Intelijensia ya simba imchunguze Henock Inonga

Intelijensia ya simba imchunguze Henock Inonga

Moja kwa moja nijikite kwenye mada,

Hapo jana sikupenda kusema chochote kuhusu simba yangu maana ningeteremsha mitusi mizito kuanzia kwa kocha na mzungu wake ningeambulia ban ya maisha humu

Wameshaongea mengi humu kuhusu ukilaza wa kocha hasa kutojua ampange nani na wakati gani hususani kumtoa chama dakika za mchana za mchezo na kumuingiza mzamilu mwenye kitambi cha kispoti ambaye kama asingekua mchezaji bila shaka angekua mvuvi wa dagaa wa kigoma, yote kwa yote muda umeshamtupa mkono

Muhimu hapa ni kuhusu perfomance ya huyu beki wetu Inonga Baka

Imethibiti beyond reasonable doubt huyu ni beki bora kweli kweli na hayo yalidhihilika msimu ulioisha pamoja na mechi mbalimbali za kimataifa alionyesha uwezo wa hali ya juu kwelikweli

Kilichonisukuma niandioe huu uzi ni kutokana na ukweli usiopingika kwamba mpira wetu unachezwa "NJE YA UWANJA'' zaidi ya asilimia 70 na zilizobaki 30 ndizo hasa mashabiki tunaendaga kuangalia pale uwanjani

Kwa mantiki hii wazee wa mjini wanayafahamu matokeo kabla hata ya mechi yenyewe kuchezwa kutokana na kuigharamikia ipasavyo miundombinu yote muhimu ya nje ya uwanja na jambo hili ndilo linaloinyima Azam ubingwa kwa kua pamoja na miundombinu imara ya viwanja,mazingira na malipo kwa wachezaji wake wao hawaamini kushiriki fitina za nje ya uwanja

Miundombinu ya nje ya uwanja yawezakua marefalii wote, kuwanunua wachezaji wapinzani "kwa maneno ya kaseja alithibitisha ndiye kipa aliyefuatwa kurubuniwa kuachia magoli kwa ahadi ya pesa nyingi, miundombinu mngine ni uchawi hamasa n.k

Kama umesoma Cuba na ukiangalia kwa jicho la mbali hawa GSM ni mamafia wa kiwango cha kutisha, za ndaaani kabisa ni kwamba moja kati ya wachezaji waliodiskas kwenye vikao vyao kumpunguza upepo ni huyu beki nyota wa kimataifa wa Congo

Zipo habari kwamba iliandaliwa mipango kabambe ya kuhakikisha anacheza chini ya kiwango kwenye mechi nyingi za simba na upo uwezekano kashavuta pesa ndefu tayari kukamilisha deal hilo

Sambamba na hilo mamagia hao wa GSM wamemtuliza presha beko huyu kwa kumuahidi kumsajili endapo atatemwa na klabu ya wekundu wa msimbazi kwa madai ya kuperfom chini ya kiwango

Sote ni mashahidi Inonga sasa baada ya deal yake hiyo kukamilika anafanya makosa ya wazi na ya kizembe kabisa

Zile tackling za kuslide alizokua anafanya kazisitisha kabisa anamfukuza mchezaji kwa nyuma akifunga anajifanya anashika kichwa hii ni hadaa tu kwa mashabiki

Rai yangu kwa intelijensia ya simba pamoja na kumfukuza mzungu baye ni mtoto wa dada yake kocha Maki ikiwezekana pamoja na Maki mwenyewe ianze kudukua mawasiliano ya mchezaji Henock Inonga Baka na ikibaini anashiriki ufirauni huu atimuliwe mara moja ama kama mtahofia kuchukuliwa na wapinzani muongezeeni mkataba kisha mtieni benchi milele

Simba nguvu moja, ila jana mbili moja!
inawezekana umeandika point ila huna akili hata punje

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Bongo haitakiwa salama hata siku moja,kuna watu watawaita wenzao wachawi,wezi,shoga,basha,mnafiki,muongo,shetani,
Lakini bila uthibitisho wowote watahukumiwa
Kwenye hukumu tutafika tumechoka sana[emoji848][emoji848][emoji848]
 
Kaka nacho fikiri tatizo n inonga kuchezeshwa namba nne tu,na siku ya simba dei nilivyoona uchezaji wake niliwaambia watu wa simba inonga akiendelea kucheza hivi ataigharimu simba .... .

Shida alishazoea kutuma sasa anatumwa...🏌🏿‍♀️
 
Moja kwa moja nijikite kwenye mada,

Hapo jana sikupenda kusema chochote kuhusu simba yangu maana ningeteremsha mitusi mizito kuanzia kwa kocha na mzungu wake ningeambulia ban ya maisha humu

Wameshaongea mengi humu kuhusu ukilaza wa kocha hasa kutojua ampange nani na wakati gani hususani kumtoa chama dakika za mchana za mchezo na kumuingiza mzamilu mwenye kitambi cha kispoti ambaye kama asingekua mchezaji bila shaka angekua mvuvi wa dagaa wa kigoma, yote kwa yote muda umeshamtupa mkono

Muhimu hapa ni kuhusu perfomance ya huyu beki wetu Inonga Baka

Imethibiti beyond reasonable doubt huyu ni beki bora kweli kweli na hayo yalidhihilika msimu ulioisha pamoja na mechi mbalimbali za kimataifa alionyesha uwezo wa hali ya juu kwelikweli

Kilichonisukuma niandioe huu uzi ni kutokana na ukweli usiopingika kwamba mpira wetu unachezwa "NJE YA UWANJA'' zaidi ya asilimia 70 na zilizobaki 30 ndizo hasa mashabiki tunaendaga kuangalia pale uwanjani

Kwa mantiki hii wazee wa mjini wanayafahamu matokeo kabla hata ya mechi yenyewe kuchezwa kutokana na kuigharamikia ipasavyo miundombinu yote muhimu ya nje ya uwanja na jambo hili ndilo linaloinyima Azam ubingwa kwa kua pamoja na miundombinu imara ya viwanja,mazingira na malipo kwa wachezaji wake wao hawaamini kushiriki fitina za nje ya uwanja

Miundombinu ya nje ya uwanja yawezakua marefalii wote, kuwanunua wachezaji wapinzani "kwa maneno ya kaseja alithibitisha ndiye kipa aliyefuatwa kurubuniwa kuachia magoli kwa ahadi ya pesa nyingi, miundombinu mngine ni uchawi hamasa n.k

Kama umesoma Cuba na ukiangalia kwa jicho la mbali hawa GSM ni mamafia wa kiwango cha kutisha, za ndaaani kabisa ni kwamba moja kati ya wachezaji waliodiskas kwenye vikao vyao kumpunguza upepo ni huyu beki nyota wa kimataifa wa Congo

Zipo habari kwamba iliandaliwa mipango kabambe ya kuhakikisha anacheza chini ya kiwango kwenye mechi nyingi za simba na upo uwezekano kashavuta pesa ndefu tayari kukamilisha deal hilo

Sambamba na hilo mamagia hao wa GSM wamemtuliza presha beko huyu kwa kumuahidi kumsajili endapo atatemwa na klabu ya wekundu wa msimbazi kwa madai ya kuperfom chini ya kiwango

Sote ni mashahidi Inonga sasa baada ya deal yake hiyo kukamilika anafanya makosa ya wazi na ya kizembe kabisa

Zile tackling za kuslide alizokua anafanya kazisitisha kabisa anamfukuza mchezaji kwa nyuma akifunga anajifanya anashika kichwa hii ni hadaa tu kwa mashabiki

Rai yangu kwa intelijensia ya simba pamoja na kumfukuza mzungu baye ni mtoto wa dada yake kocha Maki ikiwezekana pamoja na Maki mwenyewe ianze kudukua mawasiliano ya mchezaji Henock Inonga Baka na ikibaini anashiriki ufirauni huu atimuliwe mara moja ama kama mtahofia kuchukuliwa na wapinzani muongezeeni mkataba kisha mtieni benchi milele

Simba nguvu moja, ila jana mbili moja!
Looo, uzi wa kipuuzi kweli. Ungeshinda usingeandika ugoro huu.
 
Ukisikia ramli chonganishi ndiyo hii sasa! Kunatafutwa kila aina ya visingizio ili kukamatana uchawi, na pia kuangushiana jumba bovu.

Timu imefungwa, Yanga amechukua Ngao kwa mara ya pili mfululizo! Watu wajipange kwa mechi zijazo.
 
Mkuu juma kaseja wakati anahojiwa mwezi uliopita na azam tv alikiri kupokea mialiko mingi ya kuachia magoli watu hawaelewi tu,

Siku hizi mpira ni biashara kushinda kwa yanga ni kuing'arisha brand ya GSM na bidhaa zake hivyo si shida kwa GSM kuhonga hiyo mil.50
Kwa hiyo Mo hana hizo 50 millions au yeye hataki kung'arisha brand yake!?
 
Kaka nacho fikiri tatizo n inonga kuchezeshwa namba nne tu,na siku ya simba dei nilivyoona uchezaji wake niliwaambia watu wa simba inonga akiendelea kucheza hivi ataigharimu simba .... .

Shida alishazoea kutuma sasa anatumwa...🏌🏿‍♀️
Mnavyo msema hiyo Inonga, utafikiri timu nzima ilikuwa na mchezaji mmoja tu!

Ila binafsi sishangai. Maana malalamiko ni jadi yenu. Hasa pale timu yenu inapofungwa. Baadhi yenu hamjawahi kuwa na uvumilivu kama mashabiki wa Yanga.
 
Transition, Defense Unity na awareness Bado kazi kwa Simba
Mana unaona watu hawatimizi majukumu mpira ukitoka ktk mirki yao.
Kukaba Ni vitu viwili tu
1. Direction .mtu anelekea wapi
2.Space/ Option... Eneo la kuweka mpira au anaepewa

Kabla ya kumuona Inonga Kuna phase km 4 hazijatimiza majukumu yao, kulinda ni jukumu la timu nzima.
 
Itoshe kusema kuwa kwenye pesa hakuna ujamaa..licha ya mwamuzi elly sasii kuwa na mahaba na mnyama ila jana alichukua mpunga mrefu kuhakikisha kuwa maamuzi yake yanaelekea upande wa home shopping center. Soka letu linanuka milungula.
 
Magoli yote mawili ya mayele yanaonesha jinsi gani pesa inavyotembea...na itoshe kusema kuwa Beno kakolanya ni duka lingine la home shopping center
 
Mwambieni huyo Inonga acheze mpira aache masifa.Dunia imeshuhudia mabeki bora kabisa lakini wakiwa uwanjani ni mpira tuu hata hawakumbuki kama kuna mashabiki uwanjani.Sasa yeye anacheza na kamera kama muigizaji wa sinema.Hayo masifa yake utayafurahia siku timu yenu ikishinda na ikifungwa ndo kama hivi mnaona amewachomesha!

Pia huyo Henock ana ego balaa.Kama unafuatilia timu yako utakumbuka last season kuna mechi Mkude alimfokea Sana(timu ilikuwa nyuma ye anacheza na jukwaa ashangiliwe!) na unakumbuka reaction yake huyo Inonga kwa kapteni wake.Hii sasa inamfanya ajisikie hapaswi kutumwa uwanjani.Kwahiyo kucheza namba 4 hafai kwasababu anajiona mkubwa Sana kutumwa eti.So anajikuta anacheza kwa hasira amepaniki kisa katumwa na mwenzake ambaye anacheza namba 5.

Huwezi kuwa beki mzuri kama unataka ushangilie(sio ushangiliwe)kila ukiokoa....
 
Kama kawaida yenu kulia lia. Mnatafuta mbuzi wa kafara. Tatizo lako ni moja tu Inonga wakati anatoka alitaniana Mayele hivyo tu ndio chanzo chako kilipoanzia. Ni bongo tu mpira mnaufanya ni uadui.

Eti mpira 70% unachezwa nje uwanja 30% tu ndio wachezaji wanaiangaikia pale uwanjani,hii ni bongo tu ipo na watu wake. Kwa mpira ule mkali vile kila timu imecheza dakika zote kwa nguvu vile,uanze kuniambia **** mtu kahongwa?. Kuna watu mnawwaza ushindi tu,ushinde wewe mwenzio akishinda amehonga. Wakati mpira ni makosa madogo madogo yanaweza kuwagharinu.

Kwa mechi ile ya jana Yanga walikuwa kwenye form kabisa ya kushinda. Ona goli la simba lenyewe lilikuwa la kuibia bia tu,jamaa amejiegesha peke yake peke yake. Kwa marefa makini lile hakuna goli pale. Goli walilolihangakia mikia angalau lile lililogonga besela. Uje upande wa Yanga. Magoli yote ni ya kuyahangakia ma yasiyo na utata. Ona magoli waliyokosa Yanga ya wazi. Kuna ile asist ya Aziz Ki kwa Mayele wazi kabisa. Kuna lile la Morrison kule pembeni ya uwanja. Kwa mechi ya jana YANGA ilistahiri kabisa kushinda
 
Asee tusifike huku mazee

Pamoja na ujinga wake wa kucheza na jukwaa,Ila tusimbebeshe mzigo wa timu nzima..Mechi ya Jana Simba kupoteza haina excuse yoyote.Simba ndy ilitengeneza nafasi nyingi zaidi lkn ikatumia moja wakati yanga walikuja kipindi cha pili Kwa lengo moja Tu..kufunga

Nafasi mbili wametia kambani,wakaibuka washindi

Mara zote Simba anafungwa na yanga Kwa sababu ya ego,kujiona ni mkubwa na yupo level ya alhaly wakati anapikutana na timu za ndani kwe ye ligi anastrugle Sana kupata matokeo.. EGOISM NDY TATIZO LINALOICOST SIMBA

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Exactly
 
Mnavyo msema hiyo Inonga, utafikiri timu nzima ilikuwa na mchezaji mmoja tu!

Ila binafsi sishangai. Maana malalamiko ni jadi yenu. Hasa pale timu yenu inapofungwa. Baadhi yenu hamjawahi kuwa na uvumilivu kama mashabiki wa Yanga.
Kaka shabiki yeyote duniani ana kanuni mbili za uchambuzi
1.shabiki hakosei.
2.shabiki akikosea rejea kanuni namba 1.
 
Hii habari inanikumbusha fainali ya FA kule kigoma pale mukoko kaitafuta kadi nyekundu na akaipata kweli na kutolewa nje ya uwanja.kilichokuja kutokea ni kuichungulia Yanga ya Nabi kwenye instagram.
 
Back
Top Bottom