Instagram imenisaidia kupata profit ya milion 8 mwaka huu 2017

Nzuri, as long upo home, we will be tugeza😀
 
Safi man ifike hatua itambulike Instagram sio Kwa ajili ya kuonesha umevaaa nn? Na kutaka sifa Kwa watu,
 
Asikwambie mtu social network zinanguvu sana katika kutangaza biashara.Hongera sana,vijana ambao tuna lalamika hatuna ajira tujifunze kitu hapa sio tunasoma tu kama hadithi za kinamatola kula konokono.
 
Mimi nashindwa jinsi ya kupromote page ,ninaambiwa nilipie ili watu wengi waione so nashindwa namna ya kulipia kama kuna unajua nielekeza mkuu
Ili uweze kulipia ni lazima uwe na kadi ya visa mfana UBA n.k. pia ukilipia facebook wanatuma tangazo lako kwa walengwa tu, hivyo kukurhisishia kazi ya kunasa wateja.Nicheki kwenye 0713-039875 nitakusaidia, humu sipo mara kwa mara
 
Hongera sana.Jitahidi zaidi mwakani na jitahidi kuwa na matumizi mazuri ya hela ili mwishoni ufaidi zaidi faida yako
 
Hongera sana, inapendeza na kufurahisha vijana wanapojituma.
 
Mkuu t-shirts unaprint au una design then wengine wanaprint?malipo ya wateja wako wa Instagram mnalipana vip? Hapo nazungumzia wale wanaohitaji kazi soft copy mfano flier's and posters or LOGO. Hujawahi kutapeliwa??Ukinipa mwanga hapo nami nazama then ntakuja na mrejesho mwakani
 
hongera, ila angalia tra wasije wakakufuata na mashine zao za fda
 
tshirt mimi naziprint ndio kazi yangu.. kuna watu wengi wanauza tshirt wanakuja nawatengenezea logo wanazotaka kisha nawaprintia kwenye tshirt zao mimi mwenyewe...

malipo tunalipana kawaida tu maana ni wanakuja kwnagu tunaonana.. baada ya kuwasiliana via instagram na namba za simu ambazo wanazitoa instagram..... graphics design nafanya sana tu kama za fliers, banners ila kwa mfumo huo huo unakuja ofisin unalipia advance ndio nakufanyia kazi.. ukiifata unamalizia na kuchukua kazi yako

kutapeliwa sijawai zaidi ya kupata hasara tu za kuharibu tshirt wakati naiprint... ambazo ni kawaida tu na hazitokei kila siku...

sifanyi kazi yoyote ambayo haijalipiwa advance... so naanzia wapi kutapeliwa... na sitoi kazi mpaka imaliziwe iliyobaki... maana mimi nauza huduma siuzi budhaa zinazooza... kiasi cha kumkopesha mtu kuogopa zitaharibika au ku expire....

 
Wakati wengine wakifanya mzaha na mitandao ya kijamii wengine wanafanya maisha yaende kwa mitandao hiyo hiyo...binafsi yangu nakupongeza kwa kupokea ushauri wa rafiki yako na kuufanyia kazi.
Huyo rafiki yako ndiye mwema na wafaida kuliko wengine, mshikilie usimwache aende.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…