huwa zinatumiwa na wadunguaji wa aina yangu, hii ikirushwa wanaweza kuiona watu wachache sana kwa sababu huwa zinatoka kwenye mikono imara lakini pia kutoka kwa watu ambao ni wauaji wa kutisha sana” alipumzika kidogo baada ya kuona kama Jason anashangaa sana hicho kitu, Alphonce aliisimamisha na kuanza kuipeleka mbele taratibu video hiyo kisha akaikuza ndipo Jason kwa mbali alipo ona kitu kama risasi kinapita japo kilikuwa kinaonekana kwa mbali sana, alitikisa kichwa chake.
“Ina maana wauaji walikuwa wawili kwa wakati mmoja?” aliuliza akimuangalia Alphonce
“Yes, nadhani walitofautiana tu kwenye suala la muda wa kufanya mauaji ila wote wailikuwa wana lengo moja hilo hilo sasa swali ni je ni watu wawili tofauti ambao walikuwa wanaifanya hii kazi au ni watu ambao walitoka sehemu moja ila walihitaji uhakika wa kazi yao kukamilika? Ila nimeshangaa sana inakuwaje gari ya mheshimiwa raisi inaweza kupitisha risasi kirahisi sana namna hii kwani huwa hamchukui tahadhari kwa viongozi wakubwa?” Alphonce alimuuliza Jason akiwa anarudi kukaa kwenye sofa.
“Gari ya mheshimiwa huwa ina ulinzi binafsi hata kabla ya hatari kutokea lazima itoe viashiria sasa mpaka sasa sijui kilifanyika nini?”
“Kitu cha kwanza kwa sasa inatakiwa hiyo gari ipatikane ili tujiridhishe kuhusu huyu muuaji wa pili kwa sababu huyu ndiye anaonekana kuwa mlengwa na ni hatari zaidi, kwa vile risasi ya kwanza ilikuwa imepenya na mheshimiwa ikamkuta kichwani, maana yake ile risasi ya pili lazima ilimkosa maana mtu akipigwa risasi lazima atapoteza uwezo wa kukisimamisha kichwa chake na atainama hivyo kwa sehemu ambayo yeye alilengwa kichwani kama aliinama basi kuna mawili kama nyuma yake kulikuwa na mtu itakuwa ilimpata na kama hakukuwa na mtu basi ilipasua kitu chochote ndani ya hiyo gari” mtaalamu wa masuala ya udunguaji Alphonce alikuwa anatoa maelezo ambayo yalionekana kumrishisha Jason hivyo walitakiwa kufanyia sana uchunguzi juu ya jambo hilo.
Jason kuna nini hasa mpaka anajiingiza kwenye haya mambo mazito namna hii, watafanikiwa kumpata huyo muuaji? Je atatoa tamko gani kuhusu wahusika wa hayo matukio kama alivyo ahidi?.......32 inafika mwisho tukutane wakati ujao.
Wasalaam
Bux the storyteller.