Intelijensia ya simba imchunguze Henock Inonga

Intelijensia ya simba imchunguze Henock Inonga

Hahaha

Kwa hyo nyie ile miaka mi 4 mliyotawala mlikuwa mnawahonga mabeki wa yanga si ndio?

Kubalini wakati wenu umefika ukuta jipangeni vzuro tu Kama yanga ilovyojipanga

Mkishangaa kuna timu 2 zimejiimarisha zaid SINGIDA NA AZAM sio timu za kuzibeza kabisa

Sio muda wa kutoa lawama huu chukulien Kama changamoto tu hyo

Man u mwaka wa kumi sasa mambo Bado hayaendi nao vp wamehongwa na Liverpool au man city?

HAKUNA TIMU ISIYOFUNGWA DUNIANI

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Huu ni upumbavu.
Unadhani Simba ndiyo timu ya kufungwa kila siku na kinye fc?
 
Mnavyo msema hiyo Inonga, utafikiri timu nzima ilikuwa na mchezaji mmoja tu!

Ila binafsi sishangai. Maana malalamiko ni jadi yenu. Hasa pale timu yenu inapofungwa. Baadhi yenu hamjawahi kuwa na uvumilivu kama mashabiki wa Yanga.
Mbona akicheza vizuri tunamsifia humu

Tukiona kasoro tutamsema pia humu humu

Sisi mashabiki hatuna platform nyingine ya kusifia ama kukosoa zaidi ya hapa mtandaoni
 
Itoshe kusema kuwa kwenye pesa hakuna ujamaa..licha ya mwamuzi elly sasii kuwa na mahaba na mnyama ila jana alichukua mpunga mrefu kuhakikisha kuwa maamuzi yake yanaelekea upande wa home shopping center. Soka letu linanuka milungula.
Sure
 
Kama kawaida yenu kulia lia. Mnatafuta mbuzi wa kafara. Tatizo lako ni moja tu Inonga wakati anatoka alitaniana Mayele hivyo tu ndio chanzo chako kilipoanzia. Ni bongo tu mpira mnaufanya ni uadui.

Eti mpira 70% unachezwa nje uwanja 30% tu ndio wachezaji wanaiangaikia pale uwanjani,hii ni bongo tu ipo na watu wake. Kwa mpira ule mkali vile kila timu imecheza dakika zote kwa nguvu vile,uanze kuniambia **** mtu kahongwa?. Kuna watu mnawwaza ushindi tu,ushinde wewe mwenzio akishinda amehonga. Wakati mpira ni makosa madogo madogo yanaweza kuwagharinu.

Kwa mechi ile ya jana Yanga walikuwa kwenye form kabisa ya kushinda. Ona goli la simba lenyewe lilikuwa la kuibia bia tu,jamaa amejiegesha peke yake peke yake. Kwa marefa makini lile hakuna goli pale. Goli walilolihangakia mikia angalau lile lililogonga besela. Uje upande wa Yanga. Magoli yote ni ya kuyahangakia ma yasiyo na utata. Ona magoli waliyokosa Yanga ya wazi. Kuna ile asist ya Aziz Ki kwa Mayele wazi kabisa. Kuna lile la Morrison kule pembeni ya uwanja. Kwa mechi ya jana YANGA ilistahiri kabisa kushinda
Haya mambo ya mpira wa kibongo huyajui

Ndio maana azam wanauita mpira wetu kivyetuvyetu
 
Ukisikia ramli chonganishi ndiyo hii sasa! Kunatafutwa kila aina ya visingizio ili kukamatana uchawi, na pia kuangushiana jumba bovu.

Timu imefungwa, Yanga amechukua Ngao kwa mara ya pili mfululizo! Watu wajipange kwa mechi zijazo.
Always kolo's uwa wanajiona wako mbele zaidi ya Yanga,sio kosa lao wameaminishwa hivyo wakati si kweli,waache waendelee kujiona hivyo ndio nzuri sana kwetu,hawa hawatakiwi kujua shida yao ipo wapi
 
Hii habari inanikumbusha fainali ya FA kule kigoma pale mukoko kaitafuta kadi nyekundu na akaipata kweli na kutolewa nje ya uwanja.kilichokuja kutokea ni kuichungulia Yanga ya Nabi kwenye instagram.
Haya mambo yapo hivyo mara zote mpira wetu hauchezwi uwanjani ule tunaoucheki ulishachezwa jana
 
Ata manura achunguzwe mechi za derby anajitia pancha ili asicheze,miswahili mijitu ya hovyo sana
 
Itoshe kusema kuwa kwenye pesa hakuna ujamaa..licha ya mwamuzi elly sasii kuwa na mahaba na mnyama ila jana alichukua mpunga mrefu kuhakikisha kuwa maamuzi yake yanaelekea upande wa home shopping center. Soka letu linanuka milungula.
Alichukua hela mpaka akamnyima Inonga redcard
 
Ulichowaza nani niliwaza hicho hicho,kuna dot dot ukiziunganisha ukweli unakuja.
 
labda kama kakugongea mkeo ila jana alizidiwa akili... Kwa uwezo gani ahongwe..?
 
Moja kwa moja nijikite kwenye mada,

Hapo jana sikupenda kusema chochote kuhusu simba yangu maana ningeteremsha mitusi mizito kuanzia kwa kocha na mzungu wake ningeambulia ban ya maisha humu

Wameshaongea mengi humu kuhusu ukilaza wa kocha hasa kutojua ampange nani na wakati gani hususani kumtoa chama dakika za mchana za mchezo na kumuingiza mzamilu mwenye kitambi cha kispoti ambaye kama asingekua mchezaji bila shaka angekua mvuvi wa dagaa wa kigoma, yote kwa yote muda umeshamtupa mkono

Muhimu hapa ni kuhusu perfomance ya huyu beki wetu Inonga Baka

Imethibiti beyond reasonable doubt huyu ni beki bora kweli kweli na hayo yalidhihilika msimu ulioisha pamoja na mechi mbalimbali za kimataifa alionyesha uwezo wa hali ya juu kwelikweli

Kilichonisukuma niandioe huu uzi ni kutokana na ukweli usiopingika kwamba mpira wetu unachezwa "NJE YA UWANJA'' zaidi ya asilimia 70 na zilizobaki 30 ndizo hasa mashabiki tunaendaga kuangalia pale uwanjani

Kwa mantiki hii wazee wa mjini wanayafahamu matokeo kabla hata ya mechi yenyewe kuchezwa kutokana na kuigharamikia ipasavyo miundombinu yote muhimu ya nje ya uwanja na jambo hili ndilo linaloinyima Azam ubingwa kwa kua pamoja na miundombinu imara ya viwanja,mazingira na malipo kwa wachezaji wake wao hawaamini kushiriki fitina za nje ya uwanja

Miundombinu ya nje ya uwanja yawezakua marefalii wote, kuwanunua wachezaji wapinzani "kwa maneno ya kaseja alithibitisha ndiye kipa aliyefuatwa kurubuniwa kuachia magoli kwa ahadi ya pesa nyingi, miundombinu mngine ni uchawi hamasa n.k

Kama umesoma Cuba na ukiangalia kwa jicho la mbali hawa GSM ni mamafia wa kiwango cha kutisha, za ndaaani kabisa ni kwamba moja kati ya wachezaji waliodiskas kwenye vikao vyao kumpunguza upepo ni huyu beki nyota wa kimataifa wa Congo

Zipo habari kwamba iliandaliwa mipango kabambe ya kuhakikisha anacheza chini ya kiwango kwenye mechi nyingi za simba na upo uwezekano kashavuta pesa ndefu tayari kukamilisha deal hilo

Sambamba na hilo mamagia hao wa GSM wamemtuliza presha beko huyu kwa kumuahidi kumsajili endapo atatemwa na klabu ya wekundu wa msimbazi kwa madai ya kuperfom chini ya kiwango

Sote ni mashahidi Inonga sasa baada ya deal yake hiyo kukamilika anafanya makosa ya wazi na ya kizembe kabisa

Zile tackling za kuslide alizokua anafanya kazisitisha kabisa anamfukuza mchezaji kwa nyuma akifunga anajifanya anashika kichwa hii ni hadaa tu kwa mashabiki

Rai yangu kwa intelijensia ya simba pamoja na kumfukuza mzungu baye ni mtoto wa dada yake kocha Maki ikiwezekana pamoja na Maki mwenyewe ianze kudukua mawasiliano ya mchezaji Henock Inonga Baka na ikibaini anashiriki ufirauni huu atimuliwe mara moja ama kama mtahofia kuchukuliwa na wapinzani muongezeeni mkataba kisha mtieni benchi milele

Simba nguvu moja, ila jana mbili moja!
Tanzania hakuna siri hata kidogo na ukibainika ktk uhuni huu uwezekano wa kuumia ni mkubwa mno.
 
Tatizo viongozi wabahili. Wanasajili cheap players. Pamoja na msiba wa ushambuliaji butu last season tumesajili striker gani tishio? Kila mtu ameonya Simba haina DM wa maana bado hatusajili!

Pale ondoa mzungu, Victor Ikpar na leta DM na mashambuliaji katili level za Manzoki au zaidi! Kama Phiri ameshindwa kuonesha kitu kwenye training piga chini hata kwa kuvunja mkataba tafuta mtu wa maana! Huu si muda wa majaribio.

Timu imevuna mikataba mizuri wasajili vizuri badala ya ubahili.
 
Back
Top Bottom