International friendly: Tanzania (Taifa Stars) vs Ivory Coast (Les Éléphants)-Updates

International friendly: Tanzania (Taifa Stars) vs Ivory Coast (Les Éléphants)-Updates

dakika ya 89 TZ 0 -Ivory coast 1..Taifa stars wako makeniko mnooo yaani ni kuumizana tu...very unproffesional of them..sijawapenda hata kidogo..Mpaka Drogba katolewa kuogopa kuumizwa ..TZ nguvu nyingi maarifa hakuna
 
Game limeshaisha, ubao wa matokeo unasomeka kulingana na kazi ya Drogba
 
mliopo bongo mnatunyima raha sana kwa kuwa mkiwa uwanjani huwa mnachelewa sana kutuletea matokeo kwa hilo tunawalaumu sana!plz tunaomba matokeo!
 
Wamejitahidi Stars kwa kweli,japo tumefungwa hilo goli moja
 
Tukubali matokea, ila naona wamecheza sana mpira......Hongereni sana
 
Wamejitahidi Stars kwa kweli,japo tumefungwa hilo goli moja
Yeah wamejitahidi, hii inaonyesha kuna kamaendeleo flani japo bado tupo kwenye safari ya kujiweka pazuri zaidi, kwa ujumla nionavyo hii timu itakuwa na maendeleo siku hadi siku kama mipango na mwenendo ulioanzishwa kuiendeleza timu utaendelea. Ni vigumu sana kubadilika kutoka hauwezi mpaka ufikie hatua useme ninaweza, juhudi ya wachezaji kimaalifa zaidi na sio kutegemea kipaji pekee, usimamizi na uendeshaji mzuri wa chama cha soka, pamoja na ushirikiano kutoka kwa serikali, wadhamini na wananchi kwa ujumla hiyo ndio siraha ya kusonga mbele na sio kukaa tukiguna kila cku na kudhani kwamba hatuwezi. Hawa wote tunaoona wanaweza leo wameanzia mbali sana na hadi hapo walipofika imewaghalimu ... so hongera taifa stars na naomba wadau tuendelee kuiunga mkono timu yetu ya taifa,
 
Stars palyed very well na nimependa sana beki wetu wa pembeni na Nadir (plus Yondani) na Abdulhalim wamecheza vizuri, naona ngasa walimbana kiasi lakini Tegete alijaribu shuti zuri sana

Nimependa discipline yetu na kusikitishwa na baadhi ya hawa wa-kodivaa waliokuwa very harsh kwa wachezaji wetu... kama kawa marefa leo walikua below par na hawakuwalinda hawa wakuu wa soka africa, na hiki ni chanzo cha upupu kwenye mechi za kimataifa zinazochezeshwa na watu toka nje ya Tz

All in all it was a very good game, worth watching from the stand, hongera Taifa Stars
 
Can someone tell me the result of the match-Tanzania -Côte d'Ivoire...thx
 
which is a result of Tanzania-Côte d'Ivoire, please urgently - thx
 
dakika ya 89 TZ 0 -Ivory coast 1..Taifa stars wako makeniko mnooo yaani ni kuumizana tu...very unproffesional of them..sijawapenda hata kidogo..Mpaka Drogba katolewa kuogopa kuumizwa ..TZ nguvu nyingi maarifa hakuna

which is a result of Tanzania-Côte d'Ivoire, please urgently - thx

Can someone tell me the result of the match-Tanzania -Côte d'Ivoire...thx

Kweli sio.
 
yes tumefungwa,true jamaa wameogopa kuumizwa lakini strs nao wanadeserve credits hata kama ni kidogo wamejitahidi kupiga pasi ingawa kama kawaida umaliziaji ndo tatizo letu laiti tegete na ngasa wangekuwa makini kidogo tungetake the lead kipindi cha kwanza
kuna watu wao wanaangalia only on the negative side of everything sasa ina maana hakuna hata zuri moja lililovutia uwanjani?criticism gani hizo ambazo hazithamini chochote ambacho ni kizuri cha nyumbani?others are not soccer fans they are just wadandiaji tu,if you dont know football kaa kimya changia siasa,dini,jokes etc

huree stars ingawa tumefungwa
 
Yah niliangalia huo mpira na goli la drogba mi naweza kusema ni la kawaida,kwanini nasema hivo hata Ngassa na Tegete pamoja na Mgosi wanaweza wakafunga mabao kwa njia hiyo aliyofunga Drogba sema hawakuapata nafasi au kutumia nafasi ya kufunga.Taifa Starz kwa kusema kweli wamejitahidi sana pamoja na kwamba tumecheza na timu iliyo mbele kisoka! mi nawapa hongera sana Taifa Starz!

Next years tukiendelea hivi tutakuwa tishio kama alivosema Roger Millar kwenye mpambano wa Stars na cameroon kule Younde,Cameroon,Roger Millar alishangazwa na kiwango cha Stars kule Younde!
 
Taifa Stars hii hii ambayo imeshindwa ata kuchukua Challenge Cup? Labda tubadirishe kocha na sio huyu kilaza tuliye naye sasa hivi.
 
i1381_a.bmp

Taifa Stars hii hii ambayo imeshindwa ata kuchukua Challenge Cup? Labda tubadirishe kocha na sio huyu kilaza tuliye naye sasa hivi.

Kocha sio Tatizo,tatizo ni wachezaji wetu.
Mimi nitaendelea kusema Maximo ni kocha mzuri sana,hata kama ataenda bado atakua kocha mzuri tuliye wahi kuwa nae hapa Tz.

Tumefungwa sawa,lakini kikosi kimeonyesha kukua kimchezo kuliko tulivyo wahi kua huko nyuma timu yetu imekua bora sana.
 
Timu imecheza vizuri sana jana sema bahati haikuwa yetu tu,washambuliaji walijitahidi kupiga mashuti vizuri,hata mabeki walicheza vizuri sana...
 
Drogba aizamisha Taifa Stars, akiri ubora wa viwango kwa stars

Allan Goshashy

BAO la nahodha Didier Drogba kipindi cha kwanza limeipa ushindi Ivory Coast wa bao 1-0 dhidi ya Taifa Stars kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Dakika ya 37, Drogba alipachika bao hilo kwa kichwa cha kuchupia kufuatia krosi ya kiungo Emerse Fae baada ya kumzidi ujanja beki Nadir Haroub 'Cannavaro' ambaye alicheza vizuri jana.

Awali, mchezo huo uliohudhuriwa na mashabiki wengi akiwamo Rais Jakaya Kikwete na baadhi ya mawaziri wake ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu na kasi zikisaka mabao ya mapema.

Baadhi ya nafasi za kufunga ambazo Stars ilizikosa ni za dakika ya 23, kupitia kwa Mrisho Ngassa aliyekosa bao akiwa na kipa Barry.

Hata hivyo muda mfupi baadaye, beki Kolo Toure aliokoa mkwaju dhaifu wa mshambuliaji huyo wa Stars mwenye kasi aliyejaribu kumchambua kipa.

Dakika ya 12, Cannavaro alimzuia Drogba aliyekuwa akielekea langoni na pia katika dakika ya 14, lango la wenyeji lilikuwa tena katika msukosuko kutoka kwa wageni hao.

Mshambuliaji Solomon Kalou naye alijaribu kumtoka Kelvin Yondani, lakini beki huyo mahiri aliutoa mpira na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Dakika ya 36, shuti la Jerry Tegete lilipaa na kutoka nje na kufuatiwa na jaribio jingine la dakika moja baadaye baada ya kiungo Nizar Khalfan anayecheza soka ya kulipwa Canada kukosa nafasi nzuri ya kuandika bao.

Tukio pekee ni la dakika ya 31, kipindi cha kwanza baada ya taa za uwanjani hapo kuzimika kwa muda mfupi, lakini zikarejeshwa na kuufanya mchezo huo uendelee bila matatizo yoyote.

Kipindi cha pili, kocha wa Ivory Coast Vahid Halilhodzic aliwatoa wachezaji wake wote 11 wa kikosi cha kwanza cha dakika 45 za mwanzo na kuingiza wengine akijaribu kuipeleka puta Stars kwa mchezo wa kasi.

Kwa dakika 10 za kipindi hicho, vijana hao wa Ivory Coast waliipeleka puta Stars, lakini mabeki walikuwa makini na imara kuokoa hatari zote.

Nafasi pekee ya kipindi hicho cha pili ni ile iliyopotezwa na Jerry Tegete ambaye aliwachambua mabeki wa Ivory Coast pamoja na kipa wao, Boubacar Barry na kuachia mkwaju ambao uligonga mwamba na kurejea dimbani.

Kipa huyo anayecheza soka ya kulipwa nchini Ubelgiji alitolewa dakika za mwisho za mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na Vincent De Paul Angban ambaye ndiye mchezaji pekee katika kikosi hicho cha wachezaji 23 wa Ivory Coast anayecheza ligi ya nyumbani.

Kocha Marcio Maximo alifanya mabadiliko katika kikosi chake kipindi kwa kumtoa Kiggi Makassi na kuingia Mussa Hassan Mgosi na Nizar Khalfan akamwingiza Stephen Mwasika ambaye alionyesha umahiri mkubwa.

Pia, Maximo alimtoa Henry Joseph na kumwingiza Nurdin Bakari, kipindi cha kwanza.

Baada ya mchezo huo, baadhi ya wachezaji wa pande zote mbili walionyeshana ubabe huku Drogba na Nsajigwa wakisukumana.

Naye kiungo Abdulhalim Hamoud akikaribia kukunjana shati na mchezaji wa Ivory wakati wakielekea vyumba vya kubadilishia nguo.

Baada ya mchezo, Cannavaro alisema Ivory Coast walipata nafasi moja na kuitumia vizuri kupata bao ikilinganishwa na wao waliopata nafasi kadhaa na kuzikosa.

Naye Vicky Kimaro anaripoti kuwa wakati wakitoka uwanjani, wachezaji wa Ivory Coast wanashangiliwa na mashabiki huku askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiwatawanya mashabiki kwa virungu.

Lakini, mashabiki bado wamejazana uwanjani kwenye lango kuu wakiwasubiri wachezaji wa Ivory Coast watoke vyumba vya kubadilishia nguo huku Drogba akiendelea kuwa kivutio kikubwa.

Wakati wakitoka, Drogba anatia saini vitabu vya mashabiki mbalimbali waliokuwa na hamu ya kumwona.

FFU kwa upande wao wametanda kila mahali wakiwa na zana zao tayari kwa lolote linaloweza kutokea.

Ivory Coast ambao wanajiandaa kwa fainali za Afrika wanatarajiwa kushuka dimbani tena kesho dhidi ya Amavubi ya Rwanda katika mchezo mwingine wa kujipima nguvu.

Timu hiyo imepangwa dhidi ya Ghana, Burkina Faso na Togo zikiwa Kundi B katika fainali hizo zinazotarajiwa kuanza Jumapili nchini Angola.

Source: Gazeti la Mwananchi.
 
Hata hivyo muda mfupi baadaye, beki Kolo Toure aliokoa mkwaju dhaifu wa mshambuliaji huyo wa Stars mwenye kasi aliyejaribu kumchambua kipa.
wachezaji wa kibongo wanapenda sifa kama hizi na sio kucheza mpira...

Back
Top Bottom