Intelijensia ya Tanzania imekwenda likizo au imekufa?!

Kama viashiria vya kutokea kwa fujo vilikuwepo mapema(vipeperushi na sms kama alivyokiri waziri husika bungeni), kwanini hazikufanyika juhudi za kuzuia,badala yake wanajikita kupiga mabomu na kusababisha vifo!
Ni kweli mkuu, kulikua na viashiria, lakini tuna hakika kwamba hakuna kilichofanyika? Yawezekana njia iliyotumika ndio haikua sahihi lakini hatua za kuzuia zilichukuliwa. Juhudi za kuzuia si mara zote zinafanikiwa lakini onyo la kutoandamana ni juhudi mojawapo kuzuia kilichokua kimepangwa. Sidhani kama serikali ilikaa kimya, kuna matamko yalitolewa kuzuia wananchi wa Mtwala kutekeleza azma yao.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Najua ni watu muhimu sana kwa taifa lolote lile, si Tanzania tu. Lakini tuangalie utendaji kazi wao pia. je TISS wanafanya kazi kwa mfumo gani? Mimi sio mwanasheria hivyo kama nitatafsiri vibaya naomba radhi but TISS Act ya Mwaka 1996 ilosainiwa 20 January 1997, inabainisha baadhi ya mambo yafuatayo;

(PART II
................
5.-(1) Subject to the control of the Minister, the functions of the Functions
Service shall be- of TISS
(a) to obtain, correlate, and evaluate intelligence relevant to security,
and to communicate any such intelligence to the Minister and to
persons whom, and in the manner which, the Director-General
considers it to be in the interests of security;
(b) to advise Ministers, where the Director-General is satisfied that
it is necessary to do so, in respect of matters -relevant to security,
so far as those matters relate to departments or portfolios of
which they are in charge;
(c) to cooperate as far as practicable and necessary with such other
organs of state and public authorities within or outside Tanzania
as are capable of assisting the Service in the performance of its
functions.
(d) to inform the President, and any other person or authority which
the Minister may so direct, of any new area of potential espionage,
sabotage, terrorism or subversion in respect of which the Director-
General has considered it necessary to institute surveillance.

(2) It shall not be a function of the Service-
(a) to enforce measures for security; or
(b) to institute surveillance of any person or category of persons by
reason only of his or their involvement in lawful protest, or dissent
in respect of any matter affecting the Constitution, the laws or
the Government of Tanzania)

Sasa katika hayo hapo juu, tuangalie ni haki kuwanyooshea kidole moja kwa moja kama kazi yao (rejea 5 (1) d hapo juu!!! Pia rejea 2 (a) and (b). Narejea pendekezo langu, hii taasis ni nyeti na nzito, hatupaswi kuibeza kwa namna yoyote ile ilhali hata report anapewa waziri au rais au mamlaka husika tu na sio kwingineko. waweza kudhani haifanyi kazi lakini sitaki kuamini hilo.
Kwanza nikushukuru na kukupongeza kwa kunukuu sheria!

Hoja yangu hapa ni kuwa kulikuwa na kila dalili za kutokea mshindo mkuu kufuatia hotuba ya bajeti ya wizara ya nishati na madini, na hivyo walikuwa na muda wa kutosha kuchukua au kushauri namna ya kukabiliana yao! Miongoni mwa hatua za kuchukuliwa ilikuwa kulinda maeneo yote nyeti na kulinda nyumba za viongozi kwa kuzingatia yaliyotokea huko nyuma bila kuonyesha ubabe wa kipolisi mitaani!

Maafa yaliyotokea Mtwara hivi sasa hayakupaswa kutokea kama polisi wangeelekezwa nini cha kufanya kwa busara! Badala yake polisi wakaachiwa wafanye kadri wanavyojisikia na kama kawaida yao wakachukua ubabe jambo ambalo liliwapa vibaka (Mtwara wanajulikana kama "Tukale wapi") fursa ya kuingia mitaani na kuanza kufanya vurugu!

Hata hivyo bado nina imani kuwa wanaweza kurekebisha udhaifu uliotokea usijirudie tena!
 
Poa mkuu Ileje, nimekupata point yako, tuamini tu vijana wetu wanafanya kazi japo kunajitokeza madhaifu madogo madogo upande wa utekelezaji ambayo yanaweza kuharibu hata yale mazuri lakini wao wanakua hawahusiki moja kwa moja. Kitu kingine nachopenda, tusiwe na negative altitude na hawa wenzetu, asilimia kubwa ya mijadala humu JF nimeona ikipondwa lakini ikumbukwe hata kama kuna baadhi yao wanaenda kinyume na maadili yao ya kazi, basi ni wachache na wasifanye kitengo hiko kionekane kina-under perform. Uzalendo wetu uanzie ktk ku-support hii sekta muhim na sio kuipa wakati mgumu kwa kashfa na malalamiko ya kutoridhishwa na kila wanalofanya. Naamini mtu akishakua baba au mama, then mwanae ni mwanae tu, anapokosea au kupotoka, then mzazi anajitahidi kumrekebisha na kumshauri kwa upole na si kutangaza kwa majirani kwamba mwanangu hafai hata kwa dawa. Hivyo basi, najua JF ina watu tofauti tofauti. Kwa wale walio na experience ktk field hiyo, toeni mchango wenu. TZ ikianguka leo sio TISS wala serikali iliyopo, ni watanzania wote tutakua tumeanguka. Kuna muda naona kama unit ya utaifa inapotea kabisa, haipiti siku sijaona neno magamba humu ndani hata kwa issue ambayo ni nyeti. Hapa nilipo naangalia documentary ya Rwanda Genocide, jamani msiombe mpoteze amani katika nchi, huwa ni balaa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Ni jambo la kustaajabisha sana kuwa intelijensia ya Tanzania ilishindwa kubaini kutokea kwa ghasia kubwa za Mtwara!

Kumetokea nini ndani ya taasisi hiyo nyeti:
  1. Kukosekana kwa weledi?
  2. Kuwapuuza wananchi wa Mtwara?
  3. Kupuuza maoni na madai ya wana-Mtwara?
  4. Kutowajibika kwa kufanya kazi zisizowahusu wala zinazoshahibiana na ujuzi wao?
  5. Kukosa uzalendo? au
  6. Wameichoka serikali iliyopo madarakani?!

MTUNGO WA FURAHISHA BARAZA:

Hapo zamaaaaani za kale sana, palitokea mfalme mmoja akiitwa Mfalme Daudi; Siku moja alimwona mke wa Mlinzi wake anaoga. Na kwa hulka ya binadamu wa kiume asiye na kasoro popote katika maumbile yake, kumwangalia kwa kificho mwanamke akioga mtoni ni shida kubwa saana. Mfalme Daudi akaweka mpango Mlinzi wake aende vitani bila mkewe. Huku nyuma Mfalme akabaki anafanya mambo.

Swali: Je wewe unadhani ingetokea nini kama mlinzi yule angeludi kutoka vitani, akapata taarifa za yale yaliyotokea wakati hayupo, lakini Mfalme Daudi akaamua kumpa cheo kikubwa yule Mlinzi kama njia ya kufunika aibu ya kile alichokifanya na mke wa yule mlinzi, kama kutafuta kuzima hasira vile, kwa kumpa cheo kikubwa--tufanye yule Mlinzi awe Waziri Mkuu hivi. We unadhani yule Mlinzi ambaye ana akili tosha kabisa angefanya kazi yake kwa moyo wakw wote? Au angechafua historia ya mfalme huyu ili aingie katika historia ya taifa lile kama bw.--ge--- kuliko wote waliotangulia! Wewe unafikiri ni kipi hasa kingetokea?

ANGALIZO: Mambo yote yaliyoandikwa hapa ni ya kubuni!
 
Poa mkuu Ileje, nimekupata point yako, tuamini tu vijana wetu wanafanya kazi japo kunajitokeza madhaifu madogo madogo upande wa utekelezaji ambayo yanaweza kuharibu hata yale mazuri lakini wao wanakua hawahusiki moja kwa moja. Kitu kingine nachopenda, tusiwe na negative altitude na hawa wenzetu, asilimia kubwa ya mijadala humu JF nimeona ikipondwa lakini ikumbukwe hata kama kuna baadhi yao wanaenda kinyume na maadili yao ya kazi, basi ni wachache na wasifanye kitengo hiko kionekane kina-under perform. Uzalendo wetu uanzie ktk ku-support hii sekta muhim na sio kuipa wakati mgumu kwa kashfa na malalamiko ya kutoridhishwa na kila wanalofanya. Naamini mtu akishakua baba au mama, then mwanae ni mwanae tu, anapokosea au kupotoka, then mzazi anajitahidi kumrekebisha na kumshauri kwa upole na si kutangaza kwa majirani kwamba mwanangu hafai hata kwa dawa. Hivyo basi, najua JF ina watu tofauti tofauti. Kwa wale walio na experience ktk field hiyo, toeni mchango wenu. TZ ikianguka leo sio TISS wala serikali iliyopo, ni watanzania wote tutakua tumeanguka. Kuna muda naona kama unit ya utaifa inapotea kabisa, haipiti siku sijaona neno magamba humu ndani hata kwa issue ambayo ni nyeti. Hapa nilipo naangalia documentary ya Rwanda Genocide, jamani msiombe mpoteze amani katika nchi, huwa ni balaa.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Tatizo ni kwamba machinery ya kuchambua mambo na kuona kipi sahihi kufanya ni dhaifu sana inakuwa kama haipo vile. Kwa hiyo maneno mengi ya hasira unayoyaona hapa ni maneno ya desperation. Ni kama mtu anapopiga yowe wakati anayeongea naye yupo hapo hapo futi mbili kutoka kwake huyo mpiga yowe.

Watu wanatoa ushauri mwingi sana mzuri, hakuna hatua zinazochukuliwa kukidhi ushauri huo. Nikupe mfano:

Watu wamesema mara nyingi; ondoeni hawa watu wawili kwenye nafasi zao hawafai: (1) Othman Rashid atoke TISS. Waliokaa naye London wanasema ni mtu mzuri sana; ni mpole, ni mwadilifu, lakini mazingira ya hapa nyumbani hayamruhusu kufanya kazi yake vizuri. Kwa hiyo atoke tu. (2) IGP Saidi Mwema atoke kwenye ofisi ile. Hawa watu wawili wameshindwa kuziongoza taasisi zao kwa ufanisi, whatever reasons they may have. Sina haja ya kurudia matatizo rundo ambayo ni ushahidi wa hawa wakubwa wa taasisi hizo za usalama kushindwa kazi.

Taarifa zinasema IGP Mwema alishafikia umri wa kustaafu. Kwa nini kigezo hicho kisitumike kumwachisha kazi? Kuendelea kumweka kwenye ofisi ile kunatoa nafasi watu kuendelea kutangaza hayo ambayo unasema majirani wanaelezwa siri zetu. Kama hili: kwamba eti IGP Mwema ni shemeji yake Rais Kikwete, na kwamba hiyo ndo sababu pekee inayomfanya ashindwe kumwachisha kazi mara moja. Hivi kweli Tanzania haina watu wengine wanaoweza kushika nafasi hizo?

Tunawashauri hamsikii. Mnataka tushauri vipi?
 
Highlander; Inapotokea breakdown ya system, huwa haijengwi au kurekebishwa kwa mara moja na papo hapo ukaona mafanikio yake. Ni hatua kwa hatua then tutafika. Naomba nitumie huo uelewa wa watu kuhusu huyu kiongozi mkuu wa kitengo. Umesema wanaomfahamu huko London wametoa sifa hizo kwamba ni mtu mzuri sana; mpole na muadilifu. Sasa kama hivyo ndivyo, taifa hili linahitaji kiongozi gani zaidi ya mwenye sifa hizo za uadilifu? Kwann ifike hatua watanzania tuamini kiongozi mpole na muadirifu hawezi kuendana na mazingira ya kwetu hapa nyumbani kwamba hawezi kufanya kazi kwa ufanisi? May be na aliemuweka anashindwa kumtoa kwa sababu hiyo tu ya uadilifu!

Nimalizie kwa ushauri huu, gari ikianza kuchemsha sana, dawa sio kutembea na kidumu cha maji ya kuweka ktk rejeta, tafuta chanzo cha hiyo overheat ni nini. Hii habari ya system haifanyi vzr basi viongozi waachie ngazi huwa siiafiki sana sababu tunakua hatujatatua tatizo. Matatizo mengine huwa ni beyond wizara. Hivi mtu kwa mfano mtu anaposema Dr Ndalichako au Prof Mkandala wajiuzuru kisa matokeo mabaya ya form 4, huyo ataeingia si mnamwambia aje na strategy ya kutunga mitihani nyanya au kupika matokeo ili tu kuwafurahisha watanzania wengi ambao hawapokei negative result kama challenge kwao? Sikatai tuna challenge nyingi hapa karibuni zinatukumba but let think of long term solution na si short term. We need time na utamilivu kufika tunakokutaka.

Nikubaliane nawe gari ikichemsha kidumu cha maji hakileti permanent solution, lakini you might be able to drive had ufike kwa fundi ukiwa na kile kidumu ukitupe mkiziba rajeta.

Mimi nilichotaka kumaanisha ni kwamba kuna incompatibles hapa. Othaman Rashid angeweza kufanya kazi bomba sana kama angekuwa na watu compatible naye. Nina mashaka kama frequency zake za fikra zinadakwa vema na mwenyekiti wake kwenye Security Council. Ujue kuwa star kwenye mazingira ya kazi unahitaji watu wanaokuelewa, na wewe ukawa unawaelewa, na wote mkawa mnayaona mambo yaliyo sahihi kufanya kama timu. Ustar unaletwa na team work. Huwezi kuwa star bila wenzio walio makini. Hiyo ndiyo compatibility ninayoizungumza hapa. Nina mashaka na team work; kwanza kwenye Security Council, kisha kwenye ofisi yenyewe TISS. Nina mashaka hawana mshikamano kabisa. Lakini pia nina mashaka kwenye Security Council kuna mtu husimulia maembe, na mwingine anasikia Nyanya na matokeo ndo haya tunayoyaona. Pili najua kuna rookies kibao waliletwa kufanya kazi na Othman. Another incompatibility.

Watu hawana imani na taasisi. Anayelaumiwa ni Othman, kumbe inawezekana tatizo ni bosi wake. Unafanyaje hapo. Mimi ningeacha kazi kuokoa heshima ya taaluma yangu kwenye mazingira hayo, huyu jamaa anayesikia nyanya wakati wa stori ya maembe atafute mtu mwingine. Kwa hiyo pengine sikuweka wazi kigezo cha Othman kuachia ngazi ni kipi.

Umeleta hoja ya kuisoma problem tree vizuri kwenye hili suala la usalama wa Taifa. Problem inawezekana ni two-faced. Kwanza ni rookies kujazana pale in the absence of professionals wa miaka mingi; halaf ndo lipo hilo la incompatibilities za thought frequency na mwenyekiti, lakini pia baina ya watendaji pale offisini TISS. Nina mashaka that is where the problem is. Othaman akiondoka Rais anapunguza jazba za watu kuhusu kufeli kwa system ya usalama. Hilo linaleta faida za kisiasa--kidogo. Wanaojua Othman ni mtu makini wanakuwa na amani akipewa kitengo kingine kusubiri compatible presidency. Nashukuru kesi ya Said Mwema haina Mjadala. Kumpumzisha Mwema kunaweza kuleta faida nyingi sana; faida za kisiasa na za kiutendaji, vyotevyote, ukiacha hii ya minong'ono ya kung'ang'ania kumwacha mtu kwenye nafasi kwa sababu tu ni shemeji yako.

Hizi departure mbili zinao uwezo wa kuleta watu wapya ambao pengine wataleta chachu mpya kwenye Security Council tukaanza kuona utofauti. Mbona Nyerere alibadili watu kwenye hizi nafasi as frequent as it was deemed fit. Sababu za kuwaondoa Othman na Mwema kwenye nafasi zao zinatofautiana, lakini nionavyo mimi outcome inaweza kusaidia sana agenda za CCM, from a political stand point. How close can you go in calling a spade by its name kwenye hili eneo kama una taarifa Mkurugenzi haivi na wafanyakazi wake? au kama umesikia kuna bifu na mtu state house?
 
Nimekuelewa vizuri sana, mkuu. Thanx a lot. Nimejifunza jambo ktk posts zako zote.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wakuu, mjadala wenu ni mzuri! Hoja zimejengeka vizuri kila upande!

Panapo fuka moshi chini pana moto, viko visa vingi sana vinavyo ishushia heshima idara yetu hii nyeti na muhim kwa mustakabali wa Taifa letu.

Enzi za Mwalimu ilikua ni Taasisi inayoheshimika sana ndani na nje ya nchi, iko wapi ile heshima? Na kwanini leo inanyooshewa kidole kwa kiasi kilichopitiliza? Hivi ndio vitu vya kujiuliza na kukaa chini kutafakari. Kukosolewa ni sehem ya kujifunza, na kuanza upya sio ujinga!
 
MTUNGO WA FURAHISHA BARAZA:

Hapo zamaaaaani za kale sana, palitokea mfalme mmoja akiitwa Mfalme Daudi; Siku moja alimwona mke wa Mlinzi wake anaoga. Na kwa hulka ya binadamu wa kiume asiye na kasoro popote katika maumbile yake, kumwangalia kwa kificho mwanamke akioga mtoni ni shida kubwa saana. Mfalme Daudi akaweka mpango Mlinzi wake aende vitani bila mkewe. Huku nyuma Mfalme akabaki anafanya mambo.

Swali: Je wewe unadhani ingetokea nini kama mlinzi yule angeludi kutoka vitani, akapata taarifa za yale yaliyotokea wakati hayupo, lakini Mfalme Daudi akaamua kumpa cheo kikubwa yule Mlinzi kama njia ya kufunika aibu ya kile alichokifanya na mke wa yule mlinzi, kama kutafuta kuzima hasira vile, kwa kumpa cheo kikubwa--tufanye yule Mlinzi awe Waziri Mkuu hivi. We unadhani yule Mlinzi ambaye ana akili tosha kabisa angefanya kazi yake kwa moyo wakw wote? Au angechafua historia ya mfalme huyu ili aingie katika historia ya taifa lile kama bw.--ge--- kuliko wote waliotangulia! Wewe unafikiri ni kipi hasa kingetokea?

ANGALIZO: Mambo yote yaliyoandikwa hapa ni ya kubuni!
angalizo lako si la kweli,hiko kisa ni cha kweli.
 
ni m kweli walikuwa wanafanya kazi kubwa sana hasa miaka ya nyuma,hata sasa kunakazi wanazifanya,tena kwa ufasaha sana,ili mradi wanawalinda watawala,hasa ccm na maovu yake,ila yale makusudio na majukum mengine watu wengi wanayalalamikia sana sana,ni aibu kwa chombo kama hiki tutajwatajwa au watumishi wake,sana tu,enzi za mwalim haikuwa hivi,lakini chenyewe ndo kimejifikisha hapa tulipo kwa kuanzia mfumo wa upatkanaji watumishi hadi utendaji kazi wake,si ajabu leo mkubya hata umeandika hapa kesho ukambiwa unafaa njo upate kibarua.kwenye mazuri tunapasa kusifia lakini mabaya si ya kunyamazia pia,bw.mkubya,,,eh,Muhimili wa uchumi wa nchi ni BOT,ufisadi mkubwa namna ile wa EPA unapangwa na kufanikiwa?na hatua hakuna hadi kelele za kina slaa,Ndege ya kijeshi inaingia TZ na kuiba wanyama hai kisi kile?dalili na mipango ya udini na uchochezi wa vurugu za kidini? mabom kanisani?kujiingiza kisiasa namna hii?watumishi wake kuwa na kashfa za utesaji kama ya ulimboka?baadhi ya watumishi wake kuhusishwa na dili za unga na ujangili nchini bila hatua kuchukuliwa?kupika ushahid ktk case za kupikwa dhid ya raia?na hasa kushindwa kusoma public opinion,mana viongozi wanafanya yale yale yanayopingwa na wananchi,kama ufisadi n.k,ni aibu chombo hicho kufika hapa tulipo,kwa vile kimejifikisha chenyewe wacha wananchi wakiseme vibaya,ukienda bar,ukamwagiwa bia, hamna ataeshangaa,lakini ukamwagiwa bia mahakamani au ofisin kila mtu atashangaa,hawa wanaonekana kama wanasiasa na wapiga dili siku hizi,so waache watukanwe majukwaani sana(ni kweli kama mboe anavosema kuwa ni weupe kuliko shati ulilovaa.naimani sana,nadhani wengi wanaimani pia na heshma ya JWTZ,ila hata huko nako kuna watu wazuri tu,ambao kwa uzuri wao ipo siku watakuja kuwa mfano kwa idara hiyo nyeti kuondokana na wale wote waliopatkana kishkaji,na ndo hao mko bar au kwenye viombo vya usafiri"unanijua mi ni nani?
 
Tatizo ni kwamba machinery ya kuchambua mambo na kuona kipi sahihi kufanya ni dhaifu sana inakuwa kama haipo vile. Kwa hiyo maneno mengi ya hasira unayoyaona hapa ni maneno ya desperation. Ni kama mtu anapopiga yowe wakati anayeongea naye yupo hapo hapo futi mbili kutoka kwake huyo mpiga yowe.

Watu wanatoa ushauri mwingi sana mzuri, hakuna hatua zinazochukuliwa kukidhi ushauri huo. Nikupe mfano:

Watu wamesema mara nyingi; ondoeni hawa watu wawili kwenye nafasi zao hawafai: (1) Othman Rashid atoke TISS. Waliokaa naye London wanasema ni mtu mzuri sana; ni mpole, ni mwadilifu, lakini mazingira ya hapa nyumbani hayamruhusu kufanya kazi yake vizuri. Kwa hiyo atoke tu. (2) IGP Saidi Mwema atoke kwenye ofisi ile. Hawa watu wawili wameshindwa kuziongoza taasisi zao kwa ufanisi, whatever reasons they may have. Sina haja ya kurudia matatizo rundo ambayo ni ushahidi wa hawa wakubwa wa taasisi hizo za usalama kushindwa kazi.

Taarifa zinasema IGP Mwema alishafikia umri wa kustaafu. Kwa nini kigezo hicho kisitumike kumwachisha kazi? Kuendelea kumweka kwenye ofisi ile kunatoa nafasi watu kuendelea kutangaza hayo ambayo unasema majirani wanaelezwa siri zetu. Kama hili: kwamba eti IGP Mwema ni shemeji yake Rais Kikwete, na kwamba hiyo ndo sababu pekee inayomfanya ashindwe kumwachisha kazi mara moja. Hivi kweli Tanzania haina watu wengine wanaoweza kushika nafasi hizo?

Tunawashauri hamsikii. Mnataka tushauri vipi?
Unashauri au unaforce?subiri na wewe uwe rais uchague unaowataka wewe.
 
ni m kweli walikuwa wanafanya kazi kubwa sana hasa miaka ya nyuma,hata sasa kunakazi wanazifanya,tena kwa ufasaha sana,ili mradi wanawalinda watawala,hasa ccm na maovu yake,ila yale makusudio na majukum mengine watu wengi wanayalalamikia sana sana,ni aibu kwa chombo kama hiki tutajwatajwa au watumishi wake,sana tu,enzi za mwalim haikuwa hivi,lakini chenyewe ndo kimejifikisha hapa tulipo kwa kuanzia mfumo wa upatkanaji watumishi hadi utendaji kazi wake,si ajabu leo mkubya hata umeandika hapa kesho ukambiwa unafaa njo upate kibarua.kwenye mazuri tunapasa kusifia lakini mabaya si ya kunyamazia pia,bw.mkubya,,,eh,Muhimili wa uchumi wa nchi ni BOT,ufisadi mkubwa namna ile wa EPA unapangwa na kufanikiwa?na hatua hakuna hadi kelele za kina slaa,Ndege ya kijeshi inaingia TZ na kuiba wanyama hai kisi kile?dalili na mipango ya udini na uchochezi wa vurugu za kidini? mabom kanisani?kujiingiza kisiasa namna hii?watumishi wake kuwa na kashfa za utesaji kama ya ulimboka?baadhi ya watumishi wake kuhusishwa na dili za unga na ujangili nchini bila hatua kuchukuliwa?kupika ushahid ktk case za kupikwa dhid ya raia?na hasa kushindwa kusoma public opinion,mana viongozi wanafanya yale yale yanayopingwa na wananchi,kama ufisadi n.k,ni aibu chombo hicho kufika hapa tulipo,kwa vile kimejifikisha chenyewe wacha wananchi wakiseme vibaya,ukienda bar,ukamwagiwa bia, hamna ataeshangaa,lakini ukamwagiwa bia mahakamani au ofisin kila mtu atashangaa,hawa wanaonekana kama wanasiasa na wapiga dili siku hizi,so waache watukanwe majukwaani sana(ni kweli kama mboe anavosema kuwa ni weupe kuliko shati ulilovaa.naimani sana,nadhani wengi wanaimani pia na heshma ya JWTZ,ila hata huko nako kuna watu wazuri tu,ambao kwa uzuri wao ipo siku watakuja kuwa mfano kwa idara hiyo nyeti kuondokana na wale wote waliopatkana kishkaji,na ndo hao mko bar au kwenye viombo vya usafiri"unanijua mi ni nani?
wakati wa kambarage kulikua kuna challenge zake huezi sema wakati huo ndo mambo ya usalama yalikua safi sana.

~Tanzania ilishuhudia maasi ya jeshi,usalama walikuwa wapi kugundua mapema.
~nduli amini akavamia na kuteka kagera,usalama walikua wapi kugundua mapema.
~vijana waliteka ndege mjini mwanza na kuipeleka mpaka london,walikua wapi kugundua njama hizo.
~mapinduzi ya kijeshi nusra yatokee zaidi ya mara moja.
~watu wa mara kutaka kujitenga,etc.
Kila nyakati na challenge zake ,hakuna utawala humu duniani haujawahi kukumbana na challenge za kiusalama.
 
Nadhani Intelejensia yetu ni kama mbwa tu
ambaye kazi yake ni kumlinda bwana wake kwa posho ya makombo. So sad.

Nashangaa sana jambo linaanza taratibu lkn Intelejensia haina habari, linakua na kukomaa kishi linaripuka na kuleta maafa kana kwamba limetokea ghafla.

Nasikitika sana kuona Intelejensia yetu akili na macho yake yote ni kuwamulika wapinzani wa CCM tu wakati Taifa linaporomoshwa kwa ufisadi na kukosa mishikamano kwa masuala ya kipuuzi kama udini.
 
wakati wa kambarage kulikua kuna challenge zake huezi sema wakati huo ndo mambo ya usalama yalikua safi sana.

~Tanzania ilishuhudia maasi ya jeshi,usalama walikuwa wapi kugundua mapema.
~nduli amini akavamia na kuteka kagera,usalama walikua wapi kugundua mapema.
~vijana waliteka ndege mjini mwanza na kuipeleka mpaka london,walikua wapi kugundua njama hizo.
~mapinduzi ya kijeshi nusra yatokee zaidi ya mara moja.
~watu wa mara kutaka kujitenga,etc.
Kila nyakati na challenge zake ,hakuna utawala humu duniani haujawahi kukumbana na challenge za kiusalama.
Hoja zako hazina mashiko! Hayo yote uliyoorodhesha yalidhibitiwa na hatua muafaka zilichukuliwa kwa wakati na ndiyo maana hakuna hata moja lililofanikiwa!
 
MTUNGO WA FURAHISHA BARAZA:

Hapo zamaaaaani za kale sana, palitokea mfalme mmoja akiitwa Mfalme Daudi; Siku moja alimwona mke wa Mlinzi wake anaoga. Na kwa hulka ya binadamu wa kiume asiye na kasoro popote katika maumbile yake, kumwangalia kwa kificho mwanamke akioga mtoni ni shida kubwa saana. Mfalme Daudi akaweka mpango Mlinzi wake aende vitani bila mkewe. Huku nyuma Mfalme akabaki anafanya mambo.

Swali: Je wewe unadhani ingetokea nini kama mlinzi yule angeludi kutoka vitani, akapata taarifa za yale yaliyotokea wakati hayupo, lakini Mfalme Daudi akaamua kumpa cheo kikubwa yule Mlinzi kama njia ya kufunika aibu ya kile alichokifanya na mke wa yule mlinzi, kama kutafuta kuzima hasira vile, kwa kumpa cheo kikubwa--tufanye yule Mlinzi awe Waziri Mkuu hivi. We unadhani yule Mlinzi ambaye ana akili tosha kabisa angefanya kazi yake kwa moyo wakw wote? Au angechafua historia ya mfalme huyu ili aingie katika historia ya taifa lile kama bw.--ge--- kuliko wote waliotangulia! Wewe unafikiri ni kipi hasa kingetokea?

ANGALIZO: Mambo yote yaliyoandikwa hapa ni ya kubuni!
Busara hapa ni kumpa talaka mke na kusonga mbele na kazi yako kwa nguvu na ari mpya!
 
Back
Top Bottom