INSP Hadja Mfinaga: Wazazi Tusiwafiche Watoto wenye uhitaji

INSP Hadja Mfinaga: Wazazi Tusiwafiche Watoto wenye uhitaji

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-07-19 at 07.41.27_c1a3c972.jpg
Mkuu wa dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Hadja Mfinaga amewaomba wazazi wilayani humo kutowaficha watoto wenye mahitaji maalum na badala yake wawafikishe katika vituo na shule maalum ambazo zitawaendeleza kielimu.

Kauli hiyo ameitoa alipotembelea shule ya mahitaji maalum ya Murugwanza ambapo alitoa pongezi kwa walimu kwa kazi nzuri wanayofanya ya kufundisha watoto hao
WhatsApp Image 2024-07-19 at 07.41.28_15a6cf0a.jpg
Aidha aliwataka wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum kutowaficha na badala yake kuwafikikisha katika vituo husika ili wapate elimu kama watoto wengine.

Mkaguzi Mfinaga amesisitiza kuwa watoto wenye mahitaji maalum wanaouwezo mkubwa wakiwezeshwa kielimu ambapo amewaomba wazazi kutilia maanani swala hilo ili kuwakomboa watoto hao kielimu ambapo alisema kuwa elimu kwa watoto hao ni ufunguo wa maisha.

Vilevile Mkaguzi huyo amesisitiza kuwa endapo mzazi ataacha kumpatia elimu mtoto wake mwenye ulemavu atambue kuwa amefanya ukatili huku akiweka wazi kuwa Jeshi la Polisi halito muonea muhari mzazi wa aina hiyo alisema Mkuu wa dawati la Jinsia na watoto Wilaya ya Ngara.
 
Back
Top Bottom