Intelijensia ya Rwanda sio ya mchezo mchezo, kinara wa Hotel Rwanda anashangaa kujikuta Kigali Airport

Intelijensia ya Rwanda sio ya mchezo mchezo, kinara wa Hotel Rwanda anashangaa kujikuta Kigali Airport

Ndugu ukitaka angalau kujua yanayofanyika na serikali hizi duniani kote, tafuta kitabu kinaitwa SECRET MEETING OF ELDERS OF ZION, kiliandikwa miaka mingi sana walipokisoma wakubwa wa serikali ikaamuliwa kopi zote zikusanywe zitiwe moto ila kuna waliokuwa wameshakisoma wakarudia kukiandika tena.
Kama una kopi tete(soft copy) tafadhali nitupie PM mkuu ikiwa utaona hapa public haifai kukiweka
 
Wazungu wakampa uraia, akapewa tuzo nyingi kama shujaa kumbe naye ailikuwa "mdhamini" wa mauaji na msaliti wa nchi yake! (Kuna mambo mengi ya kujifunza kutoka kwa huyu jamaa hasa pale unapoona kiongozi anapewa support kubwa na mataifa ya magharibi na Marekani) Ingekuwa Tanzania Paul Rusesabagina angekuwa kiongozi wa chama cha siasa au NGO ya kutetea Haki za raia, na hata urais angegombea tu, ila kwa Rwanda ukiisaliti nchi na kuwatumikia "mabeberu" lazima wakuwinde tu!
View attachment 1568411
Unataka kusema nini Mkuu? Naona umehangaika mno kwa kuzunguka sana. Ni Kiongozi gani msaliti hapa Tanzania aliyeko kwenye NGO ama chama cha upinzani na Serikali yako tukufu imeshindwa kumshughulikia kwa makosa yake (KAMA KWELI YAPO?) UVCCM mbona mnakua wapuuzi namna hii?
 
Mkuu huyu Fred Rwegima nadhani alikua close ally/friend wa Kagame na ndio kiongozi wa mwanzo wa RPF. Ninavyoelewa kifo chake baada ya kuuwawa kule msituni ndio kulifanya PK akatishe masomo Marekani aje aongoze mapambo dhidi ya serikali ya Rwanda ya wakati ule iliyokua chini ya Juvenal Habiarimana (kama sikosei)
Fred Rwigema ndio amemkuza kagame na ndie alikuwa kiongozi mkuu wa RPF infact angekuwepo ndio angekuwa raisi wa Rwanda leo hii.....
 
Paul Rusesabina aliyekua Manager wa Hotel Rwanda akiwaokoa Watutsi wasivamiwe na kuchinjwa na Interahamwe hatimaye amefikishwa mbele ya sheria kwa makosa ya kuhusika na njama za mauji hayo hayo.

Baada ya filamu ya Hotel Rwanda kueleza kisa cha Rusesabina, wakati wote dunia ilimuona kama shujaa aliyesaidia kuokoa maisha ya makumi ya Watutsi wasio na hatia waliokimbilia Hotel Rwanda hadi pale uchunguzi ulipofanyika na kugundua naye alikua mmoja wa walioshiriki kutekeleza genocide ile. Suala kama ana hatia au la mahakama itaamua lakini kilichoacha watu midomo wazi ni namna alivyofikishwa Rwanda, maana alikua akiishi Ubelgiji na alishachukua urai wa huko.

Inasemekana alikua Dubai na alidanganywa kupanda ndege ambayo labda aliamini inaenda sehemu nyingine. Kuja kutahamaki anajikuta anashuka Kigali Airport na pingu zikimsubiri!. Kabda ya hapo kuna jamaa wa Kinyarwanda aliandika makala akisema alijipa jukumu la kufuatilia nyendo za Rusesabagina duniani kote na alifanya hivyo kwa miaka 15 na kwa kukamatwa kwa Paul Rusesabagina basi ametimiza kazi yake akiwa kama Mzalendo wa nchi yake! Maofisa wa Rwanda wanasema jamaa amerudi mwenyewe kwa hiyari yake jambo ambalo ndugu wanalikanusha wakidai kua ametekwa, na sababu ni kwamba alianza harakati za kumuondoa madarakani Rais Kagame kwa kuongoza kundi la FNL ambalo Kigali inasema ni lakigaidi.

Serikali ya rais PK kama alivyo yeye mwenyewe ina mkono mrefu na wanamsemo wao kua "There is a price to pay in betraying Rwanda" na kwamba hicho ndio kilichomkuta Paul Rusesabagina.

Sitaki kuamini kuwa alidanganywa kupanda ndege, unadanganywa vipi kuhusu kupanda ndege? Pia nimeona wengi wakidai eti labda ndege ilibadilisha route ghafla, hili nalo haliwezekani sidhani kama kuna shirika linaloweza kuchezea biashara yake kiasi hiki. Make wateja watapoteza imani na shirika husika, hapo kilichowazi ni ushirikiano usiokuwa na shaka kati ya serikali mbili yaani Rwanda na DXB, Kwa mjibu wa familia yake alikuwa Dubai, ni jinsi gani alipanda ndege kuelekea Rwanda haiwezi kuwa kwa matakwa yake bali kwa lazima na kwa ushirikiano wa serikali zote mbili. Ama alilewesha na kusafirishwa kwa mgonjwa au kama nilivosema hapo awali alitekwa na kupandishwa ndege kama VIP kupitia VIP lounge.
 
Kama "international transit hub", Dubai pana dawati kabisa kwa ajili ya vyombo kama Interpol.

Pia,kulikuwa na International Warrant ilotolewa na Rwanda ambayo inaruhusu kuingilia safari ya anaetafutwa.
Yule Alex Massawe aliwahi kukamatiwa hapo Airport Dubai na jamaa wa interpol akatakiwa kurudishwa bongo then sijui ikaishia wapi,sasa hivi yuko S/Africa anakula zake maisha tu.
 
Kweli kabisa mkuu. Wanyarwanda wenyewe japo nchi yao kijiografia ni ndogo wanaiita "great country" labda kutokana na operations kama hizi
HAKUNA LOLOTE ni udikteta mtupu
Raia yeyote atakayehatarisha nafasi ya uraisi wa PK ni kifo
mambo yote yana mwisho, hata aongeze miaka ya kutawala itafikia mwisho tu tena siku hizihzi za karibuni. ameshaua watu wengi na ndiye aliyesababisha kutunguliwa kwa ndege ya Habyarimana
 
Nenda kajifunze upya historia ya hiyo nchi na hayo mauaji yakimbari.acha kulishwa maneno bila kushirikisha akili yako.Yako mengi sana nyuma ya pazia ambayo huwezi kuyajua kirahisi.Uyo bwana ni njia tu yakumnyamazisha ili Pk aendelee namambo yake.
PAKA anafanya hizi operations kwa gharama kubwa sana, yasemekana Rusesabagina alitolewa dubai kwa ndege ya pekee na si commercial flight. Aidha, alikwenda dubai kwa mwaliko wa mfanyabiashara wa rwanda alijifanya anamuita ili wapange mipango ya maendeleo kumbe alikuwa dealer wa mipango ovu ya PAKA
 
Lazima atakuwa alirudi kwa hiari,au Rwanda walifanya kama Saudi Arabia inavyofanya,,yaani ndege inabadilishwa route na kutua Rwanda
No, alitua rwanda kwa ndege ya kipekee iliyotumwa na PAKA
 
Paul Rusesabina aliyekua Manager wa Hotel Rwanda akiwaokoa Watutsi wasivamiwe na kuchinjwa na Interahamwe hatimaye amefikishwa mbele ya sheria kwa makosa ya kuhusika na njama za mauji hayo hayo.

Baada ya filamu ya Hotel Rwanda kueleza kisa cha Rusesabina, wakati wote dunia ilimuona kama shujaa aliyesaidia kuokoa maisha ya makumi ya Watutsi wasio na hatia waliokimbilia Hotel Rwanda hadi pale uchunguzi ulipofanyika na kugundua naye alikua mmoja wa walioshiriki kutekeleza genocide ile. Suala kama ana hatia au la mahakama itaamua lakini kilichoacha watu midomo wazi ni namna alivyofikishwa Rwanda, maana alikua akiishi Ubelgiji na alishachukua urai wa huko.

Inasemekana alikua Dubai na alidanganywa kupanda ndege ambayo labda aliamini inaenda sehemu nyingine. Kuja kutahamaki anajikuta anashuka Kigali Airport na pingu zikimsubiri!. Kabda ya hapo kuna jamaa wa Kinyarwanda aliandika makala akisema alijipa jukumu la kufuatilia nyendo za Rusesabagina duniani kote na alifanya hivyo kwa miaka 15 na kwa kukamatwa kwa Paul Rusesabagina basi ametimiza kazi yake akiwa kama Mzalendo wa nchi yake! Maofisa wa Rwanda wanasema jamaa amerudi mwenyewe kwa hiyari yake jambo ambalo ndugu wanalikanusha wakidai kua ametekwa, na sababu ni kwamba alianza harakati za kumuondoa madarakani Rais Kagame kwa kuongoza kundi la FNL ambalo Kigali inasema ni lakigaidi.

Serikali ya rais PK kama alivyo yeye mwenyewe ina mkono mrefu na wanamsemo wao kua "There is a price to pay in betraying Rwanda" na kwamba hicho ndio kilichomkuta Paul Rusesabagina.
Hapo airport alikuwa amelala kiasi hafahamu ndege aliyotakiwa kupanda?? I think there is more to this than is publicly available for now.
 
Hapo airport alikuwa amelala kiasi hafahamu ndege aliyotakiwa kupanda?? I think there is more to this than is publicly available for now.
Yes Chief, there is more to this kama anavyosema mwenyewe Rais Kagame kwenye interview baada ya Rusesabagina kutiwa nguvuni
 
Back
Top Bottom