Instagram imenisaidia kupata profit ya milion 8 mwaka huu 2017

Instagram imenisaidia kupata profit ya milion 8 mwaka huu 2017

Nzuri, as long upo home, we will be tugeza😀
 
Safi man ifike hatua itambulike Instagram sio Kwa ajili ya kuonesha umevaaa nn? Na kutaka sifa Kwa watu,
 
habari wadau..

mimi ni artist tu niliyebase kwenye graphics designing, tshirt printing, posters and banners printing na proffessional photography...

nilianza business miaka kama minne iliyopita ila sikuwa na page ya social network..

so nikitoka job nilipoajiriwa.. naingia workshop na nafanya kazi za wateja wangu mdogo mdogo...

mwaka jana kuna mtu akanishauri nifungue page ya biashara instagram niwe na post kazi zangu za kila siku.. itanisaidia sana watu kujua nachofanya na kuja kwa wingi...

kweli nikaanzisha page ya tshirt tu na kuanza kupost kazi na kuweka namba za simu... kiukweli mauzo yaliongezeka sana ikawa karibu kila siku nina kazi ya mteja...

nina tabia ya kuandika kwenye daftari kila kazi nayoifanya pia kwa ajili ya mahesabu..

siku ya xmass juzi nilichukua daftari langu na kuangalia profit ambayo biashara imezalisha mwaka huu ambazo ziikuja kwa wateja waliotokea instagram.. na kukuta milion 8 na laki moja na elfu 32 ni faida from instagram...

japo hela nimezitumbua sana.. ila nimefanikiwa kufungua studio ya kisasa ya picha kwa hela ambazo ni faida ya tshirt page ya instagram

Tshirt Garage Mabibo Hostel (@tshirt_garage_mabibo_hostel) • Instagram photos and videos
Asikwambie mtu social network zinanguvu sana katika kutangaza biashara.Hongera sana,vijana ambao tuna lalamika hatuna ajira tujifunze kitu hapa sio tunasoma tu kama hadithi za kinamatola kula konokono.
 
Mimi nashindwa jinsi ya kupromote page ,ninaambiwa nilipie ili watu wengi waione so nashindwa namna ya kulipia kama kuna unajua nielekeza mkuu
Ili uweze kulipia ni lazima uwe na kadi ya visa mfana UBA n.k. pia ukilipia facebook wanatuma tangazo lako kwa walengwa tu, hivyo kukurhisishia kazi ya kunasa wateja.Nicheki kwenye 0713-039875 nitakusaidia, humu sipo mara kwa mara
 
Hongera sana.Jitahidi zaidi mwakani na jitahidi kuwa na matumizi mazuri ya hela ili mwishoni ufaidi zaidi faida yako
 
Hongera sana, inapendeza na kufurahisha vijana wanapojituma.
 
Mkuu t-shirts unaprint au una design then wengine wanaprint?malipo ya wateja wako wa Instagram mnalipana vip? Hapo nazungumzia wale wanaohitaji kazi soft copy mfano flier's and posters or LOGO. Hujawahi kutapeliwa??Ukinipa mwanga hapo nami nazama then ntakuja na mrejesho mwakani
 
hongera, ila angalia tra wasije wakakufuata na mashine zao za fda
 
tshirt mimi naziprint ndio kazi yangu.. kuna watu wengi wanauza tshirt wanakuja nawatengenezea logo wanazotaka kisha nawaprintia kwenye tshirt zao mimi mwenyewe...

malipo tunalipana kawaida tu maana ni wanakuja kwnagu tunaonana.. baada ya kuwasiliana via instagram na namba za simu ambazo wanazitoa instagram..... graphics design nafanya sana tu kama za fliers, banners ila kwa mfumo huo huo unakuja ofisin unalipia advance ndio nakufanyia kazi.. ukiifata unamalizia na kuchukua kazi yako

kutapeliwa sijawai zaidi ya kupata hasara tu za kuharibu tshirt wakati naiprint... ambazo ni kawaida tu na hazitokei kila siku...

sifanyi kazi yoyote ambayo haijalipiwa advance... so naanzia wapi kutapeliwa... na sitoi kazi mpaka imaliziwe iliyobaki... maana mimi nauza huduma siuzi budhaa zinazooza... kiasi cha kumkopesha mtu kuogopa zitaharibika au ku expire....

Mkuu t-shirts unaprint au una design then wengine wanaprint?malipo ya wateja wako wa Instagram mnalipana vip? Hapo nazungumzia wale wanaohitaji kazi soft copy mfano flier's and posters or LOGO. Hujawahi kutapeliwa??Ukinipa mwanga hapo nami nazama then ntakuja na mrejesho mwakani
 
Wakati wengine wakifanya mzaha na mitandao ya kijamii wengine wanafanya maisha yaende kwa mitandao hiyo hiyo...binafsi yangu nakupongeza kwa kupokea ushauri wa rafiki yako na kuufanyia kazi.
Huyo rafiki yako ndiye mwema na wafaida kuliko wengine, mshikilie usimwache aende.
 
Back
Top Bottom