International friendly: Tanzania (Taifa Stars) vs Ivory Coast (Les Éléphants)-Updates

Tuna mpira huo??

Uko uwanjani ama??,mpira wa Afrika unafanana aisee,so twaweza tu kuwafunga wao wametuona ndo maana wakaamua kuja kufanya trial na sisi kabla hawajaenda kupambana Angola,binafsi nina imani sana na timu yetu ya sasa,niliiona ilivyocheza na Cameroon Dar na Younde ilicheza vizuri sana.Pia hata mechi na New Zealand(ambao baadhi yetu tuliwadharau lakini June wanakipiga bondeni) tuliyowachapa 2-1 niliwaona pia,timu ni nzuri though kuna mapungufu machache sana ya kurekebisha..Tusubiri dakika 90 na tuone
 
mhh ipo kazi...kwa hiyo mastaa wameoneka kwa watazamaji for 45 mins...interesting
 
Kipindi cha pili kimeanza Ivory Coast wamepumzisha mastaa wao wote wameingiza kukosi kingine.

,..Sasa nadhani wabongo waanze kushangilia stars maana wengi walikuwa wanamshangilia Drogba na mastar wengine wanaokipiga ligi kubwa Ulaya..
 
Wakuu mbona kimya??,ni dakika ya ngapi sasa
 
Tegete anaachia bonge la shuti kwa mguu wake wa kushoto lakini unagonga mwamba wa chini duh tumewakosa kiduchu sana
 
Uko uwanjani ama??,mpira wa Afrika unafanana aisee,so twaweza tu kuwafunga wao wametuona ndo maana wakaamua kuja kufanya trial na sisi kabla hawajaenda kupambana Angola,binafsi nina imani sana na timu yetu ya sasa,niliiona ilivyocheza na Cameroon Dar na Younde ilicheza vizuri sana.Pia hata mechi na New Zealand(ambao baadhi yetu tuliwadharau lakini June wanakipiga bondeni) tuliyowachapa 2-1 niliwaona pia,timu ni nzuri though kuna mapungufu machache sana ya kurekebisha..Tusubiri dakika 90 na tuone

Thanks mkubwa kwa maelezo yako ila mimi sipo uwanjani...Je swali la haraka haraka tu tunaweza kumfananisha Drogba na Jerry Tegete??Sasa hapo tu tukipata jibu tunaweza kuelewa kwamba tunaweza kuwafunga hawa..ila kwa sisi TZ ni vigumu kidogo!!
 
Duu naona sijui tumeongezwa ila kama vipi wakaze na hilo moja tu kiwango chao kitakuwa kizuri tu!!
 
Thanks mkubwa kwa maelezo yako ila mimi sipo uwanjani...Je swali la haraka haraka tu tunaweza kumfananisha Drogba na Jerry Tegete??Sasa hapo tu tukipata jibu tunaweza kuelewa kwamba tunaweza kuwafunga hawa..ila kwa sisi TZ ni vigumu kidogo!!
Mkuu mi naona ulinganifu huu sio mzuri coz ni watu wawili wenye utofauti mkubwa sana ktk maendeleo ya soka kiujumla, lakini haina maana kuwa wachezaji wetu hawawezi kufurukuta kuwapa tabu hawa jamaa coz kama ingekuwa sisi ni vibonde kiasi hicho tungekuwa tumeshafungwa magoli yasiyohesabika ila kwa sababu wachezaji wetu nao wanaupiga mpira huohuo anaopiga drogba ndio maana matokeo yapo hivyo mpaka sasa, mimi sioni huo mpira kama unavyojua Tz bado hakuna michannel ya kuruka mpaka nchi nyingine ila mkuu naufahamu huo utofauti unaouzungumzia japo sio kwa kiwango hicho cha kuona kwamba hata kuwafunga hatuwezi, kumbuka huu ni mpira lolote linaweza tokea...
 
Mimi nasubiri goli la nne. Hii kazi ya update tuliwapa mashabiki wa Chelsick lakini naona imewashinda.
 
Mkuu mi naona ulinganifu huu sio mzuri coz ni watu wawili wenye utofauti mkubwa sana ktk maendeleo ya soka kiujumla, lakini haina maana kuwa wachezaji wetu hawawezi kufurukuta kuwapa tabu hawa jamaa coz kama ingekuwa sisi ni vibonde kiasi hicho tungekuwa tumeshafungwa magoli yasiyohesabika ila kwa sababu wachezaji wetu nao wanaupiga mpira huohuo anaopiga drogba ndio maana matokeo yapo hivyo mpaka sasa, mimi sioni huo mpira kama unavyojua Tz bado hakuna michannel ya kuruka mpaka nchi nyingine ila mkuu naufahamu huo utofauti unaouzungumzia japo sio kwa kiwango hicho cha kuona kwamba hata kuwafunga hatuwezi, kumbuka huu ni mpira lolote linaweza tokea...

Mkubwa nimekupa na thanks ila pia baada ya hapo nikasema bora wajitahidi tu tutoke nao hata hiyo 1-0 nadhani itakuwa vizuri pia!!
 
Back
Top Bottom