Unavosema ni kweli kutokana na fikra zako. Ila, umechanganya mafaili. Kuna shule za St. kayumba, English medium n international schools.
St kayumba ndio zimetapakaa, hizi sote tunazijua so hamna haja ya kuzitilia mkazo. English medium pia zina madaraja, la kawaida n la juu. Kawaida ni bora English inazungumzwa tu ila bora, wanazingatia mambo mengi nje ya kuongea English tu. Mfano, St marrys, kule bata na watoto wanalelewa kama kuku wa kienyeji. Mtoto wa St marrys English kama lugha ya Mama tu, ila ukimpa swali lenye utatanishi, utaona anajing'atang'ata. Mfano wa shule bora ni ahmes, kule sio kingereza tu, mtoto anapelekwa mbio na analazimishwa kuzingatia kila jambo linalohusiana n malezi yake bora kielimu. Mwanafunzi wa ahmes ukimpeleka hizo st kayumba zenu au local English medium schools, anafundisha kwa utuo na wanafunzi watamuelewa.
Alafu kuna International schools. Hizi ni tofauti sana. Kwanza naomba nianzie kwenye usaili wa walimu wao. Mwalimu wa somo flani ni lazima awe alipiga A kwenye somo analofundisha, lafudhi yake iwe haijaathiriwa na lugha ya mama, sio kuongea tu, ila ni lazima awe na uwezo wa kuwasiliana kwa ufanisi wa hali ya juu.
Kuna kitu kinaitwa education systems, kwa tz ni lasaba, form 6 n chuo ni 3 yrs, so mfumo wetu wa elimu ni 7.6.3, Kenya ni la 8, form 4, chuo 4, hivyo ni 8.4.4, ambapo jumla hadi mwanafunzi kumaliza ni miaka 16. Ila kwa International schools, wale wanatumia mfumo tofauti kabisaaaaa. Kwanini, Mfano sisi 7.6.3, mtoto anafundishwa vitu vingi ambavyo havitomsaidia katika maisha yake, ni kama kunywa maji ya mto maana yanaonekana ni masafi. Ila kwa International schools, mtoto anafundishwa vitu vichache vya msingi tu. Juu ya yote, hadi kuitwa international, basi inamaanisha system/mfumo wake wa elimu ni wa kimataifa. Ninamaanisha, shule nyingi zinafundisha elimu ya nchi nyingine, haswa UK. Na kwa wastani, kati ya shule 100, 95 wanafundisha British system ambayo cjafuatilia ni miaka mingapi mtoto kumaliza shule, ila ninachojua mwanao akiwa 6, upande wa British system atakuwa anamalizia chuo.
So hizo ni shule zina walimu wazuri sana na waliobobea kwenye taaluma(sio failures)* kwanza nyingi zinanunua taaluma kutoka walimu wa nchi za nje, mazingira ya shule mazuri yenye kila kitendea kazi tena venye ubora na kila kitu chao ni bora.
Ndani ya maisha yangu, nimekutana na wanafunzi kutoka shule ya strathmore pale nairobery, kwenye hafla ya music festival. Wale wanafunzi ni bora ndugu zangu. Kichwani wapo vzuri kinoma, ukiwa karibu nao lazima ujishtukie. Ile shule ni ya boys, ila nilikutana n boys wanaimba soprano zaidi hata mabinti wa shule yangu. Mwalimu wao wa music alikuwa ni mmorocco, kila item either washike no 1 sisi no 2 au vice versa. Wanafunzi wa karura tulizoea kuwaonea wote tunaokutana nao ila sio wale binadamu. Aisee kwa experience nikiyoipata, inatosha kusema kati ya ndoto yangu kubwa zaidi ni mwanangu kuja kusomea strathmore kuanzia pri hadi seco. Tukiskia International school tuache fitna, tuzipe heshima zake. Zile ni shule na ni shule kweli kweli. Umasikini usitufanye kuvikebehi vitu bora kutokana hatuwezi kuviafford. Vijana tafuteni pesa watoto wetu waje kupata elimu bora, sio bora elimu. Ni fahari sana kwa mzazi kumuona mwanae akiwa bora upstairs. International schools sio 5 stars hotels, Zile ni shule n nusu.